Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

haya mambo hayawezi kutendeka bila jk kujua. Kaweka baraka zake hapo
 
Kwenye Mwanahalisi toleo la 9 - 15 Mar 2011 kuna habari kuwa Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa. Kama ni kweli wauaji wafahamu kuwa tunawafahamu na mchezo huu wameanza siku nyingi au wanaiga wale wa zamani. Kwani waliowauwa wafuatao tunawafahamu: Imran Kombe, Kolimba, Sokoine, Malima, Amina.

Ni kwa nini polisi walizingira hotel aliyofikia Dr. Slaa pale Kahama kuanzia saa tano usiku hivi na kumtaka atoke usiku ule? Wajaribu waone kilichomtoa Kanga manyoa, kuungua shoka na kubaki mpini!
 
Kwenye Mwanahalisi toleo la 9 - 15 Mar 2011 kuna habari kuwa Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa. Kama ni kweli wauaji wafahamu kuwa tunawafahamu na mchezo huu wameanza siku nyingi au wanaiga wale wa zamani. Kwani waliowauwa wafuatao tunawafahamu: Imran Kombe, Kolimba, Sokoine, Malima, Amina.

Ni kwa nini polisi walizingira hotel aliyofikia Dr. Slaa pale Kahama kuanzia saa tano usiku hivi na kumtaka atoke usiku ule? Wajaribu waone kilichomtoa Kanga manyoa, kuungua shoka na kubaki mpini!

mkuu angalia hapo kwenye red, ninapenda kuamini kwamba ni hasira tu imekusukuma kuandika hilo neno au vinginevyo hebu tutajie mkuu
 
Kwenye Mwanahalisi toleo la 9 - 15 Mar 2011 kuna habari kuwa Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa. Kama ni kweli wauaji wafahamu kuwa tunawafahamu na mchezo huu wameanza siku nyingi au wanaiga wale wa zamani. Kwani waliowauwa wafuatao tunawafahamu: Imran Kombe, Kolimba, Sokoine, Malima, Amina.

Ni kwa nini polisi walizingira hotel aliyofikia Dr. Slaa pale Kahama kuanzia saa tano usiku hivi na kumtaka atoke usiku ule? Wajaribu waone kilichomtoa Kanga manyoa, kuungua shoka na kubaki mpini!
Mkubwa ni nimekuona kwenye jukwaa la Lisu Lisu aibuka kidedea kama ifatavyo
Tetesi na kukurupuka tofauti yake ni nini?
...sasa hapa umekurupuka hii habari kama sikosei imejadiliwa jana.
 
haya mambo hayawezi kutendeka bila jk kujua. Kaweka baraka zake hapo
Kama usemalo ni kweli basi ile kauli ya Mtikila iliyompeleka mahakamani kuwa JK ni gaidi itazamwe kwa umakini. Hivi vitendo vya aina hii ni ugaidi 100%
 
Habari nzima imenukuliwa toka gazeti MTANZANIA

Jeshi la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua. Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.

Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili “kuwapumbaza Watanzania wote” baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.

Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.

Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe


“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.

“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.

“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.

“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).

“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”

Maoni ya wanasiasa na wasomi

Baadhi ya wasomi na wanasiasa mbalimbali waliohojiwa na MTANZANIA wameshangazwa na taarifa hii ya Dk. Mwakyembe, hasa kwa msomi kama yeye kuamini masuala ya uchawi.

“Ninachoweza kumshauri kaka yangu (Mwakyembe) ni kuchapa kazi zake alizopewa za ubunge na uwaziri, akiingiza masuala ya kuamini ushirikina atakuwa anapoteza sifa yake ya usomi,” alisema mmoja wa wahadhiri.

Dk. Mwakyembe anatambulika katika Jeshi la Polisi kama mmoja wa viongozi wanaotoa maelezo yenye utata kuhusu usalama wao.

Ameibua suala hili huku kukiwa bado na kumbukumbu za yeye kupata ajali mkoani Iringa na kudai kwamba lori lililohusika lilikuwa limepangwa kumtoa uhai.

Hata hivyo, Polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni uzembe na mwendo kasi wa dereva wa Dk. Mwakyembe.
 
Jana gazeti la mtanzania linalomilikiwa na RA lilitoa taarifa ya njama za kuwaua viongoz mbalimbali hapa nchini..............tishio hilo sio la kubeza, uchunguzi ufanyike kwa umakini zaidi. Ningeomba ile intelijensia ya IGP aliyoipigia debe kuhusu vurugu za arusha ifanye kazi yake sasa
 
Suala la msingi ni jeshi na vyombo vyote husika kufuatilia hizi tuhuma ili kujua undani na ukweli wake na sio suala la wasomi na wahadhiri kuanza kumlaumu na kumshauri mwakyembe upuuzi na ujinga eti msomi mzima kuamini mambo ya uchawi -

Na labda hawajaelewa au hawajasoma na kuelewa vizuri huu waraka ni kwamba mwakyembe amejaribu kuelezea mtiririko mzima au mpango mzima ulivyosukwa kwa kuwa husisha hata waganga wa kienyeji, na kama binadamu wengine ni lazima awe na hofu juu ya maisha yake kama kweli kuna hujuma juu ya maisha yake,........

Nafikiri jeshi la polisi litakua na kazi ndogo sana kwani mwakyembe amejaribu kuwa mkweli na amewataja kwa majina karibu wahusika wote.
 
kweli mungu amlinde mikononi mwa mafisadi yote haya naamini ni mkono wa mungu vinginevyo wangeshampumzisha cku nyingi
 
Hizi ni tuhuma nzito, ILA KUAMINI USHIRIKINA HAPO NAMUONDOLEA CREDITS
 
Mhm kama kweli basi hii nchi mafisadi wanatishia hii nchi!!
 
Nasikitika kuwa mafisadi wameshaifikisha hii nchi point of no return. Mlango wa udini walioutumia wamefanikiwa, vurugu lazima zitokee. Mi nawashauri tu kuwa hata wakiwaua hao wa5, wapo maelfu wenye uchungu na uwezo wa kupigania nchi yetu.
 
Gazeti la Mwanahalisi la leo Jumatano limeeleza madai ya Dr. Mwakyembe kuwa kuna watu wana suka mpango wa kumuua.

Ameshatoa taarifa polisi akitoa vielelezo vya watu wanaoshukiwa kuhusika katika njama hizo. Amekuwa very explicit kuhusu nyendo za watu hao na magari waliyo tumia ambayo mengine yana namba za serikali, kampuni ya Voda, Caspian, n.k.

Kwa taarifa zaidi tafuta gazeti la Mwanahalisi la Jumatano leo tarehe 9.

Karibuni.
 
Amani iwe kwenu great thinkers,

Gazeti la leo la mwanahalisi nimeongozwa na kichwa cha habari cha kusikitisha kisemacho mwakyembe, Slaa, watishiwa kuuwawa. Katika habari hiyo ambapo imeambataniswa na barua ya Dr Mwakyembe kwenda jeshi la polisi akiomba ulinzi wa maisha yake, imeelezwa kuwa wapo wasomali kutoka Al shabab walioingia kupitia Kenya. Na wakenda kwa mganga aitwaye prof. majungu ambaye aliwazindika na kuwapa sharti la kuua bila kutumia silaha na wanapaswa kuanza na Mwakyembe, then Dr. Slaa.

Watu hao wanaelezwa kuwa walipokua wanatoka kwa mganga walikuwa na gari yenye namba za serikali (STK) ila walipofika mafinga walipokelewa na Hilux mayai ya VODACOM hadi morogoro ambapo walipokelewa na gari nyingine inayomilikiwa na kampuni ya CASPIAN. Walipofika dar walipokelewa na gari ya polisi na walikaa kwenye apartment iliyo ghorofani ambapo chini yake kuna msikiti wa WAARABU unaoitwa MALKAZI ulioko Kiwalani.

Hawa watu baadaye walitembelewa na Fred Lowassa na aliwapelekea mbuzi watatu, then wakaelekea dodoma ambapo walipokelewa na afisa mkuu wa polisi wakabebwa na gari ya polisi ambapo Mwakyembe ameonesha ushahidi kuwa walikagua nyumba yake ambayo amepewa na serikali kwa ajili ya kuishi atakapokuwa dodoma bungeni mwez April.

Pia mwakyembe ametaja wengine walio wenye list ya kuuwawa kuwa ni Reginald Mengi, Anna Kilango, Bernad membe. Pia Shekh Yahya ameshutumiwa /ametajwa kuwa huenda alishirikiana na hao wanaopanga mpango na Kubenea akalazimika kumuuliza kuhusu ushirika wake lkn alisema …subiri matokeo kwani kuna vigogo watakufa…


Pia gazeti linaeleza kuwa tr 5 Febr wageni wengine waliwasili kwa ndege wakitokea Uganda na walipokelewa na magari mawili; moja la polisi lenye no PT 0288 (polisi ujenzi) na la pili lenye no za kibalozi T 69 CD 82 aina ya RAV4. Anasema hawa wageni wawili walikuwa na mazungumzo ya kina na hawa wasomali wa al shabaab.

Pia Hawa alshabaab walipofika morogoro walipokelewa na na askari Sabasita wa jeshi la polisi morogoro ambapo walikaa ktk hoteli mbili tofauti; Hilux hotel na Top life na aliyewawekea booking ni mmiliki wa Morogoro hotel aliyetajwa kwa jina la Kari.


Je Great thinkers mnaonaje njama hizi?
 
Pia dr Mwakyembe ameeleza kuwa hao al shabaab walishawishiwa kuja kuwaua baada ya kuelezwa kuwa yeye (Mwakyembe) na hao wengine kina Mengi, Slaa, Kilango etc eti ni maadui wa Uislam na wamekuwa wakisaidiwa na makanisa hivyo haina budi maisha yao kukatishwa.
 
khee huyu mzee si alisema kastaafu mambo ya kutabiri....
 
Kila kitu knamwisho wake hao mafsadi wakfanikiwa kw hlo wajue sio mwisho wao itarudi kwao,hawana uwezo wakupumbaza watz wote ili tuchukulie rahc ka wanavyozani!

Tena nawatahazarisha wasije kufikiria kufanya huo mchezo wao,watabainika haraka sana! Na hao watu 7 watakua ndio chambo kwao! Ili wajue kuna watu wamejituliza hawataki bughuza nayeyote wathubutu kufanya hvyo waone kama watasalia na hii itawanyamazisha wote watakao hucka direct or indirect!

Hii nchi si yakwao peke yao niyetu sote! Wafanye ufisadi halafu waue watu,aaah... Haiwezekani!! Wakijaribu tu watajuta na ndo hapo wajue kuna majasusi waliobobea within ths land of tz!

Dr.Mwakyembe, Dr.Slaa, na wengine chapeni kazi tena kwa kujiachia na kwa moyo kabla hawajathubutu kunyosha vidole watajikuta wanaugulia mauti uti!!
 
Back
Top Bottom