Kuviziana kwenye barua za KKKT na Wizara kama suala la Zanzibar kujiunga na OIC mwaka 1992

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Kwanza ni tukio la siku 30 sasa na mtiririko (chronology) wa sakata hili uko hivi

1: Thursday, May 10, 2018
Ofisi ya Msajili Wizarani, inaandika barua yenye kumbukumbu SO.748/22. KKKT hawajui lolote kuhusu barua hiyo maana hawakuipata. Vyombo vya habari havijui kinachoendelea wizarani na barua hii haionekani mitandaoni. Haijulikana kama Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kama nao wamepelekewa

2: Tuesday, May 22, 2018
Ofisi ya Msajili Wizarani, inaandika ya pili barua yenye kumbukumbu SO.748/24. KKKT hawajui lolote kwani hawajapata barua hii na hata ile ya kwanza. Bado magazeti hayajui kinachoendelea na barua hii haionekani mitandaoni.

Haijulikani kama TEC nao wametumiwa barua kama hii. Lakini ukiangalia folio za file zinaonyesha sasa kuna mawasiliano zaidi maana namba za file zimetoka SO.748/22 kwenda SO.748/24. Je, SO.748/23 ni ya barua gani? Je, siyo barua ya TEC kama wanavyodai wengine.

3: Wednesday, May 23, 2018
Hii ni siku moja baada ya barua ya pili kuandikwa. Pia ni siku hii Mwenyekiti wa KKKT, Askofu Shoo anarudi safari kutoka Marekani na siku mbili zifuatazo anakuwa na jambo la kiaskofu kuhudumia hivyo hana taarifa na kinachoendelea Arusha makao makuu ya KKKT na wala KKKT hawana taarifa kwani barua zote hazijawafikia.

4: Friday, May 25, 2018:
KKKT makao makuu (Arusha) wanapokea barua zote mbili yaani ile ya kwanza SO.748/22 na ile ya pili SO.748/24.

Kwa sababu KKKT iko Arusha, haijulikani ilisafiri kwa njia gani kutokea ilikotokea. Je, serikali ina watumishi wake wa kusafirisha? Je, ni EMS, DHL, FEDEX?

Bado mitandao haijui lolote na barua zote mbili hazionekani mitandaoni. Haijulikani kama TEC nao wamepewa au kanisa jingine.

5: Tuesday, May 29, 2018:
Askofu Chedial Sandoro anamuwakilisha Mwenyekiti wa KKKT katika kikao cha Wizara. Mtiririko huu unaonyesha kuwa barua zile mbili zilikuwa zinamuita Wizarani. Inaonekana suala la risiti za amlipo liliongelewa hapa.

Hadi siku hii, hakuna gazeti, TV, Redio au mtandao unaojua kinachoendelea..

6: Wednesday, May 30, 2018:
Ikumbukwe ni siku moja tu baada ya Askofu Sendoro kufika ofisini. Msajili katika anaitumia KKKT barua ya tatu, sasa ina file number (SO.748/25). Hadi siku hii mitandao haijui chochote.

Barua hii inatoa siku kumi kwamba Baraza la Maaskofu KKKT linaweza kufungiwa na maaskofu (Wewe Askofu) ahakikishe ameufuta waraka ule ndani ya siku kumi yaani kufikia Saturday, June 09, 2018.

7: Tuesday, June 05, 2018:
Katibu wa KKKT anaijibu barua ya tatu (SO.748/25) ina maelezo mengi na ikiomba kuongezewa siku 30, yaani hadi Sunday, July 08, 2018 ili maaskofu wakutane na watoe majibu kama ni kuufuta au kutoufuta waraka.

Hii pia ni siku sita ya deadline ambazo KKKT walipewa na Wizara.

Barua hii ya KKKT ina muhuri wa KKKT chini kabisa kuthibitisha ni wao wameituma. Pia ina muhuri wa Wizara, juu kulia umefifia kuonyesha kwamba ni photocopy.

Hadi siku hii bado mitandao haijui lolote linaloendelea.

8: Wednesday, June 06, 2018:
Asubuhi barua ya tatu (SO.748/25) inaonekana mitandaoni, Whatsapp, Jamii Forum, Twitter, Facebook nk. Kwenye Jamii Forum imeonekana asubuhi at 09:17am.

KWa mara ya kwanza sasa jamii inaanza kujua kinachondelea. Watu wanahoji, wanatetea, wanapinga. Wachache sana wanahis barua hii ni fake.

Mchana (tuseme at 14:14) Zitto Kabwe anailaumu serikali akisema ""Tishio la serikali kwa kanisa la KKKT linapaswa kupingwa na kila mtanzania. Tukiruhusu KKKT kuingiliwa, hakuna atakayepona"".

Jioni (tuseme at 17:17) Zitto Kabwe anamtumia message Humphrey Polepole kuhusiana na barua hii, kisha Zitto anataarifu kwamba kasikia kuwa hata wakatoliki TEC wamepewa barua kama hii.

Usiku (tuseme at 20:17) Humphrey Polepole anatangaza kwamba barua hiyo haina tatizo na ananukuu Biblia kifungu cha Warumi 13: 1-5, kinachotamka kwamba binadamu anataiwa kuzitii mamlaka za dunia kwani zimewekwa na Mungu.

9: Thursday, June 07, 2018
Asubuhi (tuseme at 07:02) Magazeti matatu, yanaitaja habari ya barua hiyo yaani MWANANCHI, TANZANIA DAIMA, MTANZANIA. Wasio mitandao sasa wanaijua hali ilivyo.

Asubuhi (tuseme at 09:34) katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, James Mbatia anamuuliza Waziri Mkuu swali kuhusu barua hiyo inayoenea mitandaoni. Naibu Spika anamzuia Waziri Mkuu kujibu swali hilo kwani ni la kidini na tayari kuna muongozo wa tangu siku Saed Kubenea alipouliza swali kama hilo.

Mchana (tuseme at 13:13) Wabunge wa UKAWA, wakiwa nje ya Bunge, msemaji wakiwa Mbatia, wanashauri KKKT wasijibu barua hiyo ili tuone kitakachotokea.

Jioni (tuseme at 19:19) Twitter inasambaa ikinukuu Mkuu wa KKKT, Askofu Shoo akisema "Hajawahi kutokea kiumbe ama binadamu yoyote mwenye cheo chochote ama ulinzi wowote, anaedhani kwake ni fahari kulitisha kanisa ama kulitikisa. Kiumbe huyo ama kiongozi huyu hajazaliwa wala hatazaliwa"

Friday, June 08, 2018:
Asubuhi (tuseme at 08:05am), Jamii Forum inaonyesha barua ambayo KKKT waliijibu Wizara.

Mchana (tusema at 12:44), Waziri Mwigulu Nchemba, anatangaza kwamba barua ile ya tatu (SO.748/25) iliyoonekana mitandaoni ni batili, haina mamlaka ya Wizara. Nakala haikutumwa kwa Waziri.

Pia anatangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba ambaye jina lake limeonekana kwenye ile barua ya tatu.

Hakuna loote linalosemwa kuhusu barua mbili za kwanza yaani SO.748/24 na SO.748/24, kwani hizi hazikuonekana mitandaoni.

10: UCHAMBUZI:

Baada ya kuuona huo mtiririko wa matukio sasa ni uchambuzi binafsi wangu na wako. Binafsi naichukulia hii kama ilikuwa vita kali ya kuviaiana.

Vita hii iliendeshwa kiumakini pande zote. Upande mmoja uliiendesha kisirisiri na kama ingeenda mwishoni, tungesikia maaskofu wanaufuta ule waraka au baraza lingefutwa na kingekuw akitendo cha ghafla na tulioko nje ya nchi na mlioko nyumbani msingekuwa na la kujiandaa.

Wakuu wangekuja na hoja kwamba KKKT walipewa barua tatu na hawakujibu na hivyo hakuna wakulaumiwa kwani walipewa nafasi ya kujitetea na hizi barua zingerushwa mitandaoni kuthibitisha hilo, tena zingerusha hata zile mbili za kwanza na hata askofu Sendoro angeonekana aliitwa wizarani.

Mkakati si mdogo huu.

KWa upande wa pili, inaelekea walijua mkakati huu na wenyewe wakajiandaa kwa kuvizia kwa mbinu ya hali ya juu zaidi. Kumbuka wamepata mawasiliano ya barua zote mbili May 25, 2018. Hawakuituma mitandaoni. Kwa nini? Ingeonekana mitandaoni tusingepata utamu huu. Pia walitaka wajiridhishe kwamba wao ni wastaarabu japo walijua hali inaelekea wapi.

May 30, 2018 wakapata barua ya tatu sasa ya vitisho, tena baada ya kutoka Wizarani. na wakapewa siku kumi kuufuta waraka na siku saba kuhusu malipo.

June 05, 2018, KKKT wakaamua kuwajibu Wizara na wote tumeona majibu yao.

Sasa kwa nini wametuma June 05, 2018. KWanza ni siku nzuri maana kama mtu kakupa dealine ya siku kumi maana yake hiyo ni siku ya sita, hivyo ilishabaki siku nne tu.

Kesho yake yaani June 06, 2018 ikatumwa sasa barua ya wizara huku mitandaoni. KWa nini hapo ni patamu. ni kwa sababu kadhaa.

Ikumbukwe kwamba zile barua mbili za kwanza na hata ya tatu mawasiliano yalikuwa yanakuja KKKT. Hivyo mwenye uwezo wa kuthibitisha kwambe imetoka wizarani hayupo maana dispatch unathibitisha mpokeaji. Hivyo KKKT walisaini kwenye dispatch ya aliyeleta lakini hawakuwa na namna ya kuuthibitishia umma kwamba aliyewaletea ni wizara.

Hivyo, lazim autafute namna ya kuifanya wizara isiweze kukataa kutohusika na hii ni kwa namna ya KKKT na wao ktuma barua halafu ikaonekana imepokelewa kuke wizarani.

Ndiyo maana mitandaoni ilipoonekana ile ya Wizara, aliyeandika hakukanusha maana ukikanusha watatoa ya pili.

Hivyo utaona stratergy ya kuituma mitandaoni ya kwanza, yaani ya Wizara imeibua mengi. Kwanza watu wamepeleka maswali hata wizarani na hawakujibiwa. Swali limeulizwa bungeni, halikujibiwa. UKAWA wametoka wakashauri KKKT wasijibu lolote.

Ndipo sasa baada ya UKAWA na nchi nzima kuijadili vya kutosha ile barua ya kwanza ndiyo jana asubuhi inatoka barua yenye majiby ua KKKT kwenda wizarani. Hadi hapo stratergy imecheza kama Pele.

KWa ujumla aliyezipeleka hizi barua mitandaoni ametueleta mchezo mtamu katika historia ya mitandao. Alisoma jamii itaelekea wapi kila dakika na kaila alipoona sasa ni wakati muafaka analeta kitu kipya na wote tunabadilika mawazo.

KWa ujumla kaweza kuifanya nchi nzima tuka-panic. KWa ujumla barua ya pili ilikuwa ni lazima mtu awajibika pale Wizarani lasivyo waziri mwenyewe angewajibika.

SUALA LA ZANZIBAR KUJIUNGA NA OIC:

Suala la kujiunga na Jumuiya ya nchi za kiislamu (OIC) nalo lilikuwa hivihivi na mtukio yote hayo hayakutoka kwenye mitandao, ambayo haikuwepo, bali yalitoka kwenye gazeti la MOTOMOTO.

July 25, 1992:
Ombi linatoka kwa ofisi ya Waziri Kiongozi la Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya OIC (file WK/OIC/TS.2/1)

October 28, 1992:
Serikali ya Tanzania inatuma telex yenye namba RITX/MISC/255/92 kwenda OIC, ikisema haina kizuizi kwa Zanzibar kujiunga na OIC.

December 01, 1992:
Mkutano wa nchi za OIC, unaofanyika Jeddah, Saud Arabia, unaikubali Zanzibar kama mwanachama mpya.

December 04, 1992:
Gazeti la Daily Gulf Times linaitaja Zanzibar kujiunga na OIC.

December 16, 1992:
Asubuhi (tusema at 07:16) Gazeti la MOTOMOTO la huko nchini Tanzania (lilishakufa) linaripoti Zanzibar kujiunga na OIC. Mjadala unaanza hapo nchini.

Mchana (tusema at 11:35), Waziri wa Mambo ya Nje, Hassan Diria, anakanusha kwamba Zanzibar haijajiunga na OIC. Anasema Wizara haijatoa kibali chochote.

Msimamo wa vyama vya siasa siku hiyo ni hivi. CCM na CHADEMA siku hii wote kila mmoja alikuwa aktika Mkutano Mkuu. CCM wakiwa Dodoma, CHADEMA kikiwa ndiyo kwanza bado kimepewa usajili wa muda.

Kwa vile mkutano mkuuwa CCM ulikuwa unaendelea, wajumbe wa CCM wakaichukua ajenda hiyo kimyakimya ili iwe ya bungeni Fabruary 1992. Habari zinaendelea magazetini na has MOTOMOTO kujadili kila toleo.

January 09, 1993:
Zanzibar inakiri kwamba ilijiunga na OIC

January 20, 1993:
Kamai ya BUnge ikiongozwa na Mh. Philip Marmo inaamua kuchunguza na kuona kama kweli Zanzibar imejiunga na OIC

Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Dr. Omar Ali Juma anaitisha kikao na viongozi wa dini na kuwabembeleza kwamba Zanzibar si taifa la kiislamu kwani katiba ya nchi haina dini.

January 28, 1993:
Hassan Diria anahamiswa kutoka kuwa Waziri wa mambo ya nje na kuwa waziri Kazi na Vijana, anabadilishana Wizara na Joseph Rwegasira.

February 02, 1993:
Rais wa Zanzibar, Dr. Salmin Amour anatangaza kwamba ni kweli Zanzibar ilijiunga na OIC na haijavunja katiba ya Tanzania.

February 15, 1993:
Rais wa Zanziba, Dr. Salmin Amour anahutubia semina ya Bunge la Muungano anasema Zanzibar hajavunja mkataba wa muungano.

February 17, 1993:
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Philip Marmo, anasema Zanzibar imevuna mkataba wa Muungano.

February 18, 1993:
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Philip Marmo, anawasilisha ripoti bungeni kuhusu Zanzibar kujiunga na OIC. Bunge linataka hatua kali kwa waliohusika.

July 30, 1993:
Wabunge 55 (G55) wa CCM wanaleta taarifa ya kuleta hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika ndani ya muungano.

August 13, 1993:
Rais wa Zanzibar baada ya shinikizo la bunge na vikao vya NEC-CCM vilivyohudhuriwa na Julius Nyerere, Zanzibar inajitoa kwenye OIC.

August 24, 1993:
Bunge la Tanzania linapitisha hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika ndani ya muungano.

November 02, 1994:
Julius Nyerera anazindua kitabu cha "Uongozi wetu na hatina ya Tanzania'. Anaeleza mfululizo wa OIC, Utanganyika na Umakamu wa Rais. Anasema Waziri Mkuu, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba wanapaswa kujizulu kwa kumshauri vibaya Rais Ali Hassan Mwinyi

November 02, 1994:
Katibu mkuu wa CCM, Horace Kolimba anakataa kwamba hana kosa lolote na haoni sababu ya kujiuzulu. KWamba hakuchaguliwa na Julius Nyerere, alichaguliwa na wana CCM.

December 02, 1994:
Katibu mkuu wa CCM, Horace Kolimba anajiuzulu. Rais Mwinyi analivunja baraza la Mawaziri na kumwondoa John Malecela, kisha Cleopa Msuya anakuwa Waziri Mkuu mpya.

Hivi ndivyo matukio haya ya OIC yalivyokuwa. Kuna kukanusha kisha kuwajibika. Hili la sasa bado safari inaendelea.

 
Uchambuzi na ulinganifu mzuri.
Kumbukumbu iliyotulia kabisa
Siasa siasani ktk vitu sio siasa
Kuchezea kaa la moto motoni
Kuungua ni jadi hadi kelele kali

Bazazi
 
Walitaka wayapige makanisa kimya kimya, tatizo huko ugambani uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho.
 
Dini Zote
Ndiyo Zenye Serikali Popote Duniani
*Serikali Sehemu Kubwa Huwa Hazina Dini


Kwa Maelezo Hayo Serikali Lazima Iwe Tulivu Yaani Inapokuwa Kwenye Dini Ikumbukwe Rais Anapokwenda Kwa Viongozi Wa Dini Zote Anakuwa Mnyenyekevu
 
Bunge lilikua na meno kiasi miaka ya 90, walikua na ujasiri wa kupitisha hoja ya kuundwa serikali ya Tanganyika ndani ya muungano lakini kwa mara nyingine tena Nyerere akaharibu mchakato japokua hakua rais, he really screwed up this country with his primitive beliefs and fears
 
Walitaka wayapige makanisa kimya kimya, tatizo huko ugambani uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho.

Ukisoma uchambuzi wangu nimesema stratergy ya kanisa ilikuwa maili mia 100 zaidi ya wizara

Leo Waziri kaukana waraka...haya ndio madhara ya chama kuingilia mambo ya serikali.
Kipole pole kinakurupuka sana kila kitu kinadandia.

1.5 tril kilidandia.
Barua ya msajili kimedandia.

Polepole afungwe speed mita.
Polepole wenzako wameikana barua utaweka wapi uso wako? Nimeshakuonya wacha kukurupuka , hoyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni sahihi, hakuna asiyejua kuwa "mkulu" anapenda kusikia Sifa tu zikielekezwa kwake. na ndio maana "vyombo vya ulinzi na usalama " vitapata stahiki zao zote ukilinganisha na sectors nyingine kwa sababu wao huwa hawahoji. Ni kutii amri tu. Yaani kwao kumkosoa "mkulu" ni jinai .

Kuhusu KKKT na TEC zile nyaraka hakupendezwa nazo. Na zaidi aliumizwa sana na waraka wa KKKT. Hapo ukiongeza na chuki Binafsi kwa jamii ya watu wa kaskazini, ingetokea "ambush" ambayo kimsingi tungebaki vinywa wazi. Siamini kama Baraza lingefutwa, ila wapo wengi ndani ya baraza ambao wangeonja joto.

NB:
Hiyo plan imegonga mwamba Kama alivyosema Askofu SHOO. Na huo unaweza kuwa mwanzo wa plan B. Maaskofu wawe makini na waumini tukae mkao wa kula
 
utumishi wa umma wa awamu hii..?? yaani ni kama kila mtumishi ana bomu la muajili wake amelikumbatia...kwa maslahi ya muajili kubaki salama......
 
Uchambuzi wa namna hii unanikumbusha Jamiiforums ya enzi hizo iliyojaa watu wenye weledi Wao Sio Siku hizi Mitoto ya Facebook Na Wasap Na Instagram imemiminwa humu kuleta Vurugu
 
Asante kwa uchambuzi. Well said.

Kilicho wazi ni kuwa tuna serikali inayosimama kwenye hadaa.
 
Ni sahihi, hakuna asiyejua kuwa "mkulu" anapenda kusikia Sifa tu zikielekezwa kwake. na ndio maana "vyombo vya ulinzi na usalama " vitapata stahiki zao zote ukilinganisha na sectors nyingine kwa sababu wao huwa hawahoji. Ni kutii amri tu. Yaani kwao kumkosoa "mkulu" ni jinai .

Kuhusu KKKT na TEC zile nyaraka hakupendezwa nazo. Na zaidi aliumizwa sana na waraka wa KKKT. Hapo ukiongeza na chuki Binafsi kwa jamii ya watu wa kaskazini, ingetokea "ambush" ambayo kimsingi tungebaki vinywa wazi. Siamini kama Baraza lingefutwa, ila wapo wengi ndani ya baraza ambao wangeonja joto.

NB:
Hiyo plan imegonga mwamba Kama alivyosema Askofu SHOO. Na huo unaweza kuwa mwanzo wa plan B. Maaskofu wawe makini na waumini tukae mkao wa kula
Plan B dhidi ya kanisa ni plan B dhidi ya Mungu! Haitamwacha mtu salama! Naogopa kidole kisije kikaandika ukutani " mene mene ............"
 
Uchambuzi wa namna hii unanikumbusha Jamiiforums ya enzi hizo iliyojaa watu wenye weledi Wao Sio Siku hizi Mitoto ya Facebook Na Wasap Na Instagram imemiminwa humu kuleta Vurugu

Unaweza ku block ID zao, yaani unawapa ban mwenyewe.
 
MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI - "MUNGU ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha". Daniel 5: 25 -26.
 
Back
Top Bottom