Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

khee huyu mzee si alisema kastaafu mambo ya kutabiri....
Kazi yake sio ya kustaafu. Tena alipobanwa na Kubenea kuhusu kushiriki kwake ...amechimba mkwara na kumwambia asubiri matokeo ....
 
Siasa bana zina uchafu mwingi, na fitina, na majungu, na uongo, e.t.c - You wonder hawa watu pale Azania Front wanakaa Front Benches!

Inawezekana pia ni false-alarm au kuna some sort of preemption @ work!
 
Hawataweza,mie nadhani wanatisha watu,ili kututoa kwenye lengo kuu la ukombozi,ila hatuogopi,haturudi nyuma hadi kieleweke
 
Amani iwe kwenu great thinkers,
Gazeti la leo la mwanahalisi nimeongozwa na kichwa cha habari cha kusikitisha kisemacho mwakyembe, Slaa, watishiwa kuuwawa. Katika habari hiyo ambapo imeambataniswa na barua ya Dr Mwakyembe kwenda jeshi la polisi akiomba ulinzi wa maisha yake, imeelezwa kuwa wapo wasomali kutoka Al shabab walioingia kupitia Kenya. Na wakenda kwa mganga aitwaye prof. majungu ambaye aliwazindika na kuwapa sharti la kuua bila kutumia silaha na wanapaswa kuanza na Mwakyembe, then Dr. Slaa. Watu hao wanaelezwa kuwa walipokua wanatoka kwa mganga walikuwa na gari yenye namba za serikali (STK) ila walipofika mafinga walipokelewa na Hilux maya ya VODACOM hadi morogoro ambapo walipokelewa na gari nyingine inayomilikiwa na kampuni ya CASPIAN. Walipofika dar walipokelewa na gari ya polisi na walikaa kwenye apartment iliyo ghorofani ambapo chini yake kuna msikiti wa WAARABU unaoitwa MALKAZI ulioko ilala. Hawa watu baadaye walitembelewa na Fred Lowassa na aliwapelekea mbuzi watatu, then wakaelekea dodoma ambapo walipokelewa na afisa mkuu wa polisi wakabebwa na gari ya polisi ambapo Mwakyembe ameonesha ushahidi kuwa walikagua nyumba yake ambayo amepewa na serikali kwa ajili ya kuishi atakapokuwa dodoma bungeni mwez April. Pia mwakyembe ametaja wengine walio wenye list ya kuuwawa kuwa ni Reginald Mengi, Anna Kilango, Bernad membe. Pia Shekh Yahya ameshutumiwa /ametajwa kuwa huenda alishirikiana na hao wanaopanga mpango na Kubenea akalazimika kumuuliza kuhusu ushirika wake lkn alisema …subiri matokeo kwani kuna vigogo watakufa…

Je Great thinkers mnaonaje njama hizi?

Heshima mbele. Lakini kichwa cha thread yako hakiendani na kile kilichoko gazetini. Mwanahalisi halitaji Caspian wala Rostam katika headline ya gazeti isipokuwa ndani tu kuna habari kwamba gari moja linalomilikiwa na Caspian lilihusika katika kubeba watu fulani katika njama hizo.

Hata hivyo kama habari hii ni kweli, basi serikali ya JK ndiyo ya kulaumiwa kukaa kimya tu huku watu wanapanga mauaji. Idea hapa ni kwamba AlShabab wa Somalia ndiyo ilikuwa waonekane wahusika kutokana na hoja iliyojengwa kwamba akina Mwakyembe, Slaa etc wanatumiwa na kanisa kuwakandamiza Waisilamu humu nchini Tanzania.

Lengo kubwa hapa ni kuondoa ushahidi kwamba ni mipango ya watu wa humuhumu ndani. Bila shaka baada ya tukio, magazeti fulani yangelipwa yatangaze kwa bidii kubwa kwamba wahusika ni AlShabab -- kupoteza lengo.

Serikali ya JK ni lazima iamke kutoka usingizini na ichukuwe hatua sasa hivi -- iwakamate wahusika wote.

By the way -- IGP Mwema kisha toa ripoti ya uchunguzi wake kuhusu njama za akina Manji dhidi ya mtoto wa Mengi kumbabikizia madawa ya kulevya?
Hakufanya chochote kwani IGP aliufyata mbele ya akina Manji/Rostam clique.
 
hii habari nimeipitia,na kama ni kweli maana mh mwakyembe ameweka vielelezo vya kutosha tu mf.no za magari yaliyotumika, majina ya watu nk, kama ni kweli mkwere jk ana kazi maana mhusika mkuu ni RA na EL.
 
Heshima mbele. Lakini kichwa cha thread yako hakiendani na kile kilichoko gazetini. Mwanahalisi halitaji Caspian wala Rostam katika headline ya gazeti isipokuwa ndani tu kuna habari kwamba gari moja linalomilikiwa na Caspian lilihusika katika kubeba watu fulani katika njama hizo.
.
Mkuu nakubaliana na ww lkn hapa tumeunganisha dots....mafinga hawa al shabaab walipokelewa na gari ya VODACOM, afu MOROGORO walipokelewa na gari ya CASPIAN ambako kote huko mh RA anahisa. Pili hawa Fred Lowassa aliwwapelekea mbuzi na pia RA na EL ni marafiki wakufa kuzikana, na nne EL ameanza kupasha kwa ajili ya urais 2015......unganisha nukta mkuu...
 
Inasikitisha sana. Mkiona mitambo ya Dowans inapigiwa jaramba ili iwashwe si bure. hawa watu wasingekuwepo hasa Mwachembe ilisha washa zamani. Huu ni mwiba kwa Urais wa lowasa na rostam 2015. and belive me or not mkwele ni mmoja wa njama hizi . mimi sijawahi kumwamini hata siku moja. Naye anapenda sana kumtumia Shehe yahaya katika maisha yake. na hata wanaopinga wapo kwenye njama hizo. tunashukuru mungu amewatangulia na anaufahamu mchango wao kwa maisha ya watanzania. zoezi hilo limeshidwa , wasubili DR slaa awe rais ili wakauote moto.
 
Mafisadi mwisho wao unakuja na sasa dalili zote ziko wazi, sina chembe ya shaka kwamba kama wakiua hawa watu basi ndio mwanzo wa nchi kuanza kuvurugika kabisa..ni ajabu nchi imekua na kundi la watu wenye nguvu kubwa kuliko serikali hii ni aibu kubwa kwa hawa watawala!!
 
Pia Mwakyembe anadai kuwa hawa alshabaab walikwenda kuzindikwa kwa mganga anayeishi ndani ya Selous game reserve. Kama ujuavyo kwenye game reserve you are not allowed to live in there unless for a special purpose. Sasa huyu mganga anaishi humo kwa ruhusa ya nani? Mimi nashawishika kuamini kuwa huyu mganga amefichwa huko na vigogo kwwa ajili yao tu.
 
Nami nikuulize maana maswali ya huyu Makyembe ni mengi, kwa nini yeye, na habari hii si ilichapishwa jana kwa nini kurudiwa na naona ya jana ilikuwa na info nyingi! Mwaka huu tutasikia mengi lakin hayapunguzi makali ya maisha so, go to hell sitaki habari hizi bora nikae pembeni niwahi Loliondo tu

If this is a true story then it is now obvious: It is ISLAM vs CHRISTIANITY. Ni dhahiri sasa UDINI hatimaye umeingia rasmi Tanzania. Tumekwisha! CCM na makuwadi wake wameuza nchi rasmi. Haiwezekani walengwa wote wa kuuwawa ni wa dini fulani tu na watuhumiwa ni watu wa mipango yote ni watu wa karibu na chama tawala.
 
khee huyu mzee si alisema kastaafu mambo ya kutabiri....

siku hivi hakuna watabiri, ila ni preinformers tu. yawezekana hata yeye anahusika, hiyo kujifanya kutabiri alikuwa anasafisha njia ili watu wauawe.
 
Mwakyembe wewe mwenywe ni mchawi pia, umetaka kuua wangapi , kuhofia ubunge utaukosa?
 
Pia Mwakyembe anadai kuwa hawa alshabaab walikwenda kuzindikwa kwa mganga anayeishi ndani ya Selous game reserve. Kama ujuavyo kwenye game reserve you are not allowed to live in there unless for a special purpose. Sasa huyu mganga anaishi humo kwa ruhusa ya nani? Mimi nashawishika kuamini kuwa huyu mganga amefichwa huko na vigogo kwwa ajili yao tu.

Hivi kama hiyo story ni kweli sasa wahusika wanaogopa nini? Kwani polisi inaweza linda evil spirit? I cant read you! Yaani watu wenyewe ni wakristo then eti ushirikina ndo unaodaiwa utawadhuru na kichekesho zaidi eti wanaomba ulinzi wa polisi...something is wrong somewhere! Hivi basi hata kama hatuna imani na Mungu basi shule zitusaidie jamani.....Its now becoming too much for people of this country na imani za kusadikika za stone age; mbona tuko kwenye era ya maendeleo ya juu sana ya dot.com au ndo wenzetu wamesha ipita hiyo stage na kufikia spirituality level?
 
Habari nzima imenukuliwa toka gazeti MTANZANIA
Maoni ya wanasiasa na wasomi

Baadhi ya wasomi na wanasiasa mbalimbali waliohojiwa na MTANZANIA wameshangazwa na taarifa hii ya Dk. Mwakyembe, hasa kwa msomi kama yeye kuamini masuala ya uchawi.

"Ninachoweza kumshauri kaka yangu (Mwakyembe) ni kuchapa kazi zake alizopewa za ubunge na uwaziri, akiingiza masuala ya kuamini ushirikina atakuwa anapoteza sifa yake ya usomi," alisema mmoja wa wahadhiri.

Dk. Mwakyembe anatambulika katika Jeshi la Polisi kama mmoja wa viongozi wanaotoa maelezo yenye utata kuhusu usalama wao.

Ameibua suala hili huku kukiwa bado na kumbukumbu za yeye kupata ajali mkoani Iringa na kudai kwamba lori lililohusika lilikuwa limepangwa kumtoa uhai.

Hata hivyo, Polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni uzembe na mwendo kasi wa dereva wa Dk. Mwakyembe.

Hapo kwenye red!, Wanaojiita wasomi ni akina nani??

Ni wasomi wangapi ambao sio washirikina??

Kwa mfano Taasisi za elimu nyingi tanzania zina watu wanaoitwa Maprof na Ma Doctors lakini sio kama Udokta wa JK, Hawa jamaaaa wanaamini ushirikina kupita maelezo, Waulizeni madereva wao. Mtapata story!

Katika wasomi 10 utakaokutana nao 8 wanaamini ushirikina!

So sio Ishu mwakyembe kuzungumzia uchawi au na Nyie mnaomshangaa mwakyembe kuzungumzia uchawi Tayari dawa ya kupumbaza imeshawaingia??

Think Twice ni Mtu mzima sana DK, Ameona mengi!
 
Kwa mlolongo huu hakuna La kubeza hata moja,NI MUNGU TU MWEZA YOTE ATATENDA!
 
If this is a true story then it is now obvious: It is ISLAM vs CHRISTIANITY. Ni dhahiri sasa UDINI hatimaye umeingia rasmi Tanzania. Tumekwisha! CCM na makuwadi wake wameuza nchi rasmi. Haiwezekani walengwa wote wa kuuwawa ni wa dini fulani tu na watuhumiwa ni watu wa mipango yote ni watu wa karibu na chama tawala.

Acha ku exagerate issues wewe kama ni Uislam vs ukristo je huyo Fred Lowasa aliyetajwa ni mwisilamu? Acheni kupofushwa na siasa za kuchumia tumbo na kutumia cover ya udini wakati wenye dini zao hawana hata habari maskini...poleni mwe nikisema ujinga ni garama mwingine ataropoka nimetukana......Come'on we can do better than this
 
Hii yote ni kwa sababu ya urais 2015, wala sio kwa sababu ya ukristo na uislamu. El ana utaka urais na RA ni mshirika wake mkubwa, pia ninawasikia wanaccm wengi wanawataja taja Bernard Membe na Prof. Mark Mwandosya kwamba watakuwepo kwenye kinyanganyiro cha urais 2015, as well as Dr. Silaa anaonekana atakuwa kizingiti uchaguzi 2015. Dr. Mwakyembe na Uncle 6 wanajua siri ya Richmond inayowahusu RA na EL nao watakuwa kizingiti wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia ccm. Hao wengine kama Anna Kilango ni kelele tu kuhusu ufisadi ndio maana wameweka kwenye list ya kutolewa roho.
 
Hivi kama hiyo story ni kweli sasa wahusika wanaogopa nini? Kwani polisi inaweza linda evil spirit? I cant read you! Yaani watu wenyewe ni wakristo then eti ushirikina ndo unaodaiwa utawadhuru na kichekesho zaidi eti wanaomba ulinzi wa polisi...something is wrong somewhere! Hivi basi hata kama hatuna imani na Mungu basi shule zitusaidie jamani.....Its now becoming too much for people of this country na imani za kusadikika za stone age; mbona tuko kwenye era ya maendeleo ya juu sana ya dot.com au ndo wenzetu wamesha ipita hiyo stage na kufikia spirituality level?

Felister there are some dots you fail to connect....Hawa jamaa walikwenda kwa mganga ili kuzindikwa, wakiamini kwamba watafanikiwa kutekeleza mpango wao pasipo kukamatwa. Just like the way robbers do.....Gazeti limeandika kwamba mganga aliwaeleza kuwa ili dawa ifanye kazi wanapaswa kutokutumia silaha. Tafsiri yake ni kwamba, Yaani wawanyonge ama wawazibe pumzi au watumie njia yoyote ila kuwaua lkn waasitumie silaha, na hiyo dawa inaelezwa kwenye mwwanahalisi kuwa inanguvu kiasi kwamba itawwapumbaza wanyongwaji (kina mwakyembe ) kama ambavyo mbwa hupumbaa amwonapo chatu
 
Mwakyembe wewe mwenywe ni mchawi pia, umetaka kuua wangapi , kuhofia ubunge utaukosa?

Mh, Umejuaje mwana JF, Coz nijuavo mimi unaeza kujua mtu ni mchawi , kwa matendo yake, Kumuona kwa nguvu zilizo sawa na uchawi au kuwa mchawi kama sio Mganga wa kienyeji.

Then tupe ushahidi wa dk kuua kwa ajili ya UBUNGE.
Dah!:A S 13:
 
Back
Top Bottom