KIWAVI
JF-Expert Member
- Jan 12, 2010
- 1,817
- 699
hawezi kuzusha kiasi kile na wewe...Tumejenga taifa la watu wazushi. Daktari wa PhD anazusha. Alizusha mambo mengi akiwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge na uzushi wake unatugharimu hadi leo. Akatuaminisha kwamba Richmond na Dowans ni moja na kwamba zote zina mikono ya RA na EL. leo hii haya yote yamethibitika kuwa ni uongo na anafanya hivi ili kujiepusha na kitanzi cha uzushi wake.
Ni bahati tu kwamba watanzania ni wavivu wa kukumbuka, tumeshasahau na bado tunamuona Mwakyembe shujaa. Mtu huyo huyo kwa sababu ya uzushi wake huo aliposikia Tanesco wanataka kuinunua mitambo ya Dowans akafanya press conference na kuliambia taifa ni bora nchi iwe gizani kuliko kuinunua mitambo hiyo, sasa hivi tuko gizani na kazi iliyofanywa na kamati yake imeligharimu taifa karibu shilingi bilioni 100, mitambo ipo haiwashwi kisa ni uchochezi dhidi ya nishati ya umeme uliojengwa na mwakyembe na wahuni wenzake.
Mzushi huyu akaja tena na uongo mwingine alipopata ajali ambayo hakuna shaka ilitokana na uzembe wa dereva wake, akadai kulikuwa na lori lililokuwa likitaka kuwagonga na dereva wake alipokwepa ndipo gari likaacha njia na yeye akapata ajali. Uchunguzi wa polisi ulipofanyika ikabainika kwamba wakati ajali ikitokea alikuwa amelala na wala hakuliona lori alilokuwa akilisema...hakika huyu ana PhD ya uzushi.
Sasa kazusha jipya eti anataka kuuawa na akaandika barua kutoa ushahidi wa kutunga wa kuunga unga mambo na kuwataja watu na namba za magari mengi akijifanya ana mtandao unaompa taarifa za kila kinachotokea. Ana bahati tu kwamba tuna jeshi la polisi la wasanii ambalo linashindwa kumbana atoe ushahidi wa kina wa maelezo yake ambayo hakuna shaka yatathibitisha kuwa ni ya uzushi.
Anafanya hivi lili EL na RA waonekane ni wauaji...ajenda yake ile ile ya kuwazushia na kuwachafua wengine kwa malengo machafu ambayo ufadhili wake unatambulika kuwa ni wa wahuni wachache walio ndani ya idara moja nyeti. Ni aibu kuwa na naibu waziri tena mwenye PhD wa kiwango duni kama Mwakyembe.
Uzushi wake umelifanya taifa kupiga maktaimu na kujadili hoja moja kwa miaka minne sasa, uzushi wake umeliingiza taifa gizani na sasa anatengeneza uzushi mwingine unaoweza kuligharimu jeshi la polisi, idara ya usalama wa taifa, serikali, chama chake na watanzania kwa ujumla. Mwakyembe ni mtu hatari, ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Huyu mtu ana pepo baya, anapaswa kuangaliwa na kuchungwa sana