Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhosni, Mar 8, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anawatuhumu jeshi la polisi, usalama wa taifa, na waganga wa kienyeji

  Source: Gazeti la Mtanzania katika Mapitio ya magazeti Magic FM (Huwa sinunui magazeti ya RA)

   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  muhosini,

  Mlikuwa mnaongea naye baa fulani au?
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Kwakisa gani??mpaka auwawe??
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tafuta mtanzania la rostam
   
 5. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyo jamaa wameanza kumtafuta muda mrefu sn. Sasa km waziri anahofu ya kuuwawa na usalama wa taifa na polisi sisi raia itakuwaje? Na anayewapa order polisi na usalama wa taifa kumuuwa waziri ni nani huyo? Huo kweli usalama wa taifa upo kweli kwa maslahi ya taifa au maslahi ya JK,EL na RA?
   
 6. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  thread yako imekaaje?!naona kama maelezo hayajatosheleza mkuu
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,231
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  hii story ya Dr. Mwakiembe kutishiwa kuuliwa, niliwahi kuisikia, tena from the horses mouth!.
  Kwa jinsi nilivyomsikia, comon sense haini convince kuwa kitisho hicho ni cha kweli.
  Kwa maoni yangu, tangu ile ajali ya Mwakiembe ambaye aliihesabu kuwa ni assasination plot, kwangu binafsi, it was just natural accident!.
  Kuna confession ya would be 'sniper' ambaye ameconfess mwenyewe kwa Mwakiembe, kwa ahadi ya protection aganst prosecution ambayo ni Dr. Mwenyewe amemuahidi na kumprotect. Huyo jamaa akakubali kuconfess kila kitu on camera na DVD ikatengenezwa na kusambazwa ikiwepo kwa IGP na TISS and noth was done aganst the claimed perpetrators, ndipo Mwakiembe ana cry faul, hii nayo kwa maoni yangu binafsi, nayo ni 'sensenation' tuu za Dr.

  Angalizo: Japo hiyo story ya Mtanzania sijaisoma, kwa vile Mtanzania linamilikiwa na RA, ambaye ndiye mshirika mkubwa wa EL, na ni Mwakiembe ndiye alimpopoa EL toka kwenye ule ufalme wake, hii inaweza kuwa ni moja ya machanisim za Mtanzania kumchafua Mwakiembe ili naye aanguke!.

  Thanks to JK, ile tabia yake ya kiburi, jeuri, dharau na kutosikia la mtu, it works very positively in such scenario, hivyo no matter what, Sitta na Dr. Mwakiembe watadumu kwenye serikali ya JK. Sio kwa sababu anawapenda sana, no!, they are too risky to be left loose!.
   
 8. n

  niweze JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wengi tunajua Mwakyembe na wote Wapenda nchi yao ndani ya ccm wanaandamwa kuuliwa siku nyingi. Kinachoendelea ndani ya ccm ni ujasusi miaka mingi sasa. Leo hii tukiangalia sababu na kisa cha ccm kukaa serikali kwa kuwaburuza Watanzania tunaona madhambi tele.

  Haiwezekani chama kama ccm hakina wanaopenda nchi yao na kusema ukweli. Historia siasa duniani inatunyesha wazi kwamba chama chochote chenye madhambi na kutumia madaraka kuwanyanyasa Wananchi wake siku zote wapo watakao jitokeza kutetea Taifa lao. Ndani ya ccm mimi naamini wapo waliotaka kuwaondoa watu kama Mwinyi, Mkapa, Lowasa, Kikwete, Rostam na mafisadi wengine ila wanalindwa na walinzi wabaya na wauwaji. Haiwezekani chama kama hiki kutokuwa na wapinzani ndani ya chama. Isingefikia hatua kama hii kama ccm wenyewe wangetaka kuilinda nchi badala ya majina mabaya na wabinafsi ndani ya chama chao. Kwanini hakuna ccm asiye simama against Dowans au Richmond ilipoingia? Kwanini ccm wasimame against EPA ilipoingia? Kwanini ccm hawakupinga uongozi mbaya wa Kikwete? Tangu lini wao hawana macho wala akili kutetea Taifa? Maybe there is something psychological mandate we as Tanzanians we don't know abaout ccm.

  Mfano wa Waheshimiwa Mwakyembe na Sitta ni mkubwa kwa Taifa letu. Tunachotakiwa mchango wao tuulinde kwa kila hali na mali hata tukiweza kujitolea kuwapa ulinzi wa kimaisha yetu. Kweli mimi nimefikia hatua na kuchoka kupoteza viongozi wanaofanya kazi kwa ajili ya kulinda maslahi yangu na maslahi ya generation ya vijana na Watanzania kwa ujumla. Lazima to step up na kuwalinda viongozi kama hawa. Inawezekana wengine watasema mchango wao ni mdogo sana kwa Taifa bali mimi binafsi nakataa haya kwani wamefanya walicho weza. Nani mwingine tuseme kachangia kwa namna hii kitaifa?

  Tunapo kuwa tayari kupinga sifa mbaya za Kikwete tuwe tayari kuwalinda Mwakyembe na Sitta na vijana wengine popote walipo mikoani, serikalini, jeshi la ulinzi na polisi kwani wanatusaidia kutupa inside information na kulinda raslimali za Taifa letu. Hili ni Taifa letu sote na tulilinde kwa damu na uhai.

  tunapo pata viongozi mashujaa popote tuwalinde, tuwatuze na kuwapa moyo ili waendelee kusimama imara kuongoza na kusimama imara kufanya kazi
   
 9. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Source: Gazeti la Mtanzania katika Mapitio ya magazeti Magic FM (Huwa sinunui magazeti ya RA)
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,575
  Likes Received: 4,690
  Trophy Points: 280
  Kama ni Mtanzania haina hadhi ya kujadiliwa humu, hilo siyo gazeti bali toilet paper. TO HELL WITH ROSTAM AZIZ
   
 11. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  Afadhali umemleta, maana alianza kusahaulika. Amekuwa kimya sana huyu daktari kumbe kuna masaibu yanamwandama.
   
 12. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama ni kweli basi ni hatari sana kwa raia wa kawaida
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hata kichaa akiongea kitu sensitive, kuna kila sababu ya kuchukua caution...
  Wakuu, tusipuuze, ati kwa vile ni gazeti la Mtanzania limeandika,... hell no!
  Masuala yanayohusu Usalama wa binadamu na majaliwa yake ni sensitive kila mara...japokuwa sielewi kwanini source iwe ni Mtanzania pekee!
  Nashindwa kuelewa kauli hizo alizitolea wapi kiasi Mtanzania wakaidaka peke yao hilo, nadhani ndiyo pia source ya wengi kuneglect habari hii..
  Tulidharau gazeti la Mtanzania, lakini habari kama hii tuiweke kwenye Notebook kwa matumizi ya baadaye!...bila jazba.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,565
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  For what?
   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwenye huo mpango wapo watu wa sita(6)ambao wanatakiwa kuuwawa,na kundi al shabaab ndio walio kodiwa kufanya unyama huo,kutokana na maelezo ya kwenye mtanzania wanasema kuwa watu hao sita(6)ndio kikwazo cha uislam.
  1.Dr.mwakyembe
  2.Dr.slaa
  3.Anne kilango malecela
  4.Regnald Mengi
  5.Pr.mwandosya
  6.Bernad Membe
   
 16. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  PJ

  Mtanzania wame pre empty hii story kwa sababu ni tuhuma ambazo ziko mikononi mwa polisi. Lengo ni kuzifanya ziwe mchuzi mwepesi baada ya kuona kuwa wamestukiwa.
   
 17. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Kama kawaida yako unaropoka tu halafu utakuja kufikiria baadaye. Kweli kwa akili yako unadhani gazeti la mtanzania lipoteze muda wake tena kuweka front page hii story (peke yake) kama hamuna kitu. Mwakyembe amewaandikia police, mtanzania wameamua kuiwahi kwenye gazeti.

  Ngoja niwabandikie hapa hiyo story kama ilivyo kwenye gazeti la leo mjionee wenyewe
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  let JK be the first one to b assassinated...!!!lol
   
 19. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asema wamekodi Al Shabaab kummaliza
  *Ahusisha mganga wa kienyeji, Sheikh maarufu
  *Amwandikia IGP Mwema barua kurasa saba
  *Wasomi, wanasiasa wamshangaa, wambeza

  Na Waandishi Wetu
  [​IMG]JESHI la Polisi limejipanga kumhoji Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya ameibua tuhuma nzito dhidi ya Polisi, Usalama wa Taifa, wanasiasa, wafanyabiashara na waganga wa kinyeji, akidai kwamba wamepanga kumuua.
  Katika orodha hiyo, pia amewahusisha watu kadhaa anaodai kuwa ni Wasomali kutoka katika kundi la Al Shabaab.
  Kuhojiwa kwa mwanasiasa huyo kunatokana na taarifa yake ya maandishi aliyoipeleka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, Februari 9, mwaka huu.
  Mwanasiasa huyo ameeleza mlolongo mrefu wa kishirikina ambao anadai kwamba umefanywa ili "kuwapumbaza Watanzania wote" baada ya yeye kuuawa ili wasiwe na akili ya kuhoji mauaji hayo.
  Uchunguzi wa MTANZANIA umebaini kuwa Februari 8, mwaka huu, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi walimtaka aweke madai yake kwenye maandishi.
  Siku moja baadaye, Dk. Mwakyembe aliwasilisha taarifa yake ya maandishi. MTANZANIA imefanikiwa kuipata taarifa hiyo kutoka kwa baadhi ya wasaidizi wake wizarani ambako iliandaliwa. Ina nembo ya Serikali na anuani ya Wizara ya Ujenzi. Baadhi ya watu wanaotajwa kwenye taarifa hiyo tumehifadhi majina yao kwa sababu za kitaalum kwa kuwa bado MTANZANIA inaendelea kuwasiliana nao ili kupata ukweli.
  Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, "Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.
  Maelezo ya Barua ya Mwakiembe
  "Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.
  "Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha "abiria" hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.
  "Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a "Master", Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.
  "Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda "kulogwa" safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.
  Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia
  "Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.
  "Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga' Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni' hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa'. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
  "Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.
  "Kufuatana na ‘mganga' Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza "waliohukumiwa kifo" (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).
  "Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu' hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).
  Aelezea ushiriki wa Al Shabaab
  "Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).
  Aelezea
  "Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati' wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.
  "Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. "Utabiri" huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.
  "Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu' yamefanywa:
  "(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa "maandalizi" hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
  "(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).
  "Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a "Master" na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.
  "Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.
  "Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:
  "Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.
  "Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).
  "Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH."
  Dk. Mwakyembe anaongeza, "Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.
  "Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.
  "Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.
  "Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi' niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji."
  Maoni ya wanasiasa na wasomi
  Baadhi ya wasomi na wanasiasa mbalimbali waliohojiwa na MTANZANIA wameshangazwa na taarifa hii ya Dk. Mwakyembe, hasa kwa msomi kama yeye kuamini masuala ya uchawi.
  "Ninachoweza kumshauri kaka yangu (Mwakyembe) ni kuchapa kazi zake alizopewa za ubunge na uwaziri, akiingiza masuala ya kuamini ushirikina atakuwa anapoteza sifa yake ya usomi," alisema mmoja wa wahadhiri.
  Dk. Mwakyembe anatambulika katika Jeshi la Polisi kama mmoja wa viongozi wanaotoa maelezo yenye utata kuhusu usalama wao.
  Ameibua suala hili huku kukiwa bado na kumbukumbu za yeye kupata ajali mkoani Iringa na kudai kwamba lori lililohusika lilikuwa limepangwa kumtoa uhai.
  Hata hivyo, Polisi walifanya uchunguzi na kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni uzembe na mwendo kasi wa dereva wa Dk. Mwakyembe.
   
 20. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,964
  Trophy Points: 280
  likitumika kama toilet haliwezi kuumiza? (utani) .kuhusu mwakyembe mimi simuungi mkono achague moja kuwa moto au baridi pia kama kweli ni mpigania haki kwanini aongope kwani kina dr silaa sio watu yeye achague kama anaogopa kufa amwombe radhi rostam.
   
Loading...