Dowans: Another Richmond in making?

LAITI ZITTO ANGEUJUA UZITO

Wahenga walinena nasi tukatega sikio
Hoja walitoa waasisi tena nzito nzito
Ziumiazo ndizo nyasi wapiganapo tembo
Laiti Zitto angemdisi Idrisa wa Tanesko

Laiti Zitto angemdisi Idrisa wa Tanesko
Mbunge Kijana angehisi Dowani imedisko
Wala singedadisi uazizi wake mitambo
Angechukua bisi bisi aifungue wozo

Angechukua bisi bisi aifungue wozo
Kwa yake kasi angeunyofoa huo utumbo
Wanainchi ndio sisi tungelimuunga mkono
Laiti Zitto Mfanisi angejua tu wazito

Laiti Zitto Mfanisi angejua tu wazito
Asingelikuwa mwepesi wa kulitoa tamko
Sasa lafanya aonwe muasi wa wazalendo
Uwi mwokoeni na majasusi kijana Zitto
 

ZeMa,

msimamo upi tena.....mbona alishatoa msimamo wake hapa hapa JF
 

Good Observation....KUDOS TechMaro
 
Mwanakijiji, kwenye hili swala la Dowans, mkuu una spin spin tu.

Mwanzoni ulisema tumwachie huru Gire nunue mitambo, na kwamba Rostam ameshatushinda and what not.

soma nilichoandika.

Baadae ukamtetea Zitto, japo ukasema hukubaliani na mahitimisho yake.

Ulipoulizwa mahitimisho yako wewe ni yapi ukasema tukasome Cheche.

Kwenye Cheche kuna mahitimisho ya Jessica Fundi na Fred Katunzi.

Ukisoma Cheche utaona tunatumia "Tu" na si "Ni". na hivyo ni mahitimisho yetu.

Sasa basi, kwa sababu kwenye hili swala wewe kama Mwanakijiji unaogopa kuchukua msimamo mimi nadhani sio busara kujadili kitu na ghosti Jessica na ghosti Fredi!

well.. how do we discuss something with the "ghosti kuhani"?
 

And this has not been said but only by you!! amazing!

Kuhusu 2Pac's "me against the world" mentality, well, inawezekana ndio predicament ninayoi face all the time jamvini, our lifestyles be close captioned, against all odds we carry on. Hata hivyo, I ain't mad at cha!


you ain't no 2pac not even in a long shot!
 
Kuhusu 2Pac's "me against the world" mentality, well, inawezekana ndio predicament ninayoi face all the time jamvini, our lifestyles be close captioned, against all odds we carry on. Hata hivyo, I ain't mad at cha!

you ain't no 2pac not even in a long shot!

Oouuch! Oh my!

Here is the real 2pac....

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=VCEmTaWSPTk[/ame]
 

Kweli Mwosha huoshwa
Sasa hapa zittto kaamuwa kuvuta chake nini maana hagombei ubunge tena? Kweli inamaana Zito anapoengelea utawala wa sheria huwa anamaanisha nini.?
Mwenye njaa mpe mkate akishiba hapo ndipo utatambuwa tabia yake halisi
 
you ain't no 2pac not even in a long shot!

Ha haa aaaaaaaaaaaa

Sawa ewe Shabban Robert. Isipokuwa tu, maudhui ya fasihi zako huwa ni yale yale, kutaka kula sambusa za binadamu!

Anyhow, usiseme kwamba mahitimisho ya kwenye Cheche kuhusu msimamo wako kwenye Dowans ni yenu na wewe ukiwemo wakati mle kuna makala ya Jessica Fundi na nyingine ya Fred Katunzi. Sasa kwa nini usiseme wewe ndio Jessica au Katunzi?

Japo karibia wote hapa tu maghosti ni afadhali unapojadiliana na ghosti mwenzio unajua kuna ghosti Mwanakijiji anajadili na ghosti Jasusi, au ghosti Ogah anapelekana na ghosti Uwiano Maalum etc. etc., au ki-ghosti Kelly kina flirt flirt na li-ghosti Balantanda kesho kutwa anam feel ghosti Kibunango etc, etc, siku inaenda, bili zinalipiwa, lakini sio ghosti Kuhani anajadiliana na ghosti ambalo halijulikani kama ni ghosti Mwanakijiji au ni ghosti Jessica Fundi au ni ghosti Fred Katunzi, what the heck! Yani tayari kuna li ghosti Mwanakijiji halafu still linajificha nyumba ya ghosti Jessica!

Umesema unasapoti hoja za Zitto lakini sio mahitimisho yake. Wewe mahitimisho yako kama Mwanakijiji ni nini?
 
Nyie watu acheni ujinga! Wapinzani Tanzania wanakuaga na vi-populist rhetoric, atawakiskia kitu kinamadhara kama public opinion iko for it, nawao ndani.. In this case Zitto anaweza kweli akawa anania nzuri lakini si ajabu kapewa ka motivation.... Nyie wote humu njaa tupu, ukiambiwa 500million or 1billion kijana mdogo unaanza kuona its not so bad after all. Technically speaking its not a good idea for the Govt to purchase used equipment from a tainted company. Rostam angeweza vizuri tuu kufanya hii dili na akawanunua mawaziri wote na JK ndani vile vile its worth a lot. Huyo Zitto ndio kawa Yesu au nani mpaka asinunuliwe. He says he doesnt have a price, but that is a lie, everything and everyone has a price, and if a politician says they dont have a price... mmh THat is BS, Nyerere mwenyewe alikuwa na price (it may not always be monetary) but in this case itakuwa hela tuu. Watu wazima mnakuja humu JF talking this and that, peweni 1million dollars basi alafu tuone kama hamja mtetea Rostam. Let us critisize because we are not in a position to influence the deal.

Lakini slowly but surely public opinion inaanza kuwa na 'kaji effect' Tanzania and that is a good thing. JF, duin its part ...lol
 
Sikilizeni hiyo PodOmatic Player kwenye post #14 mwasikilize Mhe. Zitto na Mhe. Mwakyembe ndio mtaelewa, yaani Mhe. Zitto kachemka kwa kweli.
 
Last edited:

Mbona katika kukiuka taratibu mmeshikila tu suala la mitambo ya Dowans? Vipi mazungumzo yanayoendelea na IPTL na Artimus? Vipi ununuzi wa ndege za ATC? Vipi ununuzi wa Panton la Ferry? Haya mambo yalivyofanyika hiyo sheria ya manunuzi ilikuwa bado au vipi?

Hebu tusahau kama fedha hizo zinaingia mfukoni mwa Rostam na tuelekeze akili zetu kwenye mambo yafuatyo:-

1. Mgao utafanya viwanda vipunguze uzalishaji na hivyo kuikosesha serikali mapato.
2. Wafanyakazi wa viwandani watapunguzwa kazi kutokana na kupungua kwa uzalishaji. Hivi ni familia ngapi zitaathirika?
3. Viwanda vitaendeshwa kwa hasara kwa matumizi duni ya rasilimali zake.
4. Kuathirika kwa sekta zingine kama kilimo, utalii etc. kutasababisha kushuka kwa uchumi kwa ujumla.

Hivi haya yote hamyaoni jamani. Mmeshikilia tu eti afadhali nchi iingie gizani kuliko kununua mitambo ya Dowans. Are we really thinking staright au tumeingiwa na kawazimu fulani?
 
mkuu umesikia mahojiano waliofanya Zitto na Mwakyembe na ITV? Mwakyembe kasema live msimamo wa Zitto si wa kamati yake.....ni wake binafsi na anamshangaa kama ndio Zitto anaemfahamu.....Zitto hakubisha....

Sasa Mwakyembe ameacha kuwa msemaji wa kamati yake ya Madini na Nishati na karukia kuwa msemaji wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya umma. Unaona sasa tatizo la ku poke his nose kila mahala? Kama uwaziri umempitia mbali basi asubiri awamu ya tano. Njia anayotumia sasa haimsaidii sana hasa kwa huyu Rais aliyopo madarakani.
 

Kazi ipo!

Mkuu hata hizo IPTL watu wanazipigia kelele lakini ndivyo hivyo Ngoma zimeziba masikio.

Akina mwakyembe wamebainisha kinaganaga ya kwamba ktk sheria ya manunuzi iliyotungwa na Bunge ya 2004 ya kwamba SERIKALI na Idara zake haziruhusiwi na sheria hiyo kununuwa Mitumba bali ni Brand new tu.

Pia kabainisha ktk kifungu cha 72 ya kwamba kama kampuni fulani ilijihusisha kwa kudaganya ama fanya ndivyo sivyo basi haitaruhusiwa kuingia ktk mchakato wowote wa kimkataba ndani ya miaka kumi.

Bila kujali mitambo ni bora ama kutotambuwa jina la kampuni ,mimi nafikiri vifungu hivyo tayari vilikuwa vimewaka dowans inje ya ulingo.

Pili unapoongelea utawala wa sheria mimi nafikiri inapaswa kufuatwa kama ilivyo hadi pale itakapobadilishwa,mfano kama unaona sheria fulani haitendi haki lakini ipo bado ktk katiba basi itaendelea kutumika hivyohivyo vibaya kwa kutotenda haki mpaka pale vyombo husika vitakapoamuwa kuibadili,mimi nafikiri huo ndio utawala wa sheria.

Sasa wewe Mkuu unapokuja na hoja ya ajira unatumia vifungu vipi vya sheria ya kwamba ktk hali fulani ambapo hali fulani inatokea utawala wa sheria unavunjwa
 
Ndio maana kina Mwakyembe bado wanasema hapa sheria isivunjwe. Yaani kwa nini leo sheria ivunjwe ili mitambo ya Dowans inunuliwe? Kwa sababu hiyo sheria ilianzishwa kwa sababu ya kukwepa mambo kama uliyoyasema ya ATCL na Mapantoni. Yaani hiyo sheria ilifanywa ili kukwepa hayo mambo. Kuhusu kama hizo ndege na Pantoni zilinunuliwa wakati sheria haijapita sijui, lakini ndio maana sasa hivi inabidi Dowans ipigwe chini na Mitambo mipyaa yenye Warranty inunuliwe Period.
 
Ninyi subirini tu mgao ndio mtaona raha ya huu upuuzi wenu mnao usimamia kwa nguvu zenu zote.. Tena si mbali Aug/Sept 09.
 
Hapa chini :


Na hapa chini tena umemsapoti Zitto ukasema mahitimisho yake ndio hukubaliani nayo:

Hapa naomba nimtetea Zitto kidogo japo sikubaliani naye kwenye mahitimisho yake.

Sasa na wewe nijibu basi: Mahitimisho yako wewe ni yapi hayo? Kwa nini unaogopa kuyasema? Zitto kaona hakuna ubaya mashine za Dowans zikinunuliwa. Wewe mwanakijiji, sio Fred Katunzi wala Jessica Fundi, wewe Mwanakijiji mahitimisho yako ni nini?

Manake umeuambia umma wa Watanzania, kama Zitto alivyoshabikia, kwamba tununue mashine. Halafu hapo hapo unasema hukubaliani na mahitimisho yake. Wewe mahitimisho yako ni yepi hayo?
 
Kuhani,
Nimekusoma mkuu, heshima mbele ila nataka kuelewa zaiudi ujumbe wako ni upi hasa maanake naona hapa umekaa kutoa makosa au mapendekezo ya waandishi wakati hoja ni hiyo mitambo ya Dowans..
Nini wewe hitimisho lako.. na kwa nini umefikia hitimisho hilo maanake tusizunguke sana kutafutana fulani kavaa nguo gani kuhukumu jinsia ya mtu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…