Shedafa
JF-Expert Member
- May 21, 2008
- 802
- 175
Ndugu Tk maoni ya kamati ya Bunge kuhusu kutonunua mitambo chakavu ya Dowans yalitoka mwezi wa Pili mwaka jana, hivyo serikali ilikuwa na kipindi cha kutosha kuhamishia nguvu zake za kutaka kununua generators upande mwingine. Cha kushangaza hadi leo mwezi wa Tatu mwaka mwingine wako na Dowans na vitisho vya nchi kuwa giza.
1. Nakubaliana na mawazo ya kuwajibisha watu kwa kuwa suala la upungufu wa umeme lilmeonekana muda mrefu, hata hatua zilizokuwa zikichukuliwa zilikuwa za dharula ili kutupeleka kwenye hatua za kudumu. Cha kushangaza za kudumu hatuzioni?
2. Wawajibishe kwa sababu wanatumia nafasi walizonavyo kuilazimisha nchi kukiuka utaratibu iliyojiwekea, ili tu wafanikishe malengo yao. Walitakiwa kuwa na lingo term plan, na baada ya kutekeleza short term plan, sasa tungeanza kuona long term plan yao ikianza kufanya kazi. Maana wote tunafahamu kuwa umeme hautoshi, na ilionekana miaka mitatu iliyopita.