Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Ninyi subirini tu mgao ndio mtaona raha ya huu upuuzi wenu mnao usimamia kwa nguvu zenu zote.. Tena si mbali Aug/Sept 09.


Miezi 6 inatosha kabisa kutengeneza turbine ya hata 200MW hivyo bado wanamuda mzuri tu wa kuweza kununua mpya wa 100MW kwa $30-40million.
 
Na Saed Kubenea
Mwanahalisi~Maslahi ta Taifa Mbele

KELELE za sasa ndani ya serikali kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans ni jitihada zinazolenga "kukidhi maslahi binafsi," MwanaHALISI limegundua.

Vyanzo mbalimbali jijini Dar es Salaam na mikoani vimeonyesha kuwa hakuna tatizo la umeme hivi sasa nchini; wala hakuna upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme.

Uchunguzi wa gazeti hili sasa unathibitisha kuwa madai ya serikali, kwamba nchi karibu itaingia gizani kutokana na ukosefu wa umeme, hayana msingi wowote.

Kwa wiki nzima sasa serikali, ikishirikiana na Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO) wamekuwa wakitoa tahadhari kuwa iwapo mitambo ya umeme ya kampuni ya Dowans haitanunuliwa mara moja, taifa litaingia gizani wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema serikali ina nia ya kununua mitambo ya Dowans ili kukabiliana na tishio la uhaba mkubwa wa umeme kutokana na mabwawa kukauka.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid amesema kwamba mahitaji ya umeme yameongezeka nchini na kwamba kinachohitajika ni serikali kununua mitambo yote ya Dowans pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye gridi ya taifa.

Hata hivyo, taarifa ndani ya TANESCO zinasema vyanzo muhimu vya nishati hiyo, ambavyo ni mabwawa ya maji, bado viko imara na maji yako kwenye viwango thabiti vya kuzalisha umeme.

Kwa mfano, hadi juzi Jumatatu, bwawa la Mtera mkoani Dodoma lilikuwa na maji ya kutosha ya kuzalishia umeme.

Kima cha juu cha ujazo katika bwawa la Mtera ni mita 698.50 na kina cha chini kwa ajili ya uzalishaji umeme ni mita 690.00. Lakini hivi sasa Mtera ina ujazo wa mita 695.91.

Hii ina maana kwamba kile kinachoitwa, "tishio la mabwawa kukauka," hakipo katika bwawa hilo. Kinachoonekana kuwa upungufu, wataalam wamesema, hakiwezi kuleta athari yoyote kubwa katika miezi ya karibuni.

Hali kama hiyo ipo katika bwawa la Kidatu mkoani Morogoro. Hadi juzi Jumatatu, maji katika bwawa hilo yalikuwa mita 449.37. Kima cha juu cha maji kwa Kidatu ni mita 451.00 huku kima cha chini ni mita 441.00.

"Kwa maana hiyo, mpaka sasa, na kutokana na takwimu hizi, hakuna ushahidi wa mabwawa hayo kukauka au kuwa hatarini kukauka," amefafanua injinia mmoja wa TANESCO makao makuu, Dar es Salaam.


Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa imetangaza kuwa mvua kubwa zimeanza kunyesha katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga.

Wataalamu wa TANESCO wanasema ni mvua hizo ambazo zitajaza mabwawa ya Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Kidatu na Hale kabla ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu.

"Kwa mvua hizi zinazonyesha," kimeeleza chanzo chetu cha habari, "huenda zikalazimu TANESCO kuachia kingo za mabwawa na kuachia maji yatoke ili kuzuia yasibomoke."


Hadi Jumapili iliyopita, Waziri Ngeleja alikuwa ameanza kampeni kubwa akidai kuwa kununua mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans "siyo kufanya ufisadi" bali ni kuweka maslahi ya taifa kwanza.

Katika wimbo huo, Ngeleja aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe ambaye alisema anaweka mbele "maslahi ya taifa."

Lakini ni Ngeleja aliyeliambia bunge, zaidi ya miezi mitatu iliyopita, kuwa serikali haiwezi kununua mitambo hiyo kwa kuwa imetumika na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Ununuzi wa Vifaa na Huduma serikalini ya mwaka 2004.

Katika haraka isiyo ya kawaida, serikali na TANESCO wametupilia mbali ushauri wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge na kudandia Kamati ya Zitto wakidai wanatafuta bunge liwaruhusu kununua mitambo ya Dowans.

Kamati ya Nishati na Madini ilishauri TANESCO kufanya kile ambacho wanaona kimo katika uwezo na uamuzi wao. Dowans ni sehemu ya sakata la Richmond ambalo maazimio ya Bunge juu yake hayajatekelezwa na serikali.

Hata hivyo, bado serikali inakabiliwa na mgogoro wa nani hasa wajadiliane naye katika kununua mitambo ya Dowans iliyoko Ubungo, Dar es Salaam.

MwanaHALISI imebaini kuwa wakati kampuni ya Dowans ilikuwa inaweka mitambo yake na baada ya kuanza uzalishaji, haikuwa na ofisi nchini na wala mmiliki wake halisi alikuwa hajulikani.


Hadi sasa, Bunge ambalo liliunda Kamati Teule kuchunguza mkataba wa kampuni ya Richmond iliyokabidhi shughuli zake kwa Dowans, halifahamu mmiliki wa Dowans.

MwanaHALISI imegundua kuwa kuna kampuni inayoitwa Dowans Holdings SA (DH-SA) iliyosajiliwa nchini Costa Rica, Amerika ya Kusini, tarehe 1 Julai 2005 na kwamba ndiyo yenye uhusiano na Dowans iliyoko Ubungo.

Kampuni ya DH-SA ilianzishwa na mtu mmoja aitwaye Bernal Zamora Alce. Taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo gazeti hili limeona, zinaonyesha Zamora alisajili Dowans na makampuni mengine 99 yanayoishia na herufi "SA," kwa siku moja.

Taarifa zinasema kati ya makampuni hayo 100, Zamora alijitangaza kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika makampuni 52.

Hata hivyo, pamoja na utitili huo wa makampuni, imefahamika kuwa Zamora hana simu ya mkononi, hana sanduku la barua wala hajulikani mtaa anakoishi.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa kimataifa na wanasheria mashuhuri nchini Costa Rica umegundua kwamba kampuni ya Dowans haikuwa na ofisi nchini humo haikuwa na simu wala gari.

Si nchini Costa Rica tu, bali kampuni ya Dowans yenye mitambo Ubungo, kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, haikuwa na namba za simu wala ofisi; wafanyakazi wake walikuwa wanatumia ofisi za kampuni ya Caspian Limited hapa nchini.

Kampuni ya Caspian inamilikiwa na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Ni Rostam aliyethibitishia Bunge kuwa Dowans ilikuwa inatumia anuani zake.

Katika andishi lililotumwa serikalini na Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Costa Rica, kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuhusu Dowans anasema, "Dowans ni kampuni ya mfukoni iliyoanzishwa mahususi kwa ajili ya kufanya kazi maalum."

Katika mazingira haya, Dk. Rashid alipoulizwa TANESCO inajadili na nani kuhusu ununuzi wa mitambo, alijibu haraka kuwa wao hawafanyi majadiliano bali wamepeleka mapendekezo serikalini. Alisema ni serikali yenye jukumu la kununua au kutonunua mitambo hiyo.

Alipoulizwa sasa serikali itajadiliana na nani wakati mmiliki wa Dowans hajajulikana, Dk. Rashid alisema, "Hayo si yangu. Ni mambo ya wanasiasa. Sisi tumetoa ushauri kwa serikali kwamba tunataka mashine za kuzalisha umeme…"

Alipoulizwa kwa nini TANESCO isishauri serikali kutaifisha mitambo ya Dowans, kwa hoja kwamba kampuni hiyo ilitapeli serikali kwa kurithi mkataba wa Richmond kienyeji alisema, "Hilo siwezi kulizungumzia."


Waziri Ngeleja hakupatikana kujibu swali kwa nini TANESCO inataka serikali kufanya mazungumzo na Dowans badala ya kuingia katika mchakato wa zabuni.
 
Kuhani said:
Japo karibia wote hapa tu maghosti ni afadhali unapojadiliana na ghosti mwenzio unajua kuna ghosti Mwanakijiji anajadili na ghosti Jasusi, au ghosti Ogah anapelekana na ghosti Uwiano Maalum etc. etc., au ki-ghosti Kelly kina flirt flirt na li-ghosti Balantanda kesho kutwa anam feel ghosti Kibunango etc, etc, siku inaenda, bili zinalipiwa, lakini sio ghosti Kuhani anajadiliana na ghosti ambalo halijulikani kama ni ghosti Mwanakijiji au ni ghosti Jessica Fundi au ni ghosti Fred Katunzi, what the heck! Yani tayari kuna li ghosti Mwanakijiji halafu still linajificha nyumba ya ghosti Jessica!


And how did i get into ythis argument?oloo and why do you call me kighosti?...first of all i dont flirt with Balantanda or Kibunango or anybody whatsoever than my own cupcake...stop kunipakazia aisee hizi ndizo typical allegation ambazo watu wanatoa bila kuwa na evidence.......i dont mind you to comment anything ila kusema kuwa miye na flirt with boys in here that is no so cool bro....I am A list bro and not C list bila classy.
 
Nafikiri njia nzuri kwa sasa ni kuikabidhi hii tender kwa bunge ili watatua matatizo ya umeme Tanzania. They have talked the talk, may be it is a right time to let them walk the walk. Sisi tunachotaka ni umeme, longo longo zingine hazitusaidii kitu.


..ndio kilichobaki ..maana watu hapa wanaongelea ushabiki ..hii hali ya uchumi ya dunia ukichanganya na umeme wa tia maji tia maji....watu watapoteza kazi..wamesahau mwaka 2006 uzalishaji ulivoshuka na viwanda kupunguza watu..acha polution na kelele za majenereta......

serikali lazima ilaumiwe maana walijuwa hili ...walipewa plan na tanesco tangu 2006...leo wanataka kumlaumu idrissa ....sio fair.maneno mengi tu bila utekelezaji ...
 
And how did i get into ythis argument?oloo and why do you call me kighosti?...first of all i dont flirt with Balantanda or Kibunango or anybody whatsoever than my own cupcake...stop kunipakazia aisee hizi ndizo typical allegation ambazo watu wanatoa bila kuwa na evidence.......i dont mind you to comment anything ila kusema kuwa miye na flirt with boys in here that is no so cool bro....I am A list bro and not C list bila classy.

Cupcake....si unajua alikuwa anataka ku get under my skin but I'll let it slide coz you and I know what's up...hahahahahahaaaa
 
Cupcake....si unajua alikuwa anataka ku get under my skin but I'll let it slide coz you and I know what's up...hahahahahahaaaa

LOL!..Cupcake that is very true na ndiyo maana akazunguka mbuyu kwanza alikjua kuwa lazima utakuwa na patriot then ufungiwe tena...hahahah life is really good!....oh well cupcake lets go out for dinner at twist instead of kupigizana makelele na unkungul people in here....its saturday its chillaxing moment.
 
"Some will take this so seriously but to me its just an enttateinment...don't take everything so serious!.....serious make you grown old mapema kabla ya umri wako...

...Kuna watu wataingia kuanza criticize or well sikulaumu,na kuna wengine wataingia kuanza kutukana oh well God Blless you..."
 
LOL!..Cupcake that is very true na ndiyo maana akazunguka mbuyu kwanza alikjua kuwa lazima utakuwa na patriot then ufungiwe tena...hahahah life is really good!....oh well cupcake lets go out for dinner at twist instead of kupigizana makelele na unkungul people in here....its saturday its chillaxing moment.

Let's go babes...achana na huyo loser.....
 
Posted by Kelly01: "Some will take this so seriously but to me its just an enttateinment...don't take everything so serious!.....serious make you grown old mapema kabla ya umri wako...

...Kuna watu wataingia kuanza criticize or well sikulaumu,na kuna wengine wataingia kuanza kutukana oh well God Blless you..."


hahaha oh i see you do read my post uh!....i thought you are so stuborn and unhappy person ambaye hajui kuenjoy life and limted smile on his face

well that is your joke to call me Ghosti and that i firlit with boys?...ooh well as i say to my previous comment Mr Kuhani god bless you!...that was not funny at all...it was more like.................ooh whatever!
 
Calm your nerves Kelly, I do read your posts. Why shouldn't I. Mpaka wachawi wajue?
 
ha
haha oh i see you do read my post uh!....i thought you are so stuborn and unhappy person ambaye hajui kuenjoy life and limted smile on his face

well that is your joke to call me Ghosti and that i firlit with boys?...ooh well as i say to my previous comment Mr Kuhani god bless you!...that was not funny at all...it was more like.................ooh whatever!

Yeah...he is dumb like a bag rocks to not even realize that not everything is funny. And he knows damn well he mentioned you hoping that I would flip out. He could have mentioned his girlfirend (hahahaa...you know who) but decided to mention you...hhhmmmm...think about it Cupcake....
 
Phillemon Mikael,
serikali lazima ilaumiwe maana walijuwa hili ...walipewa plan na tanesco tangu 2006...leo wanataka kumlaumu idrissa ....sio fair.maneno mengi tu bila utekelezaji ...
Mkuu wangu hapa bado kabisa sintakubaliana na wewe kwa sababu tunazungumzia strategy ya shrot term kutokana na dharura iliyosababisha mitambo hii ya Dowans kuwepo nchini..

Swala la Umeme Tanzania ni sugu, ni donda ndugu lisilopona toka mwalimu alipoondoka, ndonda ambalo kwa wale wanaosifia uongozi wa Mwinyi na Mkapa wapate kufahamu kwamba haya ni matatizo yanayotokana na vyanzo vya umeme..

Kumbuka Kikwete anaingia madarakani mwaka 2006 tayari umeme wa mgao upo katikati, Mkapa kaondoka bila suluhisho, mji mzima ulikuwa unanuka deisel na kelele za generator..biashara kubwa mjini ni generator na mashine za kuvuta maji visimani..I mean, mji mkuu wa Tanzania!..

Hivyo maamuzi yaliyopitiwa 2006 ni pamoja na umeme wa dharura (short term) ambao serikali ya Kikwete ulipitisha na kuwapa Tanesco go ahead..Hili ndilo tatizo linalotuweka hapa haya maswala ya long term tuliyakuta, yapo na yataendelea hadi kesho akija kiongozi mwingine..

Tatizo ni hawa Tanesco kwanza kuingiza mashirika kama Richmond, pili kukubali upokezananji wa Richmond na Dowans wakati mashirika yote haya mawili ni FEKI..

Sasa nachotaka mimi kuelimishwa ni kitu kidogo sana.. Ikiwa hawa tanesco walipopewa mamlaka na fedha za kutuondolea matatizo ya dharura wameshindwa kuchukua hatua bora na zenye kuponya tatizo dogo Ijewe leo mnataka sisi wananchi tuamini kwamba mapendekezo yao leo hii yana nia nzuri kwetu?..

Ebu fikiria walipopewa fedha za kwanza wamezitumia kuwapa tender mashirika manne tofauti wakati iliwezekana kabisa shirika moja lichukue tender yote tena iwe mali ya Tanesco na tukapata umeme wa Uhakika (Watsila)..lakini wapo wakachukua ku lease umeme toka mashirika ambayo hayajawahi kuvua umeme maishani!..Kwa nini waliwapa Richmond shirika feki na baadaye hata kukubali mabadilishano ya Mkataba kati ya Richmond na Dowans ambayo bado pia ni shirika FEKI!..

Leo unataka mimi niamini kwamba mitambo ya Dowans tunaihitaji kiasi hicho wakati kila kitu nyuma yake kilikuwa kubambikwa!..Yes tunahitaji hizo 100MW lakini matatizo ya mwaka 2006 hayakumalizwa na dowans.. kuna mashirika mengine manne ambayo yanatoa 2/3 ya umeme ulioongezwa wakati ule..kwa hiyo msitake kutumia mwaka 2006 kama sababu wakati Dowans hawana uhusiano na mitambo ya Watsila na Aggriko..Shida zetu zipo palepale wawepo dowans ama hawapo na kwa vile sasa hivi hatuna tatizo la mvua hivyo tuna muda kiasi wa kuagizi hiyo mitambo mipya na kuifunga..wananchi wataelewa pindi kinachofanyika hapa ni dhidi ya Mafisadi!

Hayo maswala ya Paris na Dowans tutafikishana mbali kwa sababu ndipo sisi Watanzania tutapata kumfahamu nani mmliki wa shirika hilo...

Paris twende tunataka kujua undani wa shirika hili na nani aliyekubali mabadilishano kati yao na Richmond!..kwanza hawana Ofisi wala Address itakuwa starehe kubwa kusikiliza kesi hiyo!..Yaani duh naisubiri kwa hamu, mimi naomba kazi ya ofisi ya mwanasheria mkuu kuhusiana na hawa jamaa.. Wataniroga sanaaaa!!
 
..ndio kilichobaki ..maana watu hapa wanaongelea ushabiki


Hakuna yeyote anayeongea kwa ushabiki lakini watu hawataki kuona mafisadi walioidanganya serikali na Watanzania kwamba wao ni kampuni toka USA na wana HQ yao Houston, Texas na utaalamu wa hali ya juu katika kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme. Kumbe ni mafisadi tu hata ofisi hawana ni kampuni ya kwenye briefcase. Baada ya kulipwa shilingi bilioni 200 walishindwa kuzalisha hata tone la umeme bahati nzuri mungu akasikia sala zetu na kutuletea mvua za kutosha zilizojaza mabawa yetu na kuweza tena kuzalisha umeme.

Serikali imejiwekea taratibu kwamba manunuzi ya mitambo chakavu hairuhusiwi sasa kwani ghafla taratibu hizi zikiukwe. Kukataa hawa mafisadi wa Dowans wasizawadiwe tena na pia kuhakikisha taratibu za serikali za kununua mitambo zinafuuatwa ni ushabiki kweli huu!?


....hii hali ya uchumi ya dunia ukichanganya na umeme wa tia maji tia maji....watu watapoteza kazi..wamesahau mwaka 2006 uzalishaji ulivoshuka na viwanda kupunguza watu..acha polution na kelele za majenereta.........

Naam watu wanaweza kabisa kupoteza kazi, hili likitokea wa kulaumiwa ni serkali na TANESCO. Kuna miaka mitatu tangu tulipoingia kizani mara ya mwisho mnamo mwaka 2006. Kiongozi wa shirika kubwa na nyeti kama TANESCO anatakiwa akae na wataalamu wake kuangalia mahitaji ya nchi ya umeme kwa kipindi kirefu na kuwa na mikakati ni jinsi gani kampuni yake itakavyoweza kukidhi mahitaji ya nchi ya umeme. Siyo kukurupuka na kuwashinikiza Watanzania kwamba taratibu za manunuzi zipindishwe ili nchi inunue mitambo chakavu ambayo haina warranty, haijulikani ina muda gani tangu ianze kufanya kazi na tena kwa bei mbaya. Huku kukurupuka kwa Idrissa ni ushahidi tosha kwamba ameshindwa kuiongoza TANESCO na anastahili kuondolewa haraka sana.

..serikali lazima ilaumiwe maana walijuwa hili ...walipewa plan na tanesco tangu 2006...leo wanataka kumlaumu idrissa ....sio fair.maneno mengi tu bila utekelezaji ...

Naam serikali inastahili kabisa kulaumiwa. Tumewalipa mapesa mengi sana wale makaburu wa Netgroup ambao walikuwa hawajui lolote kuhusu umeme. Mpaka hii leo pesa walizolipwa ni siri kubwa ambayo inalindwa ili isijulikane na Watanzania. Mapesa waliyolipwa makaburu wale, na yale ya ununuzi wa rada na mashangingi yanayonunuliwa kila baada ya miaka miwili yangetosha kabisa kupunguza matatizo yetu ya umeme angalau kwa miaka 5 au hata 10. The so called "viongozi' wetu wako radhi kuwekeza kwenye mashangingi, vitambulisho, rada n.k. lakini siyo umeme ambayo ni nishati muhimu sana kwa nchi yeyote ile duniani ikiwemo Tanzania. Kamwe serikali haiwezi kuzikwepa lawama hizo.
 
Bubu Ataka Kusema,
Mkuu hizi zabuni za nini ikiwa wenye shida ni sisi.. kwa nini tanesco wasiende shopping wenyewe kununua mitambo wanayoitaka.. why middlemen kwa kila tunachokihitaji wakati njia za kupata mtambo unaotaka zipo..
Toka Rada, ndege ya rais tumeweka middlemen, ndege za ATCL, nasikia hata mabus ya kufufua UDA kila siku kuna mtu wa kati na kadhalika why tusiagize na kununua sisi wenyewe..
Tender hutolewa kwa kazi za contracting sio manunuzi jamani tutajifunza lini sisi wenyewe kuendesha vitu vyetu!..
 
Bob, Bubu, Keil na wengine,

kupiga kelele tumeshapiga vya kutosha sasa, hata Dr Idris amezira kuwa hawatanunua mitambo ya Dowans.......thats how JF works.....sometime people do underestimate the power of JF......this is a warning to them..........DON'T underestimate JF.

mawazo mengi mazuri yameandikwa hapa i.e. TANESCO wafanye nini......wawakilishi wao wapo hapa na ujumbe wameupata.

Binafsi ningewaomba sana TANESCO kushughulikia yafuatayo
1.Wahakikishe miradi yote tuliyonayo ina-function ktk efficiency ya atleast 75%
2.Wautekeleze ule mradi wa bonde la Rufiji

asanteni
 
There is enough water at the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) plant at the strategic Mtera Dam to generate power for many months to come, The Guardian has established. This is contrary to suggestions that the intermittent power cuts which have hit different parts of the country for the last several months were linked to fast-falling water levels at the dam.

Power generation at the two main units of the dam, which lies at the border separating Dodoma and Iringa regions, was in full swing when a reporting crew from this paper made a surprise visit to the area mid-this week.

Tanesco officials and workers at the 100-meter underground Mtera plant said water levels have stood at decent levels for the last two years and talked of stable national grid power supply unless unforeseen circumstances intervene.

The last readings taken on Tuesday showed that the water level had reached 696.07m above sea level, way above the 690m recommended as the level below which power generation is suspended.

Mtera power station acting manager Stephen Mfumbutsa said in an interview that there was gradual but steady increase in the dam`s water level since last month.

``There have been enough rains in and around catchment areas in Mbeya and Singida regions as well as other places that feed Ruaha and Kitego rivers, draining into Mtera Dam. This is good news to us because it means that power generation is assured,`` he noted.

``Water is extremely precious for us. In fact it is much like an oil reserve that no one would like to see depleted,`` he added.

The official, who gave the explanation while running through a diagram with details on the national power grid, said Mtera has two 40-MW generating units and both have been running smoothly throughout for months now.

“Power consumers have nothing to worry about because, as the trend shows, there is currently no possibility of power rationing,” a confident-looking Mfumbutsa stated.

Commenting on the causes for the recent intermittent power fluctuations in some other areas in the country, he said the situation was unfortunate but was not due to problems with their production units.

Elaborating, he said it was likely that one reason was faults originating from the power transmission lines.

Gosbert Matandu, a long-serving Mtera station technician now also serving as assistant to the operations manager at the site, then took the journalists to the dam site for a verification of the day`s water level readings.

Pointing at the yardstick (graduated iron bar), Matandu said once the water level exceeded 698.5m, the maximum level for the dam`s holding capacity, operators would be obliged to open the floodgates to avoid serious consequences.

``This is the level of water for today. The readings are closely monitored day and night to make sure that the amount of water meant to have the runners (two turbines) going was within the recommended level,``he explained.
The aim is to avoid air-sucking in case of low water level which may cause cavitations to the runners, he said.

Meanwhile, Mtera station operations manager Joseph Chomola produced a computer-monitored chat which showed monthly water level readings.
That was in an attempt to ``clear the air`` and assure consumers that power would continue to flow at both Mtera (80MW) and Kidatu station (204MW), both of which receive water from Mtera Dam.

Chomola said daily records showed that there has been a gradual increase in the level of water since the beginning of this month.
``For example, on February 1 it was 696.03 m and the readings on February 10 (the day The Guardian toured the station) was 696.07m. It is our hope that the pleasant situation will continue because the long annual rains are expected to set in shortly,`` he pointed out.

He added: ``Even if the water level were to fall by a whole two centimetres a day, God forbid, it would have taken more that 300 days to reach the minimum level of 690m``.

Plant Operator (Control Room) Alfred Machismo sat at a corner on Mtera station’s lowest floor, surrounded by several direct telephone lines and computer sets “to make sure that any unusual alarm sounded is promptly attended to”.

``As you can see, everything is running at full capacity here. We have deliberately lowered the output to 30MW and 28MW for in line with instructions from the Grid Control Centre in Dar es Salaam, popularly known as SCADA, depending on the load or consumption rate at the specific moment,`` he explained, adding: ``Things are perfect and there is no cause for consumer alarm or panic.``

A beaming Machimo then fixed his eyes on the huge control unit, as live meter readers monitored every section of the production process.

Tanesco said recently that the nation is on the verge of a power crisis and announced an ambitious plan to put up a new 400KV national grid to support its existing dilapidated power supply backbone.

The giant state-run power company blamed frequent blackouts experienced in Dar es Salaam and several other regions recently to an ``overwhelmed`` Tanesco network.

According to Tanesco, the new transition backbone is to be built from Iringa to Shinyanga through Singida Region and is to meet increased countrywide demand for electricity.
The firm`s capacity to generate and supply power has been seriously eroded over the years chiefly by a high rise in demand, sabotage of its infrastructure and transformer oil thefts.

Ensuring quality and reliable supply becomes an increasingly nagging problem as demand continues rising, officials and analysts say.

The existing 220KV and 132KV transmission system suffers from frequent voltage depressions, surges and sometimes total outages, according to Tanesco Managing Director Idris Rashidi.


* SOURCE: GUARDIAN

Am I reading this right ??
 
Zamani nilikuwa nikijiuliza shetani anawezaje kuja na kuishi miongoni mwetu wanadamu bila sisi kujua??
Nizidivyo kuishi nakupata umri nagundua kwamba ni rahisi kuliko nilivyodhani kwa ibilisi kujitoma miongoni mwa bin adamu na kujichnganya kiulaini.
Ni vipi mitambo mikubwa iliyojaa karibu eka 4 pale Ubungo iwekwe katika ardhi ya Tanzania na mtu asiye fahamika?
Ni vipi waziri apite kila kona kutaka kununua mitambo ya umeme kutoka kwa mmiriki asiyefahamika?
Ni Vipi Rostamu Azizi atoe Ofisi yake kumpa mmiliki wa kampuni ya Dowans asiye julikana?
Hivi ni kweli tulidai Uhuru ili kuwa huru? Au tulidai Uhuru kutoka kwa Waingereza ili tuwe koloni la wahuni kadhaa ndani ya nchi?

Ni vema tukae katika Giza kuliko kununua mitambo ya umeme kutoka kampuni yenye utata wa mmiliki na iliyogubikwa na kila aina ya ushetani.

Kwa sababu MH Zitto ni mmoja wa watu wanao tetea Tanesco kununua mitambo hii.

Nakuomba MH Zitto unipe jibu la swali hili.

Nani ni mmliki wa Kampuni ya Dowan.
 
Hivi hawa jamaa wawjibishwe kwa lipi?

1. Wameona kuwa huko mbele kutakuwa na upungufu wa umeme wakapendekeza uzalishwe umeme kwa mitambo iliyopo tayari installed. Kamati ya Bunge ikakataa. Hapa wana kosa gani?
2, Baada ya kukataliwa hapo juu na upungufu ukatokea pakawa na mgao kutoakana na kukataliwa na Kamamti ya Bunge. Hapa wawajibishwe vipi?

Safari hii kukitokea tatizo la umeme, wananchi watalia na Bunge tu wala sio Tanesco au Serikali..
 
Date::3/7/2009
Mkurugenzi wa Tanesco abanwa ajiuzulu kwa kashfa ya Dowans

Na Geofrey Nyang'oro
Mwananchi

SIKU moja baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutangaza kususa ununuzi wa mitambo ya Dowans, wasomi, wanasiasa na wananchi nchini wamezidi kumkaba koo Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Idrisa Rashid ajiuzulu.

Watu hao wanataka, Dk Raishid ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kueleza kuwa kwa vile watu wengi hawataki mshirika lake linunue mitambo ya Dowans basi asilaumiwe kama nchi itakuwa giza.

Sambamba na hali, Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kumwondoa katika wadhifa wake Waziri wa Nishati na Madini, Wiliiam Ngeleja na kuvunja menejimenti nzima ya Tanesco.

Maneno yaliyomweka pabaya Dk Rashid aliyasema juzi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Shirika lake, likisema lisibebeshwe lawama kwa yatakayotokea.

Alisema wananchi wa Tanzania watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, mahospitali hayatoi huduma; viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi.

Uamuzi wake huo umekuja siku mbili baada ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta kueleza kuwa msimamo wa kamati ya Nishati na Madini iliyoshauri mitambo hiyo isinunuliwe ndio msimamo wa chombo hicho cha kutunga sheria na hivyo kumaliza mvutano uliokuwepo kati ya kamati hiyo na ile ya hesabu za mashirika ya umma, inayoongozwa na Zitto Kabwe iliyounga mkono kununuliwa kwa mitambo.

Mtaalamu wa Ugonjwa wa Ukimwi, Dk Fedelis Owenya aliliambia Mwananchi Jumapili jana kwa njia ya simu kuwa kauli ya Dk Rashid inaonyesha jinsi gani kiongozi huyo aliyeteuliwa kumsaidia rais ameshindwa kufanya kazi yake.

Alisema Dk Rashid amekiuka misingi ya kazi yake ambayo ilikuwa ni kuandaa mipango ya muda mufupi na muda mrefu ya upatikanaji wa umeme na kuishauri serikali, badala yake sasa ameamua kushinikiza kununuliwa kwa mitambo hiyo na kutoa vitisho kwa wanachi na rais wake.

Kauli kwamba anawaachia wananchi kuamua wenyewe pindi nchi itakapokuwa kuwa giza ni vitisho vinavyoitaka serikali kuvunja hata sheria ya manunuzi, kitu ambacho kinaonyesha kuwa kuna nguvu nyuma yake.

Alisema hatua aliyoichukua Mkurugenzi huyo inaonyesha kuwa hujuma zinaweza kufanywa ili kukomoa wananchi, hivyo, hatua zaidi zinafaa kuchukuliwa dhidi yake.

"Hii ni nchi ya kidemokrasia,sisi tumemchagua rais na tumempa dhana ya kutuongoza,yeye kwa nafasi yake amewachagua watu watakaomsaidia katika suala zima la utendaji ili nchi iweze kuendelea,Dk Rahidi aliyeteuliwa na rais kushika nafasi hiyo, anawatishia wanchi au anamtishia rais aliyempa nafasi hiyo?alihoji Dk Owenye na kutongeza kuwa watu wa aina hii wanapaswa kushitakiwa.


Owenya aliiasa Serikali kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na sheria ya ununuzi wa umma ili kutunza na kuendeleza heshima na usitawi wa nchi na jamii yake.

Kwa upenda wake, Tundu Lisu ambaye ni mwanasheria licha ya kumtaka Dk Rashid awajibishwe pi alipendekeza uwepo uwajibikaji kisiasa na kuwataka waliomteua wawajibishwe pia.

Hayo aliyezesema juzi alipokuwa akichangia kwenye kipindi cha Kipamajoto kinachorushwa hewani na Kituo cha Television cha ITV.

Alisema kitendo cha kulazimisha ununuzi wa mitambo hiyo wakati akijua kuwa ni mitumba ni kuwatukana watanzania.

Lisu alipinga kuwepo kwa dhararu ndani ya shirika hilo na kueleza kuwa ni uharamia ulipangwa kufanyika ndani ya shirika hilo kwa kuwa wao walijua tangu siku nyingi.

Alisema kimsingi kampuni hiyo inapaswa kufikishwa mahakamani kutokana na mkataba wake kuwa tata anashangaa kuona mpaka sasa suala hilo halijafanyika.

Katika hatua nyingine mwanaharakati, Renatus Mpinga alimtaka rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Mkurugenzi huyo haraka kwa kuwa ameonyesha utovu wa nidhamu mbele ya watanzania.

Alisema kitendo chake cha kulazimisha ununuzi wa mitambo hiyo kinataka kutonyesha kuwa mitambo hiyo ndiyo bora kuliko mengine.

Naye Mtaalamu wa sheria ya Manunuzi ya Umma, Wasonga Benjemani alisema sheria ya manunuzi inaeleza wazi kuwa mzabuni akionyesha dalili za kutumia rushwa katika kupata tenda yake anatakiwa kusimamishwa kushiriki katika kufanya biashara ya serikali kwa muda wa miaka kumi au kufikishwa mahakamani.


Alisema kitendo cha Tanesco kunuia kununua mitambo hiyo iliyozua mashaka hapa nchini ulikuwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria zilizopo.

Naye Joyce Mmasi anaripoti Mbunge wa Vunjo Aloyce Kimaro amesema watu watakao liingiza taifa katika ununuzi wa mitambo ya Dowans washitakiwe na kufungwa jela.

"Ule wakati wa kukosea na kujiuzulu umepitwa na wakati, sasa hivi ni mahakamani kwa wote waovu, wazembe na wanaotumia madaraka yao vibaya, sasa ni kufungwa sio kujiuzulu," alisema.

Alisema serikali iache kutumia baadhi ya wabunge kuhalalisha uzembe. "Tujiulize hivi huku Tanesco kuna nini hadi kutaka kuvunja sheria? Haiwezekani kampuni ambazo zilizoifanya serikali nzima kujiuzulu leo tunaendelea kuzifuata," alisema Kimaro.

Kimaro alisema anashangazwa na kitendo cha mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kusimamia hesabu za mashirika ya umma alivyolikomalia suala hilo.

Naye Burhani Yakub,Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dk Idriss Rashid,amelalamikiwa kwa kauli aliyotoa wakati akijiondoa katika ununuzi wa mitambo ya Dowans Tanzania Limited ya kuwa ikiwa nchi itakuwa giza asilaumiwe.

Wananci waliohojiwa nyakati tofauti jijini hapa jana , wamesema kauli hiyo haikupaswa kutolewa na kiongozi kama yeye kwa kuwa inatoa mwanya kwa watumishi wasiokuwa na uaminifu wa Tanesco kufanya hujuma.

Malalamiko hayo waliyatoa jana kwa nyakati tofauti wakati wakielezea maoni yao juu ya kauli ya Dk Rashidi aliyotoa kwa waandishi wa habari kuelezea kujito kwa Tanesco katika ununuzi wa mitambo ya Dowans.

"Asitufanye wananchi ni wajinga,inakuwaje wang'ang'anie kununua mitambo ya Dowans ilhali wanafahamu kuwa ni mikongwe?halafu anaamua kususa baada ya Kamti ya Bunge ya Nishati na madini kuweka msimamo wake"alisema Khamisi Ali mkazi wa Makorora Jijini Tanga.

Mustafa Shembeyu wa Barabara ya 15 Jijini Tanga,alisema kauli iliyotolewa na Dk Idriss inaonyesha kuwa ameshindwa kuliendesha shirika la Tanesco hivyo anastahili kujuzulu ili kuepusha madhara kama ataendelea kuwepo.

"Ili kuinusuru Tanesco inabidi Dk Idriss ajiuzulu,kwani kwa kauli yake inaonyesha kuwa mwisho wake wa kushauri umefikia kwa Kampuni ya Dowans na kwamba hana njia nyingine ya kuweza kutafuta ufumbuzi wa tatizo la umeme nchini"alisema Sembeyu.

Kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani Wilaya ya Korogwe,Calistus Shekibaha,alisema baada ya kusikia kuwa Rais Jakaya Kikwete amemteua Dk Idriss kushika wadhifa huo alipata wasiwasi kwa kuwa ndiye anayeshutumiwa kuivuruga hata benki ya NBC.

"Kwa wale wenye mazoea ya kusoma magazeti watakumbuka mara baada ya uteuzi wa Idriss nilitoa maoni yangu katika gazeti la Mwananchi na kumwambia Rais atavuna machungu kwa kitendo chake cha kumteua Dk Idriss kuongoza Shirika nyeti kama Tanesco.

Alisema wakati Dk Idriss akiwa NBC watumishi walimlalamikia kuwa alikuwa akiendesha benki hiyo kimabavu na kusababisha mambo mengi kuharibika jambo lililosababisha wamkumbuke Mkurugenzi wao wa zamani Amon Nsekela.


Shekibaha aliipongeza Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli,William Shelukindo kwa msimamo walioonyesha katika kutetea mitambo ya Dowans isinunuliwe.

Aliitaka Serikali kutafuta mbinu za ununuzi wa mitambo mipya ili kumaliza kabisa tatizo lililopo kwani ni jambo la iabu kwa nchi ya Tanzania kuhangaikia umeme wakati ina vyanzo vingi.
 
Back
Top Bottom