Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Mimi siana shaka hata kidogo, Siyo yeye tuliye mzoea wa kushabikia na kukuwadia uozo. Harafu wanasema kirahisi tu si "kila mtu ni FISADI". Kwani Mafisadi wengine tuliwaona wakati wanafanya ufisadi lakini maneno yao yalidhihirisha kwamba kuna kitu.
 
Siku zote mimi hushangazwa sana na upeo wetu sisi wabantu wa kushughulikia matatizo tuliyonayo. Hili suala la tatizo la umeme wala si geni katika masikio ya watanzania. Lipo miaka nenda miaka rudi. Hivi inashindikana kweli kwa watu wenye akili timamu kukaa chini na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu kuliko ilivyo hivi sasa kukurupuka pindi tusikiapo kina cha maji kimeshuka kwenye vyanzo vyetu vya umeme?
Ni very common sense kujua ya kwamba, pindi mvua zisiponyesha kwa muda fulani, na hali ya hewa ya nchi yetu ni ya joto, obviously maji yatapungua, sasa maji yakipungua tufanyeje ili wananchi waweze kupata huduma ya umeme?? Sasa kama ni mitambo itafutwe ambayo itaweza kukabiliana na hali hiyo. Hayo ni maamuzi ya kikao cha siku moja na couple of follow-ups, mchezo umekwisha....lakini sio sisi watanzania....tutalirefusha suala hilo kwenye vikao visivyokwwisha almuradi tu watu wachukue posho zao.
Kuna siku moja niliwahi kuzungumzia suala hili mbele ya raia wa kigeni, waliniuliza swali moja very simple,....kwani nyinyi watanzania hamjui ya kuwa hali yenu ya hewa inasababisha vina vya maji kupungua?? Sasa inakuwaje kila mara suala hili linakuwa ni national crisis, wakati wanaimani sisi watanzania tuna akili timamu za kufikiria?? nikaona kweli kuna watu wachache wameshatu-lable watanzania wote milioni thelathini na kadhaa kuwa ni mambumbumbu...
 
Kinachonifanya nimshuku Zitto ni kubadilika kwa kauli zake: Mara anasema, issue ni kununua mitambo yoyote si lazima Dowans; mara aseme mitambo ya Dowans ni bei poa na mtambo mmoja ni mpya!? Hii ni lugha kikuadi kabisa, ameacha msimamo wake wa kutetea taifa anatetea Dowans. Sitaki awe adui wa watu wanaonuka ufisadi lakini ukaribu wake na wahariri wa Habari Corporation, Ngereja na Masha unatia shaka. Najua kumfahamu na kumshabikia Zitto.

Sijabadilika hata kidogo. Msimamo wa Kamati yangu upo wazi kabisa na kwamba hatulazimisi Dowans. Kwamba nimesema mtambo mmoja ni mpya ndivyo tulivyoambiwa na TANESCO na kuthibitishwa na mtalaamu. Hiyo fact lakini sio kinachoweza kulazimisha kuwa tununue dowans. Sina sababu ya kuisemea dowans. Ninachofaya hapa ni kuweka facts clear.

Sijabadilika na msimamo wangu ni msimamo wa kamati ya Mashirika ya Umma.
 
Hapa naomba nimtetea Zitto kidogo japo sikubaliani naye kwenye mahitimisho yake.

a. Tofauti kati yetu wengi wetu hapa na yeye ni kuwa yeye amepata nafasi ya kusikiliza kwa ukaribu pande zote zinazohusika.

b. Akiwa mjumbe wa Kamati walichukua msimamo anaousimamia. Na anasema msimamo wake ni msimamo wa hiyo kamati.

c. Siwezi kushangaa endapo tukimpa ushawishi wa kiakili na mantiki wenye kuzidi ushawishi uliotolewa na Tanesco na Wizara atachukua msimamo mwingine hasa endapo itaoneshwa kuwa walichoambiwa hakikuwa sahihi.

d. Ametoa changamoto kwa watu wanaosema kuwa ununuzi wa mitambo hii ambayo imetumika ni kinyume cha sheria inakiuka sheria ya PPR kuonesha ni kipengele gani kinakiukwa na hadi hivi sasa hakuna mtu aliyeweza kuonesha kwa hiyo kwenye suala la hoja za kisheria hakunana aliyemuonesha hivyo kwa hiyo hiyo haiwezi kuwa hoja ya kumshawishi.

e. Kwamba kwa vile hachezi ngoma inayochezwa na wengine haina maana kuwa ni lazima awe na yeye fisadi au amenunuliwa. Binafsi naamini kuwa kiongozi mzuri ni yule anayeweza kusimama peke yake dhidi ya wimbi la kufuata mkumbo. Kumbeza na kujaribu kumfanya duni kwa vile kachukua msimamo tofauti na ule unaoonekana wa wengi ni kujifanya duni na kujibeza wenyewe. Kila Mtanzania ana haki ya kuwa na maoni yake kwa kadiri anavyoamini dhamira yake kuwa iko sawa.

f. KUna wale ambao wanaonekana kuumizwa kwa vile Zitto kachukua msimamo tofauti. Hawa wanafikia mahali pa kuhoji uzalendo wake au hata kumshangaa kwanini anaonekana kuwa kinyume na matakwa ya watu. Ndugu zangu, hisia na vionjo vyetu haviwezi kamwe kutuongoza katika fikra huru. Vinatosha kutufanya tushtuke lakini havitoshi kufanye tuvuke tunakokwenda kwani kama leo Zitto kakuumiza basi kesho akifanya kingine ukafurahia unaweza kuanza kushangilia.

Kwa mtindo huo utakuwa unaishi kama unacheza kwenye bembea leo juu kesho chini! Ni lazima tuangalia mambo haya kwa kuvuka vionjo vyetu na hisia zetu na kusimama kwenye mantiki na uwezo wa kuhoji.

f. Wapo wabunge wengi wa JMT ambao hawawezi kuingia hapa na kujadiliana nasi kwa uhuru anaofanya Zitto au Slaa and as a matter of fact ningependa kweli kuona watu kama kina Dr. Idris, Ngeleja, Shelukindo na wengine waje hapa kuzungumza nasi anavyofanya Zitto tuwabane tunavyombana kijana wetu. Nasikitika hata hivyo nafasi hii tuliyonayo ya kuwasiliana na Mbunge tunaichezea kwa sababu tumejificha nyuma ya majina yetu.

Kuna vitu vingine vinasemwa mbele yake vitu ambavyo watu wanaovisema hawawezi kuthubutu kumuambia usoni. Watu hao wanafanya hivyo kwa sababu ya usiri wa kutokujulikana na hivyo wanasema tu alimradi mtu aonekane kasema kitu fulani kikali kwa mbunge Zitto. Katika hili wapo wale ambapo siwezi kushangazwa nao wana makusudio kinyume kabisa na Zitto.

Neno kwa Zitto:
Kwa nafsi yangu mwenyewe na wale ambao wanashukuru mchango wako mkubwa katika mjadala huu usife moyo au kukata tamaa. Ninaheshimu msimamo wako katika hili na kutambua kwa kadiri niwezavyo unaoongozwa na mapenzi kwa nchi yako. Siwezi kamwe kuhoji uzalendo wako au uhuru wako wa kuweza kuchagua pande kwa kadiri unavyoamini uko sahihi. Endeleza mapambano ukitambua kuwa ni katika kutokubaliana ndipo tunapopata sababu zaidi ya kukubaliana.
 
Hivi kweli Mh. Zitto na ujanja wote wa mjini unaweza kusema mtambo mmoja ni mpya na kuna mtaalamu amethibitisha??? Kweli Mh. Zitto umefika huko??

Yaani mitambo iingizwe Tanzania mwaka 2006, ifanye kazi mpaka 2008, halafu Mh. Mbunge anatuambia kuwa katika hiyo mitambo iliyoingizwa toka 2006 na kufanya kazi for over 2 yrs, kuna mtaalamu kamthibitishia na yeye kakubali kuwa ni mipya mwaka 2009!!!
 
Cant find words to thank you.
 
Nisemeje? Ngoja niwe mpole ndugu yangu.

Unakumbuka Richmond walishindwa kuzalisha umeme? Unakumbuka kuwa hata Dowans nao baada ya kurithi mkataba wa Richmond walishindwa kuzalisha umeme?
Mitambo iliyoletwa na Richmond ni mitambo mikuu kuu ambayo ilitumika katika winter olypics kule greece kuzalisha umeme. Hii ina uwezo wa 40MW tu.

Mitambo waliyoleta Dowans mwishoni mwa mwaka 2007 na huo mmoja umetumika kwa masaa 400 na unaweza kutumika kwa miaka 13 ijayo kabla ya kufanyiwa overhaul na kutumika kwa miaka 13 mingine. Ndio taarifa ya mtaalamu inasema. Ndivyo tulivyoelezwa. Kama kuna taarifa nyingine ya mtaalamu inaonesha otherwise, i am open minded and i will compare and form the right opinion.

Vipi hujaona kile kipengele cha sheria nilichoomba uniangalizie katika sheria ya manunuzi? Hapa hatushindani, tunaelimishana. Ndio sababu ya sisi kuanzisha jukwaa hili na kulipa support yote. Umeona kipengele hicho mwenzangu?
 
Sijabadilika na msimamo wangu ni msimamo wa kamati ya Mashirika ya Umma.
===========

Comrade Zitto umebadilika, na kina Lowassa wanaangalia na kucheka kweli kweli. Umetuacha kwenye mataa. Ama kweli, amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Lakini uje wewe si wa kwanza kuasi umma na kuutelekeza. Tumewaona wengi, hata wakati wa Yesu walikuwapo lakini mwisho wao haukuwa mzuri.

Zitto ndugu yangu zinduka, msimamo wako ni tofauti na msimamo wa kamati, na ni tofauti na umma wa watanzania. Ni msimamo wako binafsi, lakini tangu tulipokuchagua ujue ubinafsi wako uliwekewa mipaka. Kwa hiyo usipoteze muda wako kutulisha msimamo wako binafsi ambao kwanza tunajua nao siyo wako ni wa mafisadi wanaogaragara kwa mapigo waliyoyapata.

Mitaani watu wanasema pale CHADEMA ni mtu mmoja tu anayeweza kuaminika mpaka kaburini. Waliobaki mkionyeshwa vyeo au fedha mtaiasi CHADEMA na sasa tunaona wenyewe. Tunaanza kuogopa kuwa mtapewa hela mmdhuru mtu wa watu asiyekubali kuongwa.

Kama hukuongwa Zitto apa kwa jina la Zuberi tuone.
 
Ninaapa.

Msimamo wangu ni msimamo wa kamati na nimeuweka kwenye maandishi. Nipo very clear on this. Lakini pia kama kiongozi nimeshare taarifa nilizonazo na wengine. Kama hupendi kusikia taarifa hizo, hupendi. Lakini nimesema yote kabisa na kurekebisha kulingana na taarifa nilizo nazo. Sina motivation yeyote kutetea kampuni yeyote.

Ningekuwa mla rushwa ningekula rushwa za mashirika ya kamati yangu. Lakini nimekuwa principled na kamwe hunioni kupita pita katika mashirika kama ilivyokuwa kawaida ya wabunge wengi sana. I trust myself.
 
Penye kumi na wawili kuna Yuda Iskariote. Petro aliingia mitini akamwacha Yesu. Dema alimwacha Mtume Paulo. Kambona alimwacha Nyerere, na wengine wengi.
Mtambo huu unavyong'ang'aniwa na hata kuchafua watakatifu wetu, napatwa na mashaka kuwa Mkuu wa Kaya labda ana maslahi humo. Kila kitu ni ruksa kufikiri. Nani alijua Mzee wa Lupaso angejiuzia Kiwira? Labda na huyu ameamua kutuuzia Dowans!

Mwenye mtambo hajulikani, lakini anatangaza kuuza! Mwenye mtambo hajulikani lakini serikali iko tayari kuununua kwa bilioni mara 60, 70, 90! Kila mtu anaongeza bei anavyotaka utadhani ni Liyumba na minara ya BOT!
 
===========

Comrade Zitto umebadilika, na kina Lowassa wanaangalia na kucheka kweli kweli. Umetuacha kwenye mataa. Ama kweli, amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Lakini uje wewe si wa kwanza kuasi umma na kuutelekeza. Tumewaona wengi, hata wakati wa Yesu walikuwapo lakini mwisho wao haukuwa mzuri.

Zitto ndugu yangu zinduka, msimamo wako ni tofauti na msimamo wa kamati, na ni tofauti na umma wa watanzania. Ni msimamo wako binafsi, lakini tangu tulipokuchagua ujue ubinafsi wako uliwekewa mipaka. Kwa hiyo usipoteze muda wako kutulisha msimamo wako binafsi ambao kwanza tunajua nao siyo wako ni wa mafisadi wanaogaragara kwa mapigo waliyoyapata.

Mitaani watu wanasema pale CHADEMA ni mtu mmoja tu anayeweza kuaminika mpaka kaburini. Waliobaki mkionyeshwa vyeo au fedha mtaiasi CHADEMA na sasa tunaona wenyewe. Tunaanza kuogopa kuwa mtapewa hela mmdhuru mtu wa watu asiyekubali kuongwa.

Kama hukuongwa Zitto apa kwa jina la Zuberi tuone.
Usicheze na nguvu ya pesa......fahamu hii ni tz wale watu pale mjengoni hakuna wa kuaminika......huwa nachoka kabisa......
Mwenye mtambo hajulikani, lakini anatangaza kuuza! Mwenye mtambo hajulikani lakini serikali iko tayari kuununua kwa bilioni mara 60, 70, 90! Kila mtu anaongeza bei anavyotaka utadhani ni Liyumba na minara ya BOT!

mkuu umeumia saana isee.....mkuuu achana tanzania si unaona kama mwakilishi anasema wazi anatetea msimamo wake hatababaika yaani kaazi kweli kweli........
 
Hapa naomba nimtetea Zitto kidogo japo sikubaliani naye kwenye mahitimisho yake....

Mwanakijiji,

Unasema unamtetea Zitto japo hukubaliani na mahitimisho yake.

Naomba kukuuliza swali:

Zitto kahitimisha pendekezo kwamba mitambo ya Dowans ni sawa inunuliwe. Wewe hitimisho lako ni nini?
 
Kuhani nimesema hitimisho langu ni lile la kamati ya Bunge kwamba TANESCO wawezeshwe kununua mitambo. Sijasema TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya DOWANS. Hii sio kazi ya kamati. Mitambo gani wananunua na kutoka wapi ni kazi ya TANESCO wenyewe. Hili nimeliweka wazi kabisa katika michango yangu humu (unspinned, niliyoandika mwenyewe) ndani na pia katika barua ambayo nimeandika kwa Waziri wa Nishati na Madini. Kuhani, nipo very clear na judgement za watu humu nazichukua kama changamoto. As i said, humu JF sishindani, ninajifunza.

Msimamo wangu ni msimamo wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
 
Mitambo ya Dowans iko Tanzania kwa sasa, installed, tested and commissioned. Kama Tanesco itaweza ku-negotiate a good deal na Dowans, why not kuinunuwa? Imagine, tatizo la kusubiri kwenye kiza kipindi kisichopunguwa mwaka cha kuanza uchambuzi, uagizaji, ufungaji, majaribio hadi kuikabidhi kwa Tanesco....Duhh. Nadhani hapa inabidi tuinunuwe hii ya Dowans tu. Tena nna uhakika itakuwa kwa bei poa.
 
Kufuatia mjadala uliokuwa unaendelea humu kwa wiki moja sasa kuhusiana na mpango wa TANESCO kununua mitambo ya Dowans, na kufuatia uamuzi wa kamati ya Nishati na Madini wa Disemba 14 mwaka 2008; imekuwa ikinukuliwa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 in general terms kuwa inazuia ununuzi wa mitambo iliyotumika.

Nilipitia sheria hiyo yote na sikuona kipengele hicho cha sheria ambacho kila mtu alikuwa akinukuu bila kutaja. Niliomba pia nisaidiwe na wanaJF bila mafanikio.

Nimefanikwa kupata.

Kanuni za manunuzi ya Umma (sio sheria ya manunuzi ya Umma) kipengele cha 58(3) ndiyo inakataza manunuzi ya vifaa vilivyotumika. Sheria hutungwa na Bunge na Kanuni hutungwa na Waziri (kuhusiana na manunuzi ni Waziri wa Fedha na Uchumi).

Wanasheria waliobobea na hata kamati ya Bunge iliyojaa wanasheria waliobobea waliuambia umma kwamba Sheria inakataza. Bila kutaja kipengele na pengine bila hata kuhoji sote tukawa tunasema sheria inakataza.

Kwa nini ilkuwa hivi, sijui.

Nafurahi mafundisho aliyonipa Shivji ya kwamba doubt everything yameniwezesha kwa mara nyingine kuhoji na kutafuta ukweli.

Sasa tutasema, kanuni zinakataza. Sio sheria ya manunuzi inakataza.

Hili ni dogo, mjadala wetu upo pale pale kwamba, je uamuzi wa TANESCO kununua mitambo hii ni sahihi? Hoja ya kisheria imejibiwa humu humu JF. Hoja ya kisheria haipo. Hoja ya kimaadili (morality/ethical) ipo. Hoja ya value for money ipo. Tukate nyanga
 
Kwa upande wangu maona kununuwa mitambo ya Dowans ni sahihi kabisa, kwani kila kitu kiko wazi.

Kama kulikuwa kuna tatizo hapo kabla, lilikuwa ni tatizo la rushwa na si tatizo la mitambo. Kama tatizo limeshatambulika na linashughulikiwa ipasavyo, kwa nini tusitumie fursa hii kujipatia mitambo ambayo already ipo Tanzania? tena inafanya kazi?

Inunuliwe tu.
 
Naona hapa ni roho mbaya tu zimetawala! Rostam ni mtanzania mwenzetu anatumia mapato yake kuwekeza hapa tanzania watu wanapata ajira, Dr. Idrasa, Ngereja na wengineo wamewahi kujishikiza kimaisha kwake. Hata kama anapata super profit fedha ile ataitumia kuwekeza tena na tena. Huyu sio mlafi na mzinifu kama huyo alieko keko.

Na huyu Dowans kama mnaona ni mitumba apewe leseni asambaze umeme sambamba na tanesco isiteshe alishasema soko la umeme bongo ni nono na anaweza uza umeme sambamba na tanesco bila shida.
 
Nisemeje? Ngoja niwe mpole ndugu yangu.

Unakumbuka Richmond walishindwa kuzalisha umeme? Unakumbuka kuwa hata Dowans nao baada ya kurithi mkataba wa Richmond walishindwa kuzalisha umeme?
Mitambo iliyoletwa na Richmond ni mitambo mikuu kuu ambayo ilitumika katika winter olypics kule greece kuzalisha umeme. Hii ina uwezo wa 40MW tu.

Mitambo waliyoleta Dowans mwishoni mwa mwaka 2007 na huo mmoja umetumika kwa masaa 400 na unaweza kutumika kwa miaka 13 ijayo kabla ya kufanyiwa overhaul na kutumika kwa miaka 13 mingine. Ndio taarifa ya mtaalamu inasema. Ndivyo tulivyoelezwa. Kama kuna taarifa nyingine ya mtaalamu inaonesha otherwise, i am open minded and i will compare and form the right opinion.

Vipi hujaona kile kipengele cha sheria nilichoomba uniangalizie katika sheria ya manunuzi? Hapa hatushindani, tunaelimishana. Ndio sababu ya sisi kuanzisha jukwaa hili na kulipa support yote. Umeona kipengele hicho mwenzangu?

kwanza kabisa onus ya kuprove kwamba PPRA inaruhusu kununua mitambo chakavu ni ya kwako, wataalamu wa sheria wamesema kuwa PPRA 2004 hairuhusu kununua mitambo chakavu. Sasa wewe ndio utuambie kuwa PPRA inaruhusu kununua mitambo chakavu na vipengele vyake. Na pse usiongee mambo ya WAIVER maana hili waiver itoke kuna mengi ambayo ni nje ya scope ya hii issue.

Sasa wewe unataka kujustify kununua mitambo ya Dowans mpaka unaanza kuikemea PPRA ambayo imetungwa na BUNGE kwa ajili ya kutuokoa, ama kweli ishi uone. Sisi huku N America ukisikia watu wanasema sijui natumia constitution right yangu kutojibu maswali, huwa tunaconclude kuna walakini, na ukisikia wanasheria wanaingizwa kwenye mambo yanayohusu maslahi ya nchi na wanasiasa ujue tayari kunawalakini, na hapa ni hivyo hivyo.

Sisi tunapongangania mitambo mipya, issue yetu kubwa ni kudeal na source companies moja kwa moja ili kwa miaka 20 ijayo tusiwe na wasiwasi na mitambo. Mkuu hukuona mtambo wa SONGAS ulipoharibika, hata hawakuwa na pressure wataalamu wa GE wenyewe walifly in kwa gharama zao na kurekebisha mambo?? Sasa ukinunua uozo wa Dowans halafu ukaharibika, itakuwa vipi mkuu???? Baada ya miezi sita ya kununua mtambo wa Dowans, ukiharibika nani atatengeneza, wakati Dowans does not exist anywhere in this world?? Utasema ooh kuna wataalamu walisema miaka 13 mtambo utafanya kazi wakati hao wataalamu hawana hata insurable responsibility kwenye maneno yao??

Ukinunua kitu halafu ukakiuza hata baada ya masaa matatu tu ya ownership, kuna vitu vingi kwenye warranty na manufacture vinapotea, sasa itakuwa mitambo ambayo imefungwa na dowans ambao hata hii kazi ya umeme hawajawahi fanya popote duniani, si manufacture atatutukana hata tukitaka kununua parts?? Hivi mkuu mbona umekuwa mzito mno kuelewa hii issue ndogo, hivi kweli mambo complicated ya nchi mtayaelewa vipi???
 
Last edited:
Mimi ningemuomba muheshimiwa Zitto atuambatanishie hapa nakala nzima nzima ya maamuzi ya kamati ili tuweze kujua ni nini kimezungumzwa humo. Maana pengine tunabishana lugha tu na upeo wa kuelewa kumbe hitimisho ni lilelile.
Sasa muheshimiwa, tafadhali...tunaisubiria....
 
Back
Top Bottom