Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

zitto bado yuko sahihi kwani ushauri wake hauna hisia kama wafanyavyo sitta, mwakyembe na wenzao.

ccm wana mambo yao na zitto amewashika patamu kwani tabia yao mbaya ya kuendekeza ushabiki kwenye masilahi ya nchi imepitwa na wakati.

zitto asonge mbele na maoni yake kwani hata ile ya buzwagi sitta alimkebehi na kumwadhibu kupitia genge laooooo.

kwa nn akina sitta na wenzao hawakemei mambo chungu mbovu yaliyomo zaidi ya dowans ila kwa kuwa hili wana masilahi bianafsi wanajifanya vinara???

mangapi ushabiki wa ccm unaendelea kukumbatia na sitta kama kada amayanyamaziaaaa...

Zitto waeleimishe kuwa hizo kamati sio siasa ni utendaji na utaalamu tena unaotakiwa kuwa muwazi kila mambo kwa mustakabali wa taifa letuuu..

kwa hili zitto anazidi kuijenga chadema kwa watu MAKINI.....
 
Mwakyembe kachemsha sana....na hasa pale anapozungumzia "operation Snagara" na pia kuhusu "Posho"........sikutegemea hii toka kwake.......nilitgemea angetuchambulia vipengele vya sheria za manunuzi (yeye akiwa mwanasheria) pamoja na kutupa facts zengine ambazo wananchi hatuzijui kuhusiana hii saga........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!

Heshima yako Mkuu.

Mimi nadhani suala la posho nalo ni muhimu likatizamwa. Kwani kamati ya bunge inapaswa kupewa posho na nani? kwa nini Tanesco waliwapa posho kamati ya Zitto? Je ilitoa posho pia kwa kamati ya Shelukindo? Je wamepewa posho kiasi gani? Posho ya mwenyekiti wa kamati ni tofauti na wajumbe wengine wa kamati? Kwa nini kamati ya Zitto (na zaidi Zitto mwenyewe binafsi) inaelekea ku'side' na MD wa Tanesco? Je ni hiyo posho peke yake au kuna zaidi?

Mwakyembe pia ameibua kitu kingine muhimu sana. Kwamba bodi ya Tanesco imekataa kununuliwa kwa mitambo ya Dowans. Bodi kisheria ndio iko responsible kwa uendeshaji wa kampuni. Dr. Rashid yeye ni nani hadi akatae maamuzi ya bodi ya Tanesco? Kamati ya kina Zitto mbona haikuwauliza kina Dr Rashid ni kwa nini wanataka kwenda kinyume na maamuzi ya bodi yao?

Sheria(na kanuni) ya manunuzi ipo wazi kabisa. Mitambo lazima iwe mipya, full stop.Lazima Tanesco waitishe tender na kama Dowans wanataka ku'bid', wa'bid' tu (sheria inasisitiza uwepo wa ushindani).

Kama kamati ya Zitto walipata data/maelezo ambayo yanawafanya watoe ushauri tofauti na ushauri wa kamati ya Shelukindo, nini kinawazuia kutoa ushauri huo. Kwani ni lazima ushauri wao ufanane na ule wa kamati ya Shelukindo hata kama wanatofautiana basis? Wanataka mjadala na kamati ya Shelkukindo, kwa kanuni ipi ya Bunge? Kanuni za Bunge zipo wazi ni nini wanatakiwa kufanya, kwa nini wantaka kupindishwa kwa sheria/kanuni? Wanatakiwa wapeleke taarifa yao Bungeni na siyo kujadiliana na kamati nyingine au kulalama kwenye vyombo vya habari.

Zitto anatuambia hatuhitaji kufahamu Dowans ni kina nani, tunahitaji mitambo tu bila kujali tunauziwa na nani. Hili si kweli. Je kama anaetuuzia hana mamlaka kisheria kutuuzia itakuwaje? Inashangaza kwamba amesahau yaliyotokea kwenye saga la Richmond. Moja kati ya hadidu za rejea za kamati ya Mwakyembe ilikuwa ni kupata ukweli juu ya nani ni mmiliki wa Richmond. Mpaka leo majibu bado hayaridhishi sana, at least to me.

Naamini Mhe. Zitto atajutia msimamo wake katika hili.
 
Last edited:
zitto bado yuko sahihi kwani ushauri wake hauna hisia kama wafanyavyo sitta, mwakyembe na wenzao.

ccm wana mambo yao na zitto amewashika patamu kwani tabia yao mbaya ya kuendekeza ushabiki kwenye masilahi ya nchi imepitwa na wakati.

zitto asonge mbele na maoni yake kwani hata ile ya buzwagi sitta alimkebehi na kumwadhibu kupitia genge laooooo.

kwa nn akina sitta na wenzao hawakemei mambo chungu mbovu yaliyomo zaidi ya dowans ila kwa kuwa hili wana masilahi bianafsi wanajifanya vinara???

mangapi ushabiki wa ccm unaendelea kukumbatia na sitta kama kada amayanyamaziaaaa...

Zitto waeleimishe kuwa hizo kamati sio siasa ni utendaji na utaalamu tena unaotakiwa kuwa muwazi kila mambo kwa mustakabali wa taifa letuuu..

kwa hili zitto anazidi kuijenga chadema kwa watu MAKINI.....

Ndugu yangu Nyauba, naweza kukubaliana nawe kwenye moja tu kati ya ninayoamini unamaanisha. Nalo ni kuwa, Zitto anayo haki ya kusema anachokiamini. Basi.

Mkuu, nimesikiliza mahojiano ya waheshimiwa wote watatu (Dr. W. Slaa, Zitto na Mwakyembe) kupitia ITV jana jioni. Nilichokiona kutoka kwao ni uelewa usiolingana wa issue iliyoko mbele yetu.

Mh. Dr. W. Slaa, alielezea jinsi anavyoona inafaa kushughulikia suala la manunuzi ya mitambo ya DOWANS. Alikuwa mwangalifu sana katika kauli zake. Ila ni dhahiri kuwa busara zake hazimtumi kukubaliana na mawazo ya Zitto katika kushughulikia suala hilo. Dr. Slaa alikwepa kukosoa moja kwa moja mtazamo wa mwenzake (Zitto) kuhusiana na suala hilo. Vile vile Dr. Slaa alielezea kama ambavyo imekuwa ikielezewa hapa JF na kuomba kupata maelezo zaidi ya reports za Kamati za Bunge (Madini na Nishati na Matumizi ya Umma) kuhusiana na sakata hili.

Mh. Zitto alinisikitisha sana. Maelezo yake yalikuwa yakipingana pingana kadiri alivyokuwa akiendelea kuzungumza. Alionyesha either kutokujua alichokuwa anakiongea, au kutokiamini alichokuwa akikisema. Kwa mfano, Mh. Zitto alisema "suala ni je, mitambo hiyo inafanya kazi au lah". Kwa mtazamo wangu, kufanya kazi au kutofanya kazi kwa mitambo ya DOWANS hakuifanyi ikubalike hasa kama inatakiwa kununuliwa kinyume cha sheria. Mitambo hata iliyo chakavu na inayouzwa duniani, pia inafanya kazi. Suala ni je tuko tayari kutupilia mbali sheria za nchi yetu kwa manufaa ya DOWANS? Kama jibu ni ndio. Swali la nyingeza tunalotakiwa kujiuliza ni "Kwa manufaa ya nani"?

Nakubaliana sana na maelezo ya Mwakyembe kuhusiana na issue ya TANESCO kukusudia kununua mitambo ya DOWANS. Mwakyembe alisema kuwa:
1. TANESCO wakitaka kununua mitambo hiyo wanaweza kufanya hivyo, kama wanavyofanya kwenye manunuzi mengine yote (Bunge halihusiki kuamua juu ya hilo)
2. Kamati ya Bunge (Nishati na Madini) haioni manunuzi hayo kuwa ni sahihi kwa kuzingatia mchakato mzima wa manunuzi hayo toka mwanzo (Richmond na sasa DOWANS). Mkataba uliorithishwa kwa DOWANS, ni batili na umevunjwa. Leo hauwezi kuwa halali bila kuusafisha.
3. Sheria za manunuzi ya umma zifuatwe ili kukidhi matakwa ya sheria.
4. Na mengine mengi aliyosema

Kwa maoni yangu, suala la manunuzi ya mitambo ya DOWANS litafufua tena scandal kubwa sana ambayo ilishaanza kufifia. Scandal hiyo haina manufaa yote zaidi ya kupoteza muda tu, na labda hatua za kisheria kuchukuliwa baadae kwa watakaohusika (hata kama itakuwa ni baada ya miaka 10).

Nadhani Zitto amejiingiza kwenye mtego mbaya wa kisiasa. Mtego ambao waliomwingiza ndio wanaofahamu madhara yake. Naamini hivyo kwa kuwa yeye ndie aliewaumiza kwenye scandals nyingi ikiwemo hii ya Richmond, Buzwagi n.k. Hivyo inawezekana wanataka aonje maumivu kidogo kabla uchaguzi haujafika, na hatimae apotee kisiasa. Kama mawazo yangu si sahihi, basi serikali ndio itakayokuwa inaingizwa mkenge na Zitto. Vyovyote iwavyo, kuna mmoja ataumia sana tu.

Naamini mtego anaoingia Mheshimiwa Zitto, si tu utamgharimu yeye binafsi kama mwanasiasa, bali pia chama chake ambacho hakionekani kuweka msimamo wake kuhusiana na suala hili.
 
Wakuu suala la mitambo ya Dowans limejadiliwa mna na ktk threads mbali mbali humu jamvini. Personally nimeona ni vema tukawa na thread maalum kama mada isemavyo hapo juu. Hii ni kutokana kwamba Tanesco, Zito na kamat yake, na wale wote wanaotaka kutuaminisha kwamba ununuzi huo ni jambo la busara wanaegemea hapo.

1. Eti kuna mkaguzi kutoka ujerumani amekagua mitambo hiyo na kuiona ni ok na mingine ni mipya ikiwa imetembea for only 400 hrs.

2. Eti mitambo hii itaweza kutembea kwa miaka 13 bila kufanyiwa overhaul.

Ningependa kuanza na huyu the so called mkaguzi:

1. Anatoka kampuni gani?

2. Ana qualifications gani?

3. Ana uzoefu gani na kazi kama hii na amewahi kutumika wapi na kampuni zipi?

4. Ana bima yeyote inayotulinda iwapo ikigundulika alituingiza mkenge?

5. Anatambuliwa na Pratt and Whitney kama mkaguzi wa mitambo yao i.e is he a certified inspector?

6. Mtaalamu huyu aliletwa na Dowans au Tanesco na ni lini alianza kuwa contacted?

7. Kama ni Tanesco nini kilipelekea Tanesco kumuita mtaalamu huyu? Ina maana walikuwa na nia ya kununua mitambo hiyo kabla hata ya kuangalia taratibu zingine?

8. Alifanya kazi hiyo ya ukaguzi kwa muda gani?

9. Alitumia method gani kufanya uhakiki?

10. Tanesco ilimpataje mkaguzi huyu? Wangapi waliapply?

11. Je Tanesco ipo tayari kutoa ripoti ya mkaguzi huo?

12. Wakati wa ukaguzi Tanesco iliwakilishwa na nani? Na Dowans pia na nani?

13. Je mtaalamu huyo amewahi kuifanyia kazi yeyote Tanesco au Dowans before?

Well I know some of you might think we are now going in circles on this SAGA.
Lakini vijiswali hivi ni rahisi na vinaweza kujibiwa na Idris au mtaalam yeyote wa Tanesco aliyehusika na mchakato huu in just 10 mins tena bila hata kusoma mahali for any smart kiongozi. Cha msingi hapa na nia ya maswali haya ni kujiridhisha na kamchakatohaka kanakoonekana kujustfy ununuzi wa mitambo hii.

Pia kuna hili la mitambokuwa mipya na eti mingine imetembea masaa 400 tu. Ikumbukwe kuwa mitambo in this new tecnlogical era hauijaji kwa time based bali condition based. That applies kwenye hili la kwamba mitambo hii haitakuwa overhualed in 13 yrs. Nikiwa kama muhandisi hii sentensi naona imekaa kisiasa zaidi kwani overhauling pia ni condition based and not time based. How do you sell me an equipment and tell me it won't be overhauled in so many yrs? Nchofahamu hapa huyu jamaa atakuwa alikuwa nazungumzia PM (Preventive maintenance) ambayo inaweza kuwa say kuna za daily, monthly, yearly na labda hiyo ya say after every 5 or 10 or even 20 yrs fungua hiki au kile angalia pale na hapa. Hii ni staili ya zamani ya maintenance. You don't have to just overhaul a machine et kwa sababu imetembea masaa 100, 000. (Anyways anayehitaji ziada ya hii I am ready to debate ). Ninachoshangazwa hapa ni how huyu mkaguzi ali come up na hiyo miaka 13 -tena kwa mtambo iliyotumika?

Haya yote yanakuja just because historia ya kampuni hii formely known as Richmond ina utata. Tanesco pia ni watata, serikali ni watata. Hivyo basi kuna kila haja Tanesco itoe press release ya kuelezea mtaalam huyu namaswali hapo juu. Si mnakumbuka hata Richmond waliatuambia wamekubaliana na Pratt and Whitney kushirikiana kuzaisha zile 100 MW? of which they any written doc to support that. Sasa hili la mtaalamu mjerumani tunaaminije kirahisi rahisi? Tunamuaminije kirahisi rahisi Dr. Idris wakati ana questionable credibility? Tunaiaminije Tanesco kirahisi rahisi wakati imekuwa ikitudisapoint thousands of times?
nyambalaa

pia binafsi ningependa kufahamu ni kwa kiasi gani kamati ya nishati ya bunge imeweza kulisaidia shirika hili kiutendaji ili liweze kuwa na ufanisi zaidi hasa kwenye suala la kuondokana na mfumo wake wa sasa wa utendaji (generetaion, transmission and distribution of power).

pili uwezo mdogo wa kimenejiment unaotokana na unskilled labour, overstaffed,nk.

bottom line financial crisis inayoliumiza na kutishia uhai wa shirika hili kwanza kutokana na mfumo mbovu wa utendaji???

Halafu hizi kamati (nishati na mahesabu ya mashirika ya umma,), TANESCO, SERIKALI (WIZARA YA NISHATI) NA IKULU WANAFANYA MALUMBANO HAYA KWA AJILI/FAIDA YA NANI????????????????????????????????????????????
 
Usiku wa jana nilibahatika kuangalia ITV Channel,sina kawaida ya kusearch Tv za bongo mara kwa mara,Lakini jana niliipata bila kutarajia.Tumeskiliza taarifa ya habari, na kipindi kilichofuatia kikiendeshwa na Stephen Chuwa ambaye ndiye mwenyewe alikiandaa.Hakika nilijawa na hofu jinsi wabunge na spika wao walivyokuwa wanatupiana mpira kuhusu mitambo ya Dowans na TANESCO.Manunuzi , ununuzi,Kanuni ,kazi na sheria na Kamati za Bunge!!!
Tena nikaona pale Ikulu Bwana S.Rweyemamu na ufafanuzi wa alichosema Kikwete.Jamani kuna ubabaishaji gani wa kiasi hicho?Kila mmoja analo jambo la kuongea? Hatuna utaratibu wa kuendesha serikali,mamlaka,na vyombo vyake.Wana-JF Nisaidieni hapa!!
 
usiku wa jana nilibahatika kuangalia itv channel,sina kawaida ya kusearch tv za bongo mara kwa mara,lakini jana niliipata bila kutarajia.tumeskiliza taarifa ya habari, na kipindi kilichofuatia kikiendeshwa na stephen chuwa ambaye ndiye mwenyewe alikiandaa.hakika nilijawa na hofu jinsi wabunge na spika wao walivyokuwa wanatupiana mpira kuhusu mitambo ya dowans na tanesco.manunuzi , ununuzi,kanuni ,kazi na sheria na kamati za bunge!!!
Tena nikaona pale ikulu bwana s.rweyemamu na ufafanuzi wa alichosema kikwete.jamani kuna ubabaishaji gani wa kiasi hicho?kila mmoja analo jambo la kuongea? Hatuna utaratibu wa kuendesha serikali,mamlaka,na vyombo vyake.wana-jf nisaidieni hapa!!
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.

Hii imetusaidia tena kujua upeo wa viongozi wetu(bunge na serikali) kwa mapana zaidiii.

Kuna upuuzi mkubwa hapa unaendekezwaaaa bila kujali heshima ya wananchi wanaoweka watu madarakani...

Wote sasa wanafanya show down...... Ujinga mtupuuuu

mpaka sasa kamati ya nishati, wizara na ikulu hawajitambuiiiii.....cheap popularity..

Inaumaaa sanaaaaa
 
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.

Inaumaaa sanaaaaa

Mbona tunaambiwa bodi ya Tanesco imekataa. Hiyo Tanesco ambayo wewe (na Mh. Zitto) mnaizungumzia ni ipi? Au ya Dr Rashid? Bodi ndiyo iko responsible kwa maamuzi ya Tanesco.
 
Last edited:
Mbona tunaambiwa bodi ya Tanesco imekataa. Hiyo Tanesco ambayo wewe (na Mh. Zitto) mnaitungumzia ni ipi? Au ya Dr Rashid? Bodi ndiyo iko responsible kwa maamuzi ya Tanesco.
MD wa tanesco ni sehemu ya bodi kwa hiyo natumai mapendekezo aliyoyatoa anawakilisha bodi yake pia.

kama hawasikilizani hayo ni matatizo yao kwani mimi wala zitto hatumo ndani ya bodi ila dr idrissa natumai ni mjumbe muhimu.

lengo la bodi ni kuona taasisi wanayoisimamia inasonga mbele kwa kutoa huduma bora (in case is service based org)...kama wanakinzana waangalie corporate governace ikoje kama wanaifuataa..

hapa jamani kwa sasa SIASA imetawalaaa zaidiiiiii...
pia kwa taarifa tuu mtendaji mkuu ndo bottom line mhusika mkuu wa success au failure za organization yake kwani yeye ndo mtaalamu zaidi ya bodi....
 
MD wa tanesco ni sehemu ya bodi kwa hiyo natumai mapendekezo aliyoyatoa anawakilisha bodi yake pia.

...pia kwa taarifa tuu mtendaji mkuu ndo bottom line mhusika mkuu wa success au failure za organization yake kwani yeye ndo mtaalamu zaidi ya bodi....

Hii nadhani ni Corporate Governance mpya!
 
hapa jamani kwa sasa SIASA imetawalaaa zaidiiiiii...
pia kwa taarifa tuu mtendaji mkuu ndo bottom line mhusika mkuu wa success au failure za organization yake kwani yeye ndo mtaalamu zaidi ya bodi....

Umesikia mashitaka ya kesi ya Liyumba? Mojawapo ni kufanya maamuzi bila kuishirikisha Bodi ya BoT.

Kusema kwamba MD/CEO ndiyo mhusika mkuu hapo ni kutudanganya mchana kweupe. Yeye yuko responsible kwa Bodi na wao Bodi kazi yao ni kupokea mapendekezo/taarifa za maendeleo ya shirika/kampuni na then wanaweza kutoa ushauri, kugoma ama kukubali utekelezaji wa mependekezo yaliyotolewa na MD/CEO.
 
bado naunga mkono hoja ya zitto kushauri tununue mitambo kama tanesco walivyoshaurii.

Hii imetusaidia tena kujua upeo wa viongozi wetu(bunge na serikali) kwa mapana zaidiii.

Kuna upuuzi mkubwa hapa unaendekezwaaaa bila kujali heshima ya wananchi wanaoweka watu madarakani...

Wote sasa wanafanya show down...... Ujinga mtupuuuu

mpaka sasa kamati ya nishati, wizara na ikulu hawajitambuiiiii.....cheap popularity..

Inaumaaa sanaaaaa

Mkuu Nyauba, nilitegemea kusoma jinsi gani unavyounga mkono hoja ya Zitto kuhusiana na ununuzi wa mitambo kama TANESCO wanavyoshauri.

Ni kweli kuwa Saga hili limesaidia kutambua mengi kuhusu utendaji wa viongozi wetu. Kinachosikitisha ni kwamba wengi wa viongozi hao inaelekea kujali zaidi maslahi binafsi kuliko maslahi ya Taifa. Uzalendo katika nchi yetu uko chini kuanzia kwa viongozi hadi kwa wananchi na hii ndio sababu kubwa ya matatizo yetu mengi. Mchezo unaoendelea ni wa kisiasa. Nchi inaendeshwa kisiasa kuliko kitaalam. Kadiri muda unavyokwenda na kukaribia uchaguzi, tutashuhudia mengi zaidi yanayotia shaka. Wanasiasa wataumizana sana. Ila watakaoweza kupita kipindi hicho kigumu kisiasa watakuwa imara sana. Ukweli na uwakilishi mzuri ndio takaowawezesha wanasiasa ku-survive kipindi hicho.
 
Nimekuwa nikosoma na kufuatilia sehemu kubwa ya taarifa kuhusiana na kinachoitwa "kauli ya Zitto" kuhusiana na sakata la mitambo ya Dowans.

Tatizo nililoliona na ambalo wajumbe wengi wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma ambayo Zitto ni Mwenyekiti wake wanaliona. Tatizo lenyewe ni lile la taarifa za kwamba kamati imebariki/inashinikiza/inataka mitambo ya Dowans inunuliwe. Wajumbe wote akiwamo Zitto hawajasema LAZIMA mitambo ya Dowans inunuliwe.

Kabla ya kueleza maelezo ya wajumbe wengi wa kamati niliobahatika kuzungumza nao, niweke wazi kwamba Zitto ni Mwenyekiti (anayeongoza vikao) na kuwa Mwenyekiti (si Mwenyekiti Mtendaji) maana yake ni kufanya kazi kwa vikao na kauli zako zinazingatia vikao. Kama hivyo ndivyo tujadili KAMATI.

KAMATI ya POAC (Kamati ya Zitto) imefanya vikao vyake na katika kikao kimoja wapo walikutana na Tanesco katika kupitia hesabu za shirika hilo na kuangalia matatizo yao ya kifedha. Kama kawaida Tanesco ya Dk Rashid ikapenyeza kwa umakini mkubwa matatizo yake ya kifedha na tatizo la ongezeko la mahitaji ya umeme huku kukiwa na upungufu wa uzalishaji baada ya Dowans kutimuliwa na kadhalika.

Maelezo ya Tanesco yakawagusa wajumbe wa POAC na wakaona ni vyema wakapata maoni ya wenzao wa Kamati ya Nishati na Madini (ya kina Mwakyembe) na kwamba wakaweka wazi katika maazimio yao kwamba kuna umuhimu kwa Tanesco kusaidiwa na serikali katika kununua mitambo mipya hata ikibidi kununua ya Dowans kwa sharti la kuzingatia sheria. Ikiwamo sheria ya manunuzi ya 2004. Kwa makini kabisa kamati imesema, "haijabariki ununuzi wa mitambo ya Dowans" na kwamba kamati ya POAC wala ya Nishati na Madini hazina mamlaka ya kuidhinisha wala kuzuia manunuzi ya Tanesco.

Maelezo ya POAC hayajatofautiana na yale ya Kamati ya Nishati na Madini kwamba hata wao hawana mamlaka ya kuzuia manunuzi. Tofauti ya kamati hizi mbili ni kwamba ile ya POAC ilitaka kukaa pamoja na wenzao wa Nishati na Madini kujadiliana jinsi ya kuisaidia Tanesco kiushauri na ili wapate maelezo ya kuridhisha kuweza kuishauri serikali na ili kuzuia kutokea kwa matatizo yaliyotokea wakati wa Richmond. Suala la kununua au kutonunua ama kutaifisha mitambo ya Dowans lingekuja kujulikana baada ya kukaa pamoja.

Kuna matatizo makubwa matatu ambayo yamesababisha hali hii kufikia hatua ya kuanza kushambuliana na hata kuanza kuibuka kwa tuhuma dhidi ya wabunge husika akiwamo Zitto ambaye imefikia hata kutuhumiwa kuhongwa.

1. Tatizo la kwanza ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na Zitto mwenyewe kujiamini kupita kiasi na kuwaamini waandishi wa habari kupita kiasi. Amezungumza nao na kwa bahati mbaya sana (kwa kujua ama kutojua) waandishi hao wamepotosha kabisa kauli ya Kamati (si ya Zitto) kwa kusema kwamba kamati imebariki/inataka Dowans inunuliwe. Kamati haikusema hivyo.

2. Tatizo lingine ni lile la kauli kwamba kamati ya Nishati na Madini haijawasikiliza Tanesco, nalo limetokana na tafsiri ya baadhi ya waandishi. Maelezo ya wajumbe wa Kamati na Nishati na Madini ni kwamba wamewasikiliza Tanesco kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye alifika katika kikao cha Desemba 14, 2008. Kawaida waziri akiona amezidiwa ndipo huwaita wataalamu wake (Tanesco) kujieleza. Ngeleja alipomaliza kuwasilisha mbele ya uongozi wa Tanesco na Tanesco kutoka nje kuwaacha wabunge wajadili, Ngeleja angeweza kuomba Tanesco warudi wamsaidie, lakini aliridhika na kukubali. Waandishi wakaandika kwamba Kamati imeikatalia Wizara kununua mitambo. Kamati ya Nishati haijakanusha kama ambavyo kamati ya Zitto haijakanusha, kwa sababu ambazo naomba nizianike kwamba wanasiasa ni waoga sana kubishana na vyombo vya habari. Kimsingi hakuna kamati iliyokataa wala kubariki ununuzi wa mitambo ya Dowans.

3. Tatizo kubwa ambalo sasa limeguswa kiaina na baadhi ya wahusika akiwamo Zitto na Dk. Mwakyembe ni tatizo la kisiasa. Zitto amenukuliwa akisema kuna siasa za makundi, Mwakyembe akasema anaona kama operesheni sangara inaendelea. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa linaweza kubadili mjadala kutoka katika hoja za msingi na kuanza kwa SIASA. Kubadilika kwa hoja kutoka tatizo na kwenda kuwa SIASA.

4. Lakini pamoja na kuwa hoja si ya kisiasa, msingi wake unaweza kuwa wa kisiasa zaidi na kwamba Zitto kama mwanasiasa angepaswa kuangalia pia upande wa hatima yake kisiasa zaidi badala ya kutaka kuwa MAKINI kutenda HAKI kwa kutaka kusikiliza pande zote husika. Hilo linahitaji mjadala pekee kwa kuwa Zitto amekuwa na hulka ya kusikiliza hata wale ambao watu hawapendi kuwasikiliza. Hiyo ni hulka nzuri lakini ni HATARI SANA.

Kwa maoni yangu:

Suala la Dowans asili yake ni hoja tete ya Richmond ambayo ilisababisha kuenguliwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha (ambaye yuko kimya sana). Kuanguka kwa Waziri Mkuu ni hatua nzito katika historia ya nchi hii na kulisababisha kuvunjika kwa Baraza zima la mawaziri. Zitto alilumbana na Spika kuhusu hilo na Rais Kikwete alithibitisha maneno ya Zitto kwa kutangaza kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri.

Tukio hilo lilirudisha imani ya umma kwa vyombo vyote vya dola ambavyo walikwisha kupoteza imani navyo na kuona kwamba sasa kumbe hakuna aliye juu ya sheria. Bunge, wabunge, serikali zilipata heshima ndani na nje ya nchi. Sakata la Richmond likawa mtaji mkubwa wa kisiasa kwa wanasiasa ndani ya Bunge na hata kwa Rais. Wapinzani nao waliona kama ushindi kwao. Nchi ilichangamka na masuala mengine kama EPA na kesi za kina Mramba yakafuatia mkondo.

Sasa hivi, yeyote ambaye anathubutu kutaka kubadili HADHI ya Bunge kwa kuhalalisha kwa mlango wa nyuma maovu yaliyotokana na Richmond, atakuwa anairudisha nchi nyuma (si wanasiasa).

Jambo la msingi ni kuzingatia mambo yote ya msingi, ikiwa ni pamoja na kuangalia kwamba Dowans tunawadai bilioni 23, Dowans wametushitaki lakini pia ni kweli kwamba tuna tatizo la UMEME sasa? na Je, ni dharura? Tumejua lini tatizo? Nani awajibike kwa hili? Je, Sheria inasemaje ikiwa mtu amedanganya wakati wa manunuzi? munaendelea kufanya naye biashara? Je, hakuna mitambo mengine hata kwa bei ya ziada kidogo? Tusiponunua Dowans watapeleka wapi mitambo yao? wakinunua wafanyabiashara wengine (hao hao) watamuuzia nani umeme ikiwa tutakuwa na mitambo mipya?

TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.

Waandishi wazuri mko JF!. Safi sana. Ingependeza uchambuzi huu ukawekwa kwenye gazeti lisomwalo na wananchi wengi,wakaelimika.Saidia Umma kuyajua haya. Asante Mkuu
 
Jeuri ya sitta kuitingisha serikali inatoka wapi?? Je ni mtu makini mwenye misimamo isiyoyumba na kutaka kuona uhuru wa mihimili mitatu ya umma inaheshimiwaaa???

Au ni mwanasiasa aliyepofuka na siasa za muda mrefu na kujijengea himaya ya kutingisha wenzake(serikali) alioshiriki kwa karibu kuwafikisha (mtandao) hapo walipoo...

Kwa hili la richmond/dowans amekuwa kinara sana kuhakikisha serikali na wadau wake (fisadis) hawapati upenyoo...je ana ajenda ya siri??
 
Huyo nae keshapoteza makali, hana kitu, kuanzia alivyoanza na kuleta uongo, kafuatia kushabikia kununua mtambo wa Dowans, halafu leo leo ahamasishe tukatae kununua mtambo huo!

Opportunists, anaangalia maslahi au fulani kasema nini. Kwa vile kamati ya Zitto ilisema mtambo ununuliwe, basi akaja na kistory eti mtambo ununuliwe kwa vile mwezi wa nne kutakuwa na uhaba wa umeme!

Zitto, Mwanakijiji denounced!

Msome tena Mwanakijiji kuhusu hilo,hukumwelewa!!!
 
Recta.

ni kweli tupu maoni yako ila sasa tufanyeje kuondokana na KAULI na KUTENDA?
Binafsi naunga mkono msimamo wa Zitto/Tanesco katika hili kwa sababu tuu wao wanatusaidia kutambua uwezo wa wengine (kamati ya nishati na spika) katika kubishana, umaarufuuu kwenye masuala muhimu...

naomba mwongozo...hivi suala la kamati mbili kutoleana/kujibizana katika vyombo vya habari, pia Spika anajibu kupitia vyombo hivyooo....ni SAHIHI??

Sikufurahia tabia ya Spika (muhimili wa umma) naye kuitisha press conference bila hata kuongea na hao wanaolumbanaaaa....kuna tatizo..

Tusisahau pia tabia ya spika kubwatukaaaaaaa...
 
Wanabodi,
Asalaam Aleikum, Bwana asifiwe!
Ama kweli ukipotea JF siku moja ni sawa na mwaka mzima, mambo mengi yamenipita..Haya tena ya huyu Mh. Ngeleja mapya kwa mtindo wa Ulanguzi -Kibongo bongo.
Wakuu, nimesikia mahojiano na hakika nimebakia domo wazi pengine inawezekana kabisa Tanzania haina wasomi.. Huyu ni waziri tena mwanasheria!.. damn..
Moelex23, mkuu kama ulikuwepo yaani mchezo huu wa kuigiza wala hautakwisha kesho!.. mchezo wa kina mama _ Young and the Restless!

Jamani swala la Dowans linaeleweka wazi kuwa ni bomu haikuhitaji Sitta wala Mwakyembe kulizungumzia, ni wazi kabisa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu..Kuendelea kudai hatuna hila ni UJINGA mtupu na ufinyu wa kufikiri na ndio maana kumbe Afrika tumeshindwa kuendelea sii kwa sababu ya kukandamizwa na nchi tajiri isipokuwa adui wa maendeleo ya mwafrika ni mwafrika mwenyewe..

Jamani, huwezi kutenganisha issue ya Richmond na Dowans kwa kutumia mitambo ambayo ndiyo sababu ya sisi kuwaita Richmond nchini..hatukuwa na biashara na Richmond wala Dowans isipokuwa kupitia mitambo hiyo...
Hivi niulize gari likiwa limeingizwa nchini na mtu ambaye hana visa ya kuingia nchini na inefahamika kuwa hata passport yake ni bomu, huyu mtu anaruhusiwa kuuza hilo gari! tena kwa serikali yetu na kuliwekea vikao vya kujadili..Kwa kitambulisho gani alichotumia aliponunua hilo gari huko nje ikiwa hata pass yake ni fake na kaweza vipi kuliingiza nchini! . Haya sii ndio sawa na ununuzi wa Vogue toka Uingereza auBenz toka South..kutaka vya bure!..
Hata kama tukiacha swala la dowans nje ya mjadala huu bado hakuna kati yetu anayefahamu nani mmiliki wa mitambo hiyo kati ya Richond, Dowans au kule ilikonunuliwa au kukodishwa..Yawezekana kabisa kuwa Dowans wamerithi mkataba wa Richmond kwa ku lease mitambo hiyo toka Richond.. Na kuna uwezekano mkubwa hao Richmond wenyewe walipewa mkopo na benki ktk ununuzi wa mitambo hiyo..hivyo bado sii mali yao wanalipia deni. Na bila shaka kutokana na muda mfupi hawajaweza kumaliza deni na nina hakika Dowans wasingeweza kuinunua mitambo hiyo kwa cash ktk kipindi cha muda mfupi kama ule..(kumbukeni mapendekezo ya Lowassa)....
Inaonyesha wazi kwamba viongozi wetu wanajaribu sana kutenganisha Dowans na Richmond au Dowans kama shirika na mitambo hii wakati wanashindwa kabisa kuelezea kuwa shida yetu ni UMEME sio mitambo ya Dowans..hivyo kuvuta fikra za watu wafikirie kwamba bila mitambo hii tutakuwa tumekwama...
Kichekesho, ni kwamba sidhani kama huyo Ngeleja anaweza kununua nyumba toka kwa mtu anayefahamu kuwa ni Tapeli na kuweka madai kuwa shida yake ni mahala pa kulala..Hata kama ukihitaji nyumba kiasi gani, kumfahamu mmiliki wa nyumba ni swala linalokwenda sambamba na manunuzi yote huwezi kutenganisha laa sivyo utafungiwa kanya boya,,
By the way nimeambiwa kuwa majuzi huyo waziri alionekana akiwa karibu sana na Rostam kabla ya kutoa taarifa yake ktk vyombo vya habari!..
 
Astakafilah, mafisadi hatimaye wamejua bei ya Zitto!!!! Mh Zitto hawezi kutudanganya kwa hilo la Dowans, akumbuke maneno ya Mh mwenzake

'WATANZANIA SI MABWEGE TENA' - Dk. H. Mwakyembe (MB) Kyela, Mbeya.
 
Jeuri ya sitta kuitingisha serikali inatoka wapi?? Je ni mtu makini mwenye misimamo isiyoyumba na kutaka kuona uhuru wa mihimili mitatu ya umma inaheshimiwaaa???

Au ni mwanasiasa aliyepofuka na siasa za muda mrefu na kujijengea himaya ya kutingisha wenzake(serikali) alioshiriki kwa karibu kuwafikisha (mtandao) hapo walipoo...

Kwa hili la richmond/dowans amekuwa kinara sana kuhakikisha serikali na wadau wake (fisadis) hawapati upenyoo...je ana ajenda ya siri??

Sidhani kama ana ajenda ya siri. Ni wajibu wake.

Vyovyote atakavyofanya baadhi wataona ni tatizo. Akinyamaza atalaumiwa (ataulizwa yuko upande gani). Akikemea ununuzi,kitu kinachotarajiwa na wengi ndo kama hivyo ataonekana ana ajenda.

Ukweli ni kwamba watanzania wamebadirika hawadanganywi tena, wenye kutaka kuendelea na uongozi lazima wawe upande wao(wananchi) La sivyo...
 
Recta.

ni kweli tupu maoni yako ila sasa tufanyeje kuondokana na KAULI na KUTENDA?
Binafsi naunga mkono msimamo wa Zitto/Tanesco katika hili kwa sababu tuu wao wanatusaidia kutambua uwezo wa wengine (kamati ya nishati na spika) katika kubishana, umaarufuuu kwenye masuala muhimu...

naomba mwongozo...hivi suala la kamati mbili kutoleana/kujibizana katika vyombo vya habari, pia Spika anajibu kupitia vyombo hivyooo....ni SAHIHI??

Sikufurahia tabia ya Spika (muhimili wa umma) naye kuitisha press conference bila hata kuongea na hao wanaolumbanaaaa....kuna tatizo..

Tusisahau pia tabia ya spika kubwatukaaaaaaa...

Mkuu Nyauba, Kamati mbili za Bunge kukosoana hadharani si jambo la kujivunia. Ila kwa kuwa Kamati moja iliamua kwenda public katika issue hii, ilikuwa ni jambo lisiloshangaza kwa Kamati nyingine kujibu public pia. Kamati ya Matumizi ya Umma iliamua kutoa mapendekezo yake kwenye vyombo vya habari na si Bungeni kama ilivyotegemewa. Kamati ya Madini na Nishati isingeweza kujibu mapendekezo ya kamati ya Matumizi ya umma kupitia Bunge, kwakuwa haikufikishwa huko. Kumbuka wote hawa ni wana siasa na kuzungumza ndio siasa yenyewe. Hivyo hapo ndipo walipofikia.

Speaker wa Bunge kama alivyo kiongozi mwingine yeyote, anao wajibu wa kuingilia kauli za Kamati zake wakati wowote anapoona inafaa. Speaker ana vikao vyake maalum vya kupokea taarifa za Kamati. Sidhani kuwa ingekuwa ni busara kwake kukutana na Kamati hizo ili kuweka hali sawa. Kwakuwa hakukuwa na hali isiyo sawa, bali Kamati moja imepitiliza katika majukumu yake. Mh. Sitta katika press conf jana alisema hawezi kukaa na kukutanisha kamati hizo mbili. Sababu ni kuwa, kuna miongozo ya utendaji wa Bunge. Kamati ya Matumizi inatakiwa ipeleke taarifa yake kwa Kamati ya Madini na Nishati ili waipitie na kuona kama kuna haja ya kubadilisha mapendekezo yao kwa serikali kuhusuiana na manunuzi ya mitambo hiyo.

Kumbuka issue hii kama ingeachwa iendelee, ingeweza kulidhalilisha Bunge na serikali. Zaidi ya hayo, serikali na Bunge vingejikuta vikitofautiana sana katika vikao vya Bunge (ambavyo vina muda usiotosha kujadili kila kitu) badala ya kushughulikia mambo yenye maslahi kwa Taifa. Nadhani Speaker ametumia busara kutoa mtazamo wake na angalizo katika issue nzima (kama Kiongozi, Mtanzania na mpenda nchi yake). Serikali mara nyingi hujikuta ikiteleza kwenye mambo mengi. Hili ni mojawapo.
 
Back
Top Bottom