Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Msimamo wake tete umekuwa gharama kubwa sana kwa chama na taifa! Inasikitisha na kutisha.
Hata yeye hili atakuwa analifahamu,ila nadhani hofu yake ni kama atakubali kubadili msimamo wake wa awali kwa sasa ni kwamba atakuwa anapigia mstari yale ambayo wachangiaji wengi wamekuwa wakimhusisha nayo(kidogodogo) so anajaribu spin za hapa na pale ili kulimaliza hili,hadi sehemu nyingine anasema kuwa mjadala kuhusu sheria umeisha!!Ati umeisha????Kwamba pajulikane kulikuwa/kuna ukiukwaji wa kanuni kisha aseme kuwa mjadala umeisha!?Mbona CHADEMA ktk lile la waziri kijana walikuwa wanasisitiza kuwa he has to GO!
Cha msingi ni kuwa mh. angenyamaza tu,kuliko hii ya kwenye TV kuongea hv,na waandishi anaongea vile,JF anasema blah,blah...Atajichanganya sana na kuzidi kujitowesha!
 
jamani hivii hili la kununua mitambo ya dowans linawauma sana au kwa kuwa tuu linahusishwa na RA!!!!
Mimi binafsi sioni kosa la mh zitto kwani ameamua kuwa objective na mara nyingi yuko hivyo katika hojaa zake.

tuna madudu mengi ila tunakuwa selective katika kuyakemeaa...kwa nini?
mfano wizi mkubwa katika halmashauri zetu unaosababishwaa na watendaji wakishirikiana na wanasiasa (MADIWANI)...

Tuna bomu la IPTL,ATCL,TRL nk achilia mbali ubabaishaji wa TPA!!!!!!!!!!!!!!!!
JAMANI TUNAHITAJI KUSONGA MBELEEEE.

Nilidokeza jana tatizo la TANESCO ni zaidi ya hiyo mitambo ya DOWANS!!! Mfumo wa sasa wa uendeshaji wa TANESCO haukidhi mahitaji ya sasa. shirika hili LIFUMULIWE KISERA NA KIUTENDAJI.

Muswada ambao wabunge waliupinga kwa masilahi binafsi uliohusu uboreshaji wa sekta ya nishati naomba ujadiliwe upya katika hali ya uendelevuuuuuuuuuuuuuuu.

JANA KIKAO CHA RAISI NA WIZARA YA NISHATI NAONA AMEUNGANA NA MH ZITTO NA TANESCO!!!!! TUSUBIRI TUONEEEEEEEEEEEEE......
 
jamani hivii hili la kununua mitambo ya dowans linawauma sana au kwa kuwa tuu linahusishwa na RA!!!!
Mimi binafsi sioni kosa la mh zitto kwani ameamua kuwa objective na mara nyingi yuko hivyo katika hojaa zake.

tuna madudu mengi ila tunakuwa selective katika kuyakemeaa...kwa nini?
mfano wizi mkubwa katika halmashauri zetu unaosababishwaa na watendaji wakishirikiana na wanasiasa (MADIWANI)...

Tuna bomu la IPTL,ATCL,TRL nk achilia mbali ubabaishaji wa TPA!!!!!!!!!!!!!!!!
JAMANI TUNAHITAJI KUSONGA MBELEEEE.

Nilidokeza jana tatizo la TANESCO ni zaidi ya hiyo mitambo ya DOWANS!!! Mfumo wa sasa wa uendeshaji wa TANESCO haukidhi mahitaji ya sasa. shirika hili LIFUMULIWE KISERA NA KIUTENDAJI.

Muswada ambao wabunge waliupinga kwa masilahi binafsi uliohusu uboreshaji wa sekta ya nishati naomba ujadiliwe upya katika hali ya uendelevuuuuuuuuuuuuuuu.

JANA KIKAO CHA RAISI NA WIZARA YA NISHATI NAONA AMEUNGANA NA MH ZITTO NA TANESCO!!!!! TUSUBIRI TUONEEEEEEEEEEEEE......

Hoja zako nzuri lakini nadhani Zitto amategwa na ameshaingia kwenye kamtego. Kwa si ndo yeye aliyemzodoa Pinda Bungeni kuwa nchi iongozwe kwa misingi ya sheria? Iweje Zitto juzi anukukuliwe akisema kuwa Sheria si Msahahafu na papo hapo katika hili la Tanesco na Dowans anapingana na Sheria?

JK kuungana na Zitto katika sakata la Mitambo ya Dowans si jambo la ajabu; kwani hujui kuwa mmliki wa Dowans ndiyo Mmiliki wa Kagoda AL? Umesikia Kagoda AL amepelekwa kortini kwa pesa za EPA wakati yeye ndiye kinara wa EPA? Hata ukiondoa hilo si unajua kuna mpango wa kununua mitambo ya IPTL? Sina hakika kama na yenyewe iliingizwa ikiwa mitumba au mipya lakini ni move ileile na ikiwa ni hivyo walfikishe kwanaz muswada wa mabadiliko ya sheria ya manunuzi ya Umma na wasikurupuke tu kama inavyoonekana hapa. Wapeleke muswada wa kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ili Bunge na Wabunge wote kwa ujumla wahusike au wanaogopa kugonga mwamba!
 
Kwa Mh Zitto
Ninatumaini ungewashauri serikali pia kuacha kununua magari D.T. Dobie, Toyota Tanzania na badala yake kwenda kununua Autorec, Car Junction etc kwa ajili ya Value for money. Serikali ingekuwa imepata savings kubwa tu.
 
Hoja zako nzuri lakini nadhani Zitto amategwa na ameshaingia kwenye kamtego. Kwa si ndo yeye aliyemzodoa Pinda Bungeni kuwa nchi iongozwe kwa misingi ya sheria? Iweje Zitto juzi anukukuliwe akisema kuwa Sheria si Msahahafu na papo hapo katika hili la Tanesco na Dowans anapingana na Sheria?

JK kuungana na Zitto katika sakata la Mitambo ya Dowans si jambo la ajabu; kwani hujui kuwa mmliki wa Dowans ndiyo Mmiliki wa Kagoda AL? Umesikia Kagoda AL amepelekwa kortini kwa pesa za EPA wakati yeye ndiye kinara wa EPA? Hata ukiondoa hilo si unajua kuna mpango wa kununua mitambo ya IPTL? Sina hakika kama na yenyewe iliingizwa ikiwa mitumba au mipya lakini ni move ileile na ikiwa ni hivyo walfikishe kwanaz muswada wa mabadiliko ya sheria ya manunuzi ya Umma na wasikurupuke tu kama inavyoonekana hapa. Wapeleke muswada wa kubadilisha sheria ya manunuzi ya umma ili Bunge na Wabunge wote kwa ujumla wahusike au wanaogopa kugonga mwamba!
ningependa kufahamu ubadilishaji wa vipengele vya PPA 2004 ni mpaka bungeni au kuna vikao stahili (cabinet) au MKULU mwenyewe wanaweza kubadili kwa masilahi ya taifa???

halafu ile taarifa ya jana ikulu ilivyoripotiwa kama kuna kutegana au walishajua hisia za jamii kwani nilitegemea MKULU aongeee (kama alivyofanya na wizara ya elimu issue ya utungaji vitabu)..

eti jana ITV kurugenzi ya ikulu ikarusha text tuuuuuu huku wakionyesha wajumbe...ni utaratibu ila mbona mkulu hafungui mdomo wake live kwa hili???
 
Sijui tunaenda wapi,,,hakika kama ni hivi itatuchukua miaka mingi kufikia maendeleo endelevu,,,,,,,,,,,
 
Nimekuwa nikosoma na kufuatilia sehemu kubwa ya taarifa kuhusiana na kinachoitwa "kauli ya Zitto" kuhusiana na sakata la mitambo ya Dowans.

Tatizo nililoliona na ambalo wajumbe wengi wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma ambayo Zitto ni Mwenyekiti wake wanaliona. Tatizo lenyewe ni lile la taarifa za kwamba kamati imebariki/inashinikiza/inataka mitambo ya Dowans inunuliwe. Wajumbe wote akiwamo Zitto hawajasema LAZIMA mitambo ya Dowans inunuliwe.

Kabla ya kueleza maelezo ya wajumbe wengi wa kamati niliobahatika kuzungumza nao, niweke wazi kwamba Zitto ni Mwenyekiti (anayeongoza vikao) na kuwa Mwenyekiti (si Mwenyekiti Mtendaji) maana yake ni kufanya kazi kwa vikao na kauli zako zinazingatia vikao. Kama hivyo ndivyo tujadili KAMATI.

KAMATI ya POAC (Kamati ya Zitto) imefanya vikao vyake na katika kikao kimoja wapo walikutana na Tanesco katika kupitia hesabu za shirika hilo na kuangalia matatizo yao ya kifedha. Kama kawaida Tanesco ya Dk Rashid ikapenyeza kwa umakini mkubwa matatizo yake ya kifedha na tatizo la ongezeko la mahitaji ya umeme huku kukiwa na upungufu wa uzalishaji baada ya Dowans kutimuliwa na kadhalika.

Maelezo ya Tanesco yakawagusa wajumbe wa POAC na wakaona ni vyema wakapata maoni ya wenzao wa Kamati ya Nishati na Madini (ya kina Mwakyembe) na kwamba wakaweka wazi katika maazimio yao kwamba kuna umuhimu kwa Tanesco kusaidiwa na serikali katika kununua mitambo mipya hata ikibidi kununua ya Dowans kwa sharti la kuzingatia sheria. Ikiwamo sheria ya manunuzi ya 2004. Kwa makini kabisa kamati imesema, "haijabariki ununuzi wa mitambo ya Dowans" na kwamba kamati ya POAC wala ya Nishati na Madini hazina mamlaka ya kuidhinisha wala kuzuia manunuzi ya Tanesco.

Maelezo ya POAC hayajatofautiana na yale ya Kamati ya Nishati na Madini kwamba hata wao hawana mamlaka ya kuzuia manunuzi. Tofauti ya kamati hizi mbili ni kwamba ile ya POAC ilitaka kukaa pamoja na wenzao wa Nishati na Madini kujadiliana jinsi ya kuisaidia Tanesco kiushauri na ili wapate maelezo ya kuridhisha kuweza kuishauri serikali na ili kuzuia kutokea kwa matatizo yaliyotokea wakati wa Richmond. Suala la kununua au kutonunua ama kutaifisha mitambo ya Dowans lingekuja kujulikana baada ya kukaa pamoja.

Kuna matatizo makubwa matatu ambayo yamesababisha hali hii kufikia hatua ya kuanza kushambuliana na hata kuanza kuibuka kwa tuhuma dhidi ya wabunge husika akiwamo Zitto ambaye imefikia hata kutuhumiwa kuhongwa.

1. Tatizo la kwanza ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na Zitto mwenyewe kujiamini kupita kiasi na kuwaamini waandishi wa habari kupita kiasi. Amezungumza nao na kwa bahati mbaya sana (kwa kujua ama kutojua) waandishi hao wamepotosha kabisa kauli ya Kamati (si ya Zitto) kwa kusema kwamba kamati imebariki/inataka Dowans inunuliwe. Kamati haikusema hivyo.

2. Tatizo lingine ni lile la kauli kwamba kamati ya Nishati na Madini haijawasikiliza Tanesco, nalo limetokana na tafsiri ya baadhi ya waandishi. Maelezo ya wajumbe wa Kamati na Nishati na Madini ni kwamba wamewasikiliza Tanesco kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye alifika katika kikao cha Desemba 14, 2008. Kawaida waziri akiona amezidiwa ndipo huwaita wataalamu wake (Tanesco) kujieleza. Ngeleja alipomaliza kuwasilisha mbele ya uongozi wa Tanesco na Tanesco kutoka nje kuwaacha wabunge wajadili, Ngeleja angeweza kuomba Tanesco warudi wamsaidie, lakini aliridhika na kukubali. Waandishi wakaandika kwamba Kamati imeikatalia Wizara kununua mitambo. Kamati ya Nishati haijakanusha kama ambavyo kamati ya Zitto haijakanusha, kwa sababu ambazo naomba nizianike kwamba wanasiasa ni waoga sana kubishana na vyombo vya habari. Kimsingi hakuna kamati iliyokataa wala kubariki ununuzi wa mitambo ya Dowans.

3. Tatizo kubwa ambalo sasa limeguswa kiaina na baadhi ya wahusika akiwamo Zitto na Dk. Mwakyembe ni tatizo la kisiasa. Zitto amenukuliwa akisema kuna siasa za makundi, Mwakyembe akasema anaona kama operesheni sangara inaendelea. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa linaweza kubadili mjadala kutoka katika hoja za msingi na kuanza kwa SIASA. Kubadilika kwa hoja kutoka tatizo na kwenda kuwa SIASA.

4. Lakini pamoja na kuwa hoja si ya kisiasa, msingi wake unaweza kuwa wa kisiasa zaidi na kwamba Zitto kama mwanasiasa angepaswa kuangalia pia upande wa hatima yake kisiasa zaidi badala ya kutaka kuwa MAKINI kutenda HAKI kwa kutaka kusikiliza pande zote husika. Hilo linahitaji mjadala pekee kwa kuwa Zitto amekuwa na hulka ya kusikiliza hata wale ambao watu hawapendi kuwasikiliza. Hiyo ni hulka nzuri lakini ni HATARI SANA.

Kwa maoni yangu:

Suala la Dowans asili yake ni hoja tete ya Richmond ambayo ilisababisha kuenguliwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha (ambaye yuko kimya sana). Kuanguka kwa Waziri Mkuu ni hatua nzito katika historia ya nchi hii na kulisababisha kuvunjika kwa Baraza zima la mawaziri. Zitto alilumbana na Spika kuhusu hilo na Rais Kikwete alithibitisha maneno ya Zitto kwa kutangaza kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri.

Tukio hilo lilirudisha imani ya umma kwa vyombo vyote vya dola ambavyo walikwisha kupoteza imani navyo na kuona kwamba sasa kumbe hakuna aliye juu ya sheria. Bunge, wabunge, serikali zilipata heshima ndani na nje ya nchi. Sakata la Richmond likawa mtaji mkubwa wa kisiasa kwa wanasiasa ndani ya Bunge na hata kwa Rais. Wapinzani nao waliona kama ushindi kwao. Nchi ilichangamka na masuala mengine kama EPA na kesi za kina Mramba yakafuatia mkondo.

Sasa hivi, yeyote ambaye anathubutu kutaka kubadili HADHI ya Bunge kwa kuhalalisha kwa mlango wa nyuma maovu yaliyotokana na Richmond, atakuwa anairudisha nchi nyuma (si wanasiasa).

Jambo la msingi ni kuzingatia mambo yote ya msingi, ikiwa ni pamoja na kuangalia kwamba Dowans tunawadai bilioni 23, Dowans wametushitaki lakini pia ni kweli kwamba tuna tatizo la UMEME sasa? na Je, ni dharura? Tumejua lini tatizo? Nani awajibike kwa hili? Je, Sheria inasemaje ikiwa mtu amedanganya wakati wa manunuzi? munaendelea kufanya naye biashara? Je, hakuna mitambo mengine hata kwa bei ya ziada kidogo? Tusiponunua Dowans watapeleka wapi mitambo yao? wakinunua wafanyabiashara wengine (hao hao) watamuuzia nani umeme ikiwa tutakuwa na mitambo mipya?

TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.
 
Hapana. Usikate tamaa na kukubali matokeo kirahisi hivyo. Rejea alichosema. Mpiganaji anaenda kuongeza uzamivu kwenye elimu. Analiachia jimbo lake kwa mpinzani. Mahesabu yake ni makali. Kati ya 2010 na 2015 anajijenga zaidi kitaaluma ili awe na uwezo wa kuchambua na kuhoji kila kitu kama Profesa wake Shivji. Kisha anarudi na gia mpya 2020.Sijui gia hiyo ya kuingilia itakuwaje ila inaweza ikawa chama kipya au muungano wa vyama. Huyo ndio Rais wako mtarajiwa. Jiandae kumpa kura yako ya ndiyo.
Temea chini..!!
 
Halisi,
maelezo yako poa sana. Ila mie nimemuuliza mara mbili Zitto atuelezee walau kwa juu juu hili swala ila kaamua kukaa kimya. Sasa unaweza kusoma kuwa waandishi wa habari wameandika vibaya maelezo ya kamati/Zitto. Ila ukisoma maelezo ya Mwakyembe na ukachanganya skendo za Rashid na kumalizia uhusiano wake na RA (TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.) hapo imani na Tanesco inaanza kwisha. Simple ni kuwa aliyeumwa na nyoka, akiona unyasi anashtuka. Wao ndiyo akina Mwanameka na sisi tumekuwa akina Musa. Itabidi upinzani na CCM waje mbele ya waandishi wa habari na watupe habari kamili na ikibidi live kwenye TV sababu hasa zilizopelekea wao kununua hiyo mitambo. Kuna habari imeandikwa kuwa "Tanesco waliagizwa waende USA kuangalia bei na ghalama za mitambo mipya", Rashid hakufanya hivyo. Sasa aligoma ili asubiri kukiwa na shida ndiyo aseme kuwa "tununue mitambo ya Dowans?" Hii njia sasa imepitwa na wakati. Hela za uchaguzi wakatafute kwingine. Kwanza Rashid alete hela za Rada na kwenda Keko moja kwa moja. Kuna haja ya kuwa na Rais mwingine au Bunge lenye upinzani mkali ili kupunguza nguvu za rais.
 
Itabidi upinzani na CCM waje mbele ya waandishi wa habari na watupe habari kamili na ikibidi live kwenye TV sababu hasa zilizopelekea wao kununua hiyo mitambo..

Leo usiku saa 3.00 (EAT), MWakyembe, Zitto, Slaa watazungumzia Dowans katika ITV kipindi maalumu na baada ya siku chache kutakuwa na kipindi cha moja kwa moja kuhusiana na mjadala huo
 
Kuna habari kwamba Spika wa Bunge, Sam Sitta, amezungumza na waandishi wa habari na kuuponda mpango wa serikali kununua mitambo ya Dowans na kusema ni "WIZI MTUPU" .... Amekataa kuzikutanisha kamati za Zitto na ile ya Shelukindo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, anafanya Press Conference muda huu!!!!! pengine anatoa ufafanuzi kuhusu kauli ya kwamba Rais amesema hata sheria isizingatiwe kama ilivyochapishwa na gazeti la Mwananchi ambalo pia ndilo lilisema Zitto ataka mkitambo ya Dowans inunuliwe na Tanesco.

Tusubiri muda si mrefu::::::

Note: Wakati mitambo ya Richmond inawasili pale uwanja wa ndege wa Dar, Salva kupitia kampuni yake ya G&S alikuwa ndiye PRO wa Richmond
 
Last edited by a moderator:
Sawa sawa kabisa mkuu Halisi tumekusoma, muda si mrefu itajulikana mbivu na mbichi tu!
 
There's NO leadership in this country. Kila mtu anajisemea kivyake vyake tu🙁
 
There's NO leadership in this country. Kila mtu anajisemea kivyake vyake tu🙁

Ilibidi Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Rais na kuifukuza kazi serikali yake yote na kufanya uchaguzi baada ya miezi mitatu badala ya kusubiri 2010 lakini Bunge lenyewe nalo hovyoooooo na katiba hovyoooo maskini Tanzania nchi inayumba vibaya sana. 🙁🙁
 
Jamani ununuzi wa dowans ndo campaign funds...acheni serikali inunue mitambo!! kidumu chama cha kijani!!
 

Zitto ndugu yetu,

mark your steps na sikiliza kilio cha watanzania.

Machozi yao yasije yakakuzamisha kwa kuwatetea (kwa kujua au kutokujua) maslahi ya kikundi cha mafisadi wachache.It takes a million years to build one's reputation but it just takes a second to annihilate the same...

Take care brother...
 
Sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 husomwa pamoja na kanuni zake, hii ina maana GN. No. 97 (THE PUBLIC PROCUREMENT (GOODS, WORKS,NON-CONSULTANT SERVICES AND DISPOSAL OF PUBLIC ASSETS BY TENDER) REGULATIONS, 2005; ni sehemu ya sheria hiyo kwa kuwa zimetengenezwa chini ya sheria husika na kutangazwa katika gazeti la serikali.

Kwenye kanuni hiyo hapo juu sehemu ya IV kifungu cha 58 (1)-(6), nina vinukuu hapa chini:

"58.-(1) For the purposes of these Regulations, “motor vehicles and heavy plant” include both fixed and movable plant such as engines, boilers, lories, motor cars, motor cycles,
tractors, road rollers, motor graders, etc.

(2) The ministry responsible for matters related to electrical, machinery and mechanical engineering shall prepare detailed and acceptable schedule of requirements and specifications which shall be made available to the Authority for use by the procuring entities when procuring for such items.

(3) Motor vehicles, heavy plant and spare parts to be purchased shall be brand new

(4) The Secretary to the Cabinet may, on the direction of the Cabinet and on the advise of the ministry responsible for matters related to electrical, machinery and mechanical engineering, determine the type, make and size of motor vehicles or other motorised equipment to be procured for official use of specified state officials or other senior government officer. After that determination, the Secretary to the Cabinet shall issue a circular specifying the type, make or
size of the preferred vehicles for that purpose.

(5) The preferred motor vehicles or other motorised equipment as determined under sub-regulation (4) of this Regulation, shall be procured either directly from the manufacturer of the said motor vehicles or through competitive quotations from reputable authorised local and international
suppliers or dealers of the specified vehicles.

(6) The procurement shall require the prior written approval of the tender board."

....................Well, tuendelee kujadili.

Mh Zitto na wana JF,

..Naomba kujua....Je wakati TANESCO wana-BID kununua hiyo mitambo ya DOWANS......je walizingatia hicho kipengele No.& 5? (leave alone No3) au wali-secure Waiver kutoka kwa Waziri/Bodi ya Zabuni ili kununua direct from DOWANS?.......
 
Back
Top Bottom