Kwa muda nimekuwa msomaji wa mjadala huu,
Naona kuna haja nami kujaribu kuweka mawazo ya kwanagu kwani kama mwana JF nina kila sababu ya kuchangia.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2006 taifa liliingia mikataba mikubwa ya kukodisha mitambo kwa ajili ya kuzalisha umeme wa dharura kutokana na matatizo ya ukame ambayo inasemekana ulikumba taifa.
Mikataba ya kukodisha mitambo hiyo na gaharama zake ilikuwa kama ifuatavyo,
1.Mkataba na Richmond ambao walikuwa na mitambo ya kuzalisha 100MW ambayo inatumia gasi na Taifa tuliwalipa Dola milioni 88,700,000.
2.Mkataba na Aggreko ambao walikuwa na mitambo ya kuzalisha 40MW ,ambao tuliwalipa Dola milioni 61,000,000.
3.Mkataba na Alston Power Rentals ambao walikuwa na mitambo ya kuzalisha 40MW iliyokuwa inatumia diseli ,tuliwalipa Dola milioni 21,000,000.
4.Mkataba na Wartisila ambao walikuwa na uwezo wa kuzalisha 100MW ,tuliwalipa Euro milioni 57,550,000 .
Mikataba yote hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuweza kupata mitambo ya kukodisha na sio kununua mitambo.
Ilipofika mwaka 2008 tulifuta mikataba hiyo na wakati tayari tulishaingia kwenye gharama kubwa kiasi hicho , na kiasi cha fedha ambacho nimekitaja hapo ni kile ambacho kulikuwa kwenye mikataba , sasa walilipwa kiasi gani sijui.
Suala la kununua mitambo , kwa sasa pamoja na ukweli kuwa limechukua sura tofauti na kuwa la kisiasa na kushambuliana zaidi , ila kuna ukweli ambao haupingiki nao ni kuwa ni lazima sasa tuwekeze kununua mitambo ya kuzalisha umeme na sio kusubiri kisha tuje kuanza kukodisha mitambo ambayo inatupotezea mabilioni ya pesa kiasi hicho kama nilivyoonyesha hapo juu kuwa 2006 tulipoteza kiasi gani cha pesa.
Nafikiri mjadala uwe tununue mitambo ama tusubiri mpaka janga likitufika basi tuanze kutafuta mitambo ya kukodisha kama tulivyozoea.
Kamati ya Nishati na Madini inapaswa kutuambia kuwa tunapaswa kununua mitambo ama tunapaswa kusubiri yatufike ndipo tuanze kukodisha?
Mwaka 2006 wakati tunaenda kukodisha mitambo hiyo uchumi wa taifa uliporomoka kwa asilimia 2 sasa je?ni kipi cha muhimu kwa sasa?
Nafikiri kuwa ni muhimu sheria za nchi zikafuatwa na kuzingatiwa katika maamuzi yeyote yale ambayo tunataka kufanya ama kununua au kukodisha .
Mjadala mwema .