Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Mungu wangu mwakiembe anamponda Zitto kuwa maslahi gani ya taifa wakati alichukua mpaka na POSHO!!!!!!!
 
Siku waliokutana alikuwepo na waziri na waligundua kuwa bodi ya tanesco walikataa huu mpango.
 
Anashangaa tanesco wanatumia pesa zote hizi badala ya kugawa hata kwa wafanyakazi wakale lunch. Amekwepa kutaja mmiliki wa dowans/richmond lakini anasema kuwa anashangaa anapelekwa mtu mwingine wakati mmiliki anaachwa
 
Anakwepa sana mmliki wa dowans, anamsukumizia kamati ya zitto.anashangaa matangazo ya tanesco eti wabadili sheria. Anasema kuwa watawajibisha watu hapa kwa kuwa watu hawana vision. Anasema dowans wanawasemaji ndani ya tanesco, serikali na atakula nao na anasema kuwa mfanyabiashara ana pesa anatumia hili, anasema kuwa hapa ni ufisadi tu hakuna hata dharura yeyote hapa.
 
Anasema kuwa afadhali tuwe na giza kwani tutabadilika? Tuliambiwa tule majani tumebadilika? Na amesema kuwa kukiwa na giza watu wajiandaaa kuwajibika. Mbona wakinununua gari la mkurugenzi hawaombi kwa kamati? Anaesema kuwa hakuna cha maslahi ya taifa wala nini ila ni mtu binafsi.
 
Inatia moyo sana kuona asilimia kubwa ya wana JF wamesimama kidete katika kusimamia maslahi ya Taifa kwa kuonyesha hasara kubwa ambazo haziambatani na faida hata kidogo katika suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans. Inatia aibu sana kuona wale watu ambao tuliamini kuwa ni wakombozi wa kweli wa nchi yetu wakighafilishwa na chembe chembe za sukari ya Ufisadi na kuishia kuunga mkono Mafisadi kwenye hili suala.

Kama Rostam anataka kuendelea kuitumia mitambo yake kuzalishia umeme basi aende akaifunge nyumbani kwake na kwa wapambe wake wote pale Bongo.

Watanzania tumechoka na huu upumbavu wa kuifisadi nchi kila kukicha. Wananchi hatuoni maendeleo yoyote ya maana lakini mafisadi wanashindana kwa kuwa mabilionea kwa ufisadi nani ana nyumba kubwa na nzuri kuliko mwingine. Nani ana nyumba nyingi katka nchi za kigeni (UK, UAE, RSA an kwingineko) nani anaendesha gari la bei mbaya lilitoka hivi karibuni. Upumbavu huu unaoangamiza nchi yetu lazima tuukatae kwa nguvu zetu zote. Hatuwezi tena kukaa pembeni na kuangalia nchi ikizidi kuangamia.
 
Anasema kuwa waliwashauri kuwa wasinunue ila hawajawazuia ila wanunue tu watakutana huko mbele. Anasema kuwa dhana ya shamba la bibi ilimeisha. Anasema kuwa maneno ya zitto yamekanwa na wabunge wenzake wa kamati na hii ni siasa zake za sangara. Hakuna na cha kukutana. Anasema kuwa linalotokea sasa ni ukiukwaji wa sheria na anasikitika sana kuona akina zitto kuingia kwenye malumbano haya.

Anasema kama tanesco wana hoja wanunue mitambo ila...... Amemalia...


Karibuni chakula
 
Date::3/4/2009
Spika atoa tahadhari serikalini kuwa Richmond,Dowans ni binamu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta

Na Exuper Kachenje
Mwananchi

SAKATA la ununuzi wa mitambo ya ufuaji umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited, jana lilimgusa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta na kuamua kutoa tamko kali la kuitahadharisha serikali dhidi ya azma yake ya kutaka kuinunua mitambo hiyo yenye utata.

Spika Sitta pia ameonya kuwa mkasa wa kampuni tata ya Richmond Development (RDC) LLC uliotikisa kiasi cha kusababisha Edward Lowassa awajibike kwa kujizulu wadhifa wake wa waziri mkuu, lisifufuliwe upya kwa kutumia Dowans, ambayo ilirithishwa mkataba wa miaka miwili wa kufua umeme wa dharura.

Richmond ilishinda zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa njia iliyojaa utata kabla ya matatizo ya usajili wake kuzua maswali mengi na kusababisha Dowans warithishwe mkataba huo mwaka 2006.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Sitta alieleza nafasi ya Bunge katika kuisimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akitaka ushauri wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wa kuizuia serikali isinunue mitambo hiyo uheshimiwe.

Sitta pia alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma haikustahili kufuatwa katika kutaka ushauri kuhusu suala hilo kwa kuwa suala hilo lipo kwenye Kamati ya Nishati na Madini na kwamba kama kuna sababu mbadala, wasi ililazimika kuliwasilisha upya kwa kamati hiyo.

"Naitahadharisha serikali juu ya athari zinazoweza kujitokeza iwapo itaamua kuendelea na mchakato wa ununuzi wa mitambo ya Dowans kwa kupuuza ushauri uliotolewa na Kamati ya Nishati na Madini," alisema Spika Sitta.

Alisema: "Isisahaulike kwamba Dowans ni kampuni iliyopatikana kwa kurithishwa mradi na kampuni ya Richmond katika mazingira yenye utata ambao hadi leo ni kitendawili."

Spika Sitta alifafanua kuwa uhalali wa utaratibu wa Richmond kumkabidhi mradi Dowans ulitiliwa mashaka na kamati teule ya Bunge, na kuongeza kuwa Dowans na Richmond ni kama kitu kimoja.

"Dowans na Richmond ni mtu na binamu yake na si vigumu kukubali kuwa bado wao ni wabia hadi sasa: Pamoja na yote mkasa wa Richmond haufai kufufuliwaaa upya kupitia Dowans," alisisitiza Sitta.

Aliongeza kuwa kama kweli Tanesco na serikali inazo Dola 69 milioni za Kimarekani (sawa na Sh90 bilioni za Kitanzania) ambazo ni bei ya mtambo wa Dowans, ingezitumia fedha hizo kama sehemu ya malipo ya kununua mitambo mipya. Alisema Tanesco ingetafuta ushauri kutoka Mamlaka ya Ununuzi Serikalini (PPRA) ili taratibu za dharula zitumike kununua mitambo mipya kukabiliana na "dharula inayotabiriwa".

Sitta alihoji mantiki itakayotumiwa na Tanesco kutaka kununua mitambo ambayo inamilikiwa na kampuni ambayo imeishtaki kwenye Baraza la Usuluhishi ambalo makao yake makuu yako Paris, Ufaransa.

"Gharama za mitambo na gharama za kuikodi haviwezi kuepukwa kuwa ni sehemu ya shauri lililo Paris," anasema Sitta. "NI kwa mantiki ipi kesi baina yao iendelee na hapo hapo mdaiwa (Tanesco) anunue mitambo kutoka kwa mdai (Dowans.


"Tanzania ilikuwa ikilipa Dowans shilingi za Kitanzania milioni 152 kwa siku (Dola 120,000) sawa na Dola 42 milioni kwa mwaka).

"Pamoja na yote, mkasa wa Richmond haufai kufufuliwa upya kupitia Dowans. Tanesco/serikali waelekeze nguvu zao katika njia mbadala za kulipatia taifa umeme wa dharura, badala ya njia hii ya Dowans iliyojaa utata."

Kuhusu mvutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma na ile ya Nishati na Madini, Spika Sitta amsema si sahihi kwa kamati yoyote ya Bunge isiyo ya sekta husika, kutoa maoni yake hadharani na kuishawishi jamii kwamba Bunge lina ushauri unaopingana kuhusu suala husika.

"Si sahihi kwa Kamati yoyote ya Bunge isiyo ya sekta kutoa maoni yake hadharani na kujenga taswira kwa umma kwamba, Bunge lina ushauri unaokinzana kuhusu suala lililo mbele yake. Kamati nyingine, haina budi kupitisha ushauri na maoni yake kwenye kamati ya kisekta," alisema Sitta.

Zitto Kabwe, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza msimamo wa kamati yake kuunga mkono Shirika la Umeme (Tanesco), kuinunua mitambo ya Dowans kwa maelezo kuwa hatua itasaidia kulinusuru taifa katika janga kubwa la kukosa umeme na kwamba sheria ya manunuzi si msahafu, hivyo inaweza kubadilishwa.

Lakini Kamati ya Nishati na Madini, ambayo mwenyekiti wake ni William Shelukindo, inapinga hatua hiyo ikieleza kuwa inakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma, inayokataza serikali kununua vitu ambavyo tayari vimetumika.

Alisema ushauri kwa serikali kuhusu Tanesco kununua au kutonunua mitambo ya Dowans ulikwishatolewa kwa Wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Desemba 14 mwaka uliopita.

"Huo ndiyo ushauri rasmi na sahihi wa Bunge ninaoutambua. Kwa msingi huo hoja ya kuzikutanisha Kamati hizi mbili (ya Nishati na Madini na ya Hesabu za Mashirika ya Umma) ili kurejea uamuzi au maoni yaliyokwishatolewa na Kamati inayohusika, haina msingi," alisema Sitta.


Alisema mkondo rasmi wa ushauri kwa serikali uliokusudiwa kwenye Ibara ya 63 (2) ya katiba ikisomwa na pamoja na kanuni za Bunge za mwaka 2007 ni kupiti Bunge zima au kamati zake za kisekta kila kamati na sekta yake.

Wakati Spika Sitta akibainisha msimamo wake na wa Bunge, mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ameunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo huku akisema kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa jana inaweza kukwamisha mchakato wa ununuzi wa mitambo hiyo.

Lipumba alisema katika mfumo wa utawala bora wakati kamati za bunge zinazohusika na mambo hayo na bodi za mashirika zipo, rais hapaswi kujiingiza mapema katika mijadala.

"Katika mfumo wa utawala bora ambao una kamati za bunge zinazohusika na sekta ya umeme na manunuzi, kwa rais kujiingiza kunaweza kuwa ni kikwazo cha mchakato mzima wa ununuzi wa mitambo," alisema Profesa Lipumba.

Alifafanua kuwa, sheria ya manunuzi ya Serikali ina upungufu kwa kuwa inalazimisha ununuzi wa mitambo mipya, jambo ambalo haliwezekani kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.

"Ununuzi wa mitambo ya kibiashara katika sekta ya biashara huwezi kulazimisha ununuzi wa mitambo mipya hususan katika nchi zinazoendelea kama ya kwetu. Jambo la msingi ni kuangalia uwezo wa mitambo katika kufanya kazi na si kwamba ni mipya au mikongwe," alifafanua Lipumba na kuongeza:

"Sheria yetu ya manunuzi ni nzuri na inafaa sana kwa kununua vitu vya huduma za serikali, kama magari na vifaa vingine."

Aliitaka Tanesco kuwa wazi kwa kuwa ni wao waliosema mitambo hiyo hawaitaki hivyo kuamuwa kuvunja mkataba na Dowans iweje leo wanageuka na kusema mitambo hiyo ni mizuri na kuitaka serikali iinunuwe.

"Tanesco walituambia kuwa mitambo hiyo hawaitaki na walivunja mkataba na Dowans, sasa inakuaje leo wanageuka na kusema kwamba mitambo hiyo ni mizuri na inunuliwe kwa ajili ya kuzalishia umeme? Tunahitaji uwazi zaidi kutoka Tanesco," alihoji Profesa Lipumba.


Naye Stephen Menad ambaye ni mshauri wa masuala ya nishati na mazingira, alisema hakuna kitu kipya kwenye mitambo hiyo ya Dowans hivyo isinunuliwe na badala yake itafutwe mipya ili kuondoa mvutano baina ya wananchi na serikali.

Mussa Hassan, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyabiashara, alisema ni aibu kwa serikali kula matapishi na kwamba viongozi wasisahau yaliyotokea wakati mitambo ya Richmond ilipokuja na mwisho wake kuwaweka pabaya viongozi waliokuwa serikalini.

Anthony Chambi, ambaye ni mfanyabiashara katikati ya jiji la Dar es Salaam, alisema hataki kusikia kuhusu mitambo hiyo kwa kuwa tayari ilishaiabisha serikali. Alisema anasikia kuna kesi Ufaransa kuhusu mitambo hiyo kitu kinachomshangaza kwa nini serikali inataka kununua mitambo ambayo ina kesi.
 
Patamu......maslahi ya taifa mbele.....

Tena sio posho tu ila amesema POSHO kubwa kubwa. Sijui kama ni kejeli ya kisiasa au la... Namwachia Zitto hapa. Afadhali Slaa kajichanganya japo sikumpata vizuri ila amesimama kwenye hoja yake ya wakutane wote ili kila kilichosemwa na upande mwingine kisikike. Hapa Zitto kaingizwa mjini ila ananjia naona yakutokea.
 
Date::3/4/2009
Zitto Kabwe, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza msimamo wa kamati yake kuunga mkono Shirika la Umeme (Tanesco), kuinunua mitambo ya Dowans kwa maelezo kuwa hatua itasaidia kulinusuru taifa katika janga kubwa la kukosa umeme na kwamba sheria ya manunuzi si msahafu, hivyo inaweza kubadilishwa.

Lakini Kamati ya Nishati na Madini, ambayo mwenyekiti wake ni William Shelukindo, inapinga hatua hiyo ikieleza kuwa inakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma, inayokataza serikali kununua vitu ambavyo tayari vimetumika.

Zitto, kama ulivyoambiwa sasa wewe ndio unayeonekana kutetea fisadi-deals. Hata Spika naye anapinga DOWANS.
 
Alaa! Baada ya kumsikiliza Sitta na Mwakyembe sasa nimeelewa kwa nini Slaa na Zitto wamenunua ajenda ya Dowans dhidi ya Shelukindo. Kumbe kweli hii ni Operesheni Sangara. Dili ni kufufua ishu ya Richmond bila kuinyanyulia bango Tanesiko ya 'Dakta wa Vijisenti' ili 'Vilongola' walioponea chupuchupu nao pia waingie kitanzini. Si unakumbuka aliyekuwa Waziri Mkubwa alisema nini wakati analalama kuwa 'amedhalilishwa sana' , 'amesononeshwa sana' na 'amefedheheshwa sana'? Alisema hivi: 'Put in on the table, who is Richmond', yaani, 'Iweke wazi mezani, Richmondi ni nani'? Operesheni Sangara ya Dowans-Richmond ya Zitto-Slaa ikifanikiwa basi ukweli wote utawekwa mezani. Hapo ndipo nchi itatikisika hasa. Ole wetu. Namalizia kwa nukuu hii ya Mwalimu Nyerere kutoka kwenye ukurasa wa 46 wa kitabu chake cha 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania':

"Narudia: Kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa, na Nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa. Maana watu wengine wananong'ona nong'ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa Nchi ni mkasa na balaa kwa Nchi yoyote ile. Ndiyo maana tunatakiwa kuwateua na kuwachagua Marais wetu kwa uangalifu mkubwa; na ndiyo maana wakishachaguliwa, wanatakiwa wajiheshimu na kuwa waangalifu sana" - JKN, 1994

Mwenye sikio na asikie Mwalimu anacholiambia Taifa. Mungu Ibariki Tanzania. Wabariki viongozi wake. Amina.
 
Last edited:
Sikujua kinacho endelea hapa.kumbe kukutana na kamati inabidi kutoa posho?ZITO HEBU JIBU HILI KABLA HUJA POTEZA UELEKEO JUMLA.
Kama tangu mwezi AGOST mwaka jana,tulisha vunja mkataba na DOWANS na AGGREKO mwezi 12 mwaka jana na hatujawa gizani iweje dharura hiyo haiku tangazwa ili mchakato ufanyike wakupata umeme mapema?au ndo jamaa walikuwa kwenye mchakato wa kubuni namna ya kuibia tena serikali yetu tajiri yenye viongozi masikini wa sera za maendeleo.
Ningefurahi leo KAMA CHUWA angewakutanisha Zitto na Mwakyembe baada ya spika 'kushindwa'
 
Why govt doesn`t need to buy Dowans turbines



THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE state-run Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) has continued to come under scathing attack for its dubious plan to buy used power generation turbines from the controversial Dowans Tanzania Limited company.

Industry experts say the move is ’ill-advised’ because the government can always buy similar � but brand-new - turbines directly from a number of reputable manufacturers at a fraction of the would-be cost of buying the used Dowans power plant in Dar es Salaam.

Some of the well-known suppliers of power generation sets to different governments around the world include Wartsila, Aggreko, General Electric, and Kawasaki Gas Turbines, to name but a few.

It has also been learnt that a Tanzanian delegation actually visited the Kawasaki Gas Turbines company in the United States towards the end of 2007 to establish first-hand the true cost of such turbines.

Based on presentations made by the US company, the government would be be able to purchase 100MW power generation turbines for a cost of just $42m (approx. 58bn/-), plus shipping costs.

But surprisingly, TANESCO is pushing to buy the used Dowans machinery at an estimated cost of at least $60m (approx. 84bn/-).

Promoters of the dubious deal have also been claiming that it would cost up to $90m (approx. 126bn/-) to import similar 100MW power turbines.

According to one informed government source who preferred not to be named: ’’If you do the maths, you will see that TANESCO wants to spend close to 30bn/- more on buying the used power turbines from Dowans, than it would actually spend if it opted to buy brand-new generators directly from manufacturers and without using middlemen.’’

The source continued: ’’This whole deal smacks of corruption...Why is TANESCO pushing for this ill-advised purchase of the Dowans machinery, apparently with the help of some very vocal politicians?’’

Apart from the fact that the move being vigorously pursued by TANESCO and the Ministry of Energy and Minerals to buy the Dowans plant would amount to a contravention of the current procurement law, experts now say the plan does not make financial sense.

’’The higher-ups at TANESCO and its parent ministry are not exercising sound financial judgment in relentlessly pushing for this Dowans deal,’’ said another industry source.

It has been alleged that the power turbines at the Dowans plant in Ubungo, Dar es Salaam were refurbished and not brand-new when initially installed.

’’The Dowans turbines are at least 20 years old, and were simply overhauled before being set up at Ubungo. It would be scandalous for the government to buy such machinery,’’ said the source.

The issue has generated much public debate countrywide, even leading to a high-profile clash of opinions between notable local politicians.

Over the weekend, the vice-chairman of the parliamentary committee for energy and minerals, Dr Harrison Mwakyembe, openly expressed doubts over the sincerity of the latest TANESCO bid to justify a government purchase of the Dowans turbines.

The bid came in the form of a public statement from TANESCO Managing Director Dr Idris Rashidi, who said the speedy purchase of the Dowans plant was crucial to curb a looming possibility of available power demand in the country outstripping supply in the short-term future.

The TANESCO boss said peak time demand for power currently stands at 787 MW, while only 595 MW is actually available on the national power grid, with a forecast of demand rising to 1,331 MW by 2014.

He asserted that the state-run power utility needs to add at least 105 MW to the national grid each year to keep up with this rising demand.

Rashidi’s statement came in the wake of an ominous increase in extended power blackouts at odd hours in Dar es Salaam and other parts of the country, a phenomenon which in itself has yet to be properly explained by TANESCO.

However, Dr Mwakyembe retorted that the statement appeared little more than ’’a trick being played by the TANESCO management to hoodwink everybody.’’

He said the TANESCO boss seemed engaged in an attempt to skirt around the fact that both the TANESCO board of directors and the Bunge energy and minerals committee have already vetoed the idea of buying the Dowans machinery, as well as the reality that such a deal is prohibited under the current national procurement law.

Dr Mwakyembe is the legislator for Kyela Constituency on a ruling CCM ticket.
 
...MWAKYEMBE PALE KAPIGA SIASA kwa kiwango kikubwa ..ni utoto kuongelea hoja ya posho ya vikao vya bodi au kamati....kwani kwenye serikali yoyote hakuna kikao kisichokuwa na posho....kabla ya mwakyembe kusema kamati ya hesabu walipewa posho[si rushwa]....angesema kuwa wao kama kamati ya nishati walikataa posho ya kikao....mwakyembe ni msomi sikupenda alivyobadili hoja kuifanya ya kisiasa perse...kwa hoja nyepesi.,mimi nilitaka alete fact za upande wake.....lazima tufikie mahali tubishane kwa hoja...

My insight ni kuwa kuna kitu kinaendelea ccm,maana naona na sitta kashaingia kuitahadharisha serikali ya kikwete isidhubutu kununua mashine zile....kuna uwezekano mkubwa hapa kuwa siasa za makundi zinavuma hapo......ni wazi kama waziri wa kikwete anataka mashine zinunuliwe atakuwa anajuwa rais anafikiria nini...na anaamini muelekeo wake....sasa kwa kuwa siasa imeshaingia ....tutaendelea na malumbano hadi giza lije....hapo kambi ya kina sitta na mwakyembe watamuachia kikwete na timu yake wahangaike...na safari hii hili zigo litawaangusha maana wote ni waoga kuchukua uamuzi kuanzia kikwete,pinda,shein[wala haongeleagi],ngeleja ...du mgao uliopita aliikimbia kabisa dar......na CHADEMA wanalijuwa hili wanasubiri.....wagombane wenyewe!!!
 
...MWAKYEMBE PALE KAPIGA SIASA kwa kiwango kikubwa ..ni utoto kuongelea hoja ya posho ya vikao vya bodi au kamati....kwani kwenye serikali yoyote hakuna kikao kisichokuwa na posho....kabla ya mwakyembe kusema kamati ya hesabu walipewa posho[si rushwa]....angesema kuwa wao kama kamati ya nishati walikataa posho ya kikao....mwakyembe ni msomi sikupenda alivyobadili hoja kuifanya ya kisiasa perse...kwa hoja nyepesi.,mimi nilitaka alete fact za upande wake.....lazima tufikie mahali tubishane kwa hoja...

My insight ni kuwa kuna kitu kinaendelea ccm,maana naona na sitta kashaingia kuitahadharisha serikali ya kikwete isidhubutu kununua mashine zile....kuna uwezekano mkubwa hapa kuwa siasa za makundi zinavuma hapo......ni wazi kama waziri wa kikwete anataka mashine zinunuliwe atakuwa anajuwa rais anafikiria nini...na anaamini muelekeo wake....sasa kwa kuwa siasa imeshaingia ....tutaendelea na malumbano hadi giza lije....hapo kambi ya kina sitta na mwakyembe watamuachia kikwete na timu yake wahangaike...na safari hii hili zigo litawaangusha maana wote ni waoga kuchukua uamuzi kuanzia kikwete,pinda,shein[wala haongeleagi],ngeleja ...du mgao uliopita aliikimbia kabisa dar......na CHADEMA wanalijuwa hili wanasubiri.....wagombane wenyewe!!!

Mjadala umeisha?
 
Back
Top Bottom