Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

lakini kama kweli tunawadai dowans bilioni 10 .....hawajalipa ..na kama serikali inakosa bilioni 58 za kodi...basi tuikamate na kuitaifisha hiyo mashine ya dowans ...TRA nao walishaukamata mtambo wa AGREKO wanawadai kodi......si pesa zetu jamani....!!!...economy of scales...
 
Mjadala umeisha?

umeisha kwa kumaliza na baba yao sitta kwenye taarifa ya habari ...ameongea copy and paste ya mwakyembe...si wako kambi moja????....hakiya mungu wanamtega kikwete wote hawa kina mwakyembe na sitta et al upande huu...na upande huu CHADEMA wanapuliza puliza halafu baaadaye haoooooo wanajiweka kando wanawaachia moto wao...

patamu hapo ..tuingie mmwaka 2010 na giza tororo.....hakuna anayemtakia kikwete jema kati yao........maaana nasikia arusha na mwanza tayari wanakula mgawo....na hapo hapo utafiti uliotolewa leo kule singida unasema asilimia 98 % ya wakaazi wa vijijini tanzania hawana umeme....
 
sasa kama 98% hawana umeme hiyo dharura ya Downs inatokea wapi? itapunguza asilimia ngapi kutoka 98%.

Ndugu yangu achana na DOWNS wacha tukae GIZA ndio tutatia akili.
 
lakini kama kweli tunawadai dowans bilioni 10 .....hawajalipa ..na kama serikali inakosa bilioni 58 za kodi...basi tuikamate na kuitaifisha hiyo mashine ya dowans ...TRA nao walishaukamata mtambo wa AGREKO wanawadai kodi......si pesa zetu jamani....!!!...economy of scales...

Gazeti la Raia Mwema liliandika wiki chache zilizopita kwamba Richmond/Dowans inadaiwa na Serikali/TANESCO kiasi cha shilingi 23 billioni na kama sikosei TANESCO walifungua kesi juu ya hili deni. Cha kushangaza katika kupigia debe ununuzi wa mitambo hiyo hili deni la 23 billioni halizungumziwi kabisa, labda Dowans wamecheza ndiyo maana hilo deni halitajwi kabisa katika hichi kizungumkuti.
 
....dowans walilipwa na serikali kwa siri dola milioni 30 advance !!!pia wanadaiwa dola milioni 2..kwa kuchelewesha kuzalisha umeme....kwa hiyo tunawadai dowans ..hata kama hatutanunua mitambo itabidi tuangalie namna watakavotulipa au tutaifishe mitambo....tuwalipe difference ya deni na bei ya soko ya mitambo hiyo....
 
Alaa! Baada ya kumsikiliza Sitta na Mwakyembe sasa nimeelewa kwa nini Slaa na Zitto wamenunua ajenda ya Dowans dhidi ya Shelukindo. Kumbe kweli hii ni Operesheni Sangara. Dili ni kufufua ishu ya Richmond bila kuinyanyulia bango Tanesiko ya 'Dakta wa Vijisenti' ili 'Vilongola' walioponea chupuchupu nao pia waingie kitanzini. Si unakumbuka aliyekuwa Waziri Mkubwa alisema nini wakati analalama kuwa 'amedhalilishwa sana' , 'amesononeshwa sana' na 'amefedheheshwa sana'? Alisema hivi: 'Put in on the table, who is Richmond', yaani, 'Iweke wazi mezani, Richmondi ni nani'? Operesheni Sangara ya Dowans-Richmond ya Zitto-Slaa ikifanikiwa basi ukweli wote utawekwa mezani. Hapo ndipo nchi itatikisika hasa. Ole wetu. Namalizia kwa nukuu hii ya Mwalimu Nyerere kutoka kwenye ukurasa wa 46 wa kitabu chake cha 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania':

"Narudia: Kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa, na Nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa Nchi bila kuitikisa Nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa. Maana watu wengine wananong'ona nong'ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa Nchi ni mkasa na balaa kwa Nchi yoyote ile. Ndiyo maana tunatakiwa kuwateua na kuwachagua Marais wetu kwa uangalifu mkubwa; na ndiyo maana wakishachaguliwa, wanatakiwa wajiheshimu na kuwa waangalifu sana" - JKN, 1994

Mwenye sikio na asikie Mwalimu anacholiambia Taifa. Mungu Ibariki Tanzania. Wabariki viongozi wake. Amina.

Asante Companero kwa kuangalia upande mwingine wa shilingi - I wish this was the case. Ukweli ni kuwa haiingii akilini kwa Zitto tunayemfahamu avalie njuga swala hili akiungwa mkono japo kwa mbali na Dr. Slaa. Kama kweli ni operation sangara ndio iko kazini basi nitawavulia kofia - naona na Lipumba naye keshajitosa humo. Ninachojua kwa asilimia 99% ni kuwa Richmond ilikuwa na bonge la mkono nyuma yake - hata Dr. Msabaha alisita kuwa Bangusilo, it makes sense. Challenging them at their own game ? Well that's brilliance at its very best. Mimi nitakuwa wa kwanza ku swallow my pride and admit I overreacted. Let's keep out fingers crossed - the world is full of surprises !!
 
PM hakuna kitu kuhusu ZITTO, ameshaingia mkenge na mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.

Zitto tulikuwa naye hapa for almost 4 days tukimpa mambo ya jikoni na mikorogo itakayotokea, lakini katupuuza na kututukana.

Sasa kweli ukimpa hayo mahojiano mtu ambaye hajui Tanzania, ukamuambia guess yupi ni kutoka chama cha upinzani, si atapick Dr. mwakyembe??

Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.

Halafu Mh. Zitto usipende kuchanganya mambo kwa kumention tu vitu unavyoambiwa eti serikali inakosa bilioni 58 watu wa migodi kwenye mafuta wanayotumia kwenye private generator zao, je kisa ni sababu hatujanunua mitambo ya Dowans au kisa ni misamaha ya kijinga serikali inayotoa na jie bunge kuridhia??? Unafikiri hata kukiwa na umeme, watu wa migodi watatupa generator zao au watatumia hiyo loophole ya tax refund kwenye mafuta ya hizo generator??? Give me a break!!!
 
huu mchezo bado mbichi...nia za kina zitto na mwakyembe ni tofauti na wote ...mwisho wake hautabiriki..ila itabidi serikali ya kikwete itafute njia muafaka kivyake ..tena inayofuata utaratibu ili tusiingie gizani....akinunua mitambo kina mwakyembe wanampiga bao...tukiingia gizani ..CHADEMA wanapiga bao...

kwa kifupi kwa kikwete ugali moto ...mboga moto!!!!

subiri utakuja kuniambia..
 
Njia muafaka ni kuachana na kutumia pesa za umma kununua mitambo kwa ajili ya umeme wa dharura. Tanesco isikubali kununua umeme toka kwa kampuni binafsi kama Dowans etc., na badala yake mwenye uwezo wa kufua umeme aruhusiwe kutumia transmission lines za Tanesco kwa kulipia. Kama vile huku Marekani, unakuta sehemu unayoishi kuna kampuni za umeme zaidi ya mbili, zinatumia the same transmission lines .... wanalipia kwa owners wa hizo lines.

Serikali inabidi ipeleke resources zake kwenye long-term power plan ... kama Stiegler's gorge!
 
Mwakyembe kachemsha sana....na hasa pale anapozungumzia "operation Snagara" na pia kuhusu "Posho"........sikutegemea hii toka kwake.......nilitgemea angetuchambulia vipengele vya sheria za manunuzi (yeye akiwa mwanasheria) pamoja na kutupa facts zengine ambazo wananchi hatuzijui kuhusiana hii saga........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!
 
mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.

Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.

Teh Teh Teh

Umesahau kuwataja kina Shelukindo, Nape...na wengine wengi watakuja soon...

omarilyas
 
Mwakyembe kachemsha sana....na hasa pale anapozungumzia "operation Snagara" na pia kuhusu "Posho"........sikutegemea hii toka kwake.......nilitgemea angetuchambulia vipengele vya sheria za manunuzi (yeye akiwa mwanasheria) pamoja na kutupa facts zengine ambazo wananchi hatuzijui kuhusiana hii saga........leo hii katufanya MABWEGE.......damn!

Mwakyembe ni POLITICAL MERCENARY period....Kama hata JK anaogopa kumkaribisha jikoni ingawa umamluki wake ulisaidia kufanikiwa mipango kadhaa ya MTANDAO inashangaza kama kuna watu wanatamka kuwa tumwamini yeye kuliko Zitto.

Lazima tujue kuwa KAMATI YA SHELUKINDO inaogopa mtego wa Zitto kwani wanajua mjadala ukienda kwenye details wataumbuka na ile ripoti yao ambayo ingawa ilitusaidia kuondoa MZIZI WA UFISADI katika nafasi ya juu serikalini lakini ilikuwa ni ya kishabiki na kimafia ambayo haikufanya lolote kujua ukweli zaidi ya kuhakikisha wanafanikisha maslahi ya kisiasa ya kulinda uhalali wa CCM machoni mwa watanzania.

omarilyas
 
I have given a lot of thought about all the gaff that the fiery MP for Kigoma has had to endure over his stand on the controversial issue of Dowans turbines. After a lot of nerve racking soul-searching, I now feel differently over this thorny issue. Could this be an opportunity that leads to the bottom of the Richmond saga and unravels the mystery that surrounds the identity of its key ghost players ?

For the first time in history, it puts the executive branch on a collision course with the legislative body. I still remember with some degree of bitterness and misgiving the short-comings of the Mwakyembe report which left a lot to be desired. Daggers are now drawn and the truth like always stands a chance of raising its ugly head. Will the usual blatant disregard for the rule of law triumph over its enforcement ?
 
Nilimsikia Dr.Slaa akikinukuu kifungu cha 72(2) cha sheria ya manunuzi ya umma,lakini alipoulizwa followup question kuhusiana na kipengele hicho akakwepa....
Lakini Mwakyembe kasema very straight kuwa wao waliombwa maoni yao kuhusu ununuzi wa mitambo hiyo wakawaambia wasiinunue,period.Sasa kama wao wanaona ni sawa kuinunua au kutoinunua wafanye lolote ila iko siku watakuwa accountable kama watatumia njia zinazopingana na sheria ya manunuzi.Na nchi ikiingia gizani watawajibishwa kwa uzembe,kwani walikuwa na muda wa kutosha kununua mitambo mipya.
 
Mimi nimemsikiliza tena. Yeye kasema kuwa licha ya hali ya uzalishaji umeme kuwa nzuri etc, bado kuna upungufu wa kama 150 na huu ni lazima ujazwe. Hayo uliyoyasema kuwa hakuna ulazima kwa kweli sijayasikia. In fact anasisitiza kuwa mitambo hii ya Dowans inaweza kutuvusha hapo hivi sasa ili tusiingie gizani. Urgument kuwa nakisi hiyo imekuwepo siku zote haimaanishi kuwa iendelee kuwepo na isishughulikiwe kwa haraka.

My friend, unaandika kana kwamba Mwanakijiji amesha-delete yale mahojiano i.e. hatuwezi kuyarejea tena. Go back and listen again! Kutuvusha? Wenzako tuko gizani already and we are ready to wait for the lasting solution. Hii mambo ya kukurupuka hayasaidii. Lowasa alileta hayo mamitambo mabovu using the same justification - power crisis. Matokeo yake mitambo hata haikuzalisha umeme wenyewe. Then, bado kuna watu wanatetea ununuzi wa mitambo ileile. This is really a problem! Spika Sita anasema Dowans na Richmond ni binamu - they are one and the same thing! Na anaishangaa Serikali hata inafikiria kununua hiyo mitambo.
Yaani hata mtoto mdogo wa darasa la nne huwezi kumdanganya anunue hiyo mitambo - whether ni mipya au imetumika. Anayeuza haaminiki kwa sababu alishazulumu in the first place! Katika nchi ambazo ni makini, hiyo kampuni ingefungiwa moja kwa moja kufanya biashara na serikali (na ndani ya nchi husika). Na owners wangekuwa na kesi ya kujibu. What is your interest tk and Ngeleja and Rashid and Zitto? Are you Tanzanians?

Na Minister kwa kujua kwamba, he is talking nonsense, anamuomba Mwanakijiji amsaidie kuiweka vizuri (kufunika funika). Yaani ukimpatia "psychologist" hiyo tape, atakuambia nia ya Bw. Ngeleja (hata kama hana background ya hii issue) - personal interest. Kutokana na hayo mahojiano, huyu Bwana hastahili kuwa waziri. Anaonesha kuwa hajakomaa na hajiamini. He is so defensive rather than objective. And then, anasema yeye sio fisadi. Ana wasiwasi umeng'amua siri yake inayomfanya ateteee huu ujinga. God bless Tanzania!
 
lakini kama kweli tunawadai dowans bilioni 10 .....hawajalipa ..na kama serikali inakosa bilioni 58 za kodi...basi tuikamate na kuitaifisha hiyo mashine ya dowans ...tra nao walishaukamata mtambo wa agreko wanawadai kodi......si pesa zetu jamani....!!!...economy of scales...

nani akamate mitambo ya rostam aziz? Thubutu!
 
Spika Sitta amesema kuwa hatua ya TANESCO kunuia kununua mitambo ya DOWANS ni ufisadi mtupu na ni kinyume cha sheria. Na kama watang'ang'ania kuinunua basi bunge litachukua hatua muda ukifika. Pia amesema kuwa Zitto amekiuka kanuni za bunge kuweka maoni ya kamati yake wazi (kwa umma) badala ya kuishauri kamati ya Shelukindo. Sasa Zitto ataibuka na kusemaje?
 
zito kajimaliza mwenyewe, ila kibaya ni kwamba kaacha harufu mbaya sana chadema, hata harufu zinazopendwa na FISI zina afadhari. Kaua chama hivi hivi.
 
Kama maneno ya Mwakyembe juu ya Operation Sangara ni kweli, basi hapa niseme kitu kimoja kuwa "nilikuwa ninawa-under estimate" watu wa CHADEMA/Upunzani. Ninaweza sasa kulala usingizi mnono nikujua kuwa UPINZANI wameshakua kisiasa. Sikutegemea wawe wanafikiri mbali namna hiyo hasa ukichukulia boronga ya upinzani miaka ya nyuma.

Kama mmeanza kupanga mikakati ya mbali namna hiyo, nategemea hata mkija madarakani mtakuwa na mikakati kama hiyohiyo katika kuipeleka nchi mbele na kumaliza matatizo kadhaa ambayo kwa kweli mie yananikera sana.
1. Umeme - Hili swala liwe solved na ikibidi kwa miaka 10 ijayo tulisahau.
2. Maji safi mijini/kijijini. Hata kama yatakuwa ghali, lakini yawepo.
3. Maji machafu (sewages) kwenye miji mikubwa. Harufu mbaya zinafanya mtu ukilala basi asubuhi tumbo limejaaa gas. Hii ni aibu tena kwa jiji la Dar.
4. Usafiri mjini Dar es Salaam. Ikibidi zianze train/trams kama siyo kuanza kufikiri kujenga Metro kwa JIJI la Dar es Salaam.(always aim high).

Mengine kama shule, matibabu nk siku zote yatapanda na kushuka. Ila hayo ya juu mtu unaweza kusolve na kusahau kwa miaka kadhaa.

NB: Mikakati hiyo hata CCM walikuwa nayo, Sema tu ni ile ilikuwa ikiwapa 10-90%.
 
Back
Top Bottom