Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Ilibidi Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Rais na kuifukuza kazi serikali yake yote na kufanya uchaguzi baada ya miezi mitatu badala ya kusubiri 2010 lakini Bunge lenyewe nalo hovyoooooo na katiba hovyoooo maskini Tanzania nchi inayumba vibaya sana. 🙁🙁

Yeah...viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe....
 
Zitto I still plead with you...

By the way hivi Kikwete what's wrong with him?
 
]



TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.
[/QUOTE]
 
Kuna habari kwamba Spika wa Bunge, Sam Sitta, amezungumza na waandishi wa habari na kuuponda mpango wa serikali kununua mitambo ya Dowans na kusema ni "WIZI MTUPU" .... Amekataa kuzikutanisha kamati za Zitto na ile ya Shelukindo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, anafanya Press Conference muda huu!!!!! pengine anatoa ufafanuzi kuhusu kauli ya kwamba Rais amesema hata sheria isizingatiwe kama ilivyochapishwa na gazeti la Mwananchi ambalo pia ndilo lilisema Zitto ataka mkitambo ya Dowans inunuliwe na Tanesco.

Tusubiri muda si mrefu::::::

Note: Wakati mitambo ya Richmond inawasili pale uwanja wa ndege wa Dar, Salva kupitia kampuni yake ya G&S alikuwa ndiye PRO wa Richmond

Naomba kuuliza?

Hivi hii issue ya kununua au kutonunua kwa hiyo mitambo inaunganishwa na issue ya upungufu wa umeme... au tunajadili tukiwa tuna yetu vichwani vyetu...

Nchi hii bwana...
 
At at the end of the day, ni nafuu kuwa na upayukaji wa Sitta, kuliko ububu wa JK.
The guy is extremely politically suicidal, but most of his risky moves end up paying off.
 
Kuna habari kwamba Spika wa Bunge, Sam Sitta, amezungumza na waandishi wa habari na kuuponda mpango wa serikali kununua mitambo ya Dowans na kusema ni "WIZI MTUPU" .... Amekataa kuzikutanisha kamati za Zitto na ile ya Shelukindo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, anafanya Press Conference muda huu!!!!! pengine anatoa ufafanuzi kuhusu kauli ya kwamba Rais amesema hata sheria isizingatiwe kama ilivyochapishwa na gazeti la Mwananchi ambalo pia ndilo lilisema Zitto ataka mkitambo ya Dowans inunuliwe na Tanesco.

Tusubiri muda si mrefu::::::

Note: Wakati mitambo ya Richmond inawasili pale uwanja wa ndege wa Dar, Salva kupitia kampuni yake ya G&S alikuwa ndiye PRO wa Richmond

....kwa hiyo JK naye anataka mitambo ya DOWANS inunuliwe!!!!.....im confused.....!!
 
Hapana sijaandika barua kwa Waziri ili asupport kununua mitambo ya Dowans. Sina mamlaka ya kuingilia manunuzi ya Shirika. Shirika linapokuja kwenye Kamati yetu huwa linakuja na Bodi, ikiwakilishwa na Mwenyekiti wao wa Bodi.

Nilizungumza na Shelukindo. Nilizungumza na Mwambalaswa. Sikumpata Mwakyembe kwani huwa hapatikani kwa urahisi kwa simu na alikuwa Kahama na Mengi. Seleli sikumtafuta maana asuingeweza kusaidia. Stella Manyanya nilimtafuta.

I am always like that napokutana na suala tete. Ndio maana hata Kamati nilipoona ina sway kwa TANESCO nikasema hapana, hatuwezi kupingana na Kamati ya Nishati na Madini. Nikaatoa hoja ndani ya Kamati kwamba Kamati 2 zikutane. Wenzangu hawakutaka kukutana na kuanza kulobby kwa spika asikubali kukutana. Wakaanza kujibu kupitia press. Sikuwa na cha kufanya bali kundika barua kwa Waziri kutoa maoni ya kamati kwa majibu wa kanuni za Bunge.

I tried my level best and all documented. JF ninavyoijua itapata tu hizo documents. Walionihukumu wataona aibu tu! I am genuine, i am honest and as always i sub-ordinate my interests to those of the nation. Sijakurupuka. Wazee wanaogopa kuwa challenged na vijana.

Umesoma NIpashe la Leo? Bodi ya TANESCO ilitaka walipiwe wabunge 2 kwenda Texas kununua mitambo. Tumefikia hapo? Eti Shirika lilipie wabunge wa kamati ya Nishati na Madini, tena wawili kwenda kununua mitambo ya kuzalisha umeme. Ndio Tanzania mnayoitaka hiyo. Hata iwe miaka 1000 ukweli utadhihiri tu na tutapig mstari na kusema maslahi ya Taifa yalikuwa wapi katika hili.

Zitto, Unakuwa kama Masha? Kumuandikia Barua Rais na Waziri Mkuu barua ya maoni?
 
toleola29.jpg


tunaweza kukaa pembeni kunung'unika au kuamka na kuhamasika; tunaweza kuwa wachambuzi wa mambo wasiotaka kuchukua msimamo au tukachukua msimamo kuonesha uchambuzi wetu wa mambo. Tuna uchaguzi wa kukubali kluwa serikali ifanye ipendalo na sisi tubakie kulialia pembeni au kusimama na kunyosha mikono yetu kama maaskari wa usalama barabarani na kuiambia serikali "stop"!

Soma kijarida cha Cheche ili upate sababu za nyongeza kwanini ni suala la uzalendo, utaifa, utawala bora, na utawala wa sheria kuizuia Dowans kupata hata senti moja ya Watanzania.

Hadi hivi sasa hakuna mnunuzi mwingine yeyote ambaye yuko tayari kununua mitambo hiyo tangu tenda hiyo waitangaze karibu miezi minne iliyopita. Mnunuzi pekee ni Serikali. Serikali isiponunua Dowans watapata hasara kubwa kwani "kitawadodea".

Asante kwa wale wote ambao wamefanya kazi yao leo na matunda tumeanza kuyaona. Wale wengine ambao hawajatambua bado ni kwanini we have to stop this menace to our energy sector please read and distribute.

It is time to move from Criticism to Activism!!


Dowans must be stopped.
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Zito amekurupuka kwa hili suala la mitambo ya dowans, na sheria ya manunuzi haibadilishwi siku moja. kwa nini hawa jamaa wanaing'ang'ania sana hiyo mitambo. hata kama inafanya kazi, mwuuzaji ndiye huyo tumeshitakiana naye, na kwa kuwa ni second hand hatuihitaji kabisa. nafuu tununue mipya hata kama garama itakuwa kubwa. wasitudanganye na swala la kuingia gizani wamezoea kuongopa hao. Na suala la umeme kwetu litaendelea kuwa tatizo tu hata ikinunuliwa hiyo mitambo kwa sababu tunatumia hydropower na mvua zenyewe hazitabiliki. kazi kwelikweli.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makubaliano makuu yaliyofikiwa katika mkutano wa tathmini ya utendaji wa Serikali uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumanne, Machi 3, 2009 kati ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake:

(a) Kwamba sekta ya madini isimamiwe kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa wenye leseni za kutafuta na kuchimba madini wanazitumia kwa masharti yaliyoombewa, na kuwa wasiozitumia leseni hizo kwa kuzingatia masharti ya leseni hizo wanyang’nywe leseni hizo badala ya kuzitumia kuendesha ulanguzi tu.

(b) Kwamba zichukuliwe hatua za haraka kukomesha kabisa wizi wa mafuta ya transfoma ambao unasababisha hasara kubwa kwa taifa na kuruvuga mtandao wa kusambaza umeme kwa wananchi.

(c) Kwamba Kamishna wa Madini Nchini, kwa kutumia madaraka na mamlaka yake kisheria, achukue hatua mara moja kukomesha uchimbaji wa kokoto katika maeneo yasiyostahili, na hasa katika eneo la Kunduchi/Tegeta, Dar es Salaam ambako tayari Serikali ilikwishakupiga marufuku uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi ya wachimbaji wamerudi katika eneo hilo kuendesha uchimbaji.

(d) Kwamba ziongezwe juhudi katika uzalishaji wa umeme nchini kwa sababu programu ya taifa ya uzalishaji umeme bado iko nyuma na bado liko pengo kubwa kati ya mahitaji halisi ya umeme nchini na umeme unaozalishwa kwa sasa.

(e) Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza.

(f) Kwamba kasi iongezwe katika kuhakikisha kuwa maeneo yaliyoahidiwa umeme yanapatiwa umeme bila ucheleweshaji usiokuwa na sababu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Machi, 2009

Hivi kununua mitambo ya DOWANS ni uwekezaji mkubwa ?
 
Kwa Mh Zitto
Ninatumaini ungewashauri serikali pia kuacha kununua magari D.T. Dobie, Toyota Tanzania na badala yake kwenda kununua Autorec, Car Junction etc kwa ajili ya Value for money. Serikali ingekuwa imepata savings kubwa tu.

..........kwi kwi kwi kwi........wee Heri acha uchokozi bana......kwi kwi kwi
 
Hawa wamesha tugeuza sisi mandondocha siyo!! mimi natamani hao siku Fisadi mmoja apigwe mawe kama zamani enzi zile za .......
 
....kwa hiyo JK naye anataka mitambo ya DOWANS inunuliwe!!!!.....im confused.....!!

Ogah;

You are not aloneooooo; i am more than confused... Dhana halisi ya maendeleo inatanguliwa na misingi halisi ya discipline na si vinginevyo; sina hakika kwamba tusiponunua mitambo ya dowans hakutakuwa na vendors wengine mpaka kiama...

Hapo ndio wakenya walipotuacha... Tunapenda sana dawa za watoto kwasababu zina sukari, its a high time we swallow bitter pills to cure our inherent disease of "kama kawaida"

Nina imani sheria na taratibu za procurement si kikwazo cha uwekezaji mkubwa
 
Nimekuwa nikosoma na kufuatilia sehemu kubwa ya taarifa kuhusiana na kinachoitwa "kauli ya Zitto" kuhusiana na sakata la mitambo ya Dowans.

Tatizo nililoliona na ambalo wajumbe wengi wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma ambayo Zitto ni Mwenyekiti wake wanaliona. Tatizo lenyewe ni lile la taarifa za kwamba kamati imebariki/inashinikiza/inataka mitambo ya Dowans inunuliwe. Wajumbe wote akiwamo Zitto hawajasema LAZIMA mitambo ya Dowans inunuliwe.

Kabla ya kueleza maelezo ya wajumbe wengi wa kamati niliobahatika kuzungumza nao, niweke wazi kwamba Zitto ni Mwenyekiti (anayeongoza vikao) na kuwa Mwenyekiti (si Mwenyekiti Mtendaji) maana yake ni kufanya kazi kwa vikao na kauli zako zinazingatia vikao. Kama hivyo ndivyo tujadili KAMATI.

KAMATI ya POAC (Kamati ya Zitto) imefanya vikao vyake na katika kikao kimoja wapo walikutana na Tanesco katika kupitia hesabu za shirika hilo na kuangalia matatizo yao ya kifedha. Kama kawaida Tanesco ya Dk Rashid ikapenyeza kwa umakini mkubwa matatizo yake ya kifedha na tatizo la ongezeko la mahitaji ya umeme huku kukiwa na upungufu wa uzalishaji baada ya Dowans kutimuliwa na kadhalika.

Maelezo ya Tanesco yakawagusa wajumbe wa POAC na wakaona ni vyema wakapata maoni ya wenzao wa Kamati ya Nishati na Madini (ya kina Mwakyembe) na kwamba wakaweka wazi katika maazimio yao kwamba kuna umuhimu kwa Tanesco kusaidiwa na serikali katika kununua mitambo mipya hata ikibidi kununua ya Dowans kwa sharti la kuzingatia sheria. Ikiwamo sheria ya manunuzi ya 2004. Kwa makini kabisa kamati imesema, "haijabariki ununuzi wa mitambo ya Dowans" na kwamba kamati ya POAC wala ya Nishati na Madini hazina mamlaka ya kuidhinisha wala kuzuia manunuzi ya Tanesco.

Maelezo ya POAC hayajatofautiana na yale ya Kamati ya Nishati na Madini kwamba hata wao hawana mamlaka ya kuzuia manunuzi. Tofauti ya kamati hizi mbili ni kwamba ile ya POAC ilitaka kukaa pamoja na wenzao wa Nishati na Madini kujadiliana jinsi ya kuisaidia Tanesco kiushauri na ili wapate maelezo ya kuridhisha kuweza kuishauri serikali na ili kuzuia kutokea kwa matatizo yaliyotokea wakati wa Richmond. Suala la kununua au kutonunua ama kutaifisha mitambo ya Dowans lingekuja kujulikana baada ya kukaa pamoja.

Kuna matatizo makubwa matatu ambayo yamesababisha hali hii kufikia hatua ya kuanza kushambuliana na hata kuanza kuibuka kwa tuhuma dhidi ya wabunge husika akiwamo Zitto ambaye imefikia hata kutuhumiwa kuhongwa.

1. Tatizo la kwanza ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa na Zitto mwenyewe kujiamini kupita kiasi na kuwaamini waandishi wa habari kupita kiasi. Amezungumza nao na kwa bahati mbaya sana (kwa kujua ama kutojua) waandishi hao wamepotosha kabisa kauli ya Kamati (si ya Zitto) kwa kusema kwamba kamati imebariki/inataka Dowans inunuliwe. Kamati haikusema hivyo.

2. Tatizo lingine ni lile la kauli kwamba kamati ya Nishati na Madini haijawasikiliza Tanesco, nalo limetokana na tafsiri ya baadhi ya waandishi. Maelezo ya wajumbe wa Kamati na Nishati na Madini ni kwamba wamewasikiliza Tanesco kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, ambaye alifika katika kikao cha Desemba 14, 2008. Kawaida waziri akiona amezidiwa ndipo huwaita wataalamu wake (Tanesco) kujieleza. Ngeleja alipomaliza kuwasilisha mbele ya uongozi wa Tanesco na Tanesco kutoka nje kuwaacha wabunge wajadili, Ngeleja angeweza kuomba Tanesco warudi wamsaidie, lakini aliridhika na kukubali. Waandishi wakaandika kwamba Kamati imeikatalia Wizara kununua mitambo. Kamati ya Nishati haijakanusha kama ambavyo kamati ya Zitto haijakanusha, kwa sababu ambazo naomba nizianike kwamba wanasiasa ni waoga sana kubishana na vyombo vya habari. Kimsingi hakuna kamati iliyokataa wala kubariki ununuzi wa mitambo ya Dowans.

3. Tatizo kubwa ambalo sasa limeguswa kiaina na baadhi ya wahusika akiwamo Zitto na Dk. Mwakyembe ni tatizo la kisiasa. Zitto amenukuliwa akisema kuna siasa za makundi, Mwakyembe akasema anaona kama operesheni sangara inaendelea. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa linaweza kubadili mjadala kutoka katika hoja za msingi na kuanza kwa SIASA. Kubadilika kwa hoja kutoka tatizo na kwenda kuwa SIASA.

4. Lakini pamoja na kuwa hoja si ya kisiasa, msingi wake unaweza kuwa wa kisiasa zaidi na kwamba Zitto kama mwanasiasa angepaswa kuangalia pia upande wa hatima yake kisiasa zaidi badala ya kutaka kuwa MAKINI kutenda HAKI kwa kutaka kusikiliza pande zote husika. Hilo linahitaji mjadala pekee kwa kuwa Zitto amekuwa na hulka ya kusikiliza hata wale ambao watu hawapendi kuwasikiliza. Hiyo ni hulka nzuri lakini ni HATARI SANA.

Kwa maoni yangu:

Suala la Dowans asili yake ni hoja tete ya Richmond ambayo ilisababisha kuenguliwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha (ambaye yuko kimya sana). Kuanguka kwa Waziri Mkuu ni hatua nzito katika historia ya nchi hii na kulisababisha kuvunjika kwa Baraza zima la mawaziri. Zitto alilumbana na Spika kuhusu hilo na Rais Kikwete alithibitisha maneno ya Zitto kwa kutangaza kuvunjika kwa Baraza la Mawaziri.

Tukio hilo lilirudisha imani ya umma kwa vyombo vyote vya dola ambavyo walikwisha kupoteza imani navyo na kuona kwamba sasa kumbe hakuna aliye juu ya sheria. Bunge, wabunge, serikali zilipata heshima ndani na nje ya nchi. Sakata la Richmond likawa mtaji mkubwa wa kisiasa kwa wanasiasa ndani ya Bunge na hata kwa Rais. Wapinzani nao waliona kama ushindi kwao. Nchi ilichangamka na masuala mengine kama EPA na kesi za kina Mramba yakafuatia mkondo.

Sasa hivi, yeyote ambaye anathubutu kutaka kubadili HADHI ya Bunge kwa kuhalalisha kwa mlango wa nyuma maovu yaliyotokana na Richmond, atakuwa anairudisha nchi nyuma (si wanasiasa).

Jambo la msingi ni kuzingatia mambo yote ya msingi, ikiwa ni pamoja na kuangalia kwamba Dowans tunawadai bilioni 23, Dowans wametushitaki lakini pia ni kweli kwamba tuna tatizo la UMEME sasa? na Je, ni dharura? Tumejua lini tatizo? Nani awajibike kwa hili? Je, Sheria inasemaje ikiwa mtu amedanganya wakati wa manunuzi? munaendelea kufanya naye biashara? Je, hakuna mitambo mengine hata kwa bei ya ziada kidogo? Tusiponunua Dowans watapeleka wapi mitambo yao? wakinunua wafanyabiashara wengine (hao hao) watamuuzia nani umeme ikiwa tutakuwa na mitambo mipya?

TUZINGATIE: Rostam anamiliki 35% ya Vodacom, Dk. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Vodacom, Ngeleja alikuwa mtumishi wa Vodacom.

....wafanyabiashara watakao nunua mitambo hiyo washauriwe wapeleke Somalia......
 
Kama Rais atajiingiza kwenye ununuzi wa Dawans basi sikio la kufa halisikii dawa na si muda mrefu tutafikia ya Ginea Bissau kwani Watanzania hawakotayari kuburuzwa kwa sasa na vilevile Watanzania si mabwege kama alivyosema Mwakiyembe.Na yale aliyoyasema Mwakiyembe kuwa waliyaacha kwenye ripoti yao ili kuinusuru serikali naona yatakuwa yanaitafuna kwani inaelekea kulekule.Bora wakati ule wangefichuliwa wote na Serikali yote ingevunjika na tungekwishafanya uchaguzi upya.Ila jamani tamaa ya fedha na madaraka ni mbaya sana.Wenye nia njema na TZ muendelee kuitetea.
 
Sitta ulikuwa wapi siku zote, siku hizi unajifanya unaonge sana au kwa sabababu mtandao umekutenga ????????????
 
(e) Kwamba dhana ya tenda na Sheria ya Manunuzi isiruhusiwe kuwa kikwazo katika miradi mikubwa mikubwa ya miundombinu ya nishati, hasa ile ambako wawekezaji wanajitokeza wenyewe kuwekeza katika maeneo ambako taifa linahitaji uwekezaji mkubwa na wa haraka na ambako nchi inaonekana ilichelewa kuwekeza.
=======

Hii ina tofauti gani na:

-PM Pinda kuruhusu wanaoua Albino wauawe papo hapo bila kusubiri hatua za utawala wa sheria?

-Rais kuitisha kura za maoni ya kukamata wauaji wa Albino mwezi huu?

Ndugu zangu, tuna serikali isiyojali sheria. Rais mzima naitisha kikao Ikulu kusema, sheria zisiwe kikwazo katika kuunga mkono ufisadi.
 
mwkjjj.

zumari limelia nasi tupo kulichezaaaaa.. mambo ya dowans natumai yatatupa picha nyingine ya uwezo wa serikali hiii katika kutendaaa maamuzi yake.
 
Back
Top Bottom