Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Jamani kuna mtu anaweza kutuletea taarifa kama magari yanayotumiwa na wakurugenzi Tanesco na mawaziri Ngeleja na Malima pamoja na katibu mkuu wa wizara ya nishati yalinunuliwa mapya au yalinunuliwa yaliyotumika??????

Hata kama mmoja wao anatumia gari lililonunuliwa used, Mimi binafsi nitasupport kununua generator mitumba!!!!!!!!!
 
Kuhani nimesema hitimisho langu ni lile la kamati ya Bunge kwamba TANESCO wawezeshwe kununua mitambo. Sijasema TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya DOWANS. Hii sio kazi ya kamati. Mitambo gani wananunua na kutoka wapi ni kazi ya TANESCO wenyewe. Hili nimeliweka wazi kabisa katika michango yangu humu (unspinned, niliyoandika mwenyewe) ndani na pia katika barua ambayo nimeandika kwa Waziri wa Nishati na Madini. Kuhani, nipo very clear na judgement za watu humu nazichukua kama changamoto. As i said, humu JF sishindani, ninajifunza.

Msimamo wangu ni msimamo wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma.

Mh. Zitto,
With due respect; nafikiri ulitakiwa useme TANESCO wasinunue mitambo ya DOWANS na wakifanya hivyo utawashitaki kwa WANANCHI. Lakini kwa maelezo yako inaelekea umetishika na kiza alichotangaza another fisadi na kusahau kabisa kuwa DOWANS ni fisadi pia.

Inaelekea tuna usahaulifu wa haraka sana. Hebu tujikumbushe alivyoandika Dr.Mwakyembe kwenye ripoti yake;

This Day Feb 19, 2008
Dr Mwakyembe said Rostam was sent a summons to appear before the probe team, but dodged it by claiming he was outside the country when the committee was sitting in Dar es Salaam.

Rostam was apparently summoned for questioning on his links with the US-based Richmond Development Company LLC and UAE-based Dowans Holdings SA, after more than five witnesses had named him during earlier testimony.

Said Mwakyembe: ’’He (Rostam) was also required by our committee to explain why the postal and e-mail addresses of his own company, Caspian Construction Company Ltd, were being used by Dowans Holdings SA. The committee was also given several names of employees of Caspian who also work for Dowans Holdings SA.’’

Tusiwe wavivu na kuwasikiliza wanayosema watu ambao tayari hatuwaamini. Tufanye homework yetu otherwise, Mh. Zitto unaweza ukatumiwa kufanikisha majambo bila ya wewe kukatiwa hata kiduchu.

Unge-google au hata kuwasiliana na Pratt & Whittney etc., leo hii majibu yako yangeonekana ya kishujaa. Lakini badala yake kwenye kila unachosema kinaonekana kama utetezi kwa DOWANS. What is this 'sheria' vs 'Kanuni'? Watu wanaanza kukutilia wasiwasi kwa majibu yasiyonyooka na sidhani kama una haki ya kuwalaumu ukitilia maanani yaliyokwisha wasibu. Madaraka mara nyingi yanalevya, na kwa kupewa uenyekiti, inaelekea unaona kama unahitajika pia kuitetea kamati yako, this is wrong. Jaribu kuuliza au kupata ushauri kwa wale unaoona wana mawazo mazuri ndani ya JF ili ufanikiwe maana hakuna mtu anayejua kila kitu badala ya kupigana na JF.

Pratt & Whittney wanayo mitambo ya aina mbili mobile na grounded. Mobile ikifika site inahitaji siku 3 tu kuanza kufanya kazi. Hiyo mingine ambayo inaelekea ndio kama ya Rostam, inahitaji tu 4weeks. Ukichukulia hizi info, sidhani kama inaweza ikahitajika miezi 6 kuifikisha mitambo Dar tokea US, including airlifting kama walivyofanya akina Rostam.

Kwenye ku-google nimeona mitambo ya P&W aina ya FT8 25MW ikigharimu kati ya U$ 10-12milion. Najaribu kuwasiliana nao ingawa inaelekea bei kwao ni siri.

Zitto, you need to wake up and stop being used. How come so soon have you forgotten that;
DOWANS = ROSTAM = UFISADI?
Doesn't the tittle of this topic ring a bell to you?
 
KANUNI na sio sheria.

Mh. Zitto,

Ni kweli ni kanuni na sio sheria. Nilisema kwenye post yangu uliyonukuu kwamba, kanuni ni sehemu ya hiyo sheria husika kwa kuwa zimetungwa kwa mujibu wa sheria mama, ndo maana zinatumika zote kwa pamoja katika taratibu za manunuzi. Utakubaliana nami kuwa kwenye taratibu za "tender" na matangazo hizo kanuni na sheria hutumika sambamba. Ndio maana kwenye matangazo huandikwa maneno haya hapa chini nanukuu;

"A consultant will be selected in accordance with the procedures set out in the Public Procurement Act No. 21 of 2004 and the Public Procurement (Goods, Works,Non-consultant services and disposal of public assets by tender) Regulations, 2005 – Government Notice No. 97 of 15th April, 2005"

Kwa hiyo sheria na kanuni zinaenda pamoja na hazitenganishwi. Ukienda kinyume na kanuni ambayo imetungwa kwa mujibu wa sheria mama, unahesabika mkosaji. Katika kushughurikia mambo mbalimbali ya serikali, lugha hii hutumika sana kwamba je, " Sheria, Kanuni na Taratibu" zimefuatwa?

Mh. Zitto, tuendelee na mjadala.
 
Sasa hizo statement zako hapo mbili kwenye same reply, sijui niiamini ipi??

Yaani wewe kwenye issue ya dola $90million kulipwa dowans na kujaribu kwenda kwa manufacturer ambaye anaweza kutupa hiyo mitambo kwa about $50million tena mipya na warranty, una question safari ya wabunge wawili Ama??? Kwani safari za mwaka zinazolipiwa na serikali yetu si zaidi ya watu maelfu tena kwenye mambo yasiyo na maana kwenda kujitambulisha blah blah, sasa kwenye hili la maana unaanza kuquestion?? Aisee Mh. Yapi tena yaliyokusibu mbona unakuwa erratic kwenye hili suala??

Moelex,
Actually you dont even need to go to US to get a quotation. This is not 1945. Lift a phone, email, fax and in a matter of mins, hrs, days-----you'll have estimates of what you are looking for, and may be from tens of suppliers.

The only thing you need is guidelines/specs..........that is it.
 
Baada ya kuwashuku wabunge wenzako kuwa wanaspin sheria ili kujenga hoja zao, nawewe umefanya nini hapo chini (in red)? Hio "pale inapowezekana" hukuiongeza ili kutetea hoja zako za kuwabeba Dowans?...Kanuni inasema SHALL be Brand New, wewe unasema "pale inapowezekana". Yale yale.

Na again, wananchi wanamfuatisha mwalimu wako Prof. Shivji kwamba, DOUBT EVERYTHING!... We are just doing that.

nimespin
 
Mh. Zitto,

Ni kweli ni kanuni na sio sheria. Nilisema kwenye post yangu uliyonukuu kwamba, kanuni ni sehemu ya hiyo sheria husika kwa kuwa zimetungwa kwa mujibu wa sheria mama, ndo maana zinatumika zote kwa pamoja katika taratibu za manunuzi. Utakubaliana nami kuwa kwenye taratibu za "tender" na matangazo hizo kanuni na sheria hutumika sambamba. Ndio maana kwenye matangazo huandikwa maneno haya hapa chini nanukuu;

"A consultant will be selected in accordance with the procedures set out in the Public Procurement Act No. 21 of 2004 and the Public Procurement (Goods, Works,Non-consultant services and disposal of public assets by tender) Regulations, 2005 – Government Notice No. 97 of 15th April, 2005"

Kwa hiyo sheria na kanuni zinaenda pamoja na hazitenganishwi. Ukienda kinyume na kanuni ambayo imetungwa kwa mujibu wa sheria mama, unahesabika mkosaji. Katika kushughurikia mambo mbalimbali ya serikali, lugha hii hutumika sana kwamba je, " Sheria, Kanuni na Taratibu" zimefuatwa?

Mh. Zitto, tuendelee na mjadala.

nakubaliana nawe. ndio mjadala unakuwa mzuri. kwa hiyo kanuni za manunuzi zinakataza mitambo iliyotumika.

katika barua yangu kwa Waziri nimesema tanesco wanunue mitambo ya umeme kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
 
Mbunge Kijana, mtaalamu anamaanisha kuwa 'kanuni' hiyo ni sehemu ya 'sheria' ndio maana kanuni za aina hiyo zinatungwa - na kusomwa - chini ya sheria husika. Mkuu usijaribu kutumia fursa hii kushusha hadhi kazi ya Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza Utoaji wa Zabuni kwa Richmond (na pacha wake Dowans) na kusafisha wasifu wa aliyekuwa Waziri Mkubwa na aliyetajwa kuwa Swahiba wake. Kaka weka nguvu zako kwenye kuibana Serikali Bungeni ili itekeleze maazimio (maagizo?) ya Kamati/Bunge hasa lile azimio la kutatua hili tatizo la umeme wa dharura! Mheshimiwa usipoziba ufa wa Richmond utajenga ukuta wa Dowans!

Wakuu Companero na Ngereja, nawashukuruni sana kwa ufafanuzi wenu..........

next step itakuwa ni....endapo TANESCO wanataka ku-BID/ku-procure something what are the procedures set aside.........
..........ngoja niendeleze mabox...baadaye kidogo
 
Sasa hizo statement zako hapo mbili kwenye same reply, sijui niiamini ipi??

Yaani wewe kwenye issue ya dola $90million kulipwa dowans na kujaribu kwenda kwa manufacturer ambaye anaweza kutupa hiyo mitambo kwa about $50million tena mipya na warranty, una question safari ya wabunge wawili Ama??? Kwani safari za mwaka zinazolipiwa na serikali yetu si zaidi ya watu maelfu tena kwenye mambo yasiyo na maana kwenda kujitambulisha blah blah, sasa kwenye hili la maana unaanza kuquestion?? Aisee Mh. Yapi tena yaliyokusibu mbona unakuwa erratic kwenye hili suala??

bodi ya shirika la umma inataka kununua mitambo, inaamua kutuma wabunge. unaona ni sawa kabisa........ nakushangaa. Rashidi aliwakatalia. Wamekasirika kukosa katrip.
 
Aisee Companero na Ngereja, Ahsanteni mno maana sisi wengine watu wa Idara walituambia na kutuhakikishia kuwa PPRA 2004 hairuhusu hayo mambo ya Dowans, na ndio maana tulitaka Mh.Zitto atuonyeshe wapi PPRA inasema inaruhusu. Lakini nyie mmetupa kitu na box kabisa kwa hiyo kumbe wasiwasi wetu unalindwa na sheria za Jamhuri, kwa hiyo kidogo nitalala salama maana najua kutakuwa na price ya kupay kama mitambo ya Dowans ikinunuliwa.

All in all, at least imetusaidiia kujua lazima tutafute watu wengine bungeni kukamilisha agenda za wananchi maana Mh. Zitto naona kidogo hajui zile no no za politics, Yaani mfano Republicans right or wrong lazima wasupport Tax cuts, ukitaka kuleta mambo ya sijui nina msimamo unajiuzulu tu na kwenda huko msimamo wako unakowakilishwa.
 
nakubaliana nawe. ndio mjadala unakuwa mzuri. kwa hiyo kanuni za manunuzi zinakataza mitambo iliyotumika.

katika barua yangu kwa Waziri nimesema tanesco wanunue mitambo ya umeme kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Zitto,
Achana na hizo kanuni n.k. Make this a political issue kama sheria ina loop holes. DOWANS bado hawajaelezea mahusiano yao na Rostam, whom we know is accused of being the man behind RDC. Why should we even discuss anything that is linked to DOWANS wakati mapendekezo ya kamati ya bunge juu ya DOWANS hayajatimizwa? Am I the only one who sees this confussion?
 
bodi ya shirika la umma inataka kununua mitambo, inaamua kutuma wabunge. unaona ni sawa kabisa........ nakushangaa. Rashidi aliwakatalia. Wamekasirika kukosa katrip.

Mh. Zitto hizo petty fights zenu kwenye kamati, mimi hazinihusu. Lakini kwenye possibility ya kusave over $50 million siwezi kuanza kuquestion investigation itakayocost at most $15,000.

Ni hayo tu Mheshimiwa sababu kila siku serikali inasafirisha watu kwenda nje hata kwenye kuhudhuria seminar tu au mambo mengine ambayo hayana hata benefits kwetu.
 
Sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 husomwa pamoja na kanuni zake, hii ina maana GN. No. 97 (THE PUBLIC PROCUREMENT (GOODS, WORKS,NON-CONSULTANT SERVICES AND DISPOSAL OF PUBLIC ASSETS BY TENDER) REGULATIONS, 2005; ni sehemu ya sheria hiyo kwa kuwa zimetengenezwa chini ya sheria husika na kutangazwa katika gazeti la serikali.

Kwenye kanuni hiyo hapo juu sehemu ya IV kifungu cha 58 (1)-(6), nina vinukuu hapa chini:

...........
(5) The preferred motor vehicles or other motorised equipment as determined under sub-regulation (4) of this Regulation, shall be procured either directly from the manufacturer of the said motor vehicles or through competitive quotations from reputable authorised local and international
suppliers or dealers of the specified vehicles.

......................Neno "Shall' linapotumika kwenye sheria, linaweka msisitizo kuwa ni lazima, na sio vinginevyo.

..

.......nafikir hiyo hapo juu ina-set what TANESCO are/were supposed to be doing.....endapo kama wanataka kununua/ku-BID mitambo........sasa je TANESCO walifuata hiyo regulation hapo juu?
 
Mh. Zitto hizo petty fights zenu kwenye kamati, mimi hazinihusu. Lakini kwenye possibility ya kusave over $50 million siwezi kuanza kuquestion investigation itakayocost at most $15,000.

Ni hayo tu Mheshimiwa sababu kila siku serikali inasafirisha watu kwenda nje hata kwenye kuhudhuria seminar tu au mambo mengine ambayo hayana hata benefits kwetu.

Ukisikia vurugu ndiyo hii sasa. Wabunge kazi yao kutunga sheria. Vipi tena waingie jikoni waanze kwenda kununua mitambo? Sasa ikiwa watakosea watawajibishwaje na Bunge hilo hilo? I think Rashid was right kuwakatalia hiyo siyo kazi yao. Wao wangoje vi trip vya kutembelea mabunge mengine duniani na kusimamia chaguzi za nchi.

Hata Wabunge walio wakurugenzi katika mashirika ya umma inabidi waondolewe.
 
nakubaliana nawe. ndio mjadala unakuwa mzuri. kwa hiyo kanuni za manunuzi zinakataza mitambo iliyotumika.

katika barua yangu kwa Waziri nimesema tanesco wanunue mitambo ya umeme kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Tuko pamoja kabisa, na kama serikali itafuata sheria, kanuni na taratibu zake ambayo ni yenyewe imeziweka, basi, mitambo ya Dowans haitanunuliwa, labda kama kuna "loopholes" kwenye sheria yenyewe au kanuni zenyewe.

This is what is supposed to be. Vinginevyo, kama tuko kwenye hali mbaya sana, then, tutafanya kile wanachofanya Marekani, kuokoa uchumi wa nchi yao. Sasa justification hiyo ipo kwa sasa?

Huo ni mtizamo wangu tu.
Tuendelee kujadili na kuelimishana.
 
Kwa kuwa kanuni hutungwa na kutenguliwa na Waziri husika, basi si kazi ndogo tu kuzibadilisha? Ingekuwa ni sheria hapo mambo mengine kwani ingebidi irudi Bungeni.

Ngeleja kazi kwako... Go ahaed umekwisha ipata...
 
Article 97 ya Katiba ya JMT, kifungu cha (5), Kinalipa bunge uhuru wa kumpa mtu(waziri in this case) au idara ya serikali mamlaka ya kutengeneza kanuni "having the force of law".

Kwahio suala la kuitwa sheria au kanuni halina mashiko kwenye utekelezaji wake, as zote zinaenda sambamba kama mkuu Ngereja alivyoonyesha hapo juu.

Mheshimiwa kateleza,... kama hajateleza basi anayumbishwa na kimbunga cha Dowans...
 
hivi tunashindana hapa? sijateleza popote. sana sana nimeondoa mjadala kutoka katika emotions kuja katika issues. hili la sheria tumelimaliza na kulifunga, kwamba sheria ya manunuzi haikatazi kununua mitumba bali kanuni za manunuzi. hii ni muhimu sana maana tuikuwa tunasema tu sheria na hata mmoja akasema hapa kuwa wanasheria waliobobea wamesema sheria. nimetafuta na kuleta hapa kwamba ni kanuni za manunuzi ambazo hubadilishwa na waziri kwa GN na so bunge. hata hivyo sheria zinasomwa pamoja na kanuni na hivyo lazima tanesco wafuate.

kamati ya nishati na madini misled the public na hasa inaposema turudi bungeni. NO. let the executive do its work and we do our work of oversight.

i said tuwe sober, tusimeze spin jamani. sasa tumejua sio sheria, ni kanuni. nasisitiza hilo sana.

next?
 
Aisee Companero na Ngereja, Ahsanteni mno maana sisi wengine watu wa Idara walituambia na kutuhakikishia kuwa PPRA 2004 hairuhusu hayo mambo ya Dowans, na ndio maana tulitaka Mh.Zitto atuonyeshe wapi PPRA inasema inaruhusu. Lakini nyie mmetupa kitu na box kabisa kwa hiyo kumbe wasiwasi wetu unalindwa na sheria za Jamhuri, kwa hiyo kidogo nitalala salama maana najua kutakuwa na price ya kupay kama mitambo ya Dowans ikinunuliwa.

All in all, at least imetusaidiia kujua lazima tutafute watu wengine bungeni kukamilisha agenda za wananchi maana Mh. Zitto naona kidogo hajui zile no no za politics, Yaani mfano Republicans right or wrong lazima wasupport Tax cuts, ukitaka kuleta mambo ya sijui nina msimamo unajiuzulu tu na kwenda huko msimamo wako unakowakilishwa.

Wewe unakuwa muongo sasa na ninachukia sana uongo. Did you ask me to show where does the law allows? uongo kabisa huu. I challenged you guys to mention the section of the law banning used equips. You failed. I did show you its regulations and even mentioned the regulation. Ngereja came up to elaborate and quote the regulation. Kwa nini huwi mstaarabu kukubali uliposhindwa.

Eti umeambiwa na watu wa Idara. Idara gani hiyo iliyooza na kuruhusu ufisadi wote huu nchini. Idara gani hiyo ilishindwa kuzuia hiyo kampuni ya Richmond kupata mkataba ule. Idara gani hiyo iliyoruhusu fedha za EPA kuibiwa na kutumiwa na CCM kwenye uchaguzi? Idara gani hiyo iliyoshindwa kuzuia wizi wa MEREMETA na kumdnganya PM kuwa ni pesa za usalama wa taifa?

Kumbe ulikuwa unaambiwa na watu wa Idara ndio maana ulikuwa kama kasuku tu na kushindwa kujibu hoja zangu na badala yake unanitisha unadhain natishika. I am a man of facts and i succumb to facts. Sishindani.

Sasa huko texas si wangeenda hao watu wa idara badala ya Bodi ya Shirika la Umma kuombwa kutuma wabunge. Na unashabikia Bodi ya Shirika la Umma kutuma wabunge kwenda kununua mitambo. Thats procurement made in Tanzania.

Suala la sheria tumelimaliza. Maoni ya kamati yangu tumeshapeleka. Nadhani mjadala umekwisha.
 
Back
Top Bottom