Siungi mkono ujambazi wowote.Pia nipo tayari kusimama mwenyewe na kuelezea ninachoamini. Nipo tayari kubaki peke yangu iwapo ninachofanya ninaona ni sahihi na nipo genuine. Katika hili mimi na kamati yangu tupo genuine na hatuna maslahi yeyote zaidi ya kuona shirika linaendeshwa kwa faida na hivyo nasi kuwa na national champion.
I stand with the decision of my committee kwamba Kamati mbili zikutane na kujadili suala hili. Kiongozi lazima awe tayari kuchukua maamuzi magumu. nipo tayari kuwajibika kwa hili.
Hii nimei-copy toka Nipashe:
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amesema ni vigumu kununua mitambo ya kufua umeme ya Dowans, kwa sababu licha ya kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge,
kampuni hiyo imefungua kesi dhidi ya serikali na Tanesco katika mahakama ya usuluhishi huko Paris.
Mwakyembe amesema anashangazwa na hatua ya Tanesco kung`ania mitambo ya Dowans, wakati tayari wamiliki wake wamewashtaki serikali na Tanesco huko Ufaransa.
``Dowans wametupeleka Paris katika Mahakama ya Usuluhishi, sasa iweje tung`ang`anie kununua mitambo yao katika hali kama hii,`` alisema Dk. Mwakyembe katika mahojiano maalum na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema uamuzi wa kununua au kutonunua mitambo hiyo upo mikononi mwa Tanesco, iwapo shirika hilo linang`ang`ania kufanya hivyo
kinyume na ushauri wa maamuzi ya Bunge.
Alisema kumekuwa na ujanja ujanja mwingi unaotumiwa na menejimenti ya Tanesco kuhakikisha kwamba inafanikiwa kununua mitambo hiyo kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge.
Alisema uongozi wa Tanesco ``unafanya usanii`` katika kutaka kuhalalisha uamuzi wake wa kununua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans.
Dk. Mwakyembe ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema Tanesco imekuwa ikitafuta mbinu za kuhalalisha uamuzi wao wa kununua mitambo ya Dowans ambayo kisheria hairuhusiwi kufanya hivyo.
Dowans ambayo ilirithi mkataba batili wa kampuni tata ya Richmond Development LLC ya Marekani, haifahamiki mmiliki wake kisheria.
``Sisi tunasema kama kununua wanunue, wameomba vibali mara ngapi, wananunua sijui nguzo!!! wamekuja lini kwetu. Naamini kwenye hili wamegundua kuna kitu hakiko vizuri ndio wanataka kuhalalisha,`` alisema.
Alisema kamati yake ilitoa maoni, ila kuna ujanja wa aina fulani, ``Sijui wanataka nini, kana kwamba kamati nyingine ina mamlaka ya kupokea rufani dhidi ya kamati nyingine kuna aina fulani ya usanii kwenye uongozi wa Tanesco.``
Alifafanua kwamba 14, Desemba, 2008, kamati yake ilipokutana na uongozi wa Tanesco, Wizara ya Nishati na Madini pamoja waziri mhusika, waligundua kwamba Bodi ya Tanesco ilikaa siku 10 kabla na kukataa kata kata wazo la kununua mitambo ya Taneco.
``Hata hivyo, menejimenti ya Tanesco iliizunguka Bodi na kuja kwetu na sasa wamezunguka na kwenda kwa Kamati ya Hesabu na Mashirika ya Umma , ikiomba kibali cha kununua mitambo hiyo,`` alisema.
Alisema kazi ya Bunge ni kusimamia na sio kujiingiza katika shughuli za utendaji wa kila siku wa Tanesco, lakini akaonya kwamba iwapo itabainika kuwa taratibu zimekiukwa katika ununuzi huo na kuliingiza taifa katika balaa, wahusika watawajibishwa.
Alisema uongozi wa Tanesco, ``unafanya usanii`` katika kutaka kuhalalisha uamuzi wake wa kununua mitambo ya Dowans.
Dk. Mwakyembe alifafanua kwamba Tanesco imekuwa ikitafuta mbinu za kuhalalisha uamuzi wao wa kununua mitambo ya Dowans ambayo kisheria hairuhusiwi kufanya hivyo.
Alisema menejimenti imekuwa na ujanja ujanja mwingi kiasi cha kuizunguka kamati yake, na kuwasilisha maombi ya kununua mitambo hiyo kwa kamati nyingine ya Hesabu na Mashirika ya Umma (POC).
``Sisi tulitoa maoni, Tanesco ina ujanja wa aina fulani, sijui wanataka nini, kana kwamba kamati nyingine ina mamlaka ya kupokea rufani dhidi ya kamati nyingine,kuna aina fulani ya usanii kwenye uongozi wa Tanesco,`` alisema na kuongeza
``Kama wanataka kununua, wanunue…na sisi kazi yetu ni kusimamia tu na sio kuwaagiza kwamba wanunue au wakatae. Watakapoamua kununua wajue kwamba wanafanya hivyo kwa misingi ya kanuni na sheria, la sivyo watawajibika,`` alisema.
Akizungumzia mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans, Dk. Mwakyembe alisema anaona umepata sura ya kisiasa, na anaona kama ni mwendelezo wa Operesheni Sangara.
`
`Nimesikia na kusoma kuhusu Mwenyekiti wa POC, Zitto Kabwe kwamba kamati haijawasilikiliza Tanesco. Kamati ilikutana na Tanesco na Wizara 14 Desemba mwaka jana na kuwasikiliza, kwamba hatujawasikiliza hilo si kweli,`` alisema.
Naye mbunge wa Nzega CCM, Lucas Selelii, amesema hatua ya baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali kupigia debe ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans kinyume na maamuzi ya Bunge, inaleta wasiwasi.
Alisema ana wasiwasi kwamba huenda kuna mkono wa mtu, anayeshinikiza kununuliwa kwa mitambo hiyo, kinyume na maazimio ya Bunge.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liinunue mitambo hiyo.
`
`Kuna mkono wa mtu, tena mkono wenyewe ni wa chuma, kwanini maamuzi yetu wenyewe tunayakanyaga, kama wanapinga, turudi bungeni,`` alisema Selelii jana wakati akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake.
Alisema suala la ununuzi wa mitambo hiyo lilitolewa kama pendekezo na Kamati Teule ya Bunge na kuridhiwa na Bunge kwamba mitambo hiyo isinunuuliwe.
Alisema kwanza, katika uchunguzi wa kamati hiyo iligundulika kwamba mitambo hiyo ni mibovu na pili gharama za ununuzi wake ni kubwa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, ni makosa kwa serikali kununua vifaa ambazo vimetumika (mitumba).
Alisema kiasi cha fedha ambacho kinatakiwa ili kununua mitambo hiyo, kinaweza kununua mitambo mingine mitatu yenye ukubwa na uwezo huo huo wa kuzalisha umeme.
Selelii alisema serikali inaweza kufanikisha ununuzi huo kwa kutuma barua pepe Marekani ambako mitambo hiyo hutengenezwa au inaweza kumpeleka ambaye atashughulikia ununuzi wake na hivyo kurudi nchini akiwa na mitambo mitatu.
Alifafanua kwamba Kamati Teule ya Bunge ilikwisha kamilisha kazi na mapendekezo yake yaliridhiwa na Bunge na suala hilo sasa lipo chini ya Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge.
Alisema atashangaa iwapo Kamati hiyo ambayo ipo chini ya Mwenyekiti, William Shellukindo, itakapokiuka maazimio ya Bunge.
Kwa upande wake, Mbunge wa Karatu, Chadema, Dk. Wilbrood Slaa, alisema kinachohitajika katika suala hili ni taarifa kwa taifa.
``Tunaingizwa katika mjadala, wakati hatujui yaliyomo kwenye Kamati ya Shellukindo na wala katika Kamati ya Zitto,`` alisema na kuhoji: ``Kwa nini kamati hizi mbili kila moja inashikilia msimamo wake.``
Alisema haijulikani serikali na Tanesco walikubaliana nini katika Kamati ya Zitto, na kuongeza kuwa ni vema kujadili suala ambalo mmoja amepewa taarifa zake.
Alisema hadi sasa hakuna mtu anayejua kwa uhakikia nini yaliyomo katika Kamati hizo, suala ambalo ni gumu kulijadili.
Alisema Kamati ya Mwakyembe ilitoa taarifa kuhusu mitambo ya kufua umeme ya Dowans, kwamba serikali inaweza kupata na kununua mitambo hiyo huko inakotengenezwa tena kwa bei nafuu.
Lakini alisema: ``Tunataka kujua maazimio ya Bunge kuhusu sakala la Richmond yamefikia wapi kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, iwapo mtu amebainika kughushi na kuingia mikataba, mali zake zinatakiwa kutaifishwa.``
Alihoji iwapo mkataba wa kufua umeme wa dharura kati ya Tanesco na kampuni ya Richmond, (sasa Dowans), ulibainika kuwa umeghushiwa, sheria imefuatwa ya kutaifisha mitambo hiyo.
Alisema badala yake kuzingatia taratibu hizo za kisheria, tunazungumzia hitaji la kununua mitambo hiyo.
Hata hivyo, alisema dharura hii ya umeme si ya leo, na ina tofauti gani na ile ya miaka iliyopita.
Juzi (Jumamosi), Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuelezea hali ya umeme katika Grid ya Taifa pamoja na mambo mengine, akapendekeza kuwa mtambo wote wa Dowans ununuliwe na serikali pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye grid suala la ununuzi wa mitambo iliyotumia katika sheria ya Manunuzi iangaliwe kwa makini kwa manufaa ya sekta ya umeme na mbadala wa kununua mtambo wa Dowans ni kuagiza mara moja mitambo ya kukodisha ya umeme ya kiasi cha megawati 150 kwa njia ya dharura, ambayo inapaswa kuwepo kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.
Mhe Zito:
Kila unapojaribu kujitetea ndio unavyozidi kujichafua..... nakushauri warudishie hela waliyokuhonga!!!!