Doto Biteko njia alotengeneza Makamba ni mbovu. Kwa kuanza tengeneza yako!

Unknown2

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
2,344
4,982
Mh, kwanza nakupongeza kwa kuwa Waziri mpya wa Nishati. Nina imani na wewe!

Mhe, kutokana na imani niliyonayo kwako.. nisingependa kuona unaharibu kama alivyofanya mtangulizi wako. Hivyo basi nakushauri kufanya yafuatayo :

1. Tengua bodi aloteua Makamba. Bodi imejaa watu wenye makando kando mengi. Haiwezi kukufikisha unapotaka. Weka watu makini bila kuzingatia uswahiba, udini wala undugu.

2. Pitia mikataba yote aliyoingia Makamba. Katika hili uwe makini kweli, uwe imara na mzalendo. Mikataba isiyofaa achana nayo na penye kurekebishika fanya hivyo.

3. Fuatilia kwa kina Mradi wa Gesi ya Mtwara. Ikiwa ni pamoja na mapitio mapya ya mkataba wa waliopewa mradi.

4. Pitia upya mradi wa ujenzi wa bwawa la Nyerere. Hakika Makamba alivuruga sana pale ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa zilizojaa ukakasi!

5. Wizara yako imejaa wapiga deal wengi, wengine wanaweza kuwa wale unaowaheshimu na kuwaogopa. Hakikisha unasimamia weledi! Hata wakikutoa ukweli wako utasimama daima na kukutetea.


Nb: Nafasi ya unaibu PM ni ya utata flani na haipo kikatiba. Hakikisha unakuwa nayo makini sana.

Nakutakia kila lakheri!
 
Rais Samia ulionywa sana kuhusu huyu mtu mtafuta madili ya kujaza tumbo lake badala ya kuhudumia wananchi, kiko wapi sasa?

Hamna alichokamilisha hata kimoja zaidi ya ngonjera tu za hapa na pale, umeme vijijini haujakamilika hadi leo, licha ya kwamba awamu ya 5 ilibakiza vijiji elfu 2 nchi nzima,January Makamba ameacha mgao wa kutisha wa umeme kila kona, huku akisaini mikataba ya mabilioni ya pesa na wawekezaji hewa kutoka nje.

Legacy ya Makamba ni ipi hapo Tanesco?
 
Sinaimani na Samia..Tulikubaliana Sukuma Ganga wote waondoke yeye kamuondoa Angelina mabula basi
 
Rais Samia ulionywa sana kuhusu huyu mtu mtafuta madili ya kujaza tumbo lake badala ya kuhudumia wananchi, kiko wapi sasa?

Hamna alichokamilisha hata kimoja zaidi ya ngonjera tu za hapa na pale, umeme vijijini haujakamilika hadi leo, licha ya kwamba awamu ya 5 ilibakiza vijiji elfu 2 nchi nzima,January Makamba ameacha mgao wa kutisha wa umeme kila kona, huku akisaini mikataba ya mabilioni ya pesa na wawekezaji hewa kutoka nje.

Legacy ya Makamba ni ipi hapo Tanesco?
Kaharibu sana. Hafai kwa cheo chochote!
 
Potelea mbali hata kama kahamishiwa mambo ya nje lakini si haba kama ni madili tu kapiga ya kutosha,dili moja tu la nguzo za zege linamtosha kula yeye mpaka wajukuu.
 
Wanabebwa kweli et kahamishwa tu 😁 tuendelee kula kisamvu tu sisiii ambao baba zetu awakuwahi kadi za chama
 
Napata hisia Makamba amekasirika kupelekwa huko nje, pale Nishati palikuwa panamfaa alishajitengenezea mirija ya ulaji kwa muda mrefu ujao, akiwa na ndoto za kutumia kile atakachopata kujinufaisha kwenye safari yake ya kuusaka Urais.

Ile pesa $30milion kwa ajili ya maintanance bado mpaka leo sijaisahau, Dotto Biteko anatakiwa kuupitia ule mkataba neno kwa neno atazame tulivyopigwa na yule mbwa mwitu mwenye aliyevaa ngozi ya kondoo.
 
Back
Top Bottom