Mkuu;
Chonde chonde; kwetu kuna kamsemo; Kuona ganda la ndizi zio kuila. Umetangulia kutuhabarisha kuwa; Wenzetu Kenya walimshindwa. Hukumbuki ni nini kilimtoa kwenye lile tundu la sindano?? Huyu jamaa hali peke yake. Kumbuka kuwa, wale waliobeba mihela kwa mifuko ya sandarusi kutoka pale Bank hadi leo, hata tu kuwataja majina yao ni kukufuru. Upo hapo?? Huwezi mwita mama mkwe wako kwa jina lake. Leo, Sigh atawatajaje hao waliojibebea mihela ile?? Sio rahisi kama ufikiriavyo. Aweza chomoka hivi hivi ukimuangalia na ukaambiwa, ni marufuku kufukua kaburi lake