Don't bet against Magufuli, utaliwa...

Naona hili ni la kuzimisha ishu ya makinikia
Izimishwe kwani inanini??

Rais wetu alishasema kuna wakati halali kwa sbb ya majukumu ya taifa letu. Najua si lawyer lkn kusoma na kutoa maamuzi pia humchukulia muda mwingi na mara zote maamuzi yake ni +ve kwa wapenda haki.

So sioni uhusiano wowote kati ya hizi scandal 2.

Labda ungesema Watanzania maadili na uzalendo juu ya Taifa letu uliisha kabisa ndio mana Rais anapata tabu sana kila uchao.
 
Mleta mada kuna kitu inaitwa kufukua makaburi nakula matapishi.

Wenzako walikuja naporojo za kuhamia dodoma saivi wanasema yaliopita si ndwele tugange yajayo.

Kuweka akiba ya maneno ni jambo zuri.
 
Kama mtu alimtimua best wake, akamuondoa bila ving'ora mpiga debe wa chama chake, sidhani kama unaweza kujaribu kucheza kamari dhidi yake na ukaweka hela zako kwamba "hatafanya"... utaliwa..

Ningekuwa mimi ni Tibaijuka, Chenge n.k ningekuwa naishi kwa wasiwasi sana..
Hao dagaa, ajaribu kwa BASHITE kama yeye ni NGULI. Kifupi hao hana maslahi ya kudumu kwao.
 
Mwanakijiji na wewe unakuwa draged kirasi hivi?? Ni lini uliona takukuru wakipeleka mtu mahakamani wanaitish hadi mkutano na wandishi wa habari?? Hata hili hujaliona?? Hizi ni movie na maigizo kama mengine tu, acacia imetulia sasa ni gia lingine ili siku zisogee, na hili nalo litaisha hivi hivi

mmh mswahili halisi wewe, roho mbaya na unauchawi fulani

hata kama haitafika mbali, mkuu...kaanza kile ambacho wengi wameshindwa

nikuulize, kwa mfano magufuli asingefanya haya, wewe ungefanyaje? au hatua/safari huwa zinaanzaje??
 
mapema sana kusema usi bet against magu coz zipo area kadhaa unajua ukiweka bet against yy lazima utamla tuu mf uuzaj nyumba za silikali unaweza bet kuwa hatogusa ishu ya uuzaj nyumba za serikal wakat wa awamu iliyopita na kwa odds yyte lazima utakula tuu

pia najiuliza toka lini pccb wameanzisha utalatibu huu wa kiki coz hawa ni moja ya taasis ambazo tumezoea kuona wanafanya kaz kwa ukimya sana ila ajab leo wameita media's, kwa speed hii ipo siku tutapeleka mtu mahakaman kwa matalumbeta

,hata real Madrid akija bongo huwez bet kilahisi et kuwa atazifunga timu zote bila yeye kupoteza wala kutoa draw...so ni mapema sana ku_generalize kuwa magu ni untouchable and unpredictable...... tibaijuka be prepared mama.,

mkuu

Usikimbilie kuniita roho mbaya...kwani mangapi yamemshinda na anaishia njiani na mengi ni yao uongo tu? Haaminiki tena huyo mzee wenu
mmh mswahili halisi wewe, roho mbaya na unauchawi fulani

hata kama haitafika mbali, mkuu...kaanza kile ambacho wengi wameshindwa

nikuulize, kwa mfano magufuli asingefanya haya, wewe ungefanyaje? au hatua kuwa zinaanzaje??
 
Tunataka na waliohusika na ufisadi wa kivuko kibovu,uuzaji wa nyumba za serikali,meremeta,kagoda,n.k nao wafikishwe mahakamani pamoja na wale waliochota mabilionoi ya Escrow kupitia Stanbic kwenye mifuko ya sandarusi.
 
Mwanakijiji na wewe unakuwa draged kirasi hivi?? Ni lini uliona takukuru wakipeleka mtu mahakamani wanaitish hadi mkutano na wandishi wa habari?? Hata hili hujaliona?? Hizi ni movie na maigizo kama mengine tu, acacia imetulia sasa ni gia lingine ili siku zisogee, na hili nalo litaisha hivi hivi

Na wakifungwa ndugu yangu utasema hawajafungwa wako vacation?
 
From FACEBOOK page ya Zitto Kabwe:
Maazimio 8 yaliyopitishwa na Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow ( kumbukumbu tu. Azimio la kwanza tumeliona. Hongera Sana Serikali)

1 Bwana Harbinder Singh Seth na wengine

Bunge linaazimia kwamba, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama, vichukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, dhidi ya watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai.

2 Mitambo ya IPTL

Bunge linaazimia kwamba, Serikali iangalie uwezekano wa kuichukua mitambo ya kufua umeme wa IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa mujibu wa Sheria za nchi.

3 Mapitio ya Mikataba ya Umeme ( Azimio la Kamati teule ya Richmond)

Bunge linaazimia kwamba, Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti la Mwaka 2015/2016, Serikali iwasilishe Taarifa ya Utekelezaji wa Mapitio ya Mikataba ya Umeme;

4 Kitengo cha Rushwa kubwa

Bunge linaazimia kwamba; Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda TAKUKURU, kwa lengo la kuanzisha Taasisi mahususi itakayoshughulikia kupambana na kudhibidi vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa Taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

5 Majaji

Bunge linaazimia kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi, kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania. (Makofi)

6 Benki ya Stanbic na Benki Nyingine

Bunge linaanzimia kwamba, mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Tanzania Ltd na benki nyingine yoyote itakayogundulika kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow kuwa ni Taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (Institutions of Money Laundering Concern).

7 Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu na Bodi ya TANESCO

Bunge linaazimia kwamba, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe kwa kuishauri Mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.

8. William Ngeleja, Victor Mwambalaswa na Andrew Chenge

Bunge linaazimia kwamba, Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao kwenye Kamati husika za Kudumu za Bunge.
 
Leo tena wana CCM wote wamejitoa ufahamu wanshangilia na hili, si mlisema escrow si mali ya serikali? Na Ruge ni mfadhili wa lichama lenu ambalo soon linakufa??
 
Watu wamepiga magoti waliozoea kusimama. Betting against Magufuli is not that wise after all. Mtu atakula hadi king!

Wahamisha magoli wawe waangalifu
One cannot bet against someone who does not know his own position.

Of course don't bet against Magufuli.

He is like a non collapsing quantum wave, able to exist and not exist at once, to be against and for corruption at once, to be magnificently game changing and despicably ill prepared at once.

How do you even to bet against someone who knows no rules and makes everything as he goes along?
 
Hivi Mwanakijiji hii ni mara yako ya kwanza kuona watu wakipelekwa mahakamani?!

Labda nikukumbushe....

Lyumba baada ya "kuitia hasara" ya mabilioni ya pesa serikali, alipelekwa mahakamani na akaishia kufungwa miaka 2.

Daniel Yona na Mramba walipelekwa mahakamani kisha wakahukumiwa na kuishia kufanya usafi hospitali!!!

Yule jamaa wa Richmond nae alifikishwa mahakamani sidhani kama natakiwa kukumbusha!!!

Mafisadi EPA waliambiwa warudishe pesa staili ambayo imekuwa pia ikifanywa na JPM na walioshia kufungwa na mafisadi uchwara kama akina Maranda!!!

Sasa kinachokufanya umsifie JPM ni nini as if ni jambo jipya?! Au atavaa joho mwenyewe na kusimamia shoo?!

Yaani na maturity yako yote uliyonayo kwenye siasa bado unasukumwa na pepo nyepesi namna hii!!!!
 
Back
Top Bottom