DOKEZO Dola zimeadimika, bei ya black market ni Tzs 3000-3200 kwa noti za $.50 & 100

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tukizuia Vijana watafanya biashara gani?
Tukizuia vijana watafanya uzalishaji na kuongeza ajira. Hivi unataka kuniambia viti vya mbao vikizuiwa kuagizwa China vijana watakosa kuvitengeneza?
Tukizuia kuagiza ndala na yeboyebo watu watatembea peku?

Zuia vitenge kutoka China uone kama viwanda vya Urafiki na wenzake havikui, uone kama wakulima hawalimi pamba
 
Kwa zaidi ya siku 10 nimekuwa nikitafuta dola 12,000 kwa ajili ya kuweza kuagiza vitu fulani China.

Nimezunguka kwenye mabenki yote makubwa, jibu lao hatuna USD. Nimeenda bureau de change, nako nimezunguka sana.

Jana jioni nikafika kwenye duka moja la kubadilishia fedha, nilipoingia ndani wakaniambia hawana dola, nikatoka nje. Mlinzi akaniita, akasema dola ni Tzs 3,200/ nikasema that's too much, wakanishusha hadi 3,000/-

Mama yangu Samia Suluhu Hassan, hii hali ni mbaya, huko tunakoelekea nchi itaweza kuingia kwenye mfumuko mkubwa sana wa bei, hyper inflation, maana dola ni adimu, inapatikana kwa gharama kubwa. Hii itapelekea kupanda sana kwa bei ya bidhaa hasa ukizingatia zaidi ya 95% ya bidhaa tunazozitumia tunaagiza kutoka nje ambako tunanunua kwa pesa za kigeni
Mimi nanunua online kwa 2500/$
 
Next time tumia postal bank...wao wako chini kuliko bank zote...
Niliwahi ona mdada 1 wa nmb ukimpa anaenda bank ya posta ,so na ye anapiga kiasi fulani.....
Ila sijui Kwa ss
Dah asante mkuu ushauri mzuri umenipa, siku ile pale nilikuta crdb na nbc ndio wako wazi na nbc bei yao ilikuwa imesimamia kucha,kumbe ningeenda postal bank
 
Tukizuia vijana watafanya uzalishaji na kuongeza ajira. Hivi unataka kuniambia viti vya mbao vikizuiwa kuagizwa China vijana watakosa kuvitengeneza?
Tukizuia kuagiza ndala na yeboyebo watu watatembea peku?

Zuia vitenge kutoka China uone kama viwanda vya Urafiki na wenzake havikui, uone kama wakulima hawakimi pamba
Nini kinazuia wasifanye uzalishaji saizi?
 
Athari ya Vita ya Ukraine hiyo.

Bora uku afrika,
uko ulaya ndo kumechafuka balaa

Jana German wametangaza recession
Uingereza mfumuko wa Bei haushikiki
USA hali tete mabenki yanafilisika daily

Sahv wenye nafuu duniani labda Ni Russia na waarabu wa mAfuta

maana wao ndo wamezishikilia injini za uchumi (fuels) wanazichezesha watakavyo kufidia Hali mbaya ya uchumi duniani.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nini kinazuia wasifanye uzalishaji saizi?
Unfair competition, wewe unaweza compete na kampuni ya Kichina inayopewa ruzuku na serikali, ikakopeshwa mabilioni na benki zao, haibambikiwi kodi na bado ikija bongo inahonga officials?

Unaweza compete na kampuni inatokea nchi ina zaidi ya watu bilioni 1.3? Wakianza na domestic market wakakua vizuri wakija huku international market wakakukuta wewe manufacturer wa nchi ya watu 60M ambayo bado inaendekeza importation wanakupiga za uso mapema sana. Kwanza economies of scale wanakuzidi mbali.

Sera za nchi haziungi mkono uzalishaji. Kila mtu akipata hela anaenda funga mzigo China, nenda Kariakoo uone wanavyoshusha makontena ya mitumba ya kawaida kabisa. Watu kama Murzal walikuwa wanaagiza mafuta ya kupikia nje wanafunga kwenye madumu wanaandika made in Tanzania, ulishajiuliza kwanini COVID-19 ilivyoanza bei ya mafuta ya kupikia ikapanda sana na hatukuwa na lockdown? Kwenye makaratasi tunadai tunazalisha mafuta ila mfanyabiashara bora aagize ngano, sukari, mafuta, mchele nje aje achape label kwenye vifungashio kuliko kuzalisha ndani.
 
Mtu anaiba Tshs. Trillion 2, anazibadilisha kuwa dollar halafu anaenda kuficha nje ya nchi, unategemea nini?

Ila fanya malipo online, pesa inajibadilisha yenyewe.
Kinachouma zaidi ni kuwa Rais analitambua hilo na hajalifanyia kazi maana lazima Waziri wa Fedha ambaye ni Makamu alihusika
 
Kwann China isitoe tamko bidhaa zake zinunuliwe kwa yuan badala ya US

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Inahitajika nchi zifanye biashara ili fedha za nchi husika zipatikane.

Tukinunua kwa Yuan maana yake itabidi tupate Yuan zakutosha kutokana na China kuagiza kwetu bidhaa nyingi kwa Yuan, na yeye anunue kwetu kwa Tzs
 
Kwa zaidi ya siku 10 nimekuwa nikitafuta dola 12,000 kwa ajili ya kuweza kuagiza vitu fulani China.

Nimezunguka kwenye mabenki yote makubwa, jibu lao hatuna USD. Nimeenda bureau de change, nako nimezunguka sana.

Jana jioni nikafika kwenye duka moja la kubadilishia fedha, nilipoingia ndani wakaniambia hawana dola, nikatoka nje. Mlinzi akaniita, akasema dola ni Tzs 3,200/ nikasema that's too much, wakanishusha hadi 3,000/-

Mama yangu Samia Suluhu Hassan, hii hali ni mbaya, huko tunakoelekea nchi itaweza kuingia kwenye mfumuko mkubwa sana wa bei, hyper inflation, maana dola ni adimu, inapatikana kwa gharama kubwa. Hii itapelekea kupanda sana kwa bei ya bidhaa hasa ukizingatia zaidi ya 95% ya bidhaa tunazozitumia tunaagiza kutoka nje ambako tunanunua kwa pesa za kigeni.
Nunua Yuan kama unaagiza mzigo China
 
Sio huko tu, hadi huku msalala Imalamagigo ndanindan madola hamnaga kabisa...☹️
 
Back
Top Bottom