Ubadilishaji wa dola za $1, $5, $10 na $20 kwa kiwango tofauti na noti za $ 50 na $100 ni msimamo wa BOT au wizi uliobarikiwa na BOT?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Wana JF, nilishangaa sana siku nilipoenda nchi fulani jirani nilipotaka kubadilisha fedha, nilibadilishiwa kwa kiwango kile kile bila kujali nilikuwa nabadili noti za $1, $5, $10, $20, $50 au $100. NIkakumbuka hapa kwetu Tanzania ukienda Bureau de Change unapewa kiwango tofauti kulingana kwa noti za $1, $5, $10, $20. Angalia hapo chini, noti a $1, $5, $10 na $20 unabadilishiwa kwa Tshs 1700, lakini noti za $50 na $100 unabadilishiwa kwa Tshs 2370! Jambo la ajabu ni kwamba wao wanapokuuzia dola wanauza kwa bei ile ile bila kutofautisha wanakupa noti ipi. Hapo chini utaona noti zote za $1, $5, $10, $20, $50 au $100 zinauzwa kwa Tshs 2400. Huu ni wizi!

Sasa ninachojiuliza ni kama hii ni kanuni iliyotolewa na BOT kwamba fedha za Marekani hapa nchi zinakuwa na thamani tofauti kulingana na noti. Na, hawa watu wa Bureau de Change wanapofanya transacton na BOT, nao huwa wanapewa thamani tofauti ya kubadilisha kwa noti tofauti za USA?

Kumbuka kwamba, kama noti za Marekani zinapaswa kuwa na thamani ile ile bila kujali ni noti ya kiasi gani, basi Watanzania tumekuwa tukiibiwa na hawa wabadilisha fedha kwa muda mrefu sana, na wizi huu kubarikiwa na BOT. NI mabilioni tumeibiwa. Na kwa nini tofauti hii iwe kwa Tanzania tu? Kama Bureau de Change wamefanya hili kwa kukiuka sheria, nashauri BOT wawapige faini kulingana na walianza lini biashara, na fedha za faini ziende kununua madawati au kujenga madarasa.

1551345054585.png
 
Ndiyo hiyo ni kweli na haijaanza leo.

Hii kadhia nilikutana nayo mwezi December mwishoni 2018 hapa Arusha.

Nakumbuka maduka ya kubadilisha fedha yalikuwa yamesimamishwa.

Sasa siku hiyo nilikuwa nimechelewa imefika jioni kabisa bank zimefungwa na ninahitaji kubadili $$$$. Siku hiyo town hakuna duka lolote lakubadili fedha lilikuwa wazi ikabidi niende usa river nikakuta duka pale liko wazi. Mshituko, wakaniambia noti za chini ya 20 usd wanabadili kwa kiwango cha chini tofauti na 50 usd au 100 usd.

Pia nilikutana na hii kadhia tena Karatu (Sanya bureau de change) nilipokuwa natoka safari Ngorongoro Crater na wageni. Hii ulikuwa 25 December 2018.

Sababu walizokuwa wanatoa noti chini ya $50 hawapati faida wakibadili kwa rate inayokubalika.
 
Pole Mkuu. Hili ni suala ambalo BOT wanahitaji kulitolea maelezo. Watanzania tumefanywa sana kuwa shamba la bibi
 
Nadhani hii inatokana Na charges ambazo Huwa wana incur kwenye mabank ukienda deposit small denomination kwenye bank unachajiwa Na inategemea Na bank husika, hivo bureau de change hupunguza iyo amount ili iweze lipa deposit fee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo hiyo ni kweli na haijaanza leo.

Hii kadhia nilikutana nayo mwezi December mwishoni 2018 hapa Arusha.

Nakumbuka maduka ya kubadilisha fedha yalikuwa yamesimamishwa.

Sasa siku hiyo nilikuwa nimechelewa imefika jioni kabisa bank zimefungwa na ninahitaji kubadili $$$$. Siku hiyo town hakuna duka lolote lakubadili fedha lilikuwa wazi ikabidi niende usa river nikakuta duka pale liko wazi. Mshituko, wakaniambia noti za chini ya 20 usd wanabadili kwa kiwango cha chini tofauti na 50 usd au 100 usd.

Pia nilikutana na hii kadhia tena Karatu (Sanya bureau de change) nilipokuwa natoka safari Ngorongoro Crater na wageni. Hii ulikuwa 25 December 2018.

Sababu walizokuwa wanatoa noti chini ya $50 hawapati faida wakibadili kwa rate inayokubalika.
Sasa mbona ukienda kununua hizo noti ndogo wanakuuzia kwa rate ileile ya noti kubwa?
Hiyo faida inapunguzwa na nini?
 
Mkuu hii sio biashara ya machungwa, kuuza kulingana na ukubwa. Suala la kusema noti za 50 na 100 zinauzika kirahisi - zinauzika kirahisi wapi?
Labda anamaanisha mtu akienda kubadilisha kutaka dola,labda anataka kiasi cha $ 50,000 hatapenda apewe kwa kiasi cha noti ndogo za $ 1, 2, 5,10, au 20 sababu mzigo wa hela utakua mkubwa, atapendelra apewe noti za $ 100 na 50 ili kupunguza mzigo
 
Ingekuwa hivyo ingekuwa hata katika huduma za ndani nchini kama supermarket, cin zinakuwa na thamani ndogo kuliko iliyoonyeshwa kwa kuwa hatutaki coin, au tukilipa na noti za thamani ndogo kama Tshs 1000 basi hazihesabiwi kuwa na thamani ya Stsh 1000!

Suala la upendezi binafsi halipaswi kuwa kanuni ya kuamua thamani ya noti tofauti na ilivyoandikwa. Hilo linaweza kuwa kosa la jinai. Ndio maana hata noti zinandikwa "fedha halai kwa malipo ya Tshs 1000". Sasa wewe fedha halali kwa malipo ya $10 unaamua kwa ulevi tu iwe sawa na $7! Ngoja Trump asikie!
 
Sasa mbona ukienda kununua hizo noti ndogo wanakuuzia kwa rate ileile ya noti kubwa?
Hiyo faida inapunguzwa na nini?
Kama unaelewa lengo lao ni kutengeneza super normal profit.

Kusema kwamba hawapati faida hiyo ni janja ya njani tu.
 
Labda anamaanisha mtu akienda kubadilisha kutaka dola,labda anataka kiasi cha $ 50,000 hatapenda apewe kwa kiasi cha noti ndogo za $ 1, 2, 5,10, au 20 sababu mzigo wa hela utakua mkubwa, atapendelra apewe noti za $ 100 na 50 ili kupunguza mzigo
Hii sababu ni dhaifu.

Exchange rate ya pesa ya kigeni inapaswa iwe sawa kwa aina zote za note kama inavyoamuliwa na nguvu ya soko (demand & supply)

Hiki wanachofanya hakina tofauti na wizi.

Pia inavuruga thamani halisi ya pesa.
 
Naunga mkono hoja yako kwa nguvu zote!
 
Back
Top Bottom