DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Wewe siku usipoitaja chadema kwa masaa 24 unaweza kuwa chizi aisee yani we ni CCM lakini muda wote ni chadema hivi chadema vile.
Hivi katika yote ya kujadili kuna kitu gani cha kujadili toka kwako mkuu? We lete nyimbo mpy za kumsifu mtukufu raisi hapa basi
Ila mwambie zile milion 50 kwa kila kijiji zimeyeyukoa wapi? Pia mwambie nyumba za serikali alizopiga mnada kwa bei cheee zinarudishwa lini! Kivuko je? Au ukikipeleka jeshini.ndo basi? Kisha twambie haya yanainufaisha vipi ccm
Nje ya mada
 
Wakati magufuli ananufaika na Rambirambi za waanga wa tetemeko mwana Ccm kama wewe ulinufaika na nini?
Na je gambo alivopiga za wanafunzi wewe ulipata mgao gani?
Mtatapatapa Baada ya kusomewa Albadirl.
Jielekeze kwenye hoja....inahusu manufaa/hasara za madhila ya Lissu kwa Chadema.
 
Limewanufaisha lkn ni Viongozi (baadhi) na siyo chadema kama Chama, Mbowe kanufaika, Nyalundu kanufaika, Msigwa ingawaje yupo Lupango lkn kanufaika kuonyeshwa kwenye TV abroad, Mashinji ambaye ndiye evilman na mastermind wa game yote kanufaika, waliopoteza ni Mke wa Tundu Lisu na Familia yake kwa ujumla!
Uchambuzi mzuri.
 
Amani iwe kwenu wana JF!

Kutokana na mjadala mkubwa ulioibuka baada ya Tundu Lissu kujeruhiwa kwa risasi tarehe 7/9/2017 tumeshuhudia vituko,mijadala mingi kwenye mitandao ya kijami,Tv, Redio na Magazeti. Kuna baadhi ya wanasiasa waliutumia mwanya huo wa kujeruhiwa kwa Lissu ''kufufuka'' kisiasa.

Mjadala wa leo unataka kuangazia maoni ya wanajamvi ili kupata tathmini ya kina itakayotoa majibu halisi ni kiasi gani sakata la kujeruhiwa Tundu Lissu limeinufaisha Chadema na viongozi wake au ni kwa kiasi gani sakata hili limewadharaulisha katika jamii ya watanzania. Kwa kuchokoza mada nitatupia maeneo machache ambayo yanaweza kutumika kama vigezo katika mada hii.

  1. Ni kiasi gani Chadema na baadhi ya viongozi wamenufaika na hela za michango ya wasamaria? au michango ilikuwa hafifu?
  2. Je ni kwa kiasi ganiwamepata huruma ya wananchi? au ni kiasi gani wananchi wamewapuuza?
  3. Je dhamira yao kuichafua Tanzania katika anga za kimataifa imefanikiwa? au wameshindwa?
Kwa kuzingatia kwamba JF ni jukwaa huru ninakaribisha pia vigezo vingine na mjadala mzito zaidi katika vigezo nilivyoweka hapo juu.

Hoja hujibiwa kwa hoja na so viroja.
Je kuhusu bashite anatolewa marinda na Johanna kumenufaisha sana kisiasa
 
Wakudadavua subiri matusi, kiukweli tukio la kujeruhiwa Tundu Lissu limewadhalaurisha Sana.
Wamepima umaarufu wao na wametambua umeshuka Sana, wanakazi ya ziada.
Sehemu wanapojitutumua ni humu jukwaani tu, kifupi 2020 wanaanguko kubwa Sana
 
Kimsingi tangu EL ahamie cdm na kuwa mgombea watu wanawatizama cdm kwa jicho la kipigaji zaidi, ndio maana hisia za upigwaji haziwatoki akilini.

Na huu ndio umekuwa mtaji wa kisiasa wa ccm baada ya cdm kujichanganya.
 
Siku Tundu Lisu aliyopigwa risasi ndiyo siku ambayo Serikali yetu pmj na Bunge lote walikuwa Ikulu Dar kupokea ripoti ya iliyohusu Madini yetu (Almasi, Tanzanite &Co.), hivyo masikio na macho ya Watanzania wote yalikuwa Ikulu na (kwa kawaida) Serikali yetu ilitaka iwe hivyo, lkn baada ya Tundu Lisu kupigwa risasi kila kitu kilibadilika hkn aliyesikiliza wala kujadili tena kilichoendelea Ikulu, sasa swali langu kama Serikali yetu ilihusika ni kwa nini wachague siku hiyo ambayo walitaka attention ya nchi nzima hasa kwenye hii ripoti?

Hapa ndipo wasi wasi wangu ulipo, hivyo theory/hypothesis yangu mimi ni hii, aidha waliompiga Tundu lisu risasi ni watu wa Serikali ambao walitaka kuihujumu Serikali yetu, au ni chadema au sehemu ya chadema ambao walitaka kuondoa publicity ambayo Raisi magudfuli angeipata, ikumbukwe hii siyo mara ya kwanza Tundu Lisu amakuwa na tabia ya kukamatwa na Askari wetu wkt tukio fulani mabalo lingeipaisha Serikali yetu lingetokea, hapo ndipo alipoitibua Serikali ili kuhamisha mjadala.

Hata kulipuliwa kwa osifi za Immmmma, pia kulizima tuliokuwa tunayajadili, ...

DADA KACHUKUA 7000/- KAZI UMESHAFANYA
 
Jambo la kwanza nani kakwambia macho na masikio ya watanzania wote yalikuwa Ikulu siku ile kusikiliza utumbo? Wengi sana walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida

Pili nani kakwambia serekali yote na wabunge walikuwa Ikulu siku ile? Ulimuona DAB pale?
 
Back
Top Bottom