Dodoma: Mwanafunzi ashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kupiga na kutuma picha za ukosefu wa maji Chuo Kikuu Dodoma

Hivi yule waziri wetu aliupata wapi ujasiri wa kuzungumzia maswala ya vyoo vilijengwa na serikali ya awamu ya tano wakati huku kwetu nyumbani kuzungumzia shida ya maji imemweka mwanafunzi lockup?
 
Nimesikia Polisi wamemkamata dogo aliepiga hii picha , ana kosa gani ? Hii nchi ya kifala sana tumekuja kugeuzwa wapuuzi wote. Polisi mna mambo mengi ya kufanya ya maana kuliko hili acheni UPUMBAVU
31A26E92-F282-432A-B4D2-F06281A5AC08.jpeg
 
Unajua watu wasipojua maana ya maneno, basi maana ya neno uchochezi itatumika vibaya.

Huyo anapaswa aponezwe kwa kusema ukweli.
Serikali uchunguze na ikibainika kuwa alipiga picha ambazo si za kweli kuhusu hali ilivyo, basi achukuliwe hatua.,
Lakini ikibainika kuwa hizo picha ni za kweli, basi wanaopaswa kubeba huomzigo ni viongozi waliopewa mamlaka na nafasi za kusimamia hicho chuo.

Ila hapo naona watasema wamemuaibisha mkapa na kiongozi wa nchi kwani juzi tu hicho chuo kilipa zawadi.

Biblia inasema hivi --"Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli?" GAL. 4:16
 
Tupo mbali sana...

Hamna baya hapo...kipindupindu kiwapate wao .... ..wakae kimya?
"Mzazi wako, alilewa mpaka akajikojolea"
Wewe mtoto unatangaza kwa majirani! Unapata faida Gani? Badala ya kuwajurisha babu na bibi yako, wewe unawaambia majirani?
Sasa anaonesha shida ya maji kwa dunia nzima anategemea dunia itakuja kutatua hii shida,?kwanini hakutuma hizo picha wizarani, kwa mbunge au waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ndio ilikuwanjia ya kufikisha taarifa kwa haraka!!
 
Back
Top Bottom