IGP Camillus Wambura afanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
1000013115.jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Martin Otieno aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Tanzania
 
View attachment 2934388

Sidhani kama kufanya hivyo itasaidia kitu. Hao ambao wamekuwa wakihamishiwa Makao Makuu pasipo kupanda Cheo kwa uzoefu wangu huwa wanakuwa wamevurunda sana wakati wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi vya awali walikohamishwa.
Anyway, ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi lote linatakiwa kuvunjwa lote kabisa na kisha kuunda tena Jeshi la Polisi jipya kabisa chini ya Sheria mpya, Katiba Mpya na Uongozi mpya na Muundo Mpya wa Utendaji kazi, na wala siyo vinginevyo.
 
Sasa na wateuzi wa Raisi wanapohamishwa vituo, wanapata posho za uhamisho. Ni muendelezo wa ufujaji wa fedha za umma.
Afadhali hata hilo tatizo la ufujaji wa fedha za umma, Jezhi la Polisi Tz Lina tatizo baya zaidi na la hatari kwa umma ambalo ni kuhujumu na kudhulumu haki za msingi kabisa za watu (kudhulumu haki za kuishi na haki za watu kuishi kwa Uhuru na amani).Haya ni mambo ya hatari sana, na vituo vingi vya Polisi vinaongoza ktk uvunjifu mkubwa zaidi wa haki za binadamu hapa nchini (the grave human rights violation). Kwa kifupi ni kwamba Vituo vya Polisi siku hizi vimegeuzwa kuwa ni Vituo vya Kifo kwa watu, ukipelekwa huko tambua kwamba uhakika wa kufa ukiwa huko ni mkubwa zaidi kuliko uhakika wa kurudi salama ukiwa hai na afya njema.
 
Back
Top Bottom