Dodoma: Mwanafunzi ashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kupiga na kutuma picha za ukosefu wa maji Chuo Kikuu Dodoma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Tungu Mgaya, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma tangu jana kwa kutuhuma za kupiga na kusambaza picha inayoonesha shida ya maji chuoni hapo.

FB_IMG_1579694021998.jpg


--+
MWANAFUNZI MUYAGA TUNGU ANAYEDHANIWA KUPIGA PICHA ZA KUONYESHA TATIZO LA MAJI UDOM MIKONONI MWA POLISI DODOMA

Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesoma Sayansi ya Asili (Natural Science ) chuo kikuu cha UDOM , Mugaya Tungu alikamatwa Jan 21 mwaka 2020 akiwa chumbani kwake ndani ya bweni la Wanafunzi UDOM.

Mwanafunzi huyo alikamatwa na polisi bila kuambiwa kosa lake ni lipi na kwanini alikamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa kituo cha polisi chimwaga Dodoma.

Lakini pia rafiki yake wa karibu (jina lake limehifadhiwa) naye alifuatwa kukamatwa usiku lakini alishtukia mapema na hakuweza kulala chumbani kwake hivyo polisi walimtafuta na hawakumpata.

THRDC tumefuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi huyo na kupata taarifa kwamba mwanafunzi huyo anadhaniwa kupiga picha zinazoonyesha uhaba wa maji katika chuo kikuu cha Dodoma. Wanafunzi wanapata changamoto sana kuhusu maji hali inayowasababishia kupanga foleni muda mrefu na pengine kuchelewa masomo darasani, hivyo mwanafunzi Tungu anadaiwa kupiga picha za wanafunzi wenzake wakiwa wamepanga foleni muda mrefu na kwa wingi na hatimae kukamatwa kwake.

Wanafunzi wenzake walienda leo jan 22, 2020 mnamo sa saba mchana kwenye kituo cha polisi alipowekwa mwanafunzi Tungu lakini hawakufanikiwa kumuona. Wanafunzi wenzake baada ya kufika kituo cha polisi waliambiwa kuwa Tungu amepewa dhamana ya polisi lakini walipohoji endapo kuna mtu amemdhamini waliambiwa hayo hayawahusu.
Hata hivyo wanafunzi wenzake wamejaribu kupiga simu zake hazipatikani na mwanafunzi huyo hajaonekana bwenini mpaka sasa hivyo bado haijulikani alipo.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi Mugaya Tungu, na tutawapa taarifa kadri tutakavyobaini.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC)
Jan 22, 2020
******

UPDATES
Jana usiku, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hana taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo na polisi.

Katibu wa serikali ya wanafunzi wa chuo hiyo, Paschal Michael alisema hana taarifa zozote kuhusiana na mwanafunzi huyo ingawa amekiri kumfahamu.

“Mugaya Tungu namfahamu kweli, ila siyo kiongozi wa serikali ya wanafunzi lakini namfahamu, kuhusu kukamatwa na polisi sina taarifa na ndiyo nasikia kwako, ngoja nifuatilie nitakujulisha kinachoendelea,” alisema Michael.
 
Inabidi basi serikali kwa kupitia wizara husika itoe muongozo ni namna gani wananchi tutapata taarifa kama hizi kama mtu binafsi anakamatwa kwa kutoa taarifa ya matatizo yanayowakumba kwenye maisha yao. Sijajua huwa wanataka hizi taarifa ziishie pale pale ama ni nini?. Hatuwezi kuendelea kuishi kwenye nidhamu ya uwoga. Hapo kosa la huyu kijana ni uchochezi au upotoshaji wa umma? Kama maji ni shida kweli kwanini mnamkamata?. Kuna sheria yoyote inayomzuia mhusika kwenye taasisi kutokutoa taarifa kuhusu changamoto anazozipata?
 
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Tungu Mgaya, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma tangu jana kwa kutuhuma za kupiga na kusambaza picha inayoonesha shida ya maji chuoni hapo.View attachment 1330742
"Mzazi wako, alilewa mpaka akajikojolea"
Wewe mtoto unatangaza kwa majirani! Unapata faida Gani? Badala ya kuwajurisha babu na bibi yako, wewe unawaambia majirani?
Sasa anaonesha shida ya maji kwa dunia nzima anategemea dunia itakuja kutatua hii shida,?kwanini hakutuma hizo picha wizarani, kwa mbunge au waziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom