Dkt. Tulia: Viongozi walioapa akiwemo Mkurugenzi wa Uchaguzi wasome na kuelewa Ilani ya CCM ili kumuunga mkono Rais

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 27 Februari, 2023



Dr. Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amewaasa viongozi wote walioapa leo akiwemo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kusoma na kuielewa vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri kama sehemu ya kumuunga mkono Rais Samia na Serikali yake. Amesema kwa kuwa Rais amewaaamini, wanapaswa pia kurudisha imani hiyo kwa wananchi.

Pia, amewataka kutunza ahadi ya kiapo pamoja na Kumshauri Rais kwa hekima. Kiapo hakijasema kitaisha lini hivyo wanapaswa kuendelea kutunza siri Maisha yao yote.

Samia Suluhu Hassan
Rais Samia amesema alidhani atamaliza Mhula wake na Baraza lilelile la Mawaziri lakini haijakuwa hivyo, ndio maana amemteua Mhe. Ulega kuchukua nafasi.

Amewapongeza wote walioapa, amesema kuwa siyo kwamba waliochanguliwa/kubaki hawana makosa, bali yeye kama mama anawalea.

Mabadiliko haya pia yameingiza watu waliokuwa nje ya Serikali ili kuwafanya walete ujuzi wao. Amesema kila anayeonekana ana akili zaidi atanyofolewa aliko ili aingie Serikalini kuongeza uzoefu.

Ameeleza mpango wake wa kuanzisha wizara mpya ambazo zitatangazwa pindi mambo ya kisheria yatakapokaa sawa.

Akitaja sababu za kufanya mabadiliko haya, amesema kuwa Kutokuelewana kati ya watendaji ni miongoni mwa sababu zilizomfanya abadili Watendaji wa Wizara. Amesema hapendi tabia hii na ikiwa itatokea tena, wahusika wote wa mgogoro huo atawaondoa.
 
Sina appetite ya kuyaangalia haya magalasa yanayoshindwa taasisi/wizara moja na kubadilishwa kwenda taasisi/wizara nyingine.

Business as usual!!!
 
Huyu spika ameshashutuka kwamba hataweza kushinda yaani anaongelea mkurugenzi wa tume ya uchaguzi akasome ilami ya chama kimoja


 
Katiba ya JMT Msingi wake ni muundo wa chama kimoja ndio sababu Wakuu wa Tume ya Uchaguzi wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM
Hii nafasi haiteuliwi na mwenyekiti wa CCM bali inateuliwa na Raisi kama Majaji, mwanasheria mkuu na mabalozi. Sasa kama nilivyosema mwanasheria mkuu naye anafuata ilani ya chama au katiba
 
Tanzania bado sana, Mkurugenzi wa Uchaguzi asome ilani ya CCM ya nini? Mama anataka kusaidiwa sababu anajua fika bila ukora na uhuni uhuni hatoboi Mbeya.
 
Rais anatakiwa adhibitiwe kuteua.
1. Akiteua asiweze kutengua
2. Wateuliwa wapitie bungeni.
3. Ateuwe ndani ya miezi sita tu baada ya kuapa.
4. Ateua kama mteuliwa amefariki au kajiuzulu nafasi yake
 
Back
Top Bottom