Rais Samia aapisha Viongozi wateule Ikulu Ndogo, Tunguu, Zanzibar, leo Septemba 1, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu dogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 01 Septemba, 2023.

Rais Samia amewakumbusha viongozi walioapa kuishi kiapo chao pia. Kwa wateule wapya, amewataka kupaza sauti kwenye matatizo ya wananchi kama walivyokuwa wanafanya wakiwa wabunge wa kawaida.

Rais Samia amesema Mabadiliko haya sio adhabu, bali yamefanyika ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu wananchi, viongozi ni watumishi wa watu.

Amewaaomba viongozi hao kuwa wapole kwani upole sio ujinga, watulie watumikie watu.
 
Umeonaeee...Anafanya kama jamaa yake. Sasa inaonekana kawaida marais kwenda kwao na kujifanya wanafanya kazi wakiwa ikulu ndogo ya eneo husika.
Hii haiondoi ukweli kwamba kaenda kufanyia kazi home. Ikulu kuu ambayo ndio nyumbani na ofisi kuu ya rais ipoipo tu.
Amepoteza mvuto...hata kumuweka Biteko wana nzengo kanda yote ziwa hapati kitu kamweee....kama ana plan B sawa ila yeye hatoboi
 
Amepoteza mvuto...hata kumuweka Biteko wana nzengo kanda yote ziwa hapati kitu kamweee....kama ana plan B sawa ila yeye hatoboi
sawa mtachagua mnae mtaka na hiyo ndoo demokrasia au vip mzee wa makasiriko.
 
Umeonaeee...Anafanya kama jamaa yake. Sasa inaonekana kawaida marais kwenda kwao na kujifanya wanafanya kazi wakiwa ikulu ndogo ya eneo husika.
Hii haiondoi ukweli kwamba kaenda kufanyia kazi home. Ikulu kuu ambayo ndio nyumbani na ofisi kuu ya rais ipoipo tu.
Rais Samia ataligharimu taifa sana
 
Back
Top Bottom