Dkt. Mwinyi aondoa kodi ya sukari Zanzibar

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.

Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu la Jumbi na soko la samaki Malindi mkoa wa Mjini Magharibi leo katika ziara maalumu ya kutembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kuacha kupandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi badala yake kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Mwinyi ameisisitiza Taasisi ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki la Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.

Source - Swahilitimes
 
Pasaka haimuhusu Mwinyi yeye huhangaikia waisilamu tu siku zote, mara anawasalia mashehe waliotangulia mbele ya haki mara ataongea na Samia ili serikali ianzishe mfuko wa Hija kwa waisilamu!
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ameondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa ya Sukari

Hatua hii itawasaidia
Wafungaji kununua sukari kwa bei nafuu

Source: Ayo TV
Kufunga au kubadili ratiba ya kula toka mchana kwenda usiku

Kuna muda huwa nawaelewa sana wakatoliki na kwaresma yao ,Wao wanasisitiza matendo ya huruma na toba lakini sio kushinda njaa

Hivi kama unakula usiku kucha isipokuwa masaa kadhaa kuna shida?

Kuna wakati tuambiane ukweli,Unaacha kula mchana halafu unakula usiku kucha

Prof Janabi yeye tu anakunywa chai anakaa masaa ishirini na nne ,Wakati wa mfungo atakuwa anawasikitikia sana wanaovimbiwa usiku wa manane
 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ameondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa ya Sukari

Hatua hii itawasaidia
Wafungaji kununua sukari kwa bei nafuu

Source: Ayo TV
Kuwepo na VAT categorries kwa bidhaa zanye kuhitajika sana.

Sukari, ngano, magari
 
Kufunga au kubadili ratiba ya kula toka mchana kwenda usiku

Kuna muda huwa nawaelewa sana wakatoliki na kwaresma yao ,Wao wanasisitiza matendo ya huruma na toba lakini sio kushinda nja...
Mlishashindwa hata kabla ya kuanza.....
 
Ndo kufunga kwenyewe we ulitaka iwe je?
Lengo la kufunga ni toba na kubadili tabia,Waislam wamegeuza kufunga ni kula usiku kucha kutoka kula mchana

Tuache utapeli wa kidini,Ndio maana Mwamposa anasepa na waislam na wakatoliki kwa kuwa yeye akisema kufunga ni kufunga kweli sio kubeep
 
Mlishashindwa hata kabla ya kuanza.....
Mkuu unafahamu historia ya unachokiamini au kwa kuwa Baba ni muislam au mkristo ukafuata tu

Hizi dini za uislam na ukristo ni dini za juzi tu ,zile za kihindi ni za zamani zaidi

Watu wanahubiriwa hadithi sema hadithi za mtume

Unafahamu maana ya hadithi?

Hata hawa walokole wakienda vatican kwenye makumbusho yao ndio watajua wanachokiamini kimetoka wapi?

Kumbukumbu za ukristo zipo vatican tena za uthibitisho sio za mchongo
 
Kufunga au kubadili ratiba ya kula toka mchana kwenda usiku

Kuna muda huwa nawaelewa sana wakatoliki na kwaresma yao ,Wao wanasisitiza matendo ya huruma na toba lakini sio kushinda njaa

Hivi kama unakula usiku kucha isipokuwa masaa kadhaa kuna shida?

Kuna wakati tuambiane ukweli,Unaacha kula mchana halafu unakula usiku kucha

Prof Janabi yeye tu anakunywa chai anakaa masaa ishirini na nne ,Wakati wa mfungo atakuwa anawasikitikia sana wanaovimbiwa usiku wa manane
Mambo ya Waislam yanakutesa vipi ewe kafiri,
Unaacha kujali yako unachokoa chokoa yasiyokuhusu, kitakukuta kitu shaurilo.
 
Back
Top Bottom