Mama Mariam Mwinyi ashiriki dua ya kumuombea Rais Dkt. Mwinyi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi amesema siri ya mafanikio yaliyopatikana Miaka 3 ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi yametokana na hali ya wananchi kuwa wamoja, wasikivu, watulivu kwa kuiwezesha nchi kuwa na umoja, amani na mshikamano.

Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika Dua maalum ya kumuombea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ilioandaliwa na Maalim Bi Sania Mahmoud kwa kushirikiana na Wanawake wa Kiislamu ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 11 Novemba 2023.

IMG-20231112-WA0003.jpg
IMG-20231112-WA0004.jpg
IMG-20231112-WA0005.jpg
IMG-20231112-WA0007.jpg
IMG-20231112-WA0006.jpg
 
Back
Top Bottom