Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania amesema “Malengo makuu ya dira ya Mwaka 2025, Maisha bora kwa kila Mtanzania, Kudumisha amani, usalama na umoja katika Nchi, Utawala bora, Jamii iliyoelimika vyema na inayojifunza, tano ni uchumi imara na shindani.”
Pamoja na hatua kubwa ambayo Nchi imepiga bado kuna changamoto mbalimbali zilizosababisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2000-2025 kutofikiwa kikamilifu mfano:
“Changamoto ya umasikini wa kipato na lishe duni, kwa mujibu wa utafiti wa Mapato na Kaya, takribani 26.4% ya Watanzania wanaishi chini ya kiwango cha umasikini wa kipato, ambayo ni zaidi ya Robo na Wananchi masikini zaidi wanaishi vijijini 31.3%.
Kuna mikoa, nitataja michache Kagera, Kigoma, Singida, Tabora na Dodoma ambayo kiwango cha umasikini ni kikubwa zaidi kwa sababu mbalimbali kutokana ikiwemo matatizo ya Kihistoria na miundombinu duni.
Kiwango cha tofauti ya kipato kwa kutumia kipimo cha uwiano kiliongezeka kutoka 0.34 Mwaka 2011/12 mpaka 0.38 Mwaka 2017/18.
Katika kipindi kama hicho, kipimo hicho cha tofauti ya kipato kwa maeneo ya Mijini nacho kiliongezeka kutoka 0.37 hadi 0.41.
30% ya Watoto chini ya miaka mitano wana udumavu Nchini
Akizungumza katika uzinduzi wa Mchakato wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti wa Mapato na Kaya.
Amesema “Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2022 unaonesha kuwa 30% ya Watoto wenye Umri chini ya miaka mitano wana udumavu na 9% ya Watoto wana udumavu mkali.”
Dkt. Mpango: Elimu yetu haikidhi mahitaji ya soko la ajira
Kwa upande wa kuwa na jamii iliyoelimika na inayojifunza, tumepata mafanikio ya kuridhisha ikiwemo kuongezeka kwa Wanafunzi katika ngazi zote za elimu.
Viwango vya ufaulu vimeongezeka, uwezo wa kusoma na kuandika Nchini unakadiriwa kuwa 92%.
Pamoja na mafanikio hayo bado vijana wengi wanaomaliza masomo hawapati fursa za ajira, pia elimu yetu haikidhi mahitaji ya soko la ajira wala kuwezesha wahitimu kujiajiri.
Jitihada za kurekebisha hali hiyo zinaendelea ikiwemo kupitia sera ya elimu na mitaala.