Dkt. Godwin Gunele: Rais ni taasisi hivyo Kikatiba inabadilika kila baada ya miaka 5, hivyo Rais Samia anatumikia kipindi cha Hayati Magufuli

Labda tatizo ni katiba!
Halafu wakisha soma hiyo 37 (5) waje pia wasome ibara ya 40 ibara ndogo ya 4
IBARA YA 40(4) inasema:-

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu"

Halafu waniambie huyo wanae dai anamalizia awamu iliyo pia ya tano ni kwa mujibu wankatiba ipi maana hapa katiba inatambua kuwa hii ni awamu yake na ana nafasi moja ya kugombea kama katiba inavyo eleza hapo

WAACHE UJINGA HAWA WACHUMIA TUMBO. Eti mwanasheria nguli .. AIBU.
 
Huyu jamaa akilibyake haiko sahihi.

Ukihesabu Mawaziri wako (nazo ni taasisi) wapo zaidi ya nane. Wakati Lowassa amejiuzulu aliefuatia yaani Pinda hakwenda kumalizia kipindi Cha Lowassa Bali alienda kuanza kipindi chake.

Kuna taasisi inaitwa Ndoa hasa kwa wakatoliki inakwisha kuwa ndoa mmojawapo anapofariki na aliyebakia anayoruhusa ya kuoa au kuolewa na mwingine. Na watoto watakaozaliwa ni wa mume mpya na sio aliyekufa.

Hivyo hivyo kwenye taasisi ya Raisi. Katiba IPO wazi kitu Cha Rais kinahesabika kuwa endapo Rais aliyepo amepoteza sifa za kuwa Raisi. Na mojawapo ya sifa hizo ni pamoja na kifo.

Kinatokea kifo kwa lugha nyepesi aliyekuwa na hiyo nafasi amepoteza sifa ( maana yake mwisho wa Zama zake na mamlaka yake, na utumishi wake). Yaani lazima apatikane mtu mwingine achukue nafasi yake. Mchakato wa kumpatia mwingine kila nchi imeweka utaratibu wake. Wengine wanrudi kwenye uchaguzi, wengine aliyekuwa msaidizi wake anachukua madaraka Yale. Ndio maana masharti ya kuwa makamu wa Rais ni sawa na Yale ya Rais kwa mujibu wa katiba yetu.

Hivyo aliyekufa amekufa na mamalaka yake na utumishi wake uliishia hapo.

Tuache upotoshaji wa wazi lakini watu wapotoshaji wasipewe platform za kudanganya umma.

Najiuliza kwa Nini tangu report ya CAG iwekwe hadharani uposhaji huu umekuwa mkubwa.

"Ukitaka kupoteza uelekeo wa treni legeza vishikio vya reli" tunawaelewa
 
Kwani katiba inasemaje kuhusu ukomo wa nafasi ya Rais?
Akifa Rais yule anayechukua nafasi anakua nani?
Mihula ya urais tunahesabu miaka au yule aliyehuduma?
 
Wasome vizuri ibara ya 37 ibara ndogo ya 5 >> IBARA YA 37 (5) amabayo inasema :-

"(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais
kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais
ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi
cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka
Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na
uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote."

Halafu waje waniambie kwa sasa katiba inamtambua SAMIA SULUHU HASAN kama rais au makamu wa rais.

Halafu baada ya hapo huyo mwana sheria koko anaye jiita msomi wa sheria aje aniambie ni wapi katika katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imezungumzia hayo maswala ya awamu.
Kwani amesema katiba inamtambua kama makamu wa Rais?
 
KiKilaza anakuwa yule anakimbilia kuhesabu Awamu kuliko kuacha Agenda ndiyo zi-name Awamu. Kwani angekaa kimya tu bila kujitaja kuwa ni Kiongozi wa ngapi watanzania wangalikosa namna ya kumtofautisha na aliyemtangulia? Kwani la maana ni lipi ni kuwa na mambo ya kumtofautisha au kutofautisha na namba?
Ni rais wa awamu ya 6 hutaki hama nchi , wasukuma mmekuwaje lakini? Kwani huyo mtu wenu mungu mtu wenu magufuli aliwaambia yeye ndiye aliye iumba tanzania? Mbona mnagubu hivyo?
 
Watanzania wana vichwa vigumu....
Magufuli na Samia walichaguliwa /pair kwa miaka 5 2020/2025....
Makubaliano ni kwamba kama Magu akifa au angekuwa incapacitated kwa namna yyte Samia anamalizia na katiba ipo clear....
mambo ya kusema hii ni awamu ya sita yanatokea wp!!??
 
Akiikubali kete yako ukafeli kumwondoa 2025 kwa hiyo kete akapitishwa na chama utakaa na taasisi yake ya uraisi kwa 14years.
 
Watanzania wana vichwa vigumu....
Magufuli na Samia walichaguliwa /pair kwa miaka 5 2020/2025....
Makubaliano ni kwamba kama Magu akifa au angekuwa incapacitated kwa namna yyte Samia anamalizia na katiba ipo clear....
mambo ya kusema hii ni awamu ya sita yanatokea wp!!??
Eti Awamu ya Sita! Kwa nini anakimbilia kujinasibu Awamu ya Sita badala ya kukomaa na Agenda? Kila kitu anataka kujitofautisha na mtangulizi wake lakini wakati huo huo anasema yeye na mtangulizi wake ni kitu kilekile? Kama yeye na Mtangulizi wake ni kitu kimoja mambo ya awamu ya Sita yanatoka wapi?
 
Watanzania wana vichwa vigumu....
Magufuli na Samia walichaguliwa /pair kwa miaka 5 2020/2025....
Makubaliano ni kwamba kama Magu akifa au angekuwa incapacitated kwa namna yyte Samia anamalizia na katiba ipo clear....
mambo ya kusema hii ni awamu ya sita yanatokea wp!!??
Ni awamu ya 6 kwa sasa mh Samia amekul kiapo kipya cha urais!
 
Kama anachosema ni sahihi basi upo uwezekano samia suluhu akawa rais kwa Muda wa miaka 14, yaani ikifika mwaka 2030 samia ajenge hoja kuwa, kuanzia 2021 to 2025 hakuwa rais kamili Bali alikuwa anahudumu awamu ya tano, so 2025/2030 ndo muhula wake wa kwanza awamu ya sita na 2030 achukue fomu tena ya urais kumalizia muhula wake wa pili wa 2030/2035
duuuh
 
Mzee kasome katiba ..Kwa mujibu wa katiba Mama Samia atagombea kipindi kimoja tu cha 2025/30 kama atataka lakini.
 
Kama anachosema ni sahihi basi upo uwezekano samia suluhu akawa rais kwa Muda wa miaka 14, yaani ikifika mwaka 2030 samia ajenge hoja kuwa, kuanzia 2021 to 2025 hakuwa rais kamili Bali alikuwa anahudumu awamu ya tano, so 2025/2030 ndo muhula wake wa kwanza awamu ya sita na 2030 achukue fomu tena ya urais kumalizia muhula wake wa pili wa 2030/2035
Kama JPM angekuwa amefariki mwaka 2022 au 23 na 2024 basi mama Samia angegombea Urais mara mbili ,hio 2025/30 na 30/35
 
Kama anachosema ni sahihi basi upo uwezekano samia suluhu akawa rais kwa Muda wa miaka 14, yaani ikifika mwaka 2030 samia ajenge hoja kuwa, kuanzia 2021 to 2025 hakuwa rais kamili Bali alikuwa anahudumu awamu ya tano, so 2025/2030 ndo muhula wake wa kwanza awamu ya sita na 2030 achukue fomu tena ya urais kumalizia muhula wake wa pili wa 2030/2035
Hapo kwa kudumu miaka 14 ndio tutaona udhaifu wa katiba tulionayo na patashimbika kwa mikwaruzano ya kikatiba na kisheria.

Muda ndio mwalimu.
 
HIvi wewe Max Melo mbona unakuwa hivi!!
Yani bado unaedit mawazo ya watu hata baada ya jiwe kufa?!!
Nisingepaza sauti hawa watu wasingepaza sauti
 
Back
Top Bottom