Dkt. Godwin Gunele: Rais ni taasisi hivyo Kikatiba inabadilika kila baada ya miaka 5, hivyo Rais Samia anatumikia kipindi cha Hayati Magufuli

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Mwanasheria nguli Dr Godwin Gunele amesema Rais siyo mtu bali ni taasisi ambayo kikatiba inakaa kwa miaka 5.

Kwa maana hiyo awamu tuliyopo ni ya 5 siyo ya 6 kwa sababu Rais Samia siyo " President elect" bali ni makamu wa Rais aliyechukua nafasi ya Rais aliyefariki.

Dr Godwin anasema hata waziri mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali wataendelea na kazi hadi kufikia ukomo wa uwepo ofisini wa President elect yaani 2025.

Mjadala uko mubashara Star tv muda huu kipindi cha Ajenda.

Itaendelea.
 
Kama anachosema ni sahihi basi upo uwezekano samia suluhu akawa rais kwa Muda wa miaka 14, yaani ikifika mwaka 2030 samia ajenge hoja kuwa, kuanzia 2021 to 2025 hakuwa rais kamili Bali alikuwa anahudumu awamu ya tano, so 2025/2030 ndo muhula wake wa kwanza awamu ya sita na 2030 achukue fomu tena ya urais kumalizia muhula wake wa pili wa 2030/2035
 
Ndivyo itakavyokua!
 
Huu mvutano ni wa nini kama urais aliokuwa nao Magufuli uliisha dakika aliyokata roho na kutangazwa kwa mujibu wa sheria? Iwe awamu tano au sita inamsaidia nini mwananchi iwapo utendaji uliopo kwa sasa ni wa Samia na si Magufuli?

Hata kama tutasema ni awamu ya Magufuli, itasaidia nini wakati mwenye awamu tunayodai hayupo? Haya ni baadhi ya maswali ambayo majibu yake yataepusha mjadala usio na siha wala umuhimu kwa taifa.

Ni ushauri wa kawaida. Iwapo tunamwita Hayati Magufuli aliyekuwa rais wa Tanzania, mume wa Janet etc, yanini kung'ang'ania hii ni awamu yake?
 
Godwin ni mtoa meno kwa koleo... Hatakuwa na muda mrefu kwenye serikali ya Madame,ndo kudemka huko wakati ngoma iko mtandaoni. Hiki ni kipindi cha bajeti,ajikite huko.
 
Godwin ni mtoa meno kwa koleo... Hatakuwa na muda mrefu kwenye serikali ya Madame,ndo kudemka huko wakati ngoma iko mtandaoni. Hiki ni kipindi cha bajeti,ajikite huko.
Jombaa kumbuka yule ni mwanasheria asiyefuata upepo wa wanasiasa na sisi wapiga porojo mtandaoni!! . Yule anasimamia misingi ya taaruma yake ya sheria. Si zambi kukosea Kisha akaja mtu akatusahihisha..
 
Back
Top Bottom