Dkt. Bashiru Ally Katibu wangu kama hiki nilichokisikia kimetokea Kawe katika Uchaguzi wa CCM ni kweli, basi kazi ipo 2020

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,882
Kuna watu wangu (wana medani) jirani na Kawe niliwatembelea siku ya Jumapili na wakati huo nilikuwa sijui nini kinaendelea hadi pale wenyeji wangu hao waliponiambia kuwa, ilikuwa ni siku ya kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Nakumbuka nilikuwa eneo hilo la Kawe hadi usiku wa saa tatu ambapo kwa kujiridhisha zaidi ilinibidi nizungukie maeneo mawili muhimu ya kiuchaguzi kwa Kawe ya Mzimuni alipo mkongwe Mzee Ngonyani (ambaye inasemekana alishakatwa na hatakiwi kugombea tena ila ndiyo kinara wa fitina zote akisaidiwa na Mwenezi wake aitwae Poti Poti ) na Ukwamani alipokuwa kijana makini Sultani Jeta (ambaye kwa bahati mbaya alisema kuwa hatogombea tena kwa sababu zake binafsi).

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa CCM sitaki kujua ‘ vimbwanga ‘ vya maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam vilivyotokea hiyo juzi (Jumapili ) ila kwa kilichotokea katika haya maeneo ya Mzimuni na Ukwamani ‘ nimekitathmini ‘ kwa kina na kugundua kuwa kama wana CCM hasa nyie mlio ngazi za juu msipokuwa makini, basi kuna hatari mwakani vyama vya upinzani vikashinda na hamtoamini macho na masikio yenu.

Haya ni baadhi ya mambo niliyopata kutoka hayo maeneo ya Kawe Mzimuni na Ukwamani:

Rushwa za wazi wazi wana CCM kwa wana CCM

Usaliti wa wana CCM uliopitiliza

Fujo ambako kuna muda wana CCM walikuwa wakionyesha kuwa hata wao fani ya ubondia wanayo pia.

Ushirikina wa wazi wazi na kuna mtu mmoja wa Kawe Mzimuni ‘Mkongwe' ambaye nimemtaja hapo juu anajulikana na kuogopeka sana ‘Kiuchawi' kwani na ‘Uchawi ‘ wenyewe nao anaujua mno, kasema kwa kuwa jina lake mlilikata huko juu kwa juu basi na yeye hakubali na ataondoka na mtu ‘ kindumba' kiasi kwamba kuna baadhi ya watu (Wagombea) makini sasa wanatafakari kujitoa kwa ‘kumuogopa' huyo Mzee ambaye amedumu hapo Mzimuni kwa miaka takribani 20 ila ameshindwa tu hata kuitafutia gari ya wagonjwa Hospitali ya Shamba Kawe ambayo ipo mita chache na ofisi yake.

Upandikizaji wa watu ambako inasemekana kuna Mbunge mmoja (jina kapuni) aliandaa watu wake ambao wengine walikuwa ni wa Kiume ila walivalia ‘ Hijab' na waliletwa na Usafiri wa Bajaji (ambao aliwahonga pesa nzuri tu) ili waje wawapigie Kura za Maoni hao Wagombea wa CCM ambao huyo Mbunge ‘ Fulani ‘ anawamudu ili kama kawaida mwakani awatumie tena katika Kukisaliti Chama na aweze Kupita kama ambavyo baadhi yao walimsaidia huko nyuma ( bado nasisitiza kuwa hii ni Tetesi kwani hata Mimi GENTAMYCINE basi sijaithibitisha wala kuiamini kwa 100% )

Vitisho kwa baadhi ya wana CCM wa hayo maeneo kwamba kama hawatowapigia Kura basi Wao wakitumia Ujanja wao na kupita watakuja ‘ Kuwakoma ‘ na lazima tu watawafanyia tu Kitu mbaya. Na wengi wanaotishiwa hivi ni wale wana CCM ambao wanaendesha Bishara zao katika Soko la Kawe lile la Ukwamani na hili jipya lilipo Mzimuni pamoja na wale wengine waliopo mazuri kwa ‘ Fursa ‘ za Kibiashara.

Nikupongeze pia Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kwa ‘ Kuamuru ‘ Uchaguzi huu wa ndani wa CCM urejewe / urudiwe baada ya hizo ‘ Sarakasi ‘ ila kupitia tu huu Uzi wangu GENTAMYCINE nakuomba kama itawezekana basi nakuomba katika Siku ya Uchaguzi ( ambayo bado hamjaipanga ) tafadhali omba Msaada wa Kiusalama kutoka Kituo cha Polisi Kawe au hata ikibidi hawa Jamaa zangu wana ‘ Medani / Wanajeshi ‘ wasimamie tu hivi Vituo viwili vya MZIMUNI na UKWAMANI kwani kama hili halitotendeka basi tegema taarifa za Watu ‘ Kujeruhiana ‘ vibaya na hata ‘ Kuuana ‘ pia kwani hali si nzuri kabisa.
 
Huku Tabata Kimanga Mtaa wa Twiga amepitishwa kijana ambaye vibaka na wahalifu ni marafiki zake. Nimeshangaa
 
Mngeibiwa, mngeporwa na kujeruhiwa hadi ' mngenaniliwa ' pia vile vile Mshukuruni Katibu Mkuu Dkt. Bashiru aliyeamuru Uchaguzi urudiwe. Ni Uchaguzi uliojaa ' Vitimbi ' na ' Visa ' vya ' Kikatili ' ambavyo sikuwa Kuvisikia huko nyuma. Nadhani kuna tatizo kubwa ndani ya CCM na huenda Viongozi wa Juu ( Waandamizi ) bado hawajalijua au wanafichwa.
 
Kuna vitu vingine ambavyo hata ashuke malaika awe mwenye kiti wa CCM,ndani ya CCM haviwezi vikaisha kwa kuwa ni maisha ya CCM, rushwa ni sehemu ya maisha ya CCM, kuhubiri udini kwa wananchi ni sehemu ya maisha ya CCM, kubambikiza kesi ni sehemu ya maisha ya ccm, wizi wa kura ni sehemu ya maisha ya CCM, ubaguzi kwa wananchi ambao hawakuichagua CCM na katika hili kinara wa ubaguzi ni mwenyekiti wa taifa mwenyewe,n.k.
 
Yaani unataka kuitenganisha ccm Na rushwa, ccm Na uchawi.Ni ngumu. Yako maeneo kura za maoni zimepigwa Na wasio wanaccm tena kwa kuletwa Na wagombea ili wapite kwenye kura za maoni, Pia yako maeneo madiwani Na wabunge wameingilia michakato ili kupanga safu zao kwa ajili ya mwakani.
 
Ni Jana tu nilikua maeneo ya mbezi chini mitaa ya rainbow, kwenye kijiwe cha boda boda nilisikia wakitaja hilo jina la mzee Ngonyani. Walikua wakizungumza fitina za mzee huyo kuwepo madarakani kwa miongo kadhaa... Na dhuluma ya ardhi za watu miaka hiyo ya nyuma. Leo pia nasoma hapa kuhusu huyo mzee, inaonekana kuna jambo
 
Kuna watu wangu (wana medani) jirani na Kawe niliwatembelea siku ya Jumapili na wakati huo nilikuwa sijui nini kinaendelea hadi pale wenyeji wangu hao waliponiambia kuwa, ilikuwa ni siku ya kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Nakumbuka nilikuwa eneo hilo la Kawe hadi usiku wa saa tatu ambapo kwa kujiridhisha zaidi ilinibidi nizungukie maeneo mawili muhimu ya kiuchaguzi kwa Kawe ya Mzimuni alipo mkongwe Mzee Ngonyani (ambaye inasemekana alishakatwa na hatakiwi kugombea tena ila ndiyo kinara wa fitina zote akisaidiwa na Mwenezi wake aitwae Poti Poti ) na Ukwamani alipokuwa kijana makini Sultani Jeta (ambaye kwa bahati mbaya alisema kuwa hatogombea tena kwa sababu zake binafsi).

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa CCM sitaki kujua ‘ vimbwanga ‘ vya maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam vilivyotokea hiyo juzi (Jumapili ) ila kwa kilichotokea katika haya maeneo ya Mzimuni na Ukwamani ‘ nimekitathmini ‘ kwa kina na kugundua kuwa kama wana CCM hasa nyie mlio ngazi za juu msipokuwa makini, basi kuna hatari mwakani vyama vya upinzani vikashinda na hamtoamini macho na masikio yenu.

Haya ni baadhi ya mambo niliyopata kutoka hayo maeneo ya Kawe Mzimuni na Ukwamani:

Rushwa za wazi wazi wana CCM kwa wana CCM

Usaliti wa wana CCM uliopitiliza

Fujo ambako kuna muda wana CCM walikuwa wakionyesha kuwa hata wao fani ya ubondia wanayo pia.

Ushirikina wa wazi wazi na kuna mtu mmoja wa Kawe Mzimuni ‘Mkongwe' ambaye nimemtaja hapo juu anajulikana na kuogopeka sana ‘Kiuchawi' kwani na ‘Uchawi ‘ wenyewe nao anaujua mno, kasema kwa kuwa jina lake mlilikata huko juu kwa juu basi na yeye hakubali na ataondoka na mtu ‘ kindumba' kiasi kwamba kuna baadhi ya watu (Wagombea) makini sasa wanatafakari kujitoa kwa ‘kumuogopa' huyo Mzee ambaye amedumu hapo Mzimuni kwa miaka takribani 20 ila ameshindwa tu hata kuitafutia gari ya wagonjwa Hospitali ya Shamba Kawe ambayo ipo mita chache na ofisi yake.

Upandikizaji wa watu ambako inasemekana kuna Mbunge mmoja (jina kapuni) aliandaa watu wake ambao wengine walikuwa ni wa Kiume ila walivalia ‘ Hijab' na waliletwa na Usafiri wa Bajaji (ambao aliwahonga pesa nzuri tu) ili waje wawapigie Kura za Maoni hao Wagombea wa CCM ambao huyo Mbunge ‘ Fulani ‘ anawamudu ili kama kawaida mwakani awatumie tena katika Kukisaliti Chama na aweze Kupita kama ambavyo baadhi yao walimsaidia huko nyuma ( bado nasisitiza kuwa hii ni Tetesi kwani hata Mimi GENTAMYCINE basi sijaithibitisha wala kuiamini kwa 100% )

Vitisho kwa baadhi ya wana CCM wa hayo maeneo kwamba kama hawatowapigia Kura basi Wao wakitumia Ujanja wao na kupita watakuja ‘ Kuwakoma ‘ na lazima tu watawafanyia tu Kitu mbaya. Na wengi wanaotishiwa hivi ni wale wana CCM ambao wanaendesha Bishara zao katika Soko la Kawe lile la Ukwamani na hili jipya lilipo Mzimuni pamoja na wale wengine waliopo mazuri kwa ‘ Fursa ‘ za Kibiashara.

Nikupongeze pia Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kwa ‘ Kuamuru ‘ Uchaguzi huu wa ndani wa CCM urejewe / urudiwe baada ya hizo ‘ Sarakasi ‘ ila kupitia tu huu Uzi wangu GENTAMYCINE nakuomba kama itawezekana basi nakuomba katika Siku ya Uchaguzi ( ambayo bado hamjaipanga ) tafadhali omba Msaada wa Kiusalama kutoka Kituo cha Polisi Kawe au hata ikibidi hawa Jamaa zangu wana ‘ Medani / Wanajeshi ‘ wasimamie tu hivi Vituo viwili vya MZIMUNI na UKWAMANI kwani kama hili halitotendeka basi tegema taarifa za Watu ‘ Kujeruhiana ‘ vibaya na hata ‘ Kuuana ‘ pia kwani hali si nzuri kabisa.
Binafsi nimekushangaa wewe kwa kuyashangaa haya ndani ya SSM yetu.
 
Haya ni mambo ya ndani ya chama ukileta huku sie wengine hatuusiki.
Ahsante kwa taarifa nitajitahidi niwe nyumbani na family yangu pasi kwenda popote toka asubuhi mpaka usiku wa manane
 
Back
Top Bottom