Dk. Nchimbi tulia! Mwosha huoshwa

Dk. Nchimbi tulia! Mwosha huoshwa

Asante sana kwa maelezo yako wacha ninywe chai kwanza maana nimepata kichaa baada ya ufafanuzi wako .

Mzee Lunyungu,

Kwa kuongezea tu ni kwamba kuna kitu inaitwa TANGANYIKA LAW SOCIETY. Kwa hiyo ukiona neno TANGANYIKA usiwe unashituka sana ukiendelea kuona neno Tanganyika kwenye hizo professional societies.
 
.............SASA WAJINGA NDIO WANAOSEMA HUMU KUWA NCHIMBI ANAPINGA WASOMI,NAPE MALIZA SHULE YAKO KARNE HII UMOJA WA VIJANA WA CCM HAUWEZI RUDI NYUMA NA KUONGOZWA NA MTU AMBAE HAJAMALIZA HIGHER INSTITUTION KAMA KIONGOZI WA VIJANA CHADEMA.KATIKA WATU WOTE WALIOONYESHA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA NCHIMBI KATI YA 17 NI MMOJA TU AMBAYE NI NAPE HAJAGRADUATE NA MBAYA NI MKUBWA KWA UMRI KULIKO WENZIE..TENA FAMILIA YA MNAUYE HAIMTAMBUI ALIJITANGAZA KUWA NI MTOTO WA MNAUYE BAADA YA MZEE KUFA.INASEMEKANA BABA YAKE HALALI NI MTUSI.........

Ndugu yangu Fisadi mtoto,kweli we fisadi mtoto..kwanza hapa mimi ndo niliyetetea kuwa yapo mazuri machache ya Nchimbi nikayataja na kuomba wenye mazuri mengine wayataje,mwisho wa siku tuyapime na yanayosemwa mabaya yake!!!!!!!Ongeza nondo za uzuri wake walau ujae kijiko cha chai ili tujadili vizuri.

Hili la bwana mdogo Nape nadhani UZANDIKI huo unataka kuvuka mipaka.FITINA hii iliwahi kutumika mwaka2003/2004 alipogombea mara ya kwanza Uenyekiti wa vijana...tena nakumbuka ilikuwa gazeti la Tazama ambalo lilikuwa mahususi kumbeba Nchimbi na mtandao wakati huo na ndo maana sasa moja ya nguzo muhimu za gazeti hilo yupo UVCCM,Charles Charles ka shukrani kwa kazi nzuri.
Nakiri simfahamu sana Nape lakini machache nayafahamu juu yake maana naikumbuka vizuri hoja hii...ALIYEMPELEKA NAPE CHUO CHA SIASA KIVUKONI-CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWL.NYERERE MWAKA 2001 NI BRIG.GEN.(rtd) MOSES NNAUYE NA KUANDIKISHA KUWA NI BABA YAKE MZAZI AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA ANAMLIPIA MASOMO YALE.
-ILIPOIBULIWA HOJA YA UBABA WA NNAUYE KWA NAPE MSEMAJI WA FAMILIA MZEE GALLUS ABEID-(sasa ni mtumishi Taasisi ya Mwl.Nyerere Dar kama msaidizi wa mzee Butiku) alikuja na orodha ya watoto wa mzee Nnauye,ambayo ilitiwa sahihi na Mzee Nnauye mwenyewe tena mwaka 1983 ambayo alidai coppy iko ikulu na mahakamani kwa ajili ya shughuli za mirathi na kwa Mzee Makamba ambaye naye alithibitisha kuwa na coppy ya watoto wa mzee Nnauye yenye jina la Nape,tena limeandikwa Napalepe,hili ni jina la kimakonde lenye maana ya "HATA IWEJE ITAKUWA"
Data kwa uchache wa hoja yako, SI VIZURI KUTUMIWA, WANAKUTUMIA ILI MUMUHARIBIE KIJANA WAWATU BIAL SABABU,HAO HOJA HIYO ILIWAHI KUJA NAKUKUMBUSHA NI UZANDIKI AMBAO ULIKWISHA SHINDWA SIKU NYINGI. HIVI KAMA IPO KWENYE ORODHA YA WATOTO TENA MAHAKAMANI KWA AJILI YA MIRATHI ANAYESEMA NI MWANA FAMILIA NA HAMTAMBUI NI NANI??? HAO MAFISADI WANATAKA KUJIFANYA WASEMAJI WA FAMILIYA??? UKIHITAJI DATA ZAIDI NINAZO,ACHA KUTUMIKA WANAKUUZA.
HILO LA UMRI WA NAPE NALO LILITUMIKA WAKATI ANAGOMBEA NEC 2007,BAHATI MBAYA LIKASHINDWA DAKIKA YA MWISHO TENA JK AKAWAUMBUA "msimuonee Nape mpeni haki yake" wakajaribu kuhakikisha anaanguka huku wakidhani yupo shule India atashindwa,kila wakitathimini dogo anashinda wakataka basi walau awe wa mwisho,akawachana mashine waliotakiwa na mafisadi akiwemo Beno.Akapata kura za kishindo!!!!Ikiwa aligombea NEC akaruhusiwa leo miezi sita baadae eti manakuja na hoja ya kuzidi umri,ajabu kabisa!!Labda asitake tu yeye mwenyewe kugombea na ndio dua za wapambe wa Nchimbi na wafuasi wake maana wanajua si mchezo akiingiza jina.Ninachokumbuka huyu bwana kazaliwa mwishoni mwa mwaka 1977 na ndo maana Nchimbi kwa kuweweseka akatangaza kuwa atakayegombea awe amezaliwa 1978 anataka kumzuia Nape,jambo ambalo linamnyima usingizi.
DHAMBI YA NAPE NI MOJA TU,SI MWANAMTANDAO TENA ALIYEWAZI KUSEMA POPOTE BILA AIBU NA UKWELI WAKE UNAWATISHA MAFISADI. LA ELIMU NILICHOSIKIA TOKA KWA WAPAMBE WAKE ANAMALIZA MAY 2008 ANAKUJA NA DEGREE TENA SIO MOJA......wacha nipumue!
NADHANI WEWE SIPASWI KUKUJIBU KWA KUWA MAPENZI YAKO KWA NAPE YAMEKUPA UPOFU NA UJINGA NDANI YAKE.WHY?UNASEMA KUWA NAPE KAENDA KUSOMA MWAKA 2005 INDIA THEN ANARUDI NA DEGREE NYINGI YANI YOU MEAN ILE COMBINATION YA AJABU ULUOTUAMBIA HAPO NYUMA KUWA NI JOURNALISM,PHYSIOCOLOGY ENLISH NA FRENCH DEGREE!!!!YANI KWA AKILI YAKO NI KUWA ATA MTU AKIENDA KUSOMA MIAKA MITATU YA DEGREE YAKE KILA UNIT ATAKAYOOPT NI DEGREE,POLE...NAPE KAMA KUNA MTU ALISEMA KAPITA UMRI MWAKA JANA ALIKUWA ANAMUONEA,KWA KUWA KANUNI IKO WAZI KABISA KUWA MGOMBEA WA UVCCM LAZIMA AWE NA MIAKA CHINI YA 30 ILI ANAPOMALIZA MUDA WAKE HASIWE AMETOKA UMRI WA VIJANA,UNEC WA NAPE UTAKWISHA MWAKA 2012 HAPO ATAKUWA NA MIAKA 35.SASA KAMUULIZE ATA MWANAO WA VIDUDU MTU ALIEZALIWA NOV MWAKA 77 LEO HII ANA MIAKA MINGAPI,NI WAZI ATAKUJIBU KUWA AMETIMIZA MIAKA30 MWAKA JANA NA MWAKA HUU ATAKUWA NA MIAKA 31.TUNAFANYA UCHAGUZI WA UVCCM DEC 2008,NAPE ATAKUWA AMETIMIZA MIAKA 31 NA AMEANZA WA 32.JINA LAKE LITAKATWA.NAAPA KWA JINA LA MUNGU NLINAKATWA NA KAMA HALIKATWI ATAGALAGAZWA KAMA AMBAVYO ALIGALAGAZWA MWAKA 2003 ALIPOPATA KURA 149 DHIDI YA KURA 495 ZA COMARADE NCHIMBI.
 
Na Ndimara Tegambwage
KAMA kuna kiongozi mwenye bahati kubwa ni Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Lakini Nchimbi anataka kuharibu bahati yake. Anataka kujaribu mahakamani na siyo kwenye siasa ambako amefaulu.

Wiki iliyopita alivamia gazeti la Tanzania Daima na kuwatangazia kuwa thamani yake ni Shilingi Bilioni Moja. Nyingi au kidogo?

Aliwaambia kwamba wamemkashifu, hivyo wamwombe radhi, wafute kauli, wamjaze mifuko shilingi bilioni moja, vinginevyo atawaburuza mahakamani.

Nimeona mhariri amemkomalia Nchimbi akisema kwamba hafanyi lolote kati ya yote hayo. Hii ina maana gani? Kwamba Nchimbi atakwenda mahakamani.

Hakuna kesi nzuri ya kusikiliza kama hii. Wazee watajikongoja. Wagonjwa watapelekwa kwenye machela. Wenye ulemavu wa miguu watapewa kila msaada kufika mahakamani kusikiliza kesi hii muhimu na viziwi watapewa mkalimani.

Ni kesi muhimu kwa kuwa inataka kuthibitisha kwamba Mheshimiwa Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, amekashifiwa.

Hoja kuu hapa ni kuthibitisha. Narudia: Kuthibitisha kashfa. Kuthibitisha kuumia. Kuthibitisha kuporomoka kwa mbwembe na dadansi. Hapo ndipo bahati, na siyo heshima, ya Nchimbi itakapopotea. Twende hatua kwa hatua.

Kwanza, Nchimbi aligombea nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mwaka 2004 na kushinda. Ilikuwa makeke na mbindembinde. Akabebeshwa tuhuma, lawama na shutuma.

Potelea mbali. Tuhuma, lawama na shutuma vikazaa miaka mitano ya uenyekiti, tena bila usumbufu kutoka kwa yeyote aliyekuwa anagombea. Baraka tupu.

Pili, zikaja tuhuma, lawama na shutuma, kwamba anagawa umoja huo kwa kujenga makundi. Si lolote si chochote. Akaukwaa ukuu. Akawa Mkuu wa Wilaya ya Bunda. Amepeta bila mikwara hadi hatua nyingine. Baraka tupu.

Tatu, zikaja tuhuma, lawama na shutuma. Kwamba Nchimbi ni mwanamtandao wa Jakaya Kikwete. Ule mtandao ambao vijana wengi na wazee wasiozeeka walitaka kujitambulisha nao.

Hizi nazo zikawa tuhuma, lawama na shutuma za kheri. Nchimbi akaukwaa ukubwa. Akawa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo. Baraka tele.

Ndipo zikaja tuhuma, lawama na shutuma kuhusu Amina Chifupa aliyetaka kula mfano wa twiga. Alikuwa akitaka kula majani ya juu kabisa ya mti; akitaka kushindana na vigogo wa UVCCM au wateule wa vigogo.

Hilo liliambatana na tuhuma, lawama na shutuma juu ya mahusiano ya Nchimbi na familia ya Mohammed Mpakanjia na hadi kifo cha Amina.

Si lolote si chochote. Ikawa asubuhi, ikawa usiku, siku nyingine iko hapa. Mheshimiwa Dk. Emmanuel Nchimbi akapanda cheo: Naibu Waziri katika moja ya wizara muhimu nchini, Ulinzi.

Mungu akupe nini. Ni katika tuhuma, lawama na shutuma, ambazo Nchimbi anadai kuwa gazeti la Tanzania Daima limezirejea, ndimo amepata ukubwa wa kisiasa.

Kama tuhuma, lawama na shutuma vimezaa neema kwa Nchimbi, haijafahamika vema, yale marejeo tu ya yaliyokuwa yakisemwa yataleta kheri kiasi gani.

Uwaziri kamili? Ubalozi? Makamu wa rais? Kipi kikubwa kinakuja kinachotabiriwa na kumbukumbu za tuhuma, lawama na shutuma za muda mrefu ambazo Nchimbi hajakanusha na bahati nzuri hazijamuathiri – yeye na nafasi yake?

Na hapa ndipo linakuja suala la “mtu wa umma.” Hakuna ambaye amewahi kuongelea mke wa Nchimbi. Lakini hayo ni makosa. Naye mama huyo sharti tujue anaishije na mtu wa umma: Ni mfano mzuri wa maisha au ni kukurukakara?

Hata nyumba ndogo ya waziri siyo siri wala siyo kitu cha binafsi. Hapana. Nyumba hiyo yaweza kumchelewesha kufanya maamuzi; kusahau wajibu; kusaliti nchi; au yaweza kuwa chanzo cha kuwa chapuchapu na hivyo mfano wa kuiga. Kwa nini tusijue?

Mapato ya waziri, ukwasi wake usiolingana na mapato na hata marafiki wake wasiolingana na hadhi ya waziri, siyo mambo ya binafsi wala siri. Sharti wananchi wajue kiongozi wao vema.

Bahati mbaya haya hayajawahi kufanywa na waandishi wa habari wa Tanzania. Wameambiwa ni siri. Wameghilibiwa kuwa ni mambo ya binafsi. Kidogo kinachopenya ndicho hicho wananukuu na ndicho kimemfikisha Nchimbi pale alipo – Naibu waziri wa wizara muhimu sana.

Wapi sasa Nchimbi ameparuriwa? Wapi Nchimbi amepunguziwa hadhi? Iko wapi hadhi iliyomomonyoka kama kila tuhuma, lawama na shutuma vimezaa vyeo na “utukufu wa kisiasa?”

Kesi ya Nchimbi dhidi ya Tanzania Daima yaweza kuwa na mvuto wa karne, hasa pale Nchimbi na mawakili wake watakapokuwa wanajenga msingi wa kuhalalisha “kashfa inayozaa neema.”

Jambo moja ni muhimu sana. Historia itaendelea kurejewa. Kufutika siyo rahisi. Kwa utaratibu wa Nchimbi, vizazi na vizazi vijavyo vitashitakiwa sana na vitatakiwa kutoa zaidi mifukoni.

Bali kuna hukumu moja haifutiki nayo ni hii: Kuna yaliyotokea na yaliyotokea ni hayo yaliyokaririwa na Tanzania Daima. Hii ndiyo hukumu isiyoshindika. Twende mahakamani.
 
Mmasai kaingia Disco Bilcanas na mkuki na anachezo hivyo .Huhuhuhuhuuuuuuuuuu
 
Asante Ndimara maana uzee n dawa .Hope kijana ataelewa kwamba asichokoze nyuki watamwangukia .
 
Ndimara ni wa gazeti gani ??

Kada jadili issue iliyopo mbele yetu Ndimara kuwa gazeti gani itakusaidia kweli ? Yeye hana gazeti ila kaandikia mwanaHalisi unasemaje huwezi kuchangia hoja hadi ujue gazeti lake ?
 
Swala la gazeti la ndimara ni lazima lijadiliwe kwa sababu linatuwezesha kujua sera na mtazamo wa mwandishi.ni wazi kuwa kibanda anaandika katika gazeti la mwanahalisi hivyo ni swahiba zake .Binafsi nampongeza sana Nchimbi kwa uamuzi wa busara aliouchukua,yeye kama binadamu anaweza akaona sasa ni wakati muafaka wa sisi wote kujua ukweli wa nini kilitokea badala ya kusoma magazeti tu.Pili ataleta utamaduni mpya kwa wanasiasa kudai haki zao mahakamani pale wanapoonewa na magazeti,magazeti yatajua yanawajibika kutoa habari za kweli na bila kuonea.Nchimbi ata hivyo umekosea,mahakama inachukua muda mrefu sana.watu kama hao ni wa kumwagia tindikali tu.maana hakuna chema kwao.ukidai haki yako mahakamani wanakupinga usiende,nadhani haki aliopewa Ndimara na kubenea ndio wanaoipenda.Mungu awabaliki watesi wa ndimara na kubenea waliowalamba mapanga
 
mmmmmmmmmmmmhhh
 
Loh, hii kiboko! Ukweli uko hapo hapo. Kama ni mtu wa haki na ni muungwana ni wajibu wako kutetea na kulinda your dignity kwa njia iliyo sahihi na inayokubalika. Kweli kuna ubaya gani Nchimbi kwenda mahakamani kutoa jambo lake? Nampongeza Fisadi Mtoto kwa kuliona hilo. Hatuna haja ya kujishikia sheria mkononi.
 
Wacheni nimfafanulie Kada. Ni kwamba, Ndimara Tegambwage ndiye aliyekatwa mapanga wakati Saeed Kubenea alipomwagiwa acid (?) machoni. Ni mwandishi mkongwe, kwa sasa yuko MwanaHalisi.
 
Ha! Kumbe Ndimara ndio yule aliyekatwa mapanga? Iweje sasa anataka Nchimbi atumie njia za porini kudai haki yake ya kikatiba na inayolindwa kisheria!? Tusichanganyane! Nchimbi, najua wewe ni mpenzi wa JamboForum lakini nakusihi usifuate ushauri huo wa Ndimara maana hamtakii mema mwenzake kubenea. Alimwagiwa jicho moja sasa Ndimara anachochea watu waendelee kumwagiana, akitomwagiwa na jicho la pili? Tutaandikiwa na nani gazetini?
 
Ndimara hajasema Nchimbi atumie njia za porini ia Ndimara anachochea Nchimbi aende Mahakamani il akauingie Mkenge .Lakini at the ame time anampa maonyo maana Mahakamani atakuwa kaanza mambo mapya na yeye anayajau huenda yakawa sumu tena kali . Walisema watu hapa mara ngapi kwenda Mahakamani ? Kuanzia JK mwenyewe na wengine wengi hadi hawajafika .Ndimara anamchomekea Nchimbi aenda maana katoa masharti yote yamepigwa chini .
 
Ndugu yangu Mshobozi,
Nikweli yapo machache mazuri ya Nchimbi,lakini kumbuka...MBWA KUMUUMA BINADAMU HIYO SIYO 'NEWS' LAKINI BINADAMU KUMUUMA MBWA HIYO NI ZAIDI YA "NEWS"
Sasa nianze na yanayozaniwa mazuri ya Nchimbi;
1.AMEFANIKIWA KUUONGOZA UMOJA HUO KWA MIAKA KUMI SASA HATA KA NI KIBABE.
2.AMEFANIKIWA KUISIMAMISHA MPAKA INATUMIKA KANUNI MPYA YA UVCCM AMBAYO ILISITISHWA MWAKA 1994.
ZAIDI YA HAYA SIJUI KA KUNA JIPYA!
Lakinbi mabaya ni mengi kuliko mazuri,na tunajadili 'uhalali wa hoja aliyotoa,huku yeye akiwa no.moja kwenye kuhakikisha anaweka mtu wake UVCCM" Kifupi UNAFIKI WA KIONGOZI ALIYEKABIDHIWA DHAMANA KUBWA NA VIJANA WENZAKE.

Achebe, Nakubaliana na wewe kwamba katika mafanikio ya Nchimbi ni pamoja na kuongoza vizuri UVCCM kwa miaka kumi na kufanikiwa kupitisha kanuni mpya ya UVCCM ambayo imelenga kudumisha demokrasia ndani ya UVCCM. Kwa kukusaidia tu, mafanikio yake mengine, tena kwa uchache sana ni kama ifuatavyo;
1. Kushirikiana na Vijana wenzake kudumisha utamaduni wa uungwana ndani ya UVCCM.
2. Kujenga UVCCM yenye viongozi wasomi na wenye ari kujiendeleza kielimu na kitaaluma.
3. Kushirikiana na vijana wenzake kuijengea UVCCM uwezo zaidi wa kiuchumi.
4. Kushirikiana na Vijana wenzake kuelewesha Umma sera za Chama cha Mapinduzi. Ushindi wa CCM ndio kipimo cha kwanza cha mafanikio.
5. Kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kupitia nafasi zake mbalimbali kama vile, senior officer katika idara ya utumishi kwenye moja ya taasisi za serikali hapa nchini, Mkuu wa wilaya mojawapo hapa nchini n.k
Mambo mengine ambayo yanamuelezea yeye binafsi ni pamoja na upole wake, usikivu na busara alizojaaliwa na mwenyezi Mungu. Kama CHADEMA mtafanikiwa kumpata mtu kama huyu naamini mtakodi helikopta 100 za kufanyia sherehe, mkiruka na kujimwayamwaya angani.
 
Mmasai kaingia Disco Bilcanas na mkuki na anachezo hivyo .Huhuhuhuhuuuuuuuuuu

Kweli, Mmasai ni CCM, Disco (Bilicanas) ni CHADEMA mkuki ni Ushindi. Fisadi Mtoto umemwelewa Lunyungu? CCM ITAACHAJE USHINDI: KIONGOZI BORA ATATOKA WAPI!?
 
Achebe, Nakubaliana na wewe kwamba katika mafanikio ya Nchimbi ni pamoja na kuongoza vizuri UVCCM kwa miaka kumi na kufanikiwa kupitisha kanuni mpya ya UVCCM ambayo imelenga kudumisha demokrasia ndani ya UVCCM. Kwa kukusaidia tu, mafanikio yake mengine, tena kwa uchache sana ni kama ifuatavyo;
1. Kushirikiana na Vijana wenzake kudumisha utamaduni wa uungwana ndani ya UVCCM.
2. Kujenga UVCCM yenye viongozi wasomi na wenye ari kujiendeleza kielimu na kitaaluma.
3. Kushirikiana na vijana wenzake kuijengea UVCCM uwezo zaidi wa kiuchumi.
4. Kushirikiana na Vijana wenzake kuelewesha Umma sera za Chama cha Mapinduzi. Ushindi wa CCM ndio kipimo cha kwanza cha mafanikio.
5. Kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kupitia nafasi zake mbalimbali kama vile, senior officer katika idara ya utumishi kwenye moja ya taasisi za serikali hapa nchini, Mkuu wa wilaya mojawapo hapa nchini n.k
Mambo mengine ambayo yanamuelezea yeye binafsi ni pamoja na upole wake, usikivu na busara alizojaaliwa na mwenyezi Mungu. Kama CHADEMA mtafanikiwa kumpata mtu kama huyu naamini mtakodi helikopta 100 za kufanyia sherehe, mkiruka na kujimwayamwaya angani.

Karibu sana ndugu Sad naona ulikuwa msomaji na sasa umeamua kutetea kabisa .Hapa ni JF wako wengi hapa kama akina Kada m Chinga, Mtalii, Darisalam lakini majina ni yale yale yanajirudia nawe ongeza kundi.Naomba sasa angalau mkiwa mmesha kuja kuwatetea wenzenu kueni kama Mzee Es yeye hujenga hoja hata anashindwa lakini you can be convinced na kuunga hoja na huo unakuwa ni mkenge .Msije kulalama tu nakutoa vioja badala ya hoja .

Nchimbi sawa na Lowasa unadhani wanaweza kupokelewa Chadema ? Mie si Chadema wala msemaji wa Chadema ila nadhani Chadema wako makini mno kama kweli watdhani kiongozi wa maana ni Nchimbi.

Naomba turudi kwenye hoja iliyoko hapa .Ku spin and twisting hapa tupo tunao simamia mijadala na hoja wala si vioja .Karibu
 
Karibu sana nudgu Sad naona ulikuwa msomaji na sasa umeamua kutetea kabisa .Hapa ni JF wako wengi hapa kama akina Kada m Chinga, Mtalii, Darisalam lakini majina ni yale yale yanajirudia nawe ongeza kundi.Naomba sasa angalau mkiwa mmesha kuja kuwatetea wenzenu kueni kama Mzee Es yeye hujenga hoja hata anashindwa lakini you can be convinced na kuunga hoja na huo unakuwa ni mkenge .Msije kulalama tu nakutoa vioja badala ya hoja .

Nchimbi sawa na Lowasa unadhani wanaweza kupokelewa Chadema ? Mie si Chadema wala msemaji wa Chadema ila nadhani Chadema wako makini mno kama kweli watdhani kiongozi wa maana ni Nchimbi.
Naomba turudi kweney hoja iliyoko hapa .Ku spin and twisting hapa tupo tunao simamia mijadala na hoja wala si vioja .Karibu

Mwenye macho haambiwi Tazama!Inawezakna haupo huko!!!
 
Back
Top Bottom