anayetakiwa na RA ndiye mwenye nafasi ya kushinda unaweza ifafanua kidogo hiyo? Inaonyesha RA ana nafasi kubwa sana kwenye mustakabali wa CCM na hata nchi mtandao wake si ndiyo ulimweka JK? hebu kata issue hapo
Mkuu wangu Ushirombo,
Heshima mbele, uchaguzi siku hizi ni pesa, leo ninajua kwa mahesabu ya haraka haraka ili uwe kuwa mwenyekiti wa UV-CCM ni lazima umwage angalau Shillingi za bongo millioni 300, sasa honestly analysis Nchimbi au Ridhiwani, watazitoa wapi hizo? Siku zote ni Ra peke yake mwenye huo uwezo na ninajua kuwa huwa anawakopesha na ninajua kuwa anawadai viongozi wengi sana wa juu, ndio maana wameishiwa nguvu ambazo zamani walikuwa nazo sana, matokeo yake wameishia kukosa nafasi zote muhimu walizokuwa wanazitaka ndani ya CCM kwa sababu Asilia wamewabana pabaya, na pole pole wameanza kujiuzulu, hiyo power Mtandao walipewa na Mkapa, na inasadikiwa kuwa moja ya sababu ilikuwa ni yeye Mkapa, kujikingia na maovu yake yasisemwe wazi au kuchukuliwa hatua za kisheria ndio maana akajikita kwa Mtandao,
Lakini things are changing, maana wabunge wa CCM wamekuja juu sana, najua kuwa wabunge sasa wana agenda ya Kiwira na Bandari, ambako kote kuna mikono mizito ya mkapa, muungwana ameshaonyesha kuwa hana ubavu under political pressure, kwa hiyo more political storms are coming.
Waandishi wetu uchwara wameharibu sana kwenye ishu ya Lowassa, kwa sababu angetokea mwanahabari safi asiyekuwa na ubia na hawa wanasiasa, angeweza kufukua mengi sana behind kujiuzulu kwa Lowassa, ambayo hayatakuja kusemwa wazi kwa wananchi kuhusiana na kutoka kwake, kwa sababu ukweli ni kwamba the man was at odd na wabunge kwa muda mrefu sana, kwenye very important ishus za taifa wabunge wamekuwa wakimuonya lowassa na muungwana, kwa muda mrefu sana lakini wote walikuwa hawasikiii, sasa the time is up wabunge hawatasimamishwa tena na anybody, na huko Butiama, ninakukikishia kuwa hakuna usalama huko.
Ahsante mkuu, naomba kukakaa pembeni na huu mjadala.