Dk. Nchimbi tulia! Mwosha huoshwa

Dk. Nchimbi tulia! Mwosha huoshwa

Ndugu yangu Mshobozi,
Nikweli yapo machache mazuri ya Nchimbi,lakini kumbuka...MBWA KUMUUMA BINADAMU HIYO SIYO 'NEWS' LAKINI BINADAMU KUMUUMA MBWA HIYO NI ZAIDI YA "NEWS"
Sasa nianze na yanayozaniwa mazuri ya Nchimbi;
1.AMEFANIKIWA KUUONGOZA UMOJA HUO KWA MIAKA KUMI SASA HATA KA NI KIBABE.
2.AMEFANIKIWA KUISIMAMISHA MPAKA INATUMIKA KANUNI MPYA YA UVCCM AMBAYO ILISITISHWA MWAKA 1994.
ZAIDI YA HAYA SIJUI KA KUNA JIPYA!
Lakinbi mabaya ni mengi kuliko mazuri,na tunajadili 'uhalali wa hoja aliyotoa,huku yeye akiwa no.moja kwenye kuhakikisha anaweka mtu wake UVCCM" Kifupi UNAFIKI WA KIONGOZI ALIYEKABIDHIWA DHAMANA KUBWA NA VIJANA WENZAKE.

Endeleza kumwaga nondo Achebe hadi tufike mwisho .Maoni yote yako na wengine ni sawa ila kumnyama mnyama ndiyo dawa hapa .
 
Tanzania njema na wewe bwana ,
Ama kuona kuwa huyo Benno wakop ambaye unafikiri anaungwa mkono na Membe na JK basi hawezi kuwa anaungwa mkono na Lowassa na Nchimbi?

Muulize huyo Beno wako nani alimpa membership ya club mojawapo iliyopo katikati ya jiji la DSM na ni nani alimdhamini ili kuweza kuandikishwa?

Benno ameomba kuwa member wa club ya Legends club nani alimpa udhamini?acha kukataa mambo usiyoyajua hata siku moja.

Ama kitendo cha BENNO kuishi kwenye nyumba ya kifisadi ya Ridhiwani wewe unaona kuwa hilo nalo haliwezekani?niliwahi kuandika kuhuutatu huu wa JK na Beno na jinsi walivyokuwa wanaoperate leo nipo sijafa na nimerudi rasimi juu ya jambo hili na haswas uchaguzi wa UVCCM stay tuned to get news from the kitchen.

Nianze na wewe haki sawa na uzushi wako,

Cha kwanza kuhusu uungwaji mkono wa hao uliowataja mimi sina habari nao kwani naona ni longolongo tu kama nyingine nyingi zilizojaa masikioni mwa watanzania kama ninyi mnaopenda kula maneno ya mitaani.

Pili sidhani kama kuna club inaitwa Legend club.....fuatilia details zako kwanza halafu udhamini wa klabu hauna maana uungwaji mkono katika uongozi wa nafasi yoyote CCM. Nadhani unahitaji darasa la siasa maana kwa upeo huu fanya uchambuzi katika sekta yako ya Mishen Town. Actully tricky ya kujifanya kusaidia vijana na wanawake ndio iliyokuwa ikimpa kichwa LOWASSA akidhani hiyo itamsaidia kupata loyalty ambayo uchaguzi wa NEC ulithibitisha sivyo hadi akabebwa.

Tatu, Benno hajawahi kuishi ktk nyumba ya Ridhwani kama unavyotaka kudanganya hapa bali ni Ridhwani ndio aliokuwa akiishi katika nyumba aliyopanga pamoja na Benno. Na hiyo unayodai ya nyumba kifisadi ya Ridhwani jaribu kufuatilia ukweli na sio vijungu uchwara vyenu hapa mkidhani mtafanikisha kuwapitisha matapeli wenu kina SLAA na SANDA....never......

Unapomhusisha JK na Ridhwani ni Benno ni ujinga wa hali ya juu kwani mhusika ni Ridhwan na tena kama rafiki wa karibu wa BENNO ni jukumu lake kumsupport mwenziye kwa hali yoyote ile na huo ndio urafiki wa kweli na sio ukibaraka wenu mapokuwa na Ridhwani kujipendekeza wakati chuki binafsi zimewajaa.

I am staying tuned na uzandiki wako usiokuwa na uwezo wa kitaaluma na wala upeo wa habari za kweli....

Tanzanianjema
 
Tanzania njema,
Unajua ni nani aliyemwajiri Beno Malisa UVCCM makao makuu? unakumbukumbu kaajiriwa lini pale? Je kuna kesi yeyote aliyowahi kushinda akiutetea umoja huo kama alivyokuwa akijiita "mwanasheria mkuu wa UVCCM"???? Unajua alishindaje ujumbe wa NEC? Pesa nyingi alizotumia unajua zilikotoka?? Je wajua kwamba Lowassa amefanya mengi kwa kijana mpaka sasa,ikiwa ni pamoja na kumnunulia gari la kampeni? Unajua kwanini Beno amepewa UKAIMU NAIBU KATIBU MKUU WA UVCCM? UNAJUA ALIYEMPA??? UNAZIJUA TARATIBU ZINAZOTUMIKA KUPEWA NAFASI HIYO????...............napumua,nijibu nichambue ukweli.

Nije kwa ndugu yangu ACHEBE,

Moja,ajira ya Benno haikutokana na kupendwa ama support ya hao mafisadi kina Lowassa na wala Nchimbi bali ilitokana na CV yake ambayo hata Makala aliogopa kutokana na mazoea ya kuona vijana wa aina yake tu ndio walikuwa tayari kuchukua nafasi za utendaji Katika UVCCM. Namjua Benno tangia anaingia MLIMANI na nimekuwa karibu naye kama mdogo wangu hivyo nafuatilia karibu maendeleo yake kisiasa hivyo hilo la ajira naljua fika nani na nani wanahusika lakini sio hao unasema wewe. Nchimbi alikubali kwa kuwa alijua ukaribu wa Benno na mtoto wa mweneykiti wake na si vinginevyo.

Kuhusu kesi, kumbuka Benno ni mwanasheria wa UVCCM na sio wakili wao. Yeye ni msimamizi wa masuala ya kisheria makao makuu na sio mtetezi mahakamani hivyo unapokuja na suala la kushinda kesi nahdani unakosea.

Kuhus ushindi wa NEC katu usimhusishe na Lowassa. Benno alikuwa mgombea pekee kati yao aliyekuwa akizunguka nchi nzima kwa mabasi na daladal. Hlo ni uhakika nalo kwa nimeshuhudia zaidi ya mara mbili hayo tulipokutana mikoa fulani mimi nikiwa na majukumu mengine tofauti kabisa.

Suala la kuwa na gari ni uongo mkubwa na support ya lowassa hakuwa nayo kwani alikataa kabisa temptations hizo ambazo lowassa alikuwa akizitumia kupitia kale kajambazi na kabakaji kake Fredy Lowasa. Benno alikataa katakata kupata msaada wao. hili nina uhakika nalo asilimia 100.

Kuhusu nafasi za Ukatibu Msaidizi na hata Unaibu Katibu Mkuu yayote hayo yametokana na presha na misuto kutoka kwa JK kuhusiana na tabia ya kuwapa majukumu vijeba kama kina Thom Mwang'onda na wengineo na kuacha kuwajengea uwezo vijana wa kweli. Kama unafuatilia siasa kumbuka vijembe vya JK katika mkutano wa Dodoma mwaka 2006. Hilo ndio liliwafanya kina Nchimbi na na yule medicre Makala kuwakubali Benno na vijana wengine ili kutimiza matakwa ya JK na sio vingine.

Uteuzi wa unaibu katibu mkuu ilikuwa ni mbinu ya Nchimbi kumwengua Benno kugombea uenyekiti na sio vinginevyo. Na katu si Nchimbi wala Lowssa waliohusika hata chembe na uteuzi wa Benno kama naibu katibu mkuu. Fuatilia habari za ndani za CC kama unaweza.....hivyo vikao vingine vilikuwa vinatoa baraka tuu, maamuzi yalishafikiwa.....

Tanzanianjema
 
ACHEBE endelea kumkoma nyani kwa uwazi na nguvu nzito. Tanzanianjema ni mmoja wa vijana wa Nchimbi anauma huku na kule .Yuko na akina Zitto lakini pia na akina Membe so yeye kazi yake kuvuta huku na kule .Tunakujua wewe kijana na hapa mjini tunakuona unavyo fanya mambo yako .

Wewe ni wa kukuacha kuendelea na ujinga wako maana ni wazi u mmoja wa wale wengi wanojiona wananijua kumbe patupu kabisa....

Najua tatizo ni urafiki na ukaribu wangu na Zitto ambao wewe na wajinga wenzio CHADEMA mnaona unawapunguzia nafasi ya kumnyonya kiuchumi na kisiasa ndugu yangu huyu.......

Ukweli ni kuwa mawazo mgando yenu na ukada pofu wenu unashindwa kuelewa kuwa kuna njia tofauti za kufanya kazi za kisiasa na sio lazima kupleadge loyalty kwa makundi yenu ya kisiasa mnayoyaita vyama.

tanzanianjema
 
Uhuuu, kazi ipo. Huku naona sipawezi ngoja niende zangu kwenye thread ya Obama.
 
Wewe ni wa kukuacha kuendelea na ujinga wako maana ni wazi u mmoja wa wale wengi wanojiona wananijua kumbe patupu kabisa....

Najua tatizo ni urafiki na ukaribu wangu na Zitto ambao wewe na wajinga wenzio CHADEMA mnaona unawapunguzia nafasi ya kumnyonya kiuchumi na kisiasa ndugu yangu huyu.......

Ukweli ni kuwa mawazo mgando yenu na ukada pofu wenu unashindwa kuelewa kuwa kuna njia tofauti za kufanya kazi za kisiasa na sio lazima kupleadge loyalty kwa makundi yenu ya kisiasa mnayoyaita vyama.

tanzanianjema

Tanzaianjema upo mkulu wangu ?Naona unashuka vilivyo maneno hapa.Kata issue kaka mie naangalia kwa mbali .Kuna vibweka kwenye siasa.Mimi kama Kitila naishia zangu nakaa mbali nisome nipate raha .
 
He! Sasa haya ya nyumbani tumwachie nani? Tusikimbie matatizo yetu jamani, tusaidiane kuyatatua

Sasa kama watu wanaonyeshana jinsi wanavyowajua hao wanasiasa wa CCM, wanapolala, wanavyokula, walivyonunua magari na wanavyokwenda club, wewe unaona sisi wengine tuna cha kuchangia tena hapa?
 
Wakulu leteni nondosss, duh inabidi niipitie hii kitu yote toka mwanzo vizuri zaidi, maana damn! kuna neno hapa!
 
Haka ka dhambi ka kuweka viongozi madarakani ni kbaya Mwalimu meant well lakini sasa wengine wanakachukulia kama ujiko na kuendeleza mirdi yao na kuacha maslahi ya watu ndiyo madhara haya yanamkuta Nchimbi.Kazi ni kubwa endeleeni kutupatia habari sie yetu macho nakujifunza .
 
Irene ana chuki zake mwenyewe kwa Nchimbi

Na Zephaniaanjela

Nimeisoma kwa makini makala ya Mwandishi Irene Mark ya kumtaka Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Dk. Emmanuel Nchimbi atulie kwa vile mwosha hatimaye naye huoshwa.

Katika makala hiyo iliyoanza kuchapishwa kwanza katika gazeti la Tanzania Daima Toleo la Jumapili Machi 9, 2008, Irene amejitahidi kwa kadri awezavyo "kumshambulia" Dk. Nchimbi kama mtu binafsi zaidi tofauti na chanzo kilichopelekea achukue hatua hiyo ambayo hakika inasikitisha!

Tatizo nililoliona katika makala yake hiyo ni kuingiza ushabiki na chuki binafsi, itikadi za kisiasa huku lengo lake hasa likiwa ni kutaka kumdhalilisha kwa maslahi anayoyajua mwenyewe.

Waliokuwepo katika mkutano wa Dk. Nchimbi na waandishi wa habari, Machi 5, 2008, wanajua kile alichozungumza na kujibu vizuri maswali yote aliyoulizwa na watu kama Muhibu Saidi wa gazeti la Mwananchi, hivyo kuja na madai nje ya kile alichosema katika kikao hicho ni sawa na kufanya ukuwadi wa kisiasa kwa niaba ya Chadema, na pia inawezekana amefanya hivyo kwa nia ya kutaka kumfurahisha mwajiri wake wa kweli, Freeman Mbowe.

Dk. Nchimbi anayehusishwa na historia ya kuunda na kusimamia makundi katika Umoja wa Vijana na CCM kama taasisi za kisiasa hata siku moja hajawahi kuhusika na hilo, badala yake waandishi wa habari wasiojua siasa kama Irene ndio wamekuwa wakihadithiwa uongo na wapinzani wa CCM na kuubeba kama ulivyo bila ya kutafiti.

Kwa mfano, ni ujinga mtupu kumhusisha Dk. Nchimbi kwa namna yoyote ile na suala la mgogoro na hatimaye kusambaratika kwa ndoa ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia UVCCM, hayati Amina Chifupa, mwaka jana.

Nimejaribu kuisoma makala yake hiyo kuanzia gazetini hadi katika mtandao, lakini sikuona popote alipothibitisha kwa namna moja ama nyingine kuhusu jambo hilo iwe kwa kuonyesha ushahidi wowote usio na mashaka, badala yake ametumia uvumi wa mitaani unaoweza kuzungumzwa na mtu yeyote wakiwemo makuwadi wa fitina kwa watu.

Uandishi wa kusukumwa na utashi wa kisiasa na kujifanya mpiganaji wa mstari wa mbele kuliko hata Mbowe, Dk. Slaa na viongozi wengine wa Chadema ni kushusha hadhi ya taaluma, hivyo Irene kama anataka kuingia katika siasa ni vuzuri akatangaza hadharani ili wanasiasa pia anaowatungia uzushi kama Dk. Nchimbi nao waweze kumjibu kwa haki majukwaani ama vinginevyo kuliko kubishana kwa njia anazotaka wafanye akidhani ni watoto kama yeye.

Ni makosa makubwa kushabikia kile anachoita "kumbukumbu" ama rekodi huku akijua kwa uhakika kabisa kuwa hazipo na kumhusisha mtu na jambo kubwa kama kusambaratisha ndoa ya mume na mke, tena kwa sababu za kisiasa, suala ambalo haliingia kichwani ila labda kwa mtu asiyekuwa na akili timamu!

Kwa mfano, hivi Irene akiulizwa kuwa ndoa ya Amina Chifupa na Mohammed Mpakanjia ilikuwa na uhusiano gani na ubunge, Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM ama Unaibu Waziri wa Dk. Nchimbi atatoa ushahidi gani?

Atajitetea kwamba watu walikuwa wakizungumza na yeye akasikia ama atatoa ushahidi wa maandishi alioupata kutoka kwa Mpakanjia?

Au, kama ni kweli kuwa Dk. Nchimbi alifanya hila kuisambaratisha ndoa ya Amina ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa, Irene anataka watu waamini kuwa Mpakanjia ana akili finyu kiasi cha kufikia hatua ya kumtaliki mkewe aliyezaa naye mtoto kwa kuamini uvumi wa barabarani?

Ni ujinga mwingine mkubwa kutaka kumlazimisha Dk. Nchimbi awe anajibu kila upumbavu na tuhuma za utumbo zinazotolewa na wapinzani wake kisiasa na kuacha shughuli zake za kuitumikia nchi yake kutokana na madaraka makubwa matatu ya kisiasa aliyonayo akiwa Mbunge wa Songea Mjini, Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Wakati Irene akisema mwishoni mwa makala yake kuwa Dk. Nchimbi ni mwanasiasa asiyependa kuzungumza na vyombo vya habari, mimi nasema kiongozi huyo hapendi kuzungumzia "umbea" na majungu, na pia hapendi kuongea na waandishi wa habari wanaoandika maoni yao zaidi katika habari zao badala ya kutoa taarifa sahihi walizoziona, kusikia au kuhadithiwa kwa kuambatana na ushahidi na vielelezo vya dhati pale inapobidi kufanya hivyo.

Mwandishi wa habari anayekusanya "umbea" na kudai ni kumbukumbu zilizosemwa zamani huku mtuhumiwa akiwa kimya na bila popote pale alipojaribu angalau kumtafuta iwe kwa simu ama ofisini kwake bila mafanikio

Waandishi waliosheheni "umbea" kama Irene ndio wanaweza kuja na uvumi kutoka uchochoroni kwamba Dk. Nchimbi alimpoteza Amina kutoka kwenye anga za siasa kwa kumtengenezea zengwe kutokana na sababu anazozijua mwenyewe.

Kila ninapotaka kumshangaa mtoto huyo wa kike anayekuzwa na kulelewa Bilcanas Club ninashindwa.

Hivi Amina alikuwa na kitu gani kinachoweza kusababisha Dk. Nchimbi apoteze ubunge wake, apoteze Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM au Unaibu Waziri alionao kama siyo uongo na upeo mfupi wa kuchambua mambo?

Iko wapi nguvu anayodaiwa kuwa nayo Amina katika ulingo wa kisiasa iwe katika UVCCM, CCM na kadhalika? Angewezaje kuwa na nguvu na kufikia hadi kumtisha Dk. Nchimbi wakati alikuwa chini kabisa katika matawi akiendesha kampeni za kusaka ukamanda wa Vijana ili angalau apate jukwaa la kusemea?

Nani asiyejua kuwa Amina alikuwa akifanya hadi utapeli kwa kuahidi kutoa misaada ya kifedha kwa UVCCM kama alivyofanya katika mkoa wa Dar es Salaam, lakini "akaingia mitini" na kuwaacha solemba chipukizi aliodai kuwa angewapeleka mkutanoni Dodoma?

Kama Irene haamini haya aende kwa Katibu wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sixtus Mapunda katika jengo ilipo Studio ya Redio Uhuru, jirani na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM akaambiwe ukweli huo, tena kwa kuonyeshwa kumbukumbu za maandishi na siyo kwa hadithi za kuchonga kama anazokuja nazo yeye.

Akitoka huko aende pia awaulize Makatibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni ili katika sehemu hizo zote nako apewe uthibitisho na kisha atoe hukumu mwenyewe.

Katika hali hiyo hata bila kuzungumzia matatizo mengine makubwa aliyokuwa nayo Amina, hivi mwanasiasa kama huyo angewezaje kumtisha Dk. Nchimbi na katika jambo lipi?

Tukiachana na Amina, Irene pia anaonyesha kuwa ni mbumbumbu mkubwa kabisa wa masuala ya kisiasa anapokuja na mfano mwingine dhidi ya Dk. Nchimbi kuhusu kile anachodai ni mgogoro uliokaribia kuzuka kati yake na aliyekuwa mpinzani wake katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM, Jane Claude Mihanji.

Pamoja na kuishia kusema tu kuwa Dk. Nchimbi alihusishwa hadharani na mambo mazito kwamba alijaribu kumfanyia Mihanji, hilo nalo haliwezi kukubalika hata kidogo na ndiyo maana hata Jeshi la Polisi liliona kuwa ni uongo uliotungwa kwa malengo "machafu".

Jane alidai aliitwa nyumbani kwa Dk. Nchimbi huko Tabata jijini Dar es Salaam, na kwamba wakati wakiwa pamoja sebuleni wakizungumza na kujadiliana mambo kadhaa ya kisiasa, ghafla alikuja mtu dirishani na kupuliziwa sumu asiyoyajua, tuhuma ambazo hata mjinga kabisa hawezi kuzikubali.

Namshauri Irene aulize watu wanaojua undani na ukweli kuhusu uongo huo ili wamwambie kwa ushahidi namna Jane alivyokuwa ameahidiwa ubunge wa kuteuliwa na hatimaye Unaibu Waziri wa Habari na mmoja kati ya "vigogo" waliokuwa na nia ya kugombea urais mwaka 2005 ili amtumie kukidhi matakwa yake ya kisiasa.

"Kigogo" huyo wa CCM hakutaka Dk. Nchimbi agombee Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM kwa sababu alijua kuwa angeibuka mshindi, hivyo ili kuzuia jambo hilo akapanga kumwibulia kashfa na kumtafuta Jane ambaye bila hiyana akaingizwa "mkenge" na kujifanya kapuliziwa madawa yenye sumu sebuleni ili apofuke macho au afe kabisa.

Hata madaktari kama Maua Abeid Daftari walihoji kwenye kikao cha Kamati Kuu na "kigogo" aliyekuwa akimtumia binti huyo akashindwa kutetea uongo wake ni namna gani sumu hiyo ipulizwe sebuleni walipokuwa wawili, lakini imfuate Jane peke yake na kumuacha Dk. Nchimbi utadhani ina akili na macho.

Mkakati huo ulikuwa ni jaribio la pili la kutaka kumwengua Dk. Nchimbi baada ya awali kuletwa hoja ya umri kuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM aliyevuka miaka 30 hata kama hajafikisha 35 asigombee Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM, lakini likagonga mwamba na kusambaratishwa.

Kilichoulizwa na watu wenye busara katika Kamati Kuu ya CCM ni jinsi gani sharti hilo liwepo katika ngazi ya taifa peke yake huku kwenye matawi, kata hadi wilayani wanachama wa Umoja wa Vijana wenye umri wa zaidi hadi miaka 34 wakiwa wamegombea uenyekiti na nafasi nyingine za kuchaguliwa katika ngazi hizo na kushinda.

Wakashindwa kujibu swali la kama uchaguzi huo katika ngazi hizo zote nchini kote ufutwe na kuanza upya au kama sharti hilo la dharura lilikuwa ni maalum kwa ajili ya mtu mmoja, hivyo ikaamuliwa kuwa kanuni hiyo ya uchaguzi ianzie uchaguzi mkuu wa UVCCM unaofanyika mwaka huu kwa sababu ilichelewa kuletwa.

Hata hivyo, wale waliokuja nayo mwaka 2003 wakiwa na umri wa miaka 26 hivi leo wanasaga meno kwa vile tayari wana umri wa miaka 31, ule ambao kama walivyotaka iwe mwaka huo hivi sasa hawana sifa ya kuwania uongozi wowote katika UVCCM.

Hata madai kuwa Dk. Nchimbi ni mmoja katika kile kinachoitwa ni kundi la wanamtandao linaloaminika kuwa kinara wa siasa za kuchafuana na kupakana matope nao pia ni uongo mwingine.

Wanasiasa dhaifu ndani na nje ya CCM ndio wanaeneza uvumi huo, lakini hawataki kabisa kuzungumzia ukweli kuwa kinachowakera wengi akiwemo Irene na wale wanaomtuma kuonyesha ujinga wake ni ubora wa mikakati ya wana CCM waliokuwa wakimuunga mkono aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Jakaya Kikwete katika harakati zake za kuwania uteuzi wa kugombea urais mwaka 2005.

Katika mbio hizo, jumla ya wana CCM 11 walichukua fomu za kuwania nafasi hiyo. Mbali na Kikwete, wengine waliojaribu bahati zao ni Mzee John Malecela, Frederick Sumaye, Salim Ahmed Salim, William Shija, Idd Simba, John Shibuda, Ali Abeid Karume, Abdallah Kigoda, Mark Mwandosya na Patrick Chokala.

Hivyo, idadi hiyo ilisababisha kuwe mitandao 11 ya kusaka wadhifa huo, lakini unaong'ang'aniwa na waandishi wenye chuki zao wenyewe ni mtandao wa Kikwete utadhani Mwandosya, Malecela, Sumaye, Kigoda au Salim Ahmed Salim hawakuwa na ya kwao.

Inaeleweka kuwa Mei 3, 2005, mitandao yote hiyo iliishia hapo baada ya Kikwete kuteuliwa kuwa mgombea urais, lakini wajinga wa kufikiri na wale wenye chuki zao bado wanaeneza majungu dhidi ya viongozi kama Dk. Nchimbi waliokuwa katika kundi hilo lililoshinda kwa ubora wa mikakati.

Kina Irene hawasemi hata kidogo kama Mbowe naye alikuwa na mtandao wake alipokuwa akichuana na kina Anna Maulida Komu, Hebron Mwakagenda na wengineo katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kutoka Chadema.

Hawasemi kabisa kuwa mitandao yote ya harakati hizo huishia pale mshindi anapopatikana na kubakia mmoja tu unaowaunganisha wanachama katika ujumla wao, hivyo wanachofanya wale wanaong'anga'ania kuwepo "mtandao" wa Kikwete hadi leo katika CCM na kuwahusisha wanasiasa mahiri kama Dk. Emmanuel Nchimbi wana chuki zao wenyewe!
NAKUSHUKURU SANA KWA KUWA MKWELI NA KUMTENDEA HAKI NCHIMBI PAMOJA NA UVCCM.KWANZA KAULI YA NCHIMBI ILIKUWA NI SAHIHI KABISA KWA KUWA ILIKUWA INAWATAKA VIJANA WAANZE MWAKA WA UCHAGUZI NA WASIINGILIWE.EJN ALIUCHUKUA UMOJA WA VIJANA UKIWA UMEVUNJWA NA MKAPA KWA MIAKA ZAIDI YA MIWILI.AKANZA KUUJENGA UPYA.....ALIUKUTA UMOJA WA VIJANA UKIWA NA GRADUATE 2 TU AMBAO NI NDG KIPEPE NA ZAHORO HAJI AMBAO WALISOMA URUSI NA INDIA RESPECTIVELY...AKAUNDA KAMATI YAKE YA KWANZA YA UTEKELEZAJI AMBAPO ALIWATEUA MPAKA MAHASIMU WAKE KAMA UHAULA AMBAE ALIKUWA NI MSOMI,MONGELA AMBAE ALIKUWA PIA NI MSOMI....UHAULA AKAENDELEZA FITNA ZA KAMPENI KANA KAMA UCHAGUZI HAUKWISHA,AKAMVUMILIA.KWA KUTAMBUA UMUHIMU WA VIJANA KULEA CHIPUKIZI NA KWA KUWA UHAULA ALIKUWA MWENYEKITI WA CHIPUKIZI KWA MIAKA KUMI BASI KWA MOYO MWEMA NCHIMBI AKAMTEUA UHAULA KUONGOZA IDARA HIO.WAVIVU WA KUFIKIRI MKAONA NI UONEVU....LEO HIO ANAONDOKA UMOJA WA VIJANA KUKIWA NA GRAUATES ZAIDI YA ISHIRINI WACHACHE WAO NI:
1.EMANUEL NCHIMBI ADPA,MBA MZUMBE UNIVERSITY
2.FRANCIS ISAACK Bsc SUA
3.BENO MALISA LLB UDSM
4.YASINTA MBONEKO BA UDSM
5.MLAY Bcom UDSM
6.S KIPEPE BA LENIN UNIVERSITY
7.CHACHA MWITA-UDSM
8.ERNEST MAKUNGA-LLB OUT
9.SAID BWANAMDOGO-BA(STATISTICS),MBA UDSM
10.AMOS MAKALA-ADA IFM
11.SIXTUS MAPUNDA-BA UDSM
12.PETER MBAGO-BA UDSM
13.PETER SELUKAMBA -ADA IFM
14.GREY MWENGU-BA ED UDSM
15.HADIJA FARAJI-BA UDSM
16,COSTA KANYASU-BA OUT
SASA WAJINGA NDIO WANAOSEMA HUMU KUWA NCHIMBI ANAPINGA WASOMI,NAPE MALIZA SHULE YAKO KARNE HII UMOJA WA VIJANA WA CCM HAUWEZI RUDI NYUMA NA KUONGOZWA NA MTU AMBAE HAJAMALIZA HIGHER INSTITUTION KAMA KIONGOZI WA VIJANA CHADEMA.KATIKA WATU WOTE WALIOONYESHA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA NCHIMBI KATI YA 17 NI MMOJA TU AMBAYE NI NAPE HAJAGRADUATE NA MBAYA NI MKUBWA KWA UMRI KULIKO WENZIE..TENA FAMILIA YA MNAUYE HAIMTAMBUI ALIJITANGAZA KUWA NI MTOTO WA MNAUYE BAADA YA MZEE KUFA.INASEMEKANA BABA YAKE HALALI NI MTUSI.
 
.............SASA WAJINGA NDIO WANAOSEMA HUMU KUWA NCHIMBI ANAPINGA WASOMI,NAPE MALIZA SHULE YAKO KARNE HII UMOJA WA VIJANA WA CCM HAUWEZI RUDI NYUMA NA KUONGOZWA NA MTU AMBAE HAJAMALIZA HIGHER INSTITUTION KAMA KIONGOZI WA VIJANA CHADEMA.KATIKA WATU WOTE WALIOONYESHA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA NCHIMBI KATI YA 17 NI MMOJA TU AMBAYE NI NAPE HAJAGRADUATE NA MBAYA NI MKUBWA KWA UMRI KULIKO WENZIE..TENA FAMILIA YA MNAUYE HAIMTAMBUI ALIJITANGAZA KUWA NI MTOTO WA MNAUYE BAADA YA MZEE KUFA.INASEMEKANA BABA YAKE HALALI NI MTUSI.........

Ndugu yangu Fisadi mtoto,kweli we fisadi mtoto..kwanza hapa mimi ndo niliyetetea kuwa yapo mazuri machache ya Nchimbi nikayataja na kuomba wenye mazuri mengine wayataje,mwisho wa siku tuyapime na yanayosemwa mabaya yake!!!!!!!Ongeza nondo za uzuri wake walau ujae kijiko cha chai ili tujadili vizuri.

Hili la bwana mdogo Nape nadhani UZANDIKI huo unataka kuvuka mipaka.FITINA hii iliwahi kutumika mwaka2003/2004 alipogombea mara ya kwanza Uenyekiti wa vijana...tena nakumbuka ilikuwa gazeti la Tazama ambalo lilikuwa mahususi kumbeba Nchimbi na mtandao wakati huo na ndo maana sasa moja ya nguzo muhimu za gazeti hilo yupo UVCCM,Charles Charles ka shukrani kwa kazi nzuri.
Nakiri simfahamu sana Nape lakini machache nayafahamu juu yake maana naikumbuka vizuri hoja hii...ALIYEMPELEKA NAPE CHUO CHA SIASA KIVUKONI-CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWL.NYERERE MWAKA 2001 NI BRIG.GEN.(rtd) MOSES NNAUYE NA KUANDIKISHA KUWA NI BABA YAKE MZAZI AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA ANAMLIPIA MASOMO YALE.
-ILIPOIBULIWA HOJA YA UBABA WA NNAUYE KWA NAPE MSEMAJI WA FAMILIA MZEE GALLUS ABEID-(sasa ni mtumishi Taasisi ya Mwl.Nyerere Dar kama msaidizi wa mzee Butiku) alikuja na orodha ya watoto wa mzee Nnauye,ambayo ilitiwa sahihi na Mzee Nnauye mwenyewe tena mwaka 1983 ambayo alidai coppy iko ikulu na mahakamani kwa ajili ya shughuli za mirathi na kwa Mzee Makamba ambaye naye alithibitisha kuwa na coppy ya watoto wa mzee Nnauye yenye jina la Nape,tena limeandikwa Napalepe,hili ni jina la kimakonde lenye maana ya "HATA IWEJE ITAKUWA"
Data kwa uchache wa hoja yako, SI VIZURI KUTUMIWA, WANAKUTUMIA ILI MUMUHARIBIE KIJANA WAWATU BIAL SABABU,HAO HOJA HIYO ILIWAHI KUJA NAKUKUMBUSHA NI UZANDIKI AMBAO ULIKWISHA SHINDWA SIKU NYINGI. HIVI KAMA IPO KWENYE ORODHA YA WATOTO TENA MAHAKAMANI KWA AJILI YA MIRATHI ANAYESEMA NI MWANA FAMILIA NA HAMTAMBUI NI NANI??? HAO MAFISADI WANATAKA KUJIFANYA WASEMAJI WA FAMILIYA??? UKIHITAJI DATA ZAIDI NINAZO,ACHA KUTUMIKA WANAKUUZA.
HILO LA UMRI WA NAPE NALO LILITUMIKA WAKATI ANAGOMBEA NEC 2007,BAHATI MBAYA LIKASHINDWA DAKIKA YA MWISHO TENA JK AKAWAUMBUA "msimuonee Nape mpeni haki yake" wakajaribu kuhakikisha anaanguka huku wakidhani yupo shule India atashindwa,kila wakitathimini dogo anashinda wakataka basi walau awe wa mwisho,akawachana mashine waliotakiwa na mafisadi akiwemo Beno.Akapata kura za kishindo!!!!Ikiwa aligombea NEC akaruhusiwa leo miezi sita baadae eti manakuja na hoja ya kuzidi umri,ajabu kabisa!!Labda asitake tu yeye mwenyewe kugombea na ndio dua za wapambe wa Nchimbi na wafuasi wake maana wanajua si mchezo akiingiza jina.Ninachokumbuka huyu bwana kazaliwa mwishoni mwa mwaka 1977 na ndo maana Nchimbi kwa kuweweseka akatangaza kuwa atakayegombea awe amezaliwa 1978 anataka kumzuia Nape,jambo ambalo linamnyima usingizi.
DHAMBI YA NAPE NI MOJA TU,SI MWANAMTANDAO TENA ALIYEWAZI KUSEMA POPOTE BILA AIBU NA UKWELI WAKE UNAWATISHA MAFISADI. LA ELIMU NILICHOSIKIA TOKA KWA WAPAMBE WAKE ANAMALIZA MAY 2008 ANAKUJA NA DEGREE TENA SIO MOJA......wacha nipumue!
 
Achebe naona unaanza mambo ya Character assassination hapa .Mnyika na CCM Vijana kuna connection? CCM kuanzia Chama hdi vijana kuna wasomi wa ukweli na ku foji vyeti Nchi iko wapi ? Kama kuna wasomi na wanatumia usomi haya ya wewe kuja kulalama hapa yana maana gani ? Kwa nini msiyamalize huko huko ambako mna vijana wasomi kama akina Nchimbi nk ? Kusoma kukariri ama kusoma kweli kuwa na shule ? Yaani Nchimbi naye ni msomi ? Hebu ongelea mambo ya CCM usaidiwe ama endeleza kampeni zako bila kuwahusisha wasio wana CCM. Mnyika anakujaje hapa ?
 
Dr Aisha Kigoda hawezi kuwa kwenye kundi la Nchimbi kamwe. Aisha amesomea udaktari katika ngazi inayoitwa Assistant Medical Officer, ambao nchini Tanzania wanatambulika na pia wana leseni kutoka Baraza la Madaktari, na katika leseni zao hizo hutambuliwa na kuandikwa Dr (kabla ya jina la mhusika). Kwa hiyo Dr Aisha Kigoda "hajajiita" daktari, bali kapewa cheo hicho na Baraza la Madaktari baada ya kufikia kiwango ambacho Baraza hilo linakubali aitwe hivyo. Na wala hajafoji vyeti, maelezo yake anayotoa kwenye wasifu wake ndiyo elimu halisi aliyo nayo, na vyuo alivyosoma ni vya Tanzania na vinatambulika. Msimwonee dada wa watu.

Ngugu yangu...ni ukweli wanwitwa Dr, lakini sina uhakika kama wanastahili kuitwa hivyo mtu aliyesomea Assistant Medical Officer (AMO) akitaka kuwa full Medical Doctor...ni lazima asote tena miaka 5 pale muhimbili au kwingine hapa Tanzania. Kwa hiyo sina uhakika kama baraza linawaita hivyo ila wanajipachika na kupenda tu basi...na wala haina haja yoyote.
 
Basi kukupendezesha aitwe Half (1/2) Doctor,lakini bila ubishi wowote yeye ni Doctor anayetambulika na Wizara kwa licence anayopewa na Board of registrar same kama Doctor aliyesomea Russia anapewa diploma akija TZ Wizara inampa full doctor kama unavyotaka baada ya kumaliza intern yake, lakini ukitaka nikueleze physical performance ya huyo 1/2 Doctor na full doctor wako lazima tupate wagonjwa wawili na tuangalie TBS standard,
Hivyo basi ukiangalia kwa undani Udoctor wa Nchimbi ni tofauti sana na wa Aisha. LETE MAMBO ZAIDI
 
Hapa kwenye maandishi mekundu, sijakuelewa. Mtu akisoma udaktari Urusi akirejea nyumbani anapewa diploma [na nani],alafu akimaliza internship wizara inampa full udokta, je, waliosoma Cuba, Guyana, China n.k. inakuwaje? Hapa unatudanganya. Requirement ya wahitimu wote wa udaktari mahali na kutoka chuo chochote ni kufanya internship kwa mwaka mmoja katika hospitali ya rufaa au hospitali yoyote iliyoruhusiwa kwa shughuli hiyo. Baada ya kumaliza internship na kufaulu hiyo internship, unaenda kujisajili kenye baraza la Madaktari Tanganyika (Tanganyika Medical Board). Ukishasajiliwa unakuwa unatambulika rasmi kama daktari wa binadamu na unaruhusiwa kufanya kazi ya tiba.
 
Umesema Tanganyika M A ? Yaani baada ya miaka 46 ya Uhuru kuna sheria ya Tanganyika ?
 
Umesema Tanganyika M A ? Yaani baada ya miaka 46 ya Uhuru kuna sheria ya Tanganyika ?

Yes Lunyungu,

Zipo sheria nyingi tu zilizotungwa enzi za Tanganyika na bado zinafanya kazi Tanzania ya leo mojawapo ni hii inaitwa "Medical Practitioners and Dentists Ordinance, Cap.409"ambayo ilifanyiwa marekebisho madogo kwa kwa sheria hii "Medical Practitioners and Dentists (Ammendment) Act 1968., hizi zote zinasomwa kwa pamoja.

Hiyo sheria Cap.409 ndio inaunda Medical Council of Tanganyika, na siyo Tanganyika Medical Board kama nilivyosema hapo awali kenye post yangu ya kwanza. Sheria hiyo hiyo inaunda pia "Optical Council of Tanganyika"

Kwa hiyo usishangae, Sheria zote ambazo hujulikana kama "Ordinance" zilitungwa kabla ya Uhuru, na baada ya uhuru zinajulikana kama "Acts".

Bila shaka umeelewa.
 
Asante sana kwa maelezo yako wacha ninywe chai kwanza maana nimepata kichaa baada ya ufafanuzi wako .
 
Achebe naona unaanza mambo ya Character assassination hapa .Mnyika na CCM Vijana kuna connection? CCM kuanzia Chama hdi vijana kuna wasomi wa ukweli na ku foji vyeti Nchi iko wapi ? Kama kuna wasomi na wanatumia usomi haya ya wewe kuja kulalama hapa yana maana gani ? Kwa nini msiyamalize huko huko ambako mna vijana wasomi kama akina Nchimbi nk ? Kusoma kukariri ama kusoma kweli kuwa na shule ? Yaani Nchimbi naye ni msomi ? Hebu ongelea mambo ya CCM usaidiwe ama endeleza kampeni zako bila kuwahusisha wasio wana CCM. Mnyika anakujaje hapa ?

Ili kuweka records sahihi, aliyeleta issue ya elimu ya kiongozi wa vijana wa CHADEMA ni Fisadi Mtoto siyo ACHEBE. Tuendelee kukata mawe, maana hata majina ya wachangiaji yanaweza kukueleza ni kwanini wanaelekeza madongo kwa Vijana wa CHADEMA wakati issue iliyo kwenye discussion ni NCHIMBI na UCHAGUZI WA UVCCM!
 
Back
Top Bottom