Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
DIWANI KATA YA KAMSAMBA AMEMPONGEZA RAIS SAMIA NA MBUNGE CONDESTER KWA KUPOKEA MILIONI MIA TISA ZA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA MOMBA
Diwani wa Kata ya Kamsamba Jimbo la Momba Mhe. Kyalambwene Kakwale amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha za Miradi mbalimbali Shilingi Milioni 949,293,000 katika Kata ya Kamsamba.
Diwani wa Kata ya Kamsamba amempongeza pia Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe kwa jinsi anavyolisemea Bungeni Jimbo la Momba hatua iliyopelekea Serikali kupeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika Elimu, Afya, Zahanati, Barabara na Masoko.
Mhe. Kakwale amevitaja Vijiji vilivyopokea fedha za miradi
Kijiji cha Senga 268.32
Kijiji cha Muuyu 96.5
Kijiji cha Kamsamba Milioni
Kijiji cha Muungano Milioni 9.9
Kijiji cha Usoche Milioni 72.584
Kijiji cha Mkonko Milioni 340
Diwani Kakwale amesema hayo wakati wa Mkutano wa Mbunge Condester Sichalwe uliofanyika Shule ya Sekondari ya Wazazi Kamsamba kilichowahusisha viongozi wote wa CCM Kata ya Kamsamba, Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji.
Viongozi hao wa Kata ya Kamsamba Jimbo la Momba walielezea changamoto mbalimbali kwa Mbunge Condester Sichalwe na kuomba kuendelea kulisemea Jimbo la Momba ili miradi mbalimbali iendelee kutekelezwa kama Ilani ya CCM 2020-2025 inavyotuelekeza.
Mhe. Condester Sichalwe amesema kuwa ajenda yake kwa sasa ni kuwaleta Wataalam wa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo kwenda Kila Kijiji cha Jimbo la Momba ili kuwapa Elimu ya Kilimo chenye tija kwaajili ya kuongeza ufanisi katika sekta za uzalishaji zinavyofanyika Jimboni
Mhe. Condester Sichalwe amesema Serikali imejitahidi kutekeleza majukumu yake ikiwemo Kusambaza Umeme Vijijini, Elimu, Afya, Barabara, Ulinzi na Usalama na kuahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha maendeleo ya wananchi.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.49.jpeg72.2 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.56(1).jpeg58.8 KB · Views: 6
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.58.jpeg57.4 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.51.jpeg77.2 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.50.jpeg98.2 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.51(1).jpeg55.3 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.54.jpeg44.1 KB · Views: 5
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.52.jpeg76.7 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-28 at 21.41.53.jpeg60.1 KB · Views: 4