Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,461
12,339
1702369789871.png

Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za Wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki saa nane na dakika tisa usiku wa kuamkia leo December 12,2023.

Familia ya Dr. GeorDavie imethibitisha kutokea kwa msiba huo wa Kijana wao Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
---

Aliyekuwa Mwanamuziki, Mwandaaji na Mwongoza Video za Muziki #Tanzania, Nic Davie maarufu #DirectorNisher amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Desemba 12, 2023 huku Familia ikiwa haijaweka wazi chanzo cha kifo chake

Nisher ambaye ni Mtoto wa Mhubiri Geor Davie amewahi kuongoza Video za Wasanii mbalimbali, baadhi ni Weusi, BenPol, (Unanichora & Jikubali), Fid Q (Bongo HipHop), Baraka da Prince (Jichunge) na Young Killer ft. Fid Q (13) na kupata Tuzo ya Chaguo la Watu (Peoples Choice Awards) kama Director Bora wa Mwaka 2014
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom