Dira2023 Kwa Mabinti na Wanawake; Jipe thamani: THAMANI yako haitokani na Mwanaume

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
DIRA2023 KWA MABINTI NA WANAWAKE; JIPE THAMANI; THAMANI YAKO HAITOKANI NA MWANAUME.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani!

Na huu ndio ujumbe wenu, enyi mabinti na Wanawake. Hii iwe ndio dira yenu. Jipe THAMANI! Na katika thamani hiyo elewa kuwa sio lazima itokane na Sisi wanaume.

Ninyi ni Wake zetu, Mama zetu, Dada Zetu, Bibi zetu, shangazi na mabinti zetu. Tunawapenda, na siku zote MTU anayekupenda lazima akuambie ukweli, akupe Haki yako, akuambie nini chakufanya. Taikon nitafanya hivyo Kwa sababu ninawapenda.

Nafahamu wapo ambao ninawakera, labda Kutokana na kupishana uelewa na mitazamo. Lakini hiyo haibadili dhamiri yangu, nayo ni kuhakikisha jamii yetu inapata Watu Bora, Wanawake Bora na wanaume Bora.
Na ili kitu kiwe Bora lazima kinolewe katik misingi ya ukweli na Haki.

Wanawake eleweni kuwa thamani yenu haitokani na Sisi wanaume. Thamani ya MTU haitokani na MTU mwingine. Thamani ya mtu inatokana na MTU mwenyewe.
Thamani ya Mwanamke inatoka ndani mwake mwenyewe.

Oooh! Mwanamke ambaye hajaolewa Hana thamani! Huo ni uongo Mkubwa!
Sio lazima uolewe ili uwe na thamani.
Kinachokupa wewe thamani ni namna unavyojua kuziheshimu rasilimali zako.

1. Kuheshimu Rasilimali mwili wako.
Maumbile yako namna unavyoyathamini, unavyojitunza na kuwa msafi,
Sio unakuwa mchafu na kutojiheshimu Kwa kuruhusu kila mwanaume akupande, hiyo inakuondolea heshima yako.

Ndoa haikupi heshima kama hauheshimu Rasilimali mwili wako. Embu assume Mwanamke aliyeolewa alafu awe anafanya umalaya. Je ataheshimika? Jibu ni hapana, unaona kumbe MTU anaweza akaolewa na bado asiheshimike. Hivyo ndoa haimpi Mwanamke heshima, Bali kujitunza.

2. Kuheshimu Rasilimali Muda.
Jipe thamani Kwa kuheshimu muda wako. Sio kila mara unakaa vibarazani kupiga umbeya umbeya kama Zuzu. Nafahamu ninyi ni Wanawake umbeya Wakati mwingine kwenu ni muhimu. Lakini Isiwe muda wote. Tenga muda wako vizuri angalau muda wa umbeya uwe hata saa moja. Sio Mbaya. Kwani umbeya Kwa Wanawake ni starehe najua.

Sio muda wote unashinda sebuleni unaangalia Tamthilia za kikorea. Huko ni kutojiheshimu. Weka ratiba zako vizuri.

Kama Mwanamke jishughulishe na shughuli za uchumi hata kama ni ndogondogo, ukiwa nyumbani tengeneza ubuyu, tengeneza kashata, tengeneza barafu au ice-cream, juisi n.k.
Jipe thamani. Usisubiri kuletewa kama Zuzu au kama maiti.

Tumia muda wako vizuri, alafu uone kama kuna Kima yeyote atakusogelea.

3. Heshimu Vipaji na karama zako.
Jipe thamani mtoto wakike Kwa kuheshimu vile ulivyobarikiwa. Ninawafahamu Wanawake wengi wanaoheshimika Kwa Vipaji vyao.

Usipoteze muda, kama unajua kuimba imba, kama unajua kucheza Cheza, kama unajua kuchora chora, kama unajua u-MC kuwa MC Acha kudharau uliyobarikiwa nayo.

Hakuna mwenye kipaji anayekitumia asiheshimike dunia Hii. Kipaji hutoka kwa Mungu.

Mabinti msiwe wapuuzi ninyi ni binadamu kamili ingawaje mnayomapungufu lakini hayawazuii kuwafanya mjipe thamani.

Msipende vya burebure.
Hakuna anayependa vya bure akawa na thamani Dunia na akhera.
Ukishapenda vya Bure, unadharaulika Automatically.
Mimi Taikon nikikutana na majitu yanayopenda vitu vya Bure huwaga najua nini chakuwafanya. Dawa ya Watu wavivu inajulikana.

Watu pekee ambao mnapaswa mpate Huduma za bure ni Baba zenu na waume Zenu Basi. Au Kwa mbali Wachumba zenu na Ndugu zenu. ila Kwa hao sio lazima.

i. jishaueni, Ringeni, ninyi ndio maua ya Dunia.
Lakini sio uringe Wakati hauna thamani yoyote, tutakuona Zuzu.
Hujiheshimu unaringaje?
Hujishughulishi na kazi unaringaje, kama sio Zuzu ni nini?

Ninaposema mfanye kazi sio mfanye kama Sisi wanaume noop! Ila ni Ile kuonyesha kuwa mnajiweza na hamtaki kuwa mzigo Kwa MTU yeyote.

Pesa yenu iwe yenu Hilo hatutabadilisha, ila kumsaidia Mchumba au Mumeo sio kosa.
Tayari nilishawaonya kuwa Msiwe na Mwanaume mpumbavu hivyo mnajua ni mwanaume gani wa ku-share naye Mali zenu.

Sio wewe ndio umlishe mwanaume Zuzu Wakati anaafya njema. Nawe utakuwa Mwanamke Zuzu.
Mwanaume lazima ahenyeke, apambane Kwa ajili yake na familia yake.

Wewe kama MKE au mpenzi wake kazi yako iwe kumsaidia tuu katika majukumu na sio kumpa mzigo.

ii. Kula Raha, Kula na kunywa Kwa Afya.
Kama hujaolewa, vile vipesa uvipatavyo vitumie Kula vizuri unawiri, sio ukondeane kama huna mikono.
Kula bata.

Alafu usicheke cheke na Vimwanaume mshenzi visivyojitambua, Focus.

iii. Usifanye mambo ili upendwe na wanaume.

Ila fanya mambo kulinda thamani yako Mbele ya jamii.

Utajikuta mtumwa wa wanaume. Kuna wanaume mazuzu yasiyo na Akili. Hata uyafanyie nini hayaoni ufanyacho, hayana shukrani. Yatauumiz moyo wako, yatakunyanyasa licha ya kuwa ulimfanyia mpaka mambo yaliyokudhalilisha, lakini bado limwanaume halioni Hilo.

Usifanye vitu kumu-impress mwanaume labda mambo ya Haki na wajibu wako.

Wangapi wanavaa uchi ili wasifiwe na wapendwe na wanaume, si umewaona, zaidi ya kudharaulika, kuchezewa na kuharibiwa kuna kingine walipata. Na Sisi wanaume tunajua Kutumia udhaifu wenu.

Ati uhangaike ili Mumeo asichepuke, fanya wajibu wako. Lakini usijitese kisa MTU mwingine labda awe mtoto mdogo asiyejiweza. Lakini ujitese kisa jitu Zima huo ni Uzuzu. Usikubali kufanywa Zuzu.

Ni kweli wanaume tunatamaa lakini haitufanyi tushindwe kuwaheshimu na kuwapenda.

iv. Usimvumilie Mwanaume mpumbavu.
Hata hivyo nafahamu Wanawake wanaojielewa kamwe hawawezi kuvumilia upumbavu.

Nimeshasema;
a)Kula vizuri
b) Lala muda wa kutosha
c) Vaa vizuri, pendeza
d) Fanya shughuli zako Kwa ufanisi,
e) Muda wa umbeya piga umbeya au ingia mtandaoni kusoma udaku na umbeya wa mtandaoni,
f) Fanya mazoezi kuupa mwili wako nguvu,
g) Usicheke na Kima au MTU yeyote anayetaka kuteteresha thamani yako.

Rekebisha mapungufu na Tabia ambazo zinaharibu thamani yako.
Alafu usiumizwe kichwa Kwa nini hauolewi, Mwanaume sahihi atakuja tuu ikiwa utaweza kuimaintain thamani yako.
Lakini sio uhangaike kutafuta Wanaume wenye utajiri au Mali automatically utakuwa umejishusha thamani yako.

Weka Akili;
Wewe sio bidhaa,
Wewe sio uwanja wa vita ATI mwanaume akupige,
Wewe sio sehemu ya wanaume kutupia uchafu wao.
Wewe sio wale Wanawake wanaotafuta Sifa za kijinga.

Wewe ndiye Mwanamke msaidizi namba moja WA mwanaume katika kuitawala Dunia.
Wewe ndiye Mama wa kuleta Watoto Duniani na kuhakikisha wanakuwa Watu Bora katika Dunia. Sio uzae tuu na kutuletea panya Road.
Wewe ni chombo cha Starehe Kwa mwanaume unayempenda ambaye ni mume wako. Full stop.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu hapa umepiga mbizi kwenye lami, kwa jnsi ninavyowaelewa hawa viumbe sidhani kama kuna mtu atakuelewa na kufanyia kazi bandiko lako.!
 
Umeandika kitu kirefu sana, ila wanawake saiv wanawaza itakuaje swala la hello jua, they want to do best. No kitambaa, ni rotana. Na haya maeneo yote ni wanaume ndio wanashikilia uwezekano. Thamani na starehe zote hizi. 😂😂😂. Ni swala gumu
 
Kasikilize nfoma ya Ngwea ft Mwana FA & Lady Jay Dee - Sikiliza ndio utaelewa Ngwea alikuwa anaeleza kuhusu nini?
Hiyo ngoma imebeba ujumbe mzito Sana kuhusu wanawake.
Ingekuwa vizuri Zaidi Kama kila mwanamke aliyepo humu jf angetenga muda wake kdgo akae chini aisikilize hyo ngoma.
 
Unaposema thamani ya mwanamke haitokani na mwanaume wakati mwanamke kaumbwa kwa ajili ya mwanaume unakuwa unatuchanganya mkuu.......vinginevyo unakuwa huna tofauti na wale wanaharakati wa feminism.
 
Siku zote mwanamke anatafuta attention ya mwanaume ili apate furaha na amani;matendo kama kuvaa nusu utupu, kutafuta sana kuolewa na kupenda sana publicity.

Bible iliwahi kusema kule mwanzo wivu wa Hawa utakua kwa Adam milele means hata Hawa wa leo mwendo ni uleule.

Nadhani mwanamke hawezi kua na utulivu mwenyewe bila ku-side na mwanaume
 
Mshauri pekee wa mtoto wa Kike wa hiki kizazi ni MAZINGIRA yanayomzunguka,,,, kama hayupo kwenye mazingira stahiki basi kudra za Mwanyazi Mungu pekee ndo za kusubiriwa.. We piga keleleeeee utakavyo ila kama mazingira yanayomzunguka hayaeleweki ujue kuna msingeli mmoja ndo kazishika akili zake....
 
Hii nadhani unawalenga wanawake wale smart kichwani japo sio wengi sana lakini wapo, au na wale mapoyoyo wakisoma andiko watabadilika?
 
Back
Top Bottom