Mwanamke ameumbwa na mali ndani yake ila sio mwanaume

African Geek

JF-Expert Member
Jul 29, 2022
778
1,354
Siku hizi vijana wengi wa kiume wanaona ni haki yao kusaidiwa na mwanamke kwenye mambo ya kiuchumi, yaani mwanamme atafute na mwanamke atafute. Kuna wengine ndo wanataka walelewe kabisa yani wao ndo watafutiwe na mwanamke wapewe.

Ila nawakumbusha. Mwanamke analetwa duniani akiwa na mali ndani yake, yani mwanamke ndio mali yenyewe. Sawa sawa na mali zingine hapa duniani.

Sisi wanaume tunaletwa duniani tukiwa hatuna kitu cha kujivunia. Yaani mtoto wa kiume anakuja duniani akiwa hana thamani yoyote. Ni kazi yake sasa kupambana kuitafuta thamani yake. Na thamani ya mwanaume ni dunia yenyewe yani ahangaike nayo atafute elimu, mali, heshima, nk. Vitu hivi ndio thamani ya Mwanaume.

Usijidanganye kuwa wewe ni handsome, sijui una body kubwa. Kama hujipambanii kuitafuta thamani yako kamwe hautakuwa na thamani mbele za watu.

Mwanamke anavyozidi uzuri ndio thamani yake inazidi kupanda ila mwenzangu na mimi hata uwe handsome kiasi gani kama ni kapuku utaonekana ni kinyago tu.

MORAL OF THIS THREAD: WANAUME TUPAMBANE

💪
 
Kweli kabisa sio mwanaume una shinda dressing table kujiremba na wengine wanashinda Gym kutengeneza six packs bila kuwa na pesa mwisho wa siku ni dharau hata kuinamishwa..))
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom