Kopo la chooni lina thamani chooni na si kwenye meza ya chakula

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
#KOPO_LA_CHOONI

Kopo la chooni likikutwa kwenye meza ya chakula ni kesi kubwa, kila mtu atatukana limefikaje pale.

Ila ukienda chooni usilikute kelele ni kubwa sana, lazima tutataka kujua nani alilitoa.

Kopo la chooni lina thamani chooni na siyo kwenye meza ya chakula.

Na binadamu ni hivyohivyo;

Kuna sehemu ukienda hakuna anayeweza kuona thamani yako, tena unaweza hata kupigwa kwa nini umeenda pale;

lakini kuna sehemu usipoonekana kuna watu wanalala njaa. Kumbe kila mtu ana thamani kubwa sana katika eneo lake acha kujiona ufai

Jipe moyo kwa kila gumu ambalo unalipitia ukijua wazi kua halitodumu daima katika maisha yako.

Ukiona watu wamefanikiwa yapo magumu waliyapitia hadi kufikia katika ndoto zao.

Mungu akupe moyo Wa UVUMILIVU .
 
Ni kweli kabisaa ataa ule ugonjwa hatari unaowashinda madakitari bigwa, una bingwa wake mchimba kaburi
 
Back
Top Bottom