Kazi yenye thamani kubwa kuliko zote Duniani

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,116
22,566
Salaam, Shalom!!

INTRODUCTION.

Sifa kuu ya KAZI, ni iwe halali, pili iwe na malipo ya kuweza kukusustain maisha Yako, yaeza kuwa umejiajiri au umeajiriwa, KAZI ni KAZI, ilmradi mkono uende kinywani.

KAZI pia Si Kwa ajili ya kujipatia kipato pekee, KAZI pia ni Kwa ajili ya AFYA pia, ndo maana wenye kufanya KAZI zinazoitwa white collar jobs, lazima wafanye pia mazoezi Ili kulinda AFYA Kwa ujira au faida ya KAZI wazifanyazo.

Najua unazijua KAZI nyingi zenye kulipa, zenye kuingiza kipato kikubwa, lakini, Leo katika mada hii nakuambia IPO KAZI yenye kulipa kuliko KAZI zote, yenye thamani kubwa unazozifahamu, fuatana nami tafadhali, usijekuwa unafanya KAZI Kwa HASARA.

MADA: KUHUBIRI INJILI, NI KAZI YENYE THAMANI KUBWA, INAYOLIPA KULIKO KAZI ZOTE DUNIANI.

Ndivyo ilivyo, KAZI zote tunazofanya ni Kwa ajili ya tumbo, ikiwa tunafanya KAZI na kujihangaisha maisha yetu yote Ili kushibisha tumbo, na kuhakikisha familia na vizazi vyetu vinaishi maisha Bora, kula vizuri, kulala vizuri, kusafiri katika magari ya kifahari, kunywa nk nk, KAZI zetu ni BATILI, tunajihangaisha Kwa ajili ya CHOO.

Kula, kunywa kulala Si vitu muhimu vitupasavyo kuvihangaikia.

Ndege wa angani Wana mavazi, wanakula bila kulima shamba, wanakunywa na wanalala na kuamka kama sisi.

KWANINI KAZI YA KUHUBIRI INJILI INA THAMANI KULIKO KAZI ZOTE DUNIANI?

Sababu kuu ya kwanini KAZI ya kuhubiri INJILI ,ni yenye thamani kuliko KAZI zote ni kuwa: KUHUBIRI INJILI KUNAHUSIKA NA KUOKOA ROHO.

Roho ya mwanadamu Ina thamani kuliko kitu chochote duniani, ndo maana tajiri akiwa katika kufa, Yu tayari Kutoa kiasi chochote Cha Fedha au Mali Ili asife lakini Haiwezekani.

Hakuna KAZI au Mali yoyote iliyo na thamani zaidi ya Roho ya mwanadamu, hivyo, kuvuna Roho zilizopotea na kuzirudisha ziwe hai na kuurithi Uzima wa Milele, ni KAZI yenye thamani kuliko zote Duniani.

1. Petro alikuwa mvuvi, aliacha uvuvi na kwenda kuhubiri INJILI.

2. Mtoza ushauri, TRA officer, aliacha KAZI yake na kwenda kuhubiri INJILI.

3. Luke aliacha Udaktari wake na kwenda kuhubiri INJILI.

Nimesguhudia watu wenye KAZI nzuri wakiziacha na kwenda kuhubiri INJILI.

Wengine wameacha uinjinia, uanasheria, ualimu, nk nk na kwenda kuhubiri INJILI, hivyo kamwe usidharau wahubirio INJILI ,ukadhani wamekosa KAZI ya kufanya.

JINSI YA KUHUBIRI INJILI.

Si wote wameitwa kuwa Wachungaji, wainjilisti au watumishi direct, unaweza kuhubiri INJILI Kwa njia ZIFUATAZO.

1. Ikiwa umeajiriwa, toa pesa zako sawasawa na utakavyosemeshwa na Mungu kusupport INJILI, utakuwa na utalipwa sawa na wahubiri INJILI, sababu umeshiriki kuwapeleka.

2. Ikiwa umejiajiri pia toa sehemu ya pesa zako, support INJILI, lipia ada watoto wa wahubiri INJILI, utakuwa umefanya KAZI yenye ujira kuliko KAZI yoyote duniani.

3. Ikiwa u MKULIMA, wape maskini chakula, waambie kuwa umetumwa na YESU sawasawa na maagizo yake. Wambie Yesu awapenda.

4. Ikiwa u tajiri, lisha yatima, wajane, hudumia wagonjwa hospitali, na Wambie, Yesu amekutuma kuhubiri INJILI Kwa njia hiyo.

Ikiwa hujaokoka, huna KIBALI Cha kuhubiri INJILI, fuatisha Sala hii kupata KIBALI Cha kuhubiri INJILI;

SEMA: EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU.

Amen, Mbarikiwe nyote 🙏
 
Mtoa mada mara ya mwisho umetoa lini zaka? Ulitoa kwanani?
Huwa nalipa ZAKA, sitoi ZAKA.

Kwa maana hayupo aliyemkopesha Mungu pesa au chochote Hadi atoe kumpa Mungu msaada, Mali zote Mbinguni na duniani ni Mali yake.

Sababu ya kulipa ZAKA, ni kulinda kipato changu, AFYA, nk nk.

In short Mimi hulipa ZAKA Ili nisipungukiwe mahitaji yangu.

Na kubwa kuliko yote, hutoa Ili kuhubiri INJILI Kwa njia m alimbali.

Karibu.
 
Muwe serious wakat mwingine.
Ikiwa Mungu aliacha utukufu Mbinguni, akaja katika mwili wa mwanadamu Ili tu ahuhubiri INJILI kuokoa ROHO za WANADAMU na kuzimu,

Wewe ni nani usihubiri INJILI Kwa namna mbalimbali?

Au unajua KAZI yenye thamani, INAYOLIPA kuliko kuhubiri INJILI ututajie?
 
Hubiri INJILI Kwa namna mbalimbali Ili ujenge nyumba Yako Kwa msingi wa Dhahabu Mbinguni.

Wahubiri INJILI ni matajiri No 1. Duniani na Mbinguni.

Amen
 
Ikiwa Mungu aliacha utukufu Mbinguni, akaja katika mwili wa mwanadamu Ili tu ahuhubiri INJILI kuokoa ROHO za WANADAMU na kuzimu,

Wewe ni nani usihubiri INJILI Kwa namna mbalimbali?

Au unajua KAZI yenye thamani, INAYOLIPA kuliko kuhubiri INJILI ututajie?
Mungu gani aliyekuja duniani!? Hilo jambo sijawahi kuamini.

Sawa tufanye alikuja, kama unamgeza yeye basi usioe, usipige MUCHINGA maana ye hakumpiga mtu MUCHINGA, ufunge siku 40, usiwe na nyumba wala makazi maalum, we zurula tu kueneza neno.
 
Yesu ni Mungu,

Hawezi Kuoa, sababu Kanisa ndo bibi harusi wake.

Hubiri INJILI Kwa njia zote.

Usihangaikie choo!!
 
Huwa nalipa ZAKA, sitoi ZAKA.

Kwa maana hayupo aliyemkopesha Mungu pesa au chochote Hadi atoe kumpa Mungu msaada, Mali zote Mbinguni na duniani ni Mali yake.

Sababu ya kulipa ZAKA, ni kulinda kipato changu, AFYA, nk nk.

In short Mimi hulipa ZAKA Ili nisipungukiwe mahitaji yangu.

Na kubwa kuliko yote, hutoa Ili kuhubiri INJILI Kwa njia m alimbali.

Karibu.
Umeshawai kumlipia mtoto wa mchungaji wako ada ya shule??.........hao wako watalipiwa na nani ??
 
Mkiandika mada kama hizi hakikisheni zinakuwa fupi fupi
Acha uvivu,

Kitabu Cha page 600 utasoma Kwa muda Gani kama thread hii unaona ndefu?

Hubiri INJILI, ufanye KAZI yenye thamani kuliko zote.

Ubarikiwe.
 
Huwa nalipa ZAKA, sitoi ZAKA.

Kwa maana hayupo aliyemkopesha Mungu pesa au chochote Hadi atoe kumpa Mungu msaada, Mali zote Mbinguni na duniani ni Mali yake.

Sababu ya kulipa ZAKA, ni kulinda kipato changu, AFYA, nk nk.

In short Mimi hulipa ZAKA Ili nisipungukiwe mahitaji yangu.

Na kubwa kuliko yote, hutoa Ili kuhubiri INJILI Kwa njia m alimbali.

Karibu.

Kwenye agano jipya na la kale kulikuwa na wachungaji matajiri kama saizi ?
Zamani hicho kipindi mafuta yaliuzwa ?
 
Kwenye agano jipya na la kale kulikuwa na wachungaji matajiri kama saizi ?
Zamani hicho kipindi mafuta yaliuzwa ?
Hajawahi tokea Hadi sasa mtumishi tajiri zaidi ya Ibrahim, Daudi, na Suleiman.

Hubiri INJILI Kwa njia zote uwezavyo,

Ubarikiwe 🙏
 
Back
Top Bottom