Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Hatuja zungumzia technology tumezungumzia dini na tamaduni.


Tamaduni ndiyo inayozaa vitu kadhaa ikiwemo sayansi na teknologia.-- utamaduni wa muafrika ni uchawi na kulogana tu.
 
Hizi dini zote sita ni za Mungu mmoja au miungu tofauti?
Kiufupi naamini Mungu yupo, na amejidhihirisha wazi kabisa. Kila jamii dunia mzima nguvu ya Mungu ipo. Kuna dini kubwa sita duniani. Kote Mungu anajionesha. Kuna
~Judaism
~Christianity
~Islam
~Hinduism
~Budhism
~Sikhism
Mtawa(monk) wa kibudha anaweza fanya maajabu makubwa sana ya kutembea juu ya maji au kutembea bila kukanyaga ardhi(kupaa) Kama Yesu. Lakini si mkristu Wala mwislam.
 
Kama waarabu walikuwa na utamaduni wa kuwaua watoto wa kike hao waarabu kwa nini hawakuisha duniani? Utopolo mtupu.
Tatizo la mada yako linaanzia hapa,na limeonyesha waI kabisa lazima ukosee katika mada nzima, kwanini uijadili Dini kama Tamaduni za watu fulani na ushindwe kuijadili Dini kama dini ?

Kuifasiri Dini kama tamaduni ya watu fulani au za watu fulani kumeonyesha wazi ya kuwa hujui tamaduni ni nini na kadhalika hujui Dini ni nini. Nakupa mfano ambao unaonyesha dhahiri shahiri kuuita Uislamu ni tamaduni ya waarabu, ni kosa la kiufundi, miongoni mwa Tamaduni za Waarabu ilikuwa wanapo zaliwa watoto wa kike, wao walikuwa wanaona kama ni mkosi na kufikia hatua wakawa wana wazika wakiwa hai, ila Uislamu ulipo kuja ukakataza hili.

Sasa nakupa kanuni ya msingi kuhusu dini, hii unatakiwa uishi nayo ni kuwa "Dini imekuja kumtoa mtu katika hali duni kiutendaji na kumpeleka katika hali ya juu zaidi kiutendaji,kadhalika Dini imekuja kuzikosoa na kurekebisha katika zile mila na desturi zetu, yaani Tamaduni zetu". Katika hili kuna mifano mingi sana.

Ahsante.
 
Kwa nini unafikiri hakukuwa na haja hiyo?
Hakuna.

Lakini, naomba nikuulize swali dogo sana, unaweza kuniambia kwanini umeuliza mja alichaguliwa kuja kufikisha ujumbe Tanzania, je unafikiri kulikuwa na haja hiyo ?
 
Hakuna.

Lakini, naomba nikuulize swali dogo sana, unaweza kuniambia kwanini umeuliza mja alichaguliwa kuja kufikisha ujumbe Tanzania, je unafikiri kulikuwa na haja hiyo ?
wewe ndo umesema mola uchagua mja kwa ajili ya kupeleka ujumbe sehem.

ndo nataka unambie uyo mja alietumwa kwetu huku mimi simjui
 
Tamaduni ndiyo inayozaa vitu kadhaa ikiwemo sayansi na teknologia.-- utamaduni wa muafrika ni uchawi na kulogana tu.
Sio kweli ,wafrika na tunatamaduni nyingine nzuri pia. kumbuka ata kwa wazungu napo uchawi na kulogana kupo
 
Sio kweli ,wafrika na tunatamaduni nyingine nzuri pia. kumbuka ata kwa wazungu napo uchawi na kulogana kupo


Wewe umesikia wapi mzungu akiruka ndani ya ungo???, Muafrika anaruka ndani ya ungo kwa kutumia sayansi ya giza yenye masharti ya kishenzi, utasikia ukitaka kuruka ndani ya ungo kwanza umuue mama yako au baba yako au nduguyo wa karibu, pili unapotaka kuruka lazima uwe uchi tatu lazima ufumbe macho hadi mwisho wa safari yenu, nne lazima iwe ni usiku.

Sasa angalia sayansi ya mzungu, ipo wazi na hakuna madharti ya kishenzi kama ya Muafrika, kinachofanya ndege ya mzungu ipae angani ni Bernouli principle, lazima kuwe na hewa, lazima ndege itumie injini nk, vyote hivyo vipo wazi kwa kila mtu anayetaka, huo ni mfano mmoja ninaokupa ili uone utofauti kati ya African culture vis a vis European culture.
 
Kama waarabu walikuwa na utamaduni wa kuwaua watoto wa kike hao waarabu kwa nini hawakuisha duniani? Utopolo mtupu.
Kwanini hujiulizi kila siku watu wanakufa, na hawaishi... ?

Pili, ongeza umakini nilisema walikuwa wanaona ya kuwa na watoto wa kike ni mkosi, hili mosi, pili wakafika mbali na kuwaua watoto hao, ulipo kuja Uislamu ukakataza mila hizo.
 
Kwa nini unafikiri hakukuwa na haja hiyo?
Mimi siyo kwamba nafikiri bali majibu ninayo ya kwanini mitume hawakuanzia huku kwetu.

Sasa wewe ndiyo ujibu swali nililo uliza huko juu.
 
Sababu huki hapakuwa na haja hiyo.


Katika kila umati Allah alituma mitume, wapo mitume ambao Allah amewataja/amemuhadithia mtume SAW (ndani ya Qur'an) na wapo Mitume ambao hakuwataja, na duniani wamepita mitume zaidi ya laki moja na ushee, hadi huku Africa mitume walikuwepo kwa ajili ya makabila nk.
 
Katika kila umati Allah alituma mitume, wapo mitume ambao Allah amewataja/amemuhadithia mtume SAW (ndani ya Qur'an) na wapo Mitume ambao hakuwataja, na duniani wamepita mitume zaidi ya laki moja na ushee, hadi huku Africa mitume walikuwepo kwa ajili ya makabila nk.
Nitajie mitume walio kuwepo huku Afrika na utupe ushahidi huo.
 
Niliwahi kusoma makala fulani online kitambo sana kuwa Dunia yetu imepitia zama mbali mbali lakini mukhtadha wa makala ile uliigawa dunia katika zama tatu

1, Unknown
Zama hii ni zama ambayo binaadamu hakua anajua chochote kuhusu lolote
Yaani alikua anaishi kama wanyama na hajui kwanini vitu vinatokea, jambo pekee alilokua anajua ni kuhakikisha anajitahidi kuwa hai kwa kula na kujaamiana nk

Knowledge
Baada ya miaka mingi binaadamu akaanza kutambua baadhi ya mambo yanatokea kwasababu fulani. Na akitaka kitu fulani basi afanye hivi
Zama hii kukafanyika maendeleo makubwa ya binaadamu na mambo ya kuishi pamoja na uongozi nk yakaibuka, ubinafsi tamaa chuki na ubabe vikatawala

Superpower
Baada ya miaka mingi binaadamu wakaanza kuzidi kujiuliza kwa mambo ambayo hawakuwa na majibu nayo,,,,,,hii ikapelekea binaadamu kuanza kuamini kuna kitu kingine kina nguvu zaidi ya upeo wao wa ufahamu, maana waliona vinatokea lakini hawajui kivipi na kwanini
Hapa zikaanza kuzaliwa imani za Mungu, mizimu nk, wakajitokeza watu wanaodai kuwasiliana na Mungu mizimu nk na hapo zikazaliwa dini na mambo ya kichawi sana

Sayansi
Binaadamu wakazidi kuendelea na kuanza kupata majibu ya vitu vingi kwa kuvithibitisha kwa kupata majibu na ufumbuzi
Dunia ikaingia kwenye mapinduzi makubwa ya kisayansi na imani za kichawi na mizimu zikaanza kupungua baada ya majibu kuwa yanapatikana lakini imani ya supernaturally bado ikawepo sababu bado kuna mambo mengi hayakua na majibu pia

Sayansi na teknolojia
Hii ndio zama tuliyo nayo sasa
Watu wanaamini sana katika sayansi na teknolojia lakini supernatural bado imani hiyo ipo na ndio maana dini bado zipo

Kwa mujibu wa makala hiyo imani ya supernatural vizazi vijavyo itapotea kabisa na teknolojia pengine na kitu kipya vitashika hatamu
Dunia ya leo kuna wengi hatuamini tena kuhusu Supernatural na tunaamini katika sayansi na teknolojia
 
Back
Top Bottom