Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Nitangulie kwa kusema Utamaduni ni neno pana linalojumuisha mfumo mzima wa Maisha, lengo la Uzi huu ni kuonesha ni jinsi gani tulivyoubeba utamaduni wa kigeni na kuufanya dini zetu na pengine tumenufaika nao ama kuumizwa nao pasipo kujua.

Nitawapitisha kwenye vipengele vya utamaduni 'Culture'. Hapa Ukristo nitauita 'Jewish Culture', Uislam kama 'Arabic Culture' na dini ya mwafrika ambayo ni 'African Traditional Religion' nitaiita African Culture. Kwahiyo nitazungumzia utamaduni wa kiyahudi, kiarabu na kiafrika. Sitarajii kupata maswali ya NINI MAANA YA DINI. Hapa hiyo dini yako naijadili Kama tamaduni tu wa watu fulani.

1. Uongozi na siasa. Waafrika walikuwa na tamaduni zao za kupata kiongozi, pia sheria na kanuni zao kabla ya kuletewa tamaduni mpya za kiarabu zilizoletwa na wa Asia hasa waarabu na kiyahudi zilizoletwa na wazungu. Kwenye makabila mengi, kiongozi wa kijadi alivaa kofia mbili, ya kisiasa na kidini kwenye matambiko. Ukristo ukaleta taratibu zake, siasa na dini zilitenganishwa. Huu ni utamaduni wa kiyahudi ambao haukuwa na uhusiano kati ya makuhani na magavana wa kirumi.
Uislam Kama ilivyo utamaduni wa kiarabu. Siasa na dini hufungamana. Ndiyo maana kuna nchi zinazofuata 'Sharia' za kiislam/kiarabu katika kuamua na kuongoza. Hizo zote ni tamaduni tu za watu, siyo maagizo ya Mungu.

2. Music. Waafrika wana vyombo vyao vya muziki 'music instruments' na styles zao za uimbaji 'musical notations'. Zeze, filimbi, ngoma, pembe za wanyama nk... Wakristo wakachukua muziki wa kiyahudi na kirumi uliotajwa kwenye Biblia. Baragumu, tarumbeta, zeze, vinanda...kuwa muziki safi wa kumwimbia Mungu. Kwa wakatoliki Papa Gregory akapendekeza Tuni fulani itumike duniani kote 'Gregorian music'. Hali kadhalika Waislam na kaswida, dufu ambazo ni musical notation za kiarabu wakazifanya nyimbo za kumsifu Mungu. Ni utamaduni tu, Mungu hana aina fulani ya kuimbiwa.

3. Language. Lugha zetu za kibantu zilitumika kuomba na maombi yakapokelewa. Viongozi wa kimila walitambika kwa Lugha zao kwa Miungu yao. Wazungu wakatuletea ukristo katika lugha ya kilatini. Ibada na misa zilifanyika kwa Lugha hii kwa karne kadhaa. Warumi ndiyo walikifanya kilatini kiwe lugha ya Mungu ingawa Mambo yalibadilika badae. Uislam kwakuwa ni utamaduni wa kiarabu, wao Hadi leo huamini Mungu anajua kiarabu tu. Hakijabadilika chochote. Ni utamaduni tu, hata kichina na kijapani Mungu anakisikia.

4. Food. Chakula katika utamaduni wa kiafrika una makatazo na kanuni za kula chakula. Kulikuwa na hadithi zenye kukataza au kuruhusu chakula/mnyama fulani. Utamaduni wa kiyahudi hali kadhalika, Kuna chakula haram na kisicho haramu, ingawa warumi wamefanya yao kugeuza masndiko. Kuna wakristo wanaokula kila kitu na wale wanaochagua kulingana na mapokeo ya agano la kale la kiyahudi. Waislam pia, utamaduni wa kiarabu katika chakula umebebwa kama ulivyo. Haram na Halal ni kadiri ya utamaduni wa kiarabu ambao walifungamana sana na wayahudi. Ndiyo maana, haram zilizopo katika Agano la kale utazikuta kwenye Qur'an.

5. Art, craft and Architecture. Sanaa na ubunifu. Waafrika tulikuwa na styles zetu za ujenzi wa nyumba za kuishi na ibada michoro na mapambo. Lakini leo hii nyumba za ibada zetu ni sawa na mahekalu ya kiyahudi na kirumi kwa wakristo, kukiwa na nakshi za misalaba. Kwa waislamu nako ni ramani za nyumba za kiarabu, michoro ya kiarabu na alama za 'Mwezi' ambao ni Mungu wa kiarabu aliyeabudiwa hata kabla ya Uislam. Ni tamaduni za watu tumejitwika.

6. Social interaction. Jamii za kiafrika zilikuwa na namna yake ya kuingiliana na kuhusiana kulingana na umri na jinsia. Ukristo wa kale ulibagua sana wanawake Kama ilivyo tamaduni za kiyahudi. Mwanamke alikuwa ni mtu wa 'kusitiriwa' lakini mambo yakabadilika badae, leo hii anasimama Hadi madhabahuni.
Waislam wao wameichukua tamaduni ya kiarabu Kama ilivyo ya kumsitiri mwanamke na kumfanya kiumbe dhaifu. Hachangamani na mwanaume iwe kwenye ibada hadi matukio ya kifo. Hii ni tamaduni ya kiarabu hadi leo, si maagizo ya Mungu, Ni utamaduni tu.

7. Tradition. Hii dhana ni pana.
~Dressing style, waafrika tulikuwa na namna yetu ya uvaaji, Kama ya masai na wengine, lakini ukristu ukatuletea kanzu na majoho. Hayo ni mavazi ya makuhani wa kiyahudi, si kwamba ukivaa shuka la kimasai Mungu hakusikii. Waislam nao kanzu, juba, hijab ambayo ni mavaz ya kiarabu yakafanywa kuwa mavazi rasmi. Ni utamaduni tu, Mungu hakuagiza uvae hayo ili uwe wake.

~Eating style. Namna ya kula kwa waafrika wa zamani ni tofauti na jamii za leo zilizoathiriwa na tamaduni za kiyahudi na kiarabu. Wapo wanaoamini kuwa na namna fulani ya ukaaji,(mezani au mkeka) Mungu hapendi, kisa tu myahudi au Mwarabu alifanya hivyo. Ni tamaduni zao tumezigeuza kuwa dini.

~Festivals. Sherehe na kumbukizi za kiafrika wa kale ni tofauti na za leo. Mtoto wa kiafrika akizaliwa kulikuwa na taratibu zake hadi anaingia utu uzima. Kuanguka kitovu, siku 40... Kwa wakristo utasikia kuna ubatizo, kipaimara (kipaimara ni hatua ambayo ipo hadi leo kwa wayahudi ambao siyo wakristu).... Pasaka pia ilikuwepo kabla ya ukristo. Na Waislam wana yao kama 'Hakika'..... Ambayo hufanyiwa watoto wa kiarabu kadiri ya tamaduni zao, si maagizo ya Mungu.

~Mazishi. Waafrika tukizika kwa namna tofauti tofauti kulingana na tamaduni ya kabila husika. Kuuacha mwili kwenye mapango na kuhama makazi, kufukia chini.... Ukristu umeleta style yake na Uislam hali kadhalika. Matumizi ya sanda, jeneza, kukafini, kuosha maiti ni tamaduni tu za kiarabu na kiyahudi, siyo maagizo ya Mungu.

~Tohara. Kwa waafrika hili jambo lilikuwepo kwa baadhi ya makabila. Wengine hadi Leo hawatahiriwi. Ni utamaduni wao. Kwa wayahudi ni utamaduni wao tangu kale, hali kadhalika waarabu. Kutahiri kumefanywa Jambo la kidini ingawa Ni utamaduni tu. Si agizo la Mungu kwamba hapokei kiumbe chenye 'govi' kwenye makao yake ya milele. Wapo wazungu na waafrika ambao hadi leo hawatahiriwi.

Karibuni kwa mjadala, kusiwe na malumbano ya kupigania Utamaduni wa kiyahudi Wala kiarabu hapa. Tujadili kwa hoja. Huu ni mtazamo wangu tu, unaweza kuwaza tofauti.

Umeandika

African Traditional Religion

Hii ndio dini ya watu kutoka wapi Afrika ??
 
naomba jina la mja alichaguliwa kutuletea ujumbe tz
Hakuna.

Lakini, naomba nikuulize swali dogo sana, unaweza kuniambia kwanini umeuliza mja alichaguliwa kuja kufikisha ujumbe Tanzania, je unafikiri kulikuwa na haja hiyo ?
 
Kuna maandiko yenye akili kubwa sana(wakatoliki watanisahihisha) kama ya Saint Thomas Aquinas na Ignas of Loyola. Kama wangeishi kabla ya Biblia, maandiko yao yangetumika kama 'kitabu kitakatifu' na pengine wangeitwa Mitume wa dini fulani.

Ignatius Loyola (1491-1556), the tireless zealot for papal authority – he was the founder of the Society of Jesus (the Jesuits) – even wrote:

"We should always be disposed to believe that which appears to us to be white is really black, if the hierarchy of the church so decides."

The Reformation may have swept away some abuses perpetrated by the priesthood but lying was not one of them. Martin Luther, in private correspondence, argued:

"What harm would it do, if a man told a good strong lie for the sake of the good and for the Christian church ... a lie out of necessity, a useful lie, a helpful lie, such lies would not be against God, he would accept them."

– Martin Luther (Cited by his secretary, in a letter in Max Lenz, ed., Briefwechsel Landgraf Phillips des Grossmüthigen von Hessen mit Bucer, vol. I.)
 
Kuna maandiko yenye akili kubwa sana(wakatoliki watanisahihisha) kama ya Saint Thomas Aquinas na Ignas of Loyola. Kama wangeishi kabla ya Biblia, maandiko yao yangetumika kama 'kitabu kitakatifu' na pengine wangeitwa Mitume wa dini fulani.

aquinas-r.jpg

Thomas Aquinas (1225-74)
Masturbation

Thomas of Aquino was an Italian "scholastic" of aristocratic descent. He studied at the university of Naples and taught in Cologne and Paris. His major work Summa Theologica sought to reconcile Greek philosophy, filtered through the Arab philosopher Averroës and the Jewish philosopher Maimonides, with Christian dogmas. His liberalism included defending the execution of heretics.

"Thomas Aquinas ... thought masturbation worse than rape (because 'unnatural', in the sense of unable to lead to conception). Indeed on this ground he considers rape, incest and adultery lesser vices than masturbation, homosexuality, anal and oral intercourse, and coitus interruptus.

Again, he thought deviation from the 'missionary' position in sexual intercourse a serious sin, believing as he did that this made conception more difficult!"

– Daphne Hampson, After Christianity, p189
 
Mkuu hebu soma shairi la Inferno la Dante?
Mkuu kwahiyo unaamua kuchanganua vitu makini na vitu vya kuchekesha? Yaani Dante aandike shairi la masihara kisha wewe ulifanye reference?

Aidha Dante anaandika hili 14thc kipi kinachokuaminisha kwamba hakuwahi kupata taarifa za uwepo wa Mungu kwakua hiyo ni karne 14 baada ya Kristo na Karne 8 baada ya Muhammad S.A.W.
 
u

umekimbia mfano wako!
gadget lazima iwe na guide yake na sio kazi ya mtumiaji kuitafuta guide

sisi huu muongozo tuliletewa hatukuutafuta !

kwaivo si wetu tunatakiwa tuutafute muongozo wetu
Sijakimbia Mfano wangu Mkuu. Twende ng'adu kwa ng'adu tutaelewana.

Mwenyezi Mungu amekua akishusha Mitume na Manabii kwa kila umma uliokuwepo, baadhi ya Mitume/Manabii hao wameuawa na hao walioletewa Mwongozo huo.

Wengine waliwaletea Mwongozo wakaupokea na wengine wakaukataa. Walioupokea waliamua kushikamana nao na walioukataa kugeuka maadui wa walioupokea Mwongozo huo.

Walioshindwa walilazimika kuondoka na kwenda sehemu nyingine ambazo zingekua salama kwao. Hivyo jamii moja kubaki waamini na wengine wapingaji na hata muda ulipokwenda sana wakajiyengezea utaratibu wao wa maisha ikiwa ni pamoja na kuwahuisha wale waliowaona wametukuka kwao ndio dhana ya MASANAMU inapoingia katika dunia na hata hiyo miti mikubwa na mapamgo yalikua ni makaburi ya watu wapiofhukuliwa kuwa wema katika jamii husika.

NADHANI TUNAKWENDA SAWA
 
Mkuu siku ya kwanza naingia Mafikeng mji mkuu Wa North West nchini south Africa , barabarani nakutana na watoto wakali chuchu saa sita yako wazi kabisa halafu watu wanapishana nao hata habari Hawana ! Nikapigwa na butwaa mpaka mmoja akanisalimia dumelang!!! Niliona raha mpaka basi ,mkuu ilinibidi nizoee na mimi nikawa siwashangai hata nikukutana nao Barabarani nawasilimia tu. Mils na tamaduni zao ni vitu vya kawaida tu. Tembelea nchi hizi, Botswana ,south Africa na Swaziland (iswathini) chuchu nje nje kabisa [emoji8]
Nalog off
Ahsante Mkuu nikipata nauli nitakwenda
 
. Si agizo la Mungu kwamba hapokei kiumbe chenye 'govi' kwenye makao yake ya milele. Wapo wazungu na waafrika ambao hadi leo hawatahiriwi.

Mjadala unaanzia hapa kwenye GOVI, je wewe unetahiriwa au bado??!!
 
Sio kila kitabu ni kitabu cha kufanyia reference Mkuu, kwanza muandishi Alice Werner hana mandate ya kuandika alichokiandika kwakua.

Mtoto wa saba baba akizurura huko duniani, ikiwepo Newzeland, USA na hatimaye kuweka makazi yake Tonbridge England.

Alice Werner hakuwa akijua chochote kuhusu Afrika hadi alipotembelea Nyasaland na ndipo alipoanza kusoma kwa Profesa kuhusu Swahili na ubantu.

"You can't be Roman than Roman themselves"

*************
Sipingi waafrika kwamba tulikua na Tamaduni na taratibu zetu lakini Dini haukuwa utamaduni wa jamii fulani.
 
Ili swala la dini kuna mida unalibeba kama lilivyo na muda unaacha kama lilivyo ..mimi kwa upande wangu nishaacha kutoq sadaka na mchango wowote kanisani ,nikitoa ni mia 5 mwisho. Wakati mwingine sadaka yangu naona nipeleke kwa wenye uhitaji

Shs 500/=, yaani Jero??!!, halafu unatamba humu ndani ya ukumbi wa Jf kwamba eti nawe huwa unatoa pesa!!!??, kweli wewe ni Tajiri kichwa sio Tajiri pesa.
 
Nawish kila mtu atizame Documentary Ya ,Story of God with Morgan Freeman,..mzee huyu anasafiri kila pembe ya Dunia kujifunza na kutoa elimu kuhusu dini / Mila na desturi za Jamii mbalimbali...
 
ongezea na Movie ya PK
 
Nitangulie kwa kusema Utamaduni ni neno pana linalojumuisha mfumo mzima wa Maisha, lengo la Uzi huu ni kuonesha ni jinsi gani tulivyoubeba utamaduni wa kigeni na kuufanya dini zetu na pengine tumenufaika nao ama kuumizwa nao pasipo kujua.

Nitawapitisha kwenye vipengele vya utamaduni 'Culture'. Hapa Ukristo nitauita 'Jewish Culture', Uislam kama 'Arabic Culture' na dini ya mwafrika ambayo ni 'African Traditional Religion' nitaiita African Culture. Kwahiyo nitazungumzia utamaduni wa kiyahudi, kiarabu na kiafrika. Sitarajii kupata maswali ya NINI MAANA YA DINI. Hapa hiyo dini yako naijadili Kama tamaduni tu wa watu fulani.

1. Uongozi na siasa. Waafrika walikuwa na tamaduni zao za kupata kiongozi, pia sheria na kanuni zao kabla ya kuletewa tamaduni mpya za kiarabu zilizoletwa na wa Asia hasa waarabu na kiyahudi zilizoletwa na wazungu. Kwenye makabila mengi, kiongozi wa kijadi alivaa kofia mbili, ya kisiasa na kidini kwenye matambiko. Ukristo ukaleta taratibu zake, siasa na dini zilitenganishwa. Huu ni utamaduni wa kiyahudi ambao haukuwa na uhusiano kati ya makuhani na magavana wa kirumi.
Uislam Kama ilivyo utamaduni wa kiarabu. Siasa na dini hufungamana. Ndiyo maana kuna nchi zinazofuata 'Sharia' za kiislam/kiarabu katika kuamua na kuongoza. Hizo zote ni tamaduni tu za watu, siyo maagizo ya Mungu.

2. Music. Waafrika wana vyombo vyao vya muziki 'music instruments' na styles zao za uimbaji 'musical notations'. Zeze, filimbi, ngoma, pembe za wanyama nk... Wakristo wakachukua muziki wa kiyahudi na kirumi uliotajwa kwenye Biblia. Baragumu, tarumbeta, zeze, vinanda...kuwa muziki safi wa kumwimbia Mungu. Kwa wakatoliki Papa Gregory akapendekeza Tuni fulani itumike duniani kote 'Gregorian music'. Hali kadhalika Waislam na kaswida, dufu ambazo ni musical notation za kiarabu wakazifanya nyimbo za kumsifu Mungu. Ni utamaduni tu, Mungu hana aina fulani ya kuimbiwa.

3. Language. Lugha zetu za kibantu zilitumika kuomba na maombi yakapokelewa. Viongozi wa kimila walitambika kwa Lugha zao kwa Miungu yao. Wazungu wakatuletea ukristo katika lugha ya kilatini. Ibada na misa zilifanyika kwa Lugha hii kwa karne kadhaa. Warumi ndiyo walikifanya kilatini kiwe lugha ya Mungu ingawa Mambo yalibadilika badae. Uislam kwakuwa ni utamaduni wa kiarabu, wao Hadi leo huamini Mungu anajua kiarabu tu. Hakijabadilika chochote. Ni utamaduni tu, hata kichina na kijapani Mungu anakisikia.

4. Food. Chakula katika utamaduni wa kiafrika una makatazo na kanuni za kula chakula. Kulikuwa na hadithi zenye kukataza au kuruhusu chakula/mnyama fulani. Utamaduni wa kiyahudi hali kadhalika, Kuna chakula haram na kisicho haramu, ingawa warumi wamefanya yao kugeuza masndiko. Kuna wakristo wanaokula kila kitu na wale wanaochagua kulingana na mapokeo ya agano la kale la kiyahudi. Waislam pia, utamaduni wa kiarabu katika chakula umebebwa kama ulivyo. Haram na Halal ni kadiri ya utamaduni wa kiarabu ambao walifungamana sana na wayahudi. Ndiyo maana, haram zilizopo katika Agano la kale utazikuta kwenye Qur'an.

5. Art, craft and Architecture. Sanaa na ubunifu. Waafrika tulikuwa na styles zetu za ujenzi wa nyumba za kuishi na ibada michoro na mapambo. Lakini leo hii nyumba za ibada zetu ni sawa na mahekalu ya kiyahudi na kirumi kwa wakristo, kukiwa na nakshi za misalaba. Kwa waislamu nako ni ramani za nyumba za kiarabu, michoro ya kiarabu na alama za 'Mwezi' ambao ni Mungu wa kiarabu aliyeabudiwa hata kabla ya Uislam. Ni tamaduni za watu tumejitwika.

6. Social interaction. Jamii za kiafrika zilikuwa na namna yake ya kuingiliana na kuhusiana kulingana na umri na jinsia. Ukristo wa kale ulibagua sana wanawake Kama ilivyo tamaduni za kiyahudi. Mwanamke alikuwa ni mtu wa 'kusitiriwa' lakini mambo yakabadilika badae, leo hii anasimama Hadi madhabahuni.
Waislam wao wameichukua tamaduni ya kiarabu Kama ilivyo ya kumsitiri mwanamke na kumfanya kiumbe dhaifu. Hachangamani na mwanaume iwe kwenye ibada hadi matukio ya kifo. Hii ni tamaduni ya kiarabu hadi leo, si maagizo ya Mungu, Ni utamaduni tu.

7. Tradition. Hii dhana ni pana.
~Dressing style, waafrika tulikuwa na namna yetu ya uvaaji, Kama ya masai na wengine, lakini ukristu ukatuletea kanzu na majoho. Hayo ni mavazi ya makuhani wa kiyahudi, si kwamba ukivaa shuka la kimasai Mungu hakusikii. Waislam nao kanzu, juba, hijab ambayo ni mavaz ya kiarabu yakafanywa kuwa mavazi rasmi. Ni utamaduni tu, Mungu hakuagiza uvae hayo ili uwe wake.

~Eating style. Namna ya kula kwa waafrika wa zamani ni tofauti na jamii za leo zilizoathiriwa na tamaduni za kiyahudi na kiarabu. Wapo wanaoamini kuwa na namna fulani ya ukaaji,(mezani au mkeka) Mungu hapendi, kisa tu myahudi au Mwarabu alifanya hivyo. Ni tamaduni zao tumezigeuza kuwa dini.

~Festivals. Sherehe na kumbukizi za kiafrika wa kale ni tofauti na za leo. Mtoto wa kiafrika akizaliwa kulikuwa na taratibu zake hadi anaingia utu uzima. Kuanguka kitovu, siku 40... Kwa wakristo utasikia kuna ubatizo, kipaimara (kipaimara ni hatua ambayo ipo hadi leo kwa wayahudi ambao siyo wakristu).... Pasaka pia ilikuwepo kabla ya ukristo. Na Waislam wana yao kama 'Hakika'..... Ambayo hufanyiwa watoto wa kiarabu kadiri ya tamaduni zao, si maagizo ya Mungu.

~Mazishi. Waafrika tukizika kwa namna tofauti tofauti kulingana na tamaduni ya kabila husika. Kuuacha mwili kwenye mapango na kuhama makazi, kufukia chini.... Ukristu umeleta style yake na Uislam hali kadhalika. Matumizi ya sanda, jeneza, kukafini, kuosha maiti ni tamaduni tu za kiarabu na kiyahudi, siyo maagizo ya Mungu.

~Tohara. Kwa waafrika hili jambo lilikuwepo kwa baadhi ya makabila. Wengine hadi Leo hawatahiriwi. Ni utamaduni wao. Kwa wayahudi ni utamaduni wao tangu kale, hali kadhalika waarabu. Kutahiri kumefanywa Jambo la kidini ingawa Ni utamaduni tu. Si agizo la Mungu kwamba hapokei kiumbe chenye 'govi' kwenye makao yake ya milele. Wapo wazungu na waafrika ambao hadi leo hawatahiriwi.

Karibuni kwa mjadala, kusiwe na malumbano ya kupigania Utamaduni wa kiyahudi Wala kiarabu hapa. Tujadili kwa hoja. Huu ni mtazamo wangu tu, unaweza kuwaza tofauti.
ukristo sio jewish culture ni western culture
 
Kwanza huwa nawashangaa sana mnapo pinga mambo ambayo hamna elimu nayo kabisa.

Mola wetu hupeleka ujumbe kulingana na hali za watu wake, na huchagua mja miongoni mwa waja wake ili awafikishie ujumbe wengine, kwa maana ya uongozi. Huu utaratibu ulianza tangu zama za nabii Nuhu na hii ni baada ya watu kuanza kufanya Ushirikina, na kuabudu viumbe mbali na Muumba. Utaratibu huu ukaensa mpaka ulipo komea katika bara la Arabu, kama sehemu ya kuanzia kisha ujumbe huo na utaratibu huo ukaamriwa ufikishwe duniani kote, kwahiyo huko ulipo anzia ni sehemu ambazo watu wa hulo walikuwa wanafanya maovu makubwa sana kuzidi sehemu nyingine. Hil

Kwanini hujibu swali langu na kwanini utake jibu liwe "utashi" ?

Usitake nipinge jambo ambalo hata ukipewa miaka mia huwezi kulithibitisha. Ninacho kitaka toka kwako kwanza ututhibitishie haya unayo yaandika, nilikukanya kijana ya kuwa hapa tunaongelea elimu siyo habari za pauka pakawa, weka akilini hilo. Kama ni kusema tu kila mtu anaweza kusema analo taka, ila hapa tunaangalia ukweli wa mambo, sasa wewe tuonyeshe ukweli wa haya unayo yaandika,ili tukuulize maswali.

Mola wetu ana vitu vifuatavyo, ana Wills (Mashi'at) na ana Wants (Irada) yaani huwa akitaka jambo litokee hutokea hata kama halipendi, mathalani leo hii ameruhusu ufisadi uwepo duniani ila hapendi waja wake wawe mafisadi, na ndiyo maana akaweka mlango wa toba, akaleta ujumbe na akatuonyesha madhara ya kufanya ufisadi. Huyu ndiyo Mola wetu mlezi.
Hii mada mbona haijalenga Uislam tu? Mbona mna inferiority complex kiasi hiki? Mbona mnamtetea Sana Mungu wenu kwa nguvu kwanini musimuache ajitetee meenyewe? Sioni upande wa piki humu wakilalamika.
 
Back
Top Bottom