Hauko sahihi mkuu..
Mbona mifano ya "inge" ipo mingi sana....
Angalia tu mpaka katika Qurani ipo mingi sana..
قُل لَّوْ شَاءَ اللَّهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
[ YUNUS - 16 ]
Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii?
Unaona neni "angeli" hapo....
Hapo maana yake ni hoja kubwa hiyo kwamba lau Mungu ANGELITAKA msemaji asingewasomea.
Kutumia neno "angelitaka " ni hoja ambayo inatufikirisha kuwa je kweli angelitaka ingekuwa hivyo.
Sasa kutumika kwa neno angeli au ingeli hakufanyi kitu kisiwe hoja bali kinafanya hoja hiyo lau ingekuwa kinyume chake.
Sasa kwa mtazamo wako unaweza kusema hata hiyo aya msemaji hakupaswa kutumia neno "engeli" kwa kuwa tu haijatokea hivyo ambavyo amesema.
Sasa unatakiwa ujibu hoja,na sio kukimbia hoja kwa sababu imetumika neno ingeli au angeli..
Pia angalia aya nyingine..
لو أراد الله أن يتخذ ولدا لاصطفى مما يخلق ما يشاء سبحانه هو الله الواحد القهار
[ AZZUMAR - 4 ]
Lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka kuwa na mwana, basi bila ya shaka angeli teua amtakaye katika alio waumba. Subhanahu, Ametakasika na hayo! Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo.
Qurani imetumia neno "ANGELI.."
kwa maana ya kuwa laiti ingekuwa hivyo.
Na kutumia neno angelitaka katika aya hiyo hakujafanya hoja isiwe hoja,bali ni hoja hasa,ila wewe ungeliikataa kwa sababu ya neno angeli ambalo humaanisha lau ingekuwa hivyo.
Sasa hao wanachuoni unaowadai ikiwa kama hawataki neno "ingeli au angeli" basi wagahamishe kuwa Qurani imetumia mara nyingi sana maneno hayo.
Katika hili sidhani kama una hoja madhubuti ya kukamatia...