Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Kabla ya uislam waarabu walikuwa kwenye "ENZI ya ujinga "
Uislam ulipo kuja ukawafundisha stara.
Jinsi ya kuabudu,jinsi ya kula,jinsi ya kuoa, kuishi na watu n.k.
Uislam unajitegemea. Ndo maana hata mmakonde wa mtwara anaweza kuwa muislam na kusoma quran.
utofauti unaanzia wapi mkuu?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Hapa hiyo dini yako naijadili Kama tamaduni tu wa watu fulani.
Tatizo la mada yako linaanzia hapa,na limeonyesha waI kabisa lazima ukosee katika mada nzima, kwanini uijadili Dini kama Tamaduni za watu fulani na ushindwe kuijadili Dini kama dini ?

Kuifasiri Dini kama tamaduni ya watu fulani au za watu fulani kumeonyesha wazi ya kuwa hujui tamaduni ni nini na kadhalika hujui Dini ni nini. Nakupa mfano ambao unaonyesha dhahiri shahiri kuuita Uislamu ni tamaduni ya waarabu, ni kosa la kiufundi, miongoni mwa Tamaduni za Waarabu ilikuwa wanapo zaliwa watoto wa kike, wao walikuwa wanaona kama ni mkosi na kufikia hatua wakawa wana wazika wakiwa hai, ila Uislamu ulipo kuja ukakataza hili.

Sasa nakupa kanuni ya msingi kuhusu dini, hii unatakiwa uishi nayo ni kuwa "Dini imekuja kumtoa mtu katika hali duni kiutendaji na kumpeleka katika hali ya juu zaidi kiutendaji,kadhalika Dini imekuja kuzikosoa na kurekebisha katika zile mila na desturi zetu, yaani Tamaduni zetu". Katika hili kuna mifano mingi sana.

Ahsante.
 
swala la mungu kuleta vitabu ndo hua silielewi kabisa.
kwamba mungu anategemea maandishi kufikia watu wake?
ambao hawajui kusoma ?
ambao bado hawajifikiwa na vitabu mpaka sasa (wapo) ana mpango gani nao?

hizi vitabu vya dini ni utashi wa binadamu tu.
Huu unaitwa utaratibu, na utaratibu huu unatupa mafunzo sisi wanadamu kufanya mambo yetu kwa utaratibu pia.

Katika utaratibu wa Mola wetu, ni kuwa aliweka ujumbe wake utufikie sisi kupitia mitume na manabii wake, huku akiambatanisha vitabu, sababu kilicho andikwa kimeandikwa na vitabu huwa vinapewa umri mrefu sana. Utaratibu huo ni kama ule alio uweka katika kuwepo usiku na mchana, au kifo na uhai, uzima na maradhi na mfano wake.

Unapo sema Vitabu ni utashi wa mwanadamu, unatakiwa ututhibitishie hilo, ila kama unaandika tu kwa kujisikia kuandika, kaa ukijua unaidhulumu akili yako ya kuifanya isifanye kazi yake vizuri, na hili ni tatizo la kujitakia, tafakari katika uhalisia.

Watu ambao hawajafikiwa na vitabu, wapo na wanatambulika na wana jina lao maalumu (Katika Uislam watu hawa wameongelewa, ila jina lao kidogo limenitoka) hawa watakuja kufufuliwa siku ya malipo, watapewa mtihani watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto.

Mola hategemi uandishi, kwani angetaka kutujaza wote elimu ya kumjua yeye angefanya hili kwake ni sahali mno, ila ameamua kuweka utaratibu huo kisha akaweka na njia za kuupata huo ujumbe.
 
Asante mkuu
Uzi umekuwa mfupi labda kutokana na uvivu wangu wa kuandika. Hayo yote uliyoorodhedha sijayatolea ufafanuzi lakini yapo vema na wazi katika 'culture'
~uwepo wa nafsi
~simulizi za maisha ya kaburi
~uwepo wa pepo na moto
~kuhusu roho
~maisha baada ya kifo
Hayo yote yanaingia kwenye 'Myths and Lengends' imani na Hadithi. Kuna hadithi nyingi za kiarabu na za kiafrika(kulingana na kabila husika) zinazoelezea hayo yote. Hadithi na imani hizo pengine tumezigeuza kuwa sehemu ya dini, Waarabu na wazungu walipofika Afrika walitukuta tuna knowledge kuhusu Roho, pepo,maisha baada ya kifo....yote yalikuwapo. Wakaleta yao.
Fasihi ilitumika sana kuaminisha watu vitu km toharani,mbiguni na motoni...Dante Alighieri ni mmoja wa hao wana fasihi waliouweka Ukristo katika ulingo.
 
Kabla ya uislam waarabu walikuwa kwenye "ENZI ya ujinga "
Uislam ulipo kuja ukawafundisha stara.
Jinsi ya kuabudu,jinsi ya kula,jinsi ya kuoa, kuishi na watu n.k.
Uislam unajitegemea. Ndo maana hata mmakonde wa mtwara anaweza kuwa muislam na kusoma quran.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
kumbe uislam ulikuja kwa ajili ya WAARABU wa enzi ya ujinga!

uoni sisi tumebeba mzigo si wetu tumekopi tamaduni za watu

sisi tulikua na taratibu zetu kula,kuvaa,salamu,ibada

kwaio mpaka hapa uislam ulikua hautuhusu.
 
Ebu soma kwanza hayo maelezo. Kuhusu dini ya waarabu
kumbe uislam ulikuja kwa ajili ya WAARABU wa enzi ya ujinga!

uoni sisi tumebeba mzigo si wetu tumekopi tamaduni za watu

sisi tulikua na taratibu zetu kula,kuvaa,salamu,ibada

kwaio mpaka hapa uislam ulikua hautuhusu.
Screenshot_20200718-235418.jpg

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Huu unaitwa utaratibu, na utaratibu huu unatupa mafunzo sisi wanadamu kufanya mambo yetu kwa utaratibu pia
sijui kwa nini huu utaratibu aliupeleka uarabuni?
Unapo sema Vitabu ni utashi wa mwanadamu, unatakiwa ututhibitishie hilo, ila kama unaandika tu kwa kujisikia kuandika, kaa ukijua unaidhulumu akili yako ya kuifanya isifanye kazi yake vizuri, na hili ni tatizo la kujitakia, tafakari katika uhalisia.
ni utashi wa nani?
mi najua ni kazi ya mudy na maswhiba zake ambao ni binadamu .pinga
Watu ambao hawajafikiwa na vitabu, wapo na wanatambulika na wana jina lao maalumu (Katika Uislam watu hawa wameongelewa, ila jina lao kidogo limenitoka) hawa watakuja kufufuliwa siku ya malipo, watapewa mtihani watakao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto.
kwaio mungu anafurahia kuona watu wake wanaishi bila kufata taratibu zake.
 
sijui kwa nini huu utaratibu aliupeleka uarabuni?
Kwanza huwa nawashangaa sana mnapo pinga mambo ambayo hamna elimu nayo kabisa.

Mola wetu hupeleka ujumbe kulingana na hali za watu wake, na huchagua mja miongoni mwa waja wake ili awafikishie ujumbe wengine, kwa maana ya uongozi. Huu utaratibu ulianza tangu zama za nabii Nuhu na hii ni baada ya watu kuanza kufanya Ushirikina, na kuabudu viumbe mbali na Muumba. Utaratibu huu ukaensa mpaka ulipo komea katika bara la Arabu, kama sehemu ya kuanzia kisha ujumbe huo na utaratibu huo ukaamriwa ufikishwe duniani kote, kwahiyo huko ulipo anzia ni sehemu ambazo watu wa hulo walikuwa wanafanya maovu makubwa sana kuzidi sehemu nyingine. Hil
ni utashi wa nani?
Kwanini hujibu swali langu na kwanini utake jibu liwe "utashi" ?
mi najua ni kazi ya mudy na maswhiba zake ambao ni binadamu .pinga
Usitake nipinge jambo ambalo hata ukipewa miaka mia huwezi kulithibitisha. Ninacho kitaka toka kwako kwanza ututhibitishie haya unayo yaandika, nilikukanya kijana ya kuwa hapa tunaongelea elimu siyo habari za pauka pakawa, weka akilini hilo. Kama ni kusema tu kila mtu anaweza kusema analo taka, ila hapa tunaangalia ukweli wa mambo, sasa wewe tuonyeshe ukweli wa haya unayo yaandika,ili tukuulize maswali.

sijui kwa nini huu utaratibu aliupeleka uarabuni?

ni utashi wa nani?
mi najua ni kazi ya mudy na maswhiba zake ambao ni binadamu .pinga

kwaio mungu anafurahia kuona watu wake wanaishi bila kufata taratibu zake.
Mola wetu ana vitu vifuatavyo, ana Wills (Mashi'at) na ana Wants (Irada) yaani huwa akitaka jambo litokee hutokea hata kama halipendi, mathalani leo hii ameruhusu ufisadi uwepo duniani ila hapendi waja wake wawe mafisadi, na ndiyo maana akaweka mlango wa toba, akaleta ujumbe na akatuonyesha madhara ya kufanya ufisadi. Huyu ndiyo Mola wetu mlezi.
 
Uislam ni dini ya WOTE..
Sio mwarabu, mzungu au muafrica au mmarekani.
Maana uislam unahubiri mungu MMOJA NA WA KWELI.
U tamaduni wa muafrica wa kuabudu mizimu na Mawe na miti WALIKUWA WAMEPOTEA
unazunguka palepale .
kama ni ivyo basi mudy alienda kubadilisha utamaduni na kuwapa dini WAARABU

sisi huku wabongo ilikua inatuhusu nini wakati tulikua na taratibu zetu.

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Mola wetu hupeleka ujumbe kulingana na hali za watu wake, na huchagua mja miongoni mwa waja wake ili awafikishie ujumbe wengine, kwa maana ya uongozi.
naomba jina la mja alichaguliwa kutuletea ujumbe tz
 
Back
Top Bottom