Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Uovu gani uliokuwa unafanywa na watu weupe na waarabu ambao haukuwa unafanyika Africa na sehemu nyingine za dunia?
Kwanza nakusahihisha, Uislamu umegawanyika sehemu kuu mbili, moja Uislamu wa Ujumla ambao huu upo hata kabla ya nabii Ibrahiim. Uislamu khasa (maalumu ambao amekuja nao mtume).

Bila shaka kabisa,Waafrika hatukufikia makosa na uovu ambao walikuwa wanafanya watu weupe. Kwahiyo kila jambo lazima liwe lina mwanzo wake kisha lina tangaa.
 
Kama Allah hakuwaleta Waafrika na kwingine mitume umejuaje wasingewaua?
Africa na sehemu nyingine za dunia walikuwa hawaabadu binadamu?
Unaifahamu historia ya dunia vizuri?
Mingi sana, hakuna watu walio kuwa wana vitimbi kuwazidi hao, wao walikuwa wakiletewa mitume wana waua, wakifanyiwa miujiza wanakanusha, mpaka wakawa wanaletewa vyakula toka mbinguni lakini mwisho wa siku wanakadhibisha na kutenda maovu, bali waliwafanya binadamu wenzao kuwa ndiyo miungu na mfano wake.
 
Umeandika vizuri dini ni sehemu ya utamaduni, sisi kama waafrika tumeacha tamaduni zetu na kukumbatia za wageni na kuziona ndio sahihi zaidi.

Waafrika leo ndio tunazijua dini kuliko hata hao walotuletea. Cha ajabu ni kwamba matatizo karibu yote makubwa yako huku njaa, ujinga, umasikini magonjwa n.k

Na hakuna kitu kinachokera na tulicho haribiwa na hawa jamaa wa dini hizi kama kuacha majina yetu ya asili yaani kadri mtu anavyoitwa jina gumu lkn lenye mahadhi ya uzungu/uyahudi na uarabu ndo mtu anavyojiona bora na kastaarabika , poor us
 
Nitangulie kwa kusema Utamaduni ni neno pana linalojumuisha mfumo mzima wa Maisha, lengo la Uzi huu ni kuonesha ni jinsi gani tulivyoubeba utamaduni wa kigeni na kuufanya dini zetu na pengine tumenufaika nao ama kuumizwa nao pasipo kujua.

Nitawapitisha kwenye vipengele vya utamaduni 'Culture'. Hapa Ukristo nitauita 'Jewish Culture', Uislam kama 'Arabic Culture' na dini ya mwafrika ambayo ni 'African Traditional Religion' nitaiita African Culture. Kwahiyo nitazungumzia utamaduni wa kiyahudi, kiarabu na kiafrika. Sitarajii kupata maswali ya NINI MAANA YA DINI. Hapa hiyo dini yako naijadili Kama tamaduni tu wa watu fulani.

1. Uongozi na siasa. Waafrika walikuwa na tamaduni zao za kupata kiongozi, pia sheria na kanuni zao kabla ya kuletewa tamaduni mpya za kiarabu zilizoletwa na wa Asia hasa waarabu na kiyahudi zilizoletwa na wazungu. Kwenye makabila mengi, kiongozi wa kijadi alivaa kofia mbili, ya kisiasa na kidini kwenye matambiko. Ukristo ukaleta taratibu zake, siasa na dini zilitenganishwa. Huu ni utamaduni wa kiyahudi ambao haukuwa na uhusiano kati ya makuhani na magavana wa kirumi.
Uislam Kama ilivyo utamaduni wa kiarabu. Siasa na dini hufungamana. Ndiyo maana kuna nchi zinazofuata 'Sharia' za kiislam/kiarabu katika kuamua na kuongoza. Hizo zote ni tamaduni tu za watu, siyo maagizo ya Mungu.

2. Music. Waafrika wana vyombo vyao vya muziki 'music instruments' na styles zao za uimbaji 'musical notations'. Zeze, filimbi, ngoma, pembe za wanyama nk... Wakristo wakachukua muziki wa kiyahudi na kirumi uliotajwa kwenye Biblia. Baragumu, tarumbeta, zeze, vinanda...kuwa muziki safi wa kumwimbia Mungu. Kwa wakatoliki Papa Gregory akapendekeza Tuni fulani itumike duniani kote 'Gregorian music'. Hali kadhalika Waislam na kaswida, dufu ambazo ni musical notation za kiarabu wakazifanya nyimbo za kumsifu Mungu. Ni utamaduni tu, Mungu hana aina fulani ya kuimbiwa.

3. Language. Lugha zetu za kibantu zilitumika kuomba na maombi yakapokelewa. Viongozi wa kimila walitambika kwa Lugha zao kwa Miungu yao. Wazungu wakatuletea ukristo katika lugha ya kilatini. Ibada na misa zilifanyika kwa Lugha hii kwa karne kadhaa. Warumi ndiyo walikifanya kilatini kiwe lugha ya Mungu ingawa Mambo yalibadilika badae. Uislam kwakuwa ni utamaduni wa kiarabu, wao Hadi leo huamini Mungu anajua kiarabu tu. Hakijabadilika chochote. Ni utamaduni tu, hata kichina na kijapani Mungu anakisikia.

4. Food. Chakula katika utamaduni wa kiafrika una makatazo na kanuni za kula chakula. Kulikuwa na hadithi zenye kukataza au kuruhusu chakula/mnyama fulani. Utamaduni wa kiyahudi hali kadhalika, Kuna chakula haram na kisicho haramu, ingawa warumi wamefanya yao kugeuza masndiko. Kuna wakristo wanaokula kila kitu na wale wanaochagua kulingana na mapokeo ya agano la kale la kiyahudi. Waislam pia, utamaduni wa kiarabu katika chakula umebebwa kama ulivyo. Haram na Halal ni kadiri ya utamaduni wa kiarabu ambao walifungamana sana na wayahudi. Ndiyo maana, haram zilizopo katika Agano la kale utazikuta kwenye Qur'an.

5. Art, craft and Architecture. Sanaa na ubunifu. Waafrika tulikuwa na styles zetu za ujenzi wa nyumba za kuishi na ibada michoro na mapambo. Lakini leo hii nyumba za ibada zetu ni sawa na mahekalu ya kiyahudi na kirumi kwa wakristo, kukiwa na nakshi za misalaba. Kwa waislamu nako ni ramani za nyumba za kiarabu, michoro ya kiarabu na alama za 'Mwezi' ambao ni Mungu wa kiarabu aliyeabudiwa hata kabla ya Uislam. Ni tamaduni za watu tumejitwika.

6. Social interaction. Jamii za kiafrika zilikuwa na namna yake ya kuingiliana na kuhusiana kulingana na umri na jinsia. Ukristo wa kale ulibagua sana wanawake Kama ilivyo tamaduni za kiyahudi. Mwanamke alikuwa ni mtu wa 'kusitiriwa' lakini mambo yakabadilika badae, leo hii anasimama Hadi madhabahuni.
Waislam wao wameichukua tamaduni ya kiarabu Kama ilivyo ya kumsitiri mwanamke na kumfanya kiumbe dhaifu. Hachangamani na mwanaume iwe kwenye ibada hadi matukio ya kifo. Hii ni tamaduni ya kiarabu hadi leo, si maagizo ya Mungu, Ni utamaduni tu.

7. Tradition. Hii dhana ni pana.
~Dressing style, waafrika tulikuwa na namna yetu ya uvaaji, Kama ya masai na wengine, lakini ukristu ukatuletea kanzu na majoho. Hayo ni mavazi ya makuhani wa kiyahudi, si kwamba ukivaa shuka la kimasai Mungu hakusikii. Waislam nao kanzu, juba, hijab ambayo ni mavaz ya kiarabu yakafanywa kuwa mavazi rasmi. Ni utamaduni tu, Mungu hakuagiza uvae hayo ili uwe wake.

~Eating style. Namna ya kula kwa waafrika wa zamani ni tofauti na jamii za leo zilizoathiriwa na tamaduni za kiyahudi na kiarabu. Wapo wanaoamini kuwa na namna fulani ya ukaaji,(mezani au mkeka) Mungu hapendi, kisa tu myahudi au Mwarabu alifanya hivyo. Ni tamaduni zao tumezigeuza kuwa dini.

~Festivals. Sherehe na kumbukizi za kiafrika wa kale ni tofauti na za leo. Mtoto wa kiafrika akizaliwa kulikuwa na taratibu zake hadi anaingia utu uzima. Kuanguka kitovu, siku 40... Kwa wakristo utasikia kuna ubatizo, kipaimara (kipaimara ni hatua ambayo ipo hadi leo kwa wayahudi ambao siyo wakristu).... Pasaka pia ilikuwepo kabla ya ukristo. Na Waislam wana yao kama 'Hakika'..... Ambayo hufanyiwa watoto wa kiarabu kadiri ya tamaduni zao, si maagizo ya Mungu.

~Mazishi. Waafrika tukizika kwa namna tofauti tofauti kulingana na tamaduni ya kabila husika. Kuuacha mwili kwenye mapango na kuhama makazi, kufukia chini.... Ukristu umeleta style yake na Uislam hali kadhalika. Matumizi ya sanda, jeneza, kukafini, kuosha maiti ni tamaduni tu za kiarabu na kiyahudi, siyo maagizo ya Mungu.

~Tohara. Kwa waafrika hili jambo lilikuwepo kwa baadhi ya makabila. Wengine hadi Leo hawatahiriwi. Ni utamaduni wao. Kwa wayahudi ni utamaduni wao tangu kale, hali kadhalika waarabu. Kutahiri kumefanywa Jambo la kidini ingawa Ni utamaduni tu. Si agizo la Mungu kwamba hapokei kiumbe chenye 'govi' kwenye makao yake ya milele. Wapo wazungu na waafrika ambao hadi leo hawatahiriwi.

Karibuni kwa mjadala, kusiwe na malumbano ya kupigania Utamaduni wa kiyahudi Wala kiarabu hapa. Tujadili kwa hoja. Huu ni mtazamo wangu tu, unaweza kuwaza tofauti.
Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba waislamu baadhi yao wanamzarau na kumkejeli mkristu, na mkristu vile vile baadi yao wanamzarau na kumkejeli muislamu. Wanasahau kuwa sisi sote ni waafrika tu, ni asili moja, dini tuliletewa kwa meli na majahazi. Msinielewe vibaya
 
Nani alikufundisha hivi?
Unafahamu waarabu sio watu weupe?
Soma kitabu kiitwacho "Definition of an Arab" cha Mwanazuoni mbora aitwaye "Ibn Taymiyyah".

Niambie Waarabu ni watu gani ?
 
Kama Allah hakuwaleta Waafrika na kwingine mitume umejuaje wasingewaua?
Africa na sehemu nyingine za
Mbona unauliza swali la uongo ? Huwa hatujibu juu ya maswali ambayo hayapo na hayatakuwepo. Kwahiyo jibu langu sijui, labda unithibitishie wewe kwamba wange waua.

Pili, unaoenaka hujaelewa nilichokiandika ndiyo maana umeuliza swali la Uongo. Hoja ya msingi siyo kujua au kutokujua, hoja ni sababu inayo fanya mitume wapelekwe sehemu husika.
 
Wewe umesikia wapi mzungu akiruka ndani ya ungo???, Muafrika anaruka ndani ya ungo kwa kutumia sayansi ya giza yenye masharti ya kishenzi, utasikia ukitaka kuruka ndani ya ungo kwanza umuue mama yako au baba yako au nduguyo wa karibu, pili unapotaka kuruka lazima uwe uchi tatu lazima ufumbe macho hadi mwisho wa safari yenu, nne lazima iwe ni usiku.

Sasa angalia sayansi ya mzungu, ipo wazi na hakuna madharti ya kishenzi kama ya Muafrika, kinachofanya ndege ya mzungu ipae angani ni Bernouli principle, lazima kuwe na hewa, lazima ndege itumie injini nk, vyote hivyo vipo wazi kwa kila mtu anayetaka, huo ni mfano mmoja ninaokupa ili uone utofauti kati ya African culture vis a vis European culture.
Labda kwa msaada tu ili ujue wazungu ndio wanga kuliko sisi:-
  • The grand grimoire huki kitabu kiliandikwa na nan kama sio wao.
  • The book of soyga & codex gigas
  • Robert doll na Annabelle Kwan alitoka afrika?
  • Na ndio maana ata jamii za kishetani zote zimeanzia.kwao
Ila tu kwasababu wanapenda kujioma watakatifu ushirikina wao wanauficha wetu ndio.wamauona
 
Na hakuna kitu kinachokera na tulicho haribiwa na hawa jamaa wa dini hizi kama kuacha majina yetu ya asili yaani kadri mtu anavyoitwa jina gumu lkn lenye mahadhi ya uzungu/uyahudi na uarabu ndo mtu anavyojiona bora na kastaarabika , poor us
Ni hatari mkuu, kwa kweli huwa naumia sana kuona tunabaguana kwa misingi ya kidini.

Leo hii kuna tofauti kama sio chuki kubwa sana kati ya waislamu na wakristo, huwa naumia sana.
 
Nitajie mitume walio kuwepo huku Afrika na utupe ushahidi huo.


Sio Africa tu bali duniani pote pale ambapo watu waliishi Allah aliwapelekea waonyaji (mitume) ili watu hao wamuabudu Allah pekee ambalo ndilo kusudi la kuumbwa kwetu, Mtu akikosa Muongozo huwa mshirikina.

Mtume (saw) kuna manabii amehadithiwa habari zao na Mungu na wapo ambao hakuhadithiwa, ambao hakuhadithiwa ndio wale waliokuja kwa ajili ya watu wa Africa, Australia, America ya kusini na kaskazini, China nk, manabii wengi waliohadithiwa habari zao ni kutoka Mashariki ya kati.
 
Labda kwa msaada tu ili ujue wazungu ndio wanga kuliko sisi:-
  • The grand grimoire huki kitabu kiliandikwa na nan kama sio wao.
  • The book of soyga & codex gigas
  • Robert doll na Annabelle Kwan alitoka afrika?
  • Na ndio maana ata jamii za kishetani zote zimeanzia.kwao
Ila tu kwasababu wanapenda kujioma watakatifu ushirikina wao wanauficha wetu ndio.wamauona


Wewe hujanielewa aslan, ni hivi; mzungu elimu yake ya sayansi ipo wazi kwa kila mtu ajichotee, haina masharti ya kishenzi nk, kama ilivyokuwa kwa elimu za waafrika za kutoa kafara za watu nk.

Mimi sijasema kwamba hakuna uchawi kwa wazungu, mimi ninasema kwamba elimu ya mzungu haina uchawi na ipo wazi (explicit) na ndiyo maana mzungu kaishika dunia materially, hiyo ni kutokana na culture yao vis a vis African culture.

Tutasubiri sana, unless we change.
 
Nitajie mtume mmoja tu wa Allah kutoka makabila ya Africa


Hata nikikutajia mmoja utaamini??

Manabii walitumwa na Allah kwa watu wote katika sehemu mbalimbali za dunia,, sio kila habari ya kila nabii imesimuliwa kwani katika zama hizo za kabla ya Isa (as) dunia haikuwa imechangamana (integrated) isitoshe elimu ilikuwa finyu kiasi kwamba historia hazikuwa documented jinsi zilivyokuwa documented katika mashariki ya kati nk.
 
Sio Africa tu bali duniani pote pale ambapo watu waliishi Allah aliwapelekea waonyaji (mitume) ili watu hao wamuabudu Allah pekee ambalo ndilo kusudi la kuumbwa kwetu, Mtu akikosa Muongozo huwa mshirikina.

Mtume (saw) kuna manabii amehadithiwa habari zao na Mungu na wapo ambao hakuhadithiwa, ambao hakuhadithiwa ndio wale waliokuja kwa ajili ya watu wa Africa, Australia, America ya kusini na kaskazini, China nk, manabii wengi waliohadithiwa habari zao ni kutoka Mashariki ya kati.
Nimekuuliza swali nitajie hao mitume na hao manabii.
 
Nimekuuliza swali nitajie hao mitume na hao manabii.


Nikutajie mitume na manabii gani ambao hata mtukufu wa daraja mtume (saw) hakutajiwa??!!!-- mimi ni nani mbele ya mtukufu mtume (saw) !!!?.

Swali lako halina mantiki na elimu yako ya Qur'an ina mashaka.
 
Nikutajie mitume na manabii gani ambao hata mtukufu wa daraja mtume (saw) hakutajiwa??!!!-- mimi ni nani mbele ya mtukufu mtume (saw) !!!?.

Swali lako halina mantiki na elimu yako ya Qur'an ina mashaka.
Sasa kama unajua kabisa hawakutajwa wewe umejuaje kama walikuwepo Afrika na hizo nchi ulizo zitaja ? Mboba huna umakini kabisa ? Au umeamua kukisia tu ?

Wewe nani amekwambia hao ambao hawakutajwa ndiyo walikuwepo huku Afrika ? Sasa hapa ndipo utakapo ona swali langu lina mantiki au halina ? Bila shaka utakuwa umeandika ili kujifurahisha, na ulitakiwa uishie kule kule na uaingetaja nchi ili uwe salama. Ila kwa kuja tako chini, hapa unatakiwa utuwekee ushidi. Nasubiri huo ushahidi.
 
Back
Top Bottom