Nchini Tanzania kumezuka mtafaruku mkubwa juu kile WAISLAM wanachokiita ni MFUMO KRISTO, katika baadhi ya madai yao ni kuwa WAKRISTO kwa kushirikiana na serekali wanaendesha dhuluma na hujuma dhidi ya Uislam.
nimewiwa kuandika haya kutokana na kile ninachokiona kuwa ni UTAPELI MKUBWA unaofanywa na wajanja wachache kujinufaisha KISIASA na KIUCHUMI kwa kupitia mgongo wa DINI huku wakipanda mbegu za chuki na uadui kwenye jamii yetu.
BIBLIA na QURANI vinamtambua SHETANI kama BABA wa uwongo na yeyote anayesema uwongo anaunganishwa na Shetani katika uwongo wake na kuwa kitu kimoja yaani 'shetani' ambaye kwa wakristo wanapaswa kumkemea 'KATIKA JINA LA YESU' na waislam 'KUMLAANI KWA MUJIBU WA QURANI' "ADHUBILAH MINA SHAITWAN RAJIM"
1- katika madai ya baadhi ya wale wanaoupinga MFUMO KRISTO wanamtaja DR SLAA kuwa mwaka wa 1992 alipokuwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu la kanisa katoliki TEC akishirikiana na CCT{jumuiya ya makanisaTanzania} walisaini MoU[Memorundum of Understand] kati ya kanisa na serekali,
huu ni uzushi mkubwa, kwani DR SLAA aliondoka TEC mwaka 1991 na siyo 1992, huu ni uongo mkubwa wa shetani anayepaswa kukemewa kwa JINA LA YESU na KULAANIWA KWA MUJIBU WA QURAN "ADHUBILAHI MINA SHAITWANI RAJIM", inavyoonekana hii ni hoja ya KISIASA iliyotengenezwa kipropaganda ili kumdhoofisha mwanasiasa huyu. Hapa napata wasiwasi na kujihoji, ikiwa wamethubutu kudanganya katika hili dogo, JE HAWATAACHA KUTUDANGANYA KATIKA MAMBO MAKUBWA PIA?
2- Watoa madai wanahoji "KWA NINI MKATABA WENYEWE USAINIWE KWA SIRI" hii kwa kweli ni hoja ya KITOTO, ninajua vema ya kuwa wanajua na kutambua kuwa sheria ya jamhuri ya muungano wa Tanzania zinabainisha wazi kuwa "MIKATABA NI SIRI YA SEREKALI" hili halipingiki kwani imekuwa hivyo tangu mwanzo hadi sasa, na wakati huu ndipo watu wanapiga kelele kutaka kipengele hicho cha sheria kifutwe na mikataba yote iwekwe hadharani, hivyo huu ni UWONGO wa pili wa watu hawa wanaopinga mfumo kristo. Vile vile wanasahau kuwa Edward Lowassa alisaini mkataba kama serekali yeye akiwa ni waziri anayetekeleza armi na maagizo halali ya mwenyekiti wa baraza la mawaziri Ndg Al hadji Ali Hassan Mwinyi.
3- watu hao wanadai kuwa "MoU ni njama dhidi ya Uislam", dai hili ni dai la UZUSHI wa kishetani dhidi ya serekali na kanisa, ikiwa MoU ni njama dhidi ya uislam, mbona IMAMU MKUU WA MADHEHEBU YA WAISLAM WA SHIA DUNIANI 'AGA KHANI' amesaini MoU na serekali?. JE MoU ya IMAMU huyu na serekali ni NJAMA DHIDI YA NANI?
4- wazushi hawa wanahoji, uhalali wa uwepo wa "UBALOZI WA VATCAN " nchini. malalamiko ya uwepo wa ubalozi huu yamezuliwa sana kutokana Tanzania kutokuwa mwanachama wa OIC, wakati wakitambua kuwa Vatcan ni nchi huru ndani ya nchi kama ilivyo kwa TAIWANI ambayo nayo ina balozi sehemu mbalimbali duniani japokuwa TAIWAN sii mwanachama wa UMOJA WA MATAIFA UNO, na ingawa TAIWAN inatambulika kama sehemu ya CHINA,
Hii ina maana kwamba OIC sii nchi bali ni taasisi tofauti na hii la VATCAN, wakitambua hilo vema wakahoji "KWA NINI BALOZI WA VATCANI AWAJIBIKE KWA PAPA" ambaye ni MKUU wa KANISA KATOLIKI linaloendesha mfumo kristo? kwa hoja hii wakawaaminisha watu kuwa huu ni uwakala wa aina yake na ni UDINI MKUBWA. lakini wakati huo huo wanashindwa kujihoji juu balozi wa IRANI ambaye moja kwa moja humwakilisha A SUPREME LEADER 'AYATOLLAH KHOMENEY' kiongozi wa kidini. Hapa napo najihoji JE UWAKILISHI HUU WA KIONGOZI MKUU WA KISHIA NDANI YA TANZANIA NAO SII UDINI?
nchini Msumbiji yupo Sheikh mmoja ameandika kitabu kiitwacho "GOVERNANCE AND VULNERABILITTY IN NORTHEN MOZAMBIQUE" eneo hili la kaskazini ndilo linalokaliwa na waislam wengi nchini humo ambao ni 20% ya wakazi wote wa Msumbiji. madai yao ni kuwa serekali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na kanisa linaendesha njama na hujuma dhidi ya waislam na ndiyo maana eneo hilo limekuwa masikini na watoto wao hawaendi shule kwa sababu ya dhuluma za MFUMO KRISTO. wakati huo huo MSUMBIJI ni moja kati ya mataifa masikini zaidi duniani yenye idadi ya watu wanaofikia takribani milioni 19. watu milioni 16 wanaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku na watu milioni 11 hawana maji safi ya kunywa.
jambo la kushangaza ni kuwa nchi hii ni mwanachama wa OIC. swali linakuja ' KWA NINI NCHI HII ISITAJIRIKE WAKATI IPO OIC" vile vile najihoji "IKIWA OIC IMESHINDWA KUWASAIDIA WATU 16MILION WA MSUMBIJI, ITAWEZAKE KUWASADIA WATU WA TANZANIA WAPATAO TAKRIBANI 45MILIONI?" mbali na hivyo najiuliza swali jingine "JE NI KWANINI WAISLAM WA MSUMBIJI WANALALAMIKA WAKATI NCHI YAO NI MWANACHAMA WA JUMUIYA YA NCHI ZA KIISLAM' HAPO NDIPO NAPATA WASIWASI juu ya uhalali wa madai ya mfumo kristo kwani AINA ya UANDISHI wa kitabu hicho unafanana sana na ule wa MOHAMMED SAID,
Hii inaonyesha kwamba hili ni dili la wajanja walilolitengeneza na kuwalaghai watu ili kujipatia utajiri kwa kuuza KASETI, VITABU, CD na DVD kwa namna moja ama nyingine kwa kutumia uwongo huu mwingi na udanganyifu mkubwa ili kufikia malengo yao ya kisera tu,
my take
"IF YOU DON'T KNOW WHERE YOUR COMING FROM, YOU WILL DON'T KNOW WHERE YOUR GOING"
MWANAWAVITTO