Dhana duni ya 'Mfumo Kristo' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana duni ya 'Mfumo Kristo'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babu Lao, Mar 29, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kila kukicha, unajitokeza ushahidi kwamba kiwango cha kufikiri miongoni mwa wa-Tanzania wengi ni duni. Siku hizi, kwa mfano, imeibuka hii dhana ya mfumo Kristo.

  Walioibuni dhana hii na ambao wanaieneza wana ajenda ya kujenga hoja kuwa mfumo wa utawala na uchumi Tanzania unaendeshwa kwa misingi ya kiKristu, na kwa lengo la kuwanufaisha wa-Kristu na kuwakandamiza na kuwanyima wa-Islam fursa na haki wanazostahili, katika nyanja mbali mbali, kama vile elimu na uongozi.

  Hii ndio dhana ya msingi ya hiki kinachoitwa mfumo Kristo. Wanaojenga hoja hii wanadai kuwa serikali ya Tanzania yenyewe inaendeshwa na maaskofu kama sehemu ya uendelezaji wa huu wanaouita mfumo Kristo.

  Kwanza napenda kusema, kama ninavyosema daima, kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake. Uhuru huu ni pamoja na uhuru wa kuyahoji au kuyapinga mawazo ya wengine, kufuatana na mchakato wa kujielimisha na kutafakari masuala. Ni pamoja na uhuru wa kuyapinga mawazo yako mwenyewe.

  Nashangaa kwa nini mfumo mbovu uhusishwe na jina la Yesu Kristu. Dini zote mbili, u-Islam na u-Kristu, zinamtambua na kumheshimu Yesu. Yesu anatambuliwa kama Mungu katika u-Kristu. Na katika u-Islam, anatambuliwa kama mtume maarufu. Dini zote zinamheshimu sana Yesu.

  Kama mfumo wa Tanzania umeoza kama inavyosemwa, hauwezi kuwa mfumo Kristo. Kuuita mfumo Kristo ni dhihaka isiyo kifani. Huwezi kuuhusisha uchafu wowote na Mungu au mtume. Kama kweli maaskofu wanaendekeza na kuulinda mfumo wa dhuluma, wanakiuka mafundisho na maadili ya Kristo. Huu si mfumo Kristo. Mfumo Kristo ni mfumo wa haki na maadili aliyotufundisha Kristo.

  Sidhani kama inahitaji akili ya pekee sana kuitambua hoja hii. Lakini ni wazi kuwa watu wengi Tanzania wana kiwango duni cha kufikiri au kuelewa mambo. Kwa dhana yao ya mfumo Kristo, wanaudhihaki u-Kristo, na pia wanaudhihaki u-Islam. Ila, kutokana na akili zao duni, hawatambui hilo. Kilichopo ni kuwaombea dua njema, waweze kujitambua na kujirekebisha.

  Source: http://hapakwetu.blogspot.com%20/
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  jukwaa la dini would have been appropriate.. hapa kwenye jukwaa la siasa naona unataka kuchafua hewa tu!!
   
 3. k

  kiche JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo la watanzania wengi awapendi kuumiza kichwa kwa kufikiri na kufanya milinganisho,lile linalo kuja mbele ndiyo wanalolitendea kazi kwa muda huo uliopo,kuna mambo mengi ya hovyo yamekuwa yakienezwa na wana siasa kuonyesha kuwa kuna udini.

  Kwa mtu mwenye mawazo madogo yanamwingia lakini kwa mtu makini lazima ajiulize nini maana ya kauli hii,watanzania wenzangu naomba tuwe makini kwa kauli za hovyo za wanasiasa za kutaka kutugawa, suala la udini halipo hila ni mafisadi wanataka kutuchanganya tusifikirie mambo ya msingi ya taifa letu,naomba tuamke wakristo na waislamu tupinge uovu huu wa watu wachache ambao kwa umoja wetu kamwe hawawezi kushinda.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  mie sidhani kama upo sahihi, kwani dini inayozungumzwa hapo chanzo chake ni siasa na ndio maana kaileta huku kwenye siasa. Na hata angeipeleka kwenye jukwaa la dini ungejibu vipi hoja yake, mwaga vitu. au ndo kusema ni ukweli mtupu usiopingika?
   
 5. e

  emalau JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Great thinking
   
 6. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nafikiri waislam wanamtambua YESU (Nabii Issa bin Maryam) sidhani kama wanamtambua KRISTU !!!!
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Thursday, 27 May 2010 10:21 0diggsdigg

  Mussa Mkama
  MAASKOFU waliohudhuria mkutano wa siku moja wa Jukwaa la Wakristo, juzi walifanya kazi ya ziada kupata nakala ya waraka ulioandaliwa na mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alitumia mkutano huoo kuusambaza.

  Mkutano huo ulikuwa wa kuzindua chombo hicho kikubwa cha mshikamano baina ya Wakristo, lakini Mchungaji Mtikila, ambaye anaongoza kanisa la Full Salvation, aliutumia kugawa takriban nakala 60.
  Alikuwa akigawa waraka ambao ulisababisha polisi kuvamia nyumba yake iliyo Mikocheni na kufanya upekuzi kabla ya kuondoka na mwanasiasa huyo ambaye pia ni kiongozi wa kiroho na kwenda kumuhoji kituo cha polisi kwa saa kadhaa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

  Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi ina nakala yake, unazungumzia harakati za kuwaamsha waumini wa dini ya Kikristo kuamka kutetea dini yao dhidi ya utawala wa sasa ambao mchungaji huyo anautuhumu kuwa unawabagua.

  Waraka huo pia unawataja watu mbalimbali, kuanzia Rais Kikwete, viongozi wengine wa kisiasa na watu maarufu ukiwahusisha na tuhuma mbalimbali kubwa.
  Maaskofu kadhaa walionekana kumfuata Mtikila ili kupata nakala ya waraka huo ambao mchungaji huyo alikuwa amebeba nakala zake kwenye mkoba wa mkononi.

  “Nilikuja na nakala chahe sana... 60 tu, zikaisha na wengine wakawa wanautaka tena," alisema Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuzindua chombo hicho ambacho kazi yake kuu itakuwa ni kutetea haki za Wakristo.

  "Nimegawa hapa kwa sababu viongozi wenyewe waliutaka ndiyo nikaona niwape; nisiwe mchoyo,” alisema Mtikila.

  Mtikila alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuzaliwa kwa tatizo kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka ajihadhari, akidai kuwa ajira yake sasa ipo kwenye "danger zone (sehemu ya hatari).”
  Mtikila, ambaye ana ujasiri wa kutoa kauli zisizo na simile, alisema jukwaa hilo ni gharika kubwa kwa Rais Kikwete kwa sababu alizodai kuwa kiongozi huyo wa nchi ni adui mkubwa wa Ukristo.

  “Wakristo nchini tupo milioni 27 hivyo ajira ya JK hivi sasa ipo shakani," alisema.
  Viongozi wa makanisa ambayo yalishirika katika kuunda jukwaa hilo ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).
  Ndugu mtanzania upo sahihi theoretically lakini practically hicho hapo juu nilichohighlight kwa red ndo kinachotendeka. tafakari, chukua hatua.
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Haya mfungua maada
  Nasubiri kupata uwiano wa kweli...... il a hilo la nyama ndio linaniacha hoi
   
 9. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hizi mada za mara mfumo kristo mara mafumo islamu havitusadii kitu. Ni kama ushindani usiokuwa na maana na mwisho wake hakuna mshindi isipokuwa pande zote kubaki na maumivu tu. Tuangalie mambo ambayo yanaweza kutuunganisha zaidi kuliko kuangalia mambo yanayotugawa. Kwa sasa tungekazania katiba.
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Ok, endeleeni na malumbano....
  Nilikosea njia! Kumradhi, wajameni!
  You are doing a wonderful job! You are truly CCM ambassadors!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  so what is your opinion? bila kubase upande wowote lakini
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Soma post # 10.
  That is my opinion.
   
 13. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  udini live,mdini ni yule ambaye haijui dini yake vizuri
   
 14. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mfumo islam look somalia.angalia N.sudan wanavyo watesa south waislam mna asil ya Ubaguzi tena ule mbaya sana,kwa taarifa yenu muslim wil never conqurer this world by any means. Endeleeni kujilipua ,kuamini mapepo,kuoa vitoto,na lile neno la "kiyama"mko kwenye kiyama chenu wenyewe hapa duniani sajawahi ona imani inayoeleza uongo kama muslim .mna vurugu za maono sana.
   
 15. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hii mada si mahala pake... au umetumwa na chama kuja kuvuruga JF.. Maana CCM itikadi yao ni udini ndani ya chadema.. udini ndani ya siasa kila mahala wanaleta udini.. ili issues za maana zisiwe discussed
   
 16. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hii mada haina tija kwetu sote, tumeoleana tumezaliana tunaishi nyumba za kupanga pamoja, tunazikana na mambo meengi. yako mengi ya maana ya kujadili hili halijengi zaidi ya kutuacha sote hakuna aliye pata faidi. NAWASIHI WANAJF TUACHANE NALO.
   
 17. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Fikra mbinuko
   
 18. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Halafu sasa waislamu janja yao wakati wote ni kulalamika huku wakijua nafsini mwao kuwa wanasema uongo.........
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Nashukuru umekumbusha mfumo islam mwingine km huu ambao mimi nikifikiria sana huwa nachukia kupita kiasi...........kwa nini waislamu watuchinjie nyama eti......alafu kule mikoani mbona tunachinja wenyewe bila kutumia huu mfumo islamu?...........jamani ubaguzi huu wa kidini hapa tz unatokana na nini hasa?.........naamini wakristo wangekuwa ndiyo wachinjaji km ilivyo sasa kwa waislamu zamani maandamano yangekwisha kufanyika

   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana bila hii dini dinia inge-enjoy sana maisha lakini ukitaka kufanya mabo yako lazima ufikiria madhara ya uislamu.....
  -ukitaka kusafirisha mzigo wako toka ng'ambo kwa njia ya bahari unakumbuka waislamu maharamia wa kisomali
  -ukitaka kuwa busy na shughuli unakuta muislam yeye anakaa tu vijiweni na kunywa chai lakini maisha yake mazuri
  .......

   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...